Kichinjwa cha Ahlu al-Kitab

Kutoka wikishia

Kichinjwa cha Ahlul-Kitab (Kiarabu: ذبيحة أهل الكتاب) ni mnyama aliye chinjwa na wafuasi wa dini fulani miongoni mwa dini za watu walioshushiwa kitabu na Mwenye Ezi Mungu. [1] Kulingana na maelezo ya Sheikh Bahai (aliyafariki mwaka 1031 Hijiria), wengi wa wanazuoni wa madhehebu ya Shia kama vile Sheikh Tusi, [2] Sheikh Mufid, [3] na Sayyid Murtada, [4] wanaamini kuwa ni haramu kula nyama ya mnyama aliye chinjwa na watu Ahlul- Kitab, [5] hata kama wataja jina la Mwenye Ezi Mungu wakati wa kumchinja myanama huyo. [6] Imam Khomeini pia anashikilia maoni sawa na wanazuoni hawa. [7] Kundi hili la wanazuoni, wakirejelea Hadithi mbali mbali, [8] wanasema kwamba; maana ya uhalali wa kula "chakula cha watu wa kitabu" ulioelezwa katika Aya ya 5 ya Surat al-Maidah, ni chakula kama vile nafaka, sio nyama ya mnyama aliyechinjwa na watu wa dini hizo (Ahlu al-Kitab). [9] Pia, kulingana na maoni ya kundi hili la wanazuoni, viungo vya mwili na ngozi ya wanyama wenye damu inayotiririka (wakati wa kuchinjwa kwao) waliochinjwa na Ahlul-Kitab, husisabiwa kuwa ni nyama nyamafu na najisi, na haiwezekani (haijuzu) kutumia ngozi zao. [10]

Kulingana na maelezo ya Sheikh Bahai; Ni wachache tu miongoni mwa wanazuoni wanaomini kuwa ni halali kula nyama ya kichinjwa kilichochinjwa Ahlu al-Kitab. [11] Al-Allama Hilli ameyaegemeza maoni haya kwa Ibn Abi Aqeel [12] na Ibn Junaid Isfahani. [13] Kulingana na maoni ya Sheikh Saduqu [14] na Muhaddith Ardabili, [15] ni kwamba; Si haramu kula nyama ya wanyama hao ikiwa wachinjachi hao walitaja jina la Mungu pale walipokuwa wakiwachinja wanyama hao. [16] Ni vyema ieleweke kwamba; Wanyama waojadiliwa hapa ni wale wanyama tu ambao ni halali kuliwa nyama zao kulingana na dini ya Kiislamu.

Kuna kazi kadhaa zilizo andikwa kuhusiana na mada hii, ikiwa ni pamoja na:

  • Kitabu تحریم ذبائح اهل الکتاب (Kuharamishwa kwa Vichinjwa vya Ahlu al-Kitab), kilichoandikwa na Sheikh Mufid (aliyafariki mwaka 413 Hijiria). Sheikh Mufid Katika kitabu hichi, akirejelea Qur'an, hadithi, na ijmaa (mawafikiano ya fatwa ya wanazuoni), ametoa hoja kadhaa za kuunga mkono maoni yasemayo kwamba; Ni haramu kula nyama ya kichinjwa kilicho chinjwa na Ahlul-Kitab. [18] Pia ameeleza sababu za kupinga maoni ya wale wanaoamini uhalali wa wa kula nyama hizo. [19]
  • Kitabu حرمة ذبائح اهل الکتاب (Uharamu wa Vichinjwa vya Ahlu al-Kitab), kilichoandikwa na Sheikh Bahai (aliyafariki mwaka 1031 Hijiria). Kitabu hichi kiliandikwa kwa ombi la Shah Abbas Safawi. [21] Sheikh Bahai katika kitabu hichi, kwanza kabisa alielezea maoni ya wanazuoni wa Kishia na Kisunni juu ya suala hili. [22] Kisha akaeleza kwamba; yeye ana shaka kuhusu iwapo nyama ya kuchinja na watu wa Ahlu al-kitab ni haramu au la. Kiuhalisia Sheikh Bahai aliepuka kutoa fatwa na kuonesha wazi mawazo yake juu ya suala hili, bali alieleza maoni yake kwa sentensi isemayo kwamba; "Mungu anajua ukweli wa mambo ulivyo."[23]

Rejea

Vyanzo