Khawlah bint Mandhur
Khawlah bint Mandhur bin Dhabban al-Fazari (Kiarabu: خولة بنت منظور بن زبّان الفزارية) ni mke wa Imamu Hassan Mujtaba (a.s) na mama wa Hassan al-Muthanna. Alikuwa mke wa kwanza wa Muhammad bin Talha ambaye aliuawa katika vita vya Jamal na baada ya hapo akaolewa na Imamu Hassan Mujtaba (a.s).[1] Mama wa Khawlah alikuwa Malika bint Kharijah bin Sanan.[2]
Kwa mujibu wa ripoti baada ya kuuawa Muhammad yaani mume wa kwanza wa Khawlah, Abdallah bin Zubair aliyekuwa shemeji yake (yaani mume wa dadake), alitoa pendekezo kwa Imamu Hassan ili amuoe Khawla na Imam akaafiki. Pendekezo hilo lilitolewa hali ya kuwa baba yake hayupo. Baada ya baba yake kufahamu hilo, mwanzo alichukia lakini baadaye akaridhia.[3] Hata hivyo Baqir Sharif al-Qurashi mtafiti wa historia (aliaga dunia 1433 Hijria) ametilia shaka usahihi wa ripoti hii na kuitaja kuwa, inakinzana na hadhi na heshima ya Imam Hassan (a.s) na akatoa ushahidi wa kutokuwa kwake sahihi.[4] Kadhalika baadhi wamezungumzia kifo au kupewa talaka Khawla kabla ya Imamu Hassan kufa shahidi[5] na wengine wamezungumzia kuolewa kwake na Abdallah bin Zubair baada ya kufa shahidi Imamu Hassan.[6] Hata hivyo kwa mujibu wa Baqir Qurashi, Khawla alikuwa mke wa Imamu Hassan Mujtaba mpaka mwishoni mwa umri wake na hakuolewa hata baada ya Imamu kuuawa shahidi.[7] Imekuja katika kitabu cha Al-Aamali fil Mushkilat al-Qur’aniyah wal hukm wal Ahadith al-Nabawiyah cha Abdul-Rahman bin Qassim (aliaga dunia 339 Hijria): Khawlah alikuwa na wasiwasi mno wa kuuawa shahidi Imamu Hassan na alikuwa hana raha. Baba yake akiwa na lengo la kumliwaza alitunga betui kadhaa za mashairi:
نبئت خولة امس قد جزعت * من ان تنوب نوائب الدهر
[8]لاتجزعی یا خول و اصطبری * ان الکرام بنوا علی الصبر
Tafsiri: Jana nimepata habari kwamba, Khawlah anasononeka na kuhuzunika kutokana na misiba na masaibu ya dunia. Ewe Khawlah! Usihuzunike, kuwa na subira.
Khawlah alizaa watoto watatu na Muhammad bin Talha ambao ni Ibrahim, Dawud na Ummu Qassim.[9]