Iqtisaduna (Kitabu)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Iqtisaduna)
Iqtisaduna

Iqtisaduna (Kiarabu: اقتصادنا) ni kitabu kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr kinachousiana na fani ya uchumi wa Kiislamu. Kitabu hichi kinatambulisha na kukosoa nadharia za uchumi wa Ujamaa (Marxism) na Ubepari (Capitalism), kisha kinatoa mwelekeo na nadharia za mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. Lengo kuu la uandishi wa kitabu hichi; ni kubainisha misingi ya uchumi wa Kiislamu na tofauti zake na mifumo mingine mikuu ya kiuchumi ilitawala ulimwenguni. Moja ya nadharia muhimu zaidi ya Shahidi al-Sadr kuhusiana na uchumi wa Kiislamu, iliyo jadiliwa katika kitabu hichi, ni ile nadharia yake maarufu iitwayo nadharia ya Manṭiqat al-Faragh (eneo lenye ukosefu wa maagizo (ya kidini) ya moja kwa moja). Kuna tafsiri mbalimbali za kitabu hichi kwa lugha Kifarsi, na miongoni mwazo ni tafsiri iitwayo “Iqtisad Maa”, kilichotafsiriwa na Sayyid Muhammad Mahdi Barahani na Sayyid Abulqasim Husseini Jerfaa.

Mwandishi

Makala asili: Sayyid Muhammad Baqir Al-Sadr
Sayyid Muhammad Baqir Sadr, mwandishi wa kitabu Iqtisaduna

Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr alizaliwa mnamo tarehe 10 Esfand mwaka 1313 Shamsia (25 Dhul-Qa'dah 1353 Hijiria) sawa na tarehe 1 Machi mwaka 1935 Miladia huko Kadhimein. Mnamo mwaka 1400 Hijiria/1359 Shamsia sawa na mwaka 1981 Miladia, alikamatwa na serikali ya Ba'ath (ya Iraq) akiwa pamoja na dada yake, (Bint al-Huda al-Sadr), kisha kuuawa wote wawili kishahidi.[1] Mbali na kuwa kiongozi wa kidini, Al-Sadr pia alishikilia uongozi wa kisiasa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq naye ndiye mwanzilishi wa chama cha Hizb al-Da'wa al-Islamiyya. [2]

Al-Sadr alitoa nadharia mpya kwenye uwanja wa taaluma mbalimbali za Kiislamu kama vile; Usul al-fiqhi, fiqhi, falsafa ya siasa na epistemolojia. Baadhi ya nadharia zake maarufu ni nadharia ya Haq al-Ta’a, [3] Manṭiqat al-Faragh[4] na Tawalud Dhati Ma'arifa.[5] Miongoni mwa kazi zake andishi muhimu zaidi ni; kitabu Falsafatuna, Iqtisaduna, Duroos fi 'Ilm al-Usuli (maarufu kwa jina la “Halaqat”) na “al-Usus al-Mantiqiyya lil-Istiqra”.[6]

Motisha wa Uandishi

Shahidi Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr, katika utangulizi wa toleo la kwanza la kitabu chake, akiainisha lengo la uandishi wa kitabu hicho amesema kuwa; hili ni jaribio la awali la kuchunguza kwa kina mawazo ya kiuchumi ya Uislamu na kuyawasilisha kwa njia ya mfumo mmoja kamili. Akiendelea na maelezo yake aliendelea kusema kuwa; lengo lake hasa lilikuwa ni kufafanua misingi na nadharia msingi za uchumi wa Kiislamu, ili kuonesha tofauti zilizopo kati yake na mifumo mingine mikubwa ya kiuchumi duniani, na kuiweka kuufuma muktadha mafundisho ya Uislamu kuhusiana na mada hiyo kwenye mfumo mmoja.[7] Pia, alisisitiza kwamba; kushindwa kuunda mipango ya maisha kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu kunasababisha kuzorota na kupoteza mahitaji ya kiroho na kukosa majibu sahihi kwa ajili ya kukidhi mahitaji hayo. Kwa msingi huo, Al-Sadr alijitahidi vya kutosha katika kuonesha kuwa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ndio mfumo pekee unaoweza kutoa majibu yanayokidhi mahitaji ya kiroho na kwenye jamii za mwanadamu mbali mbali.[8]

Thamani Hadhi ya Kielimu ya Kitabu

Licha ya kupita zaidi ya nusu karne tangu kuchapishwa kwa kitabu cha “Iqtisaduna” (Uchumi Wetu), ila bado kitabu hichi kinaendelea kuhisabiwa kuwa ni mojawapo ya vitabu muhimu na maarufu zaidi katika uwanja wa uchumi wa Kiislamu. Kitabu hichi kimeendelea kuwa ndio rejeo kuu katika vyuo vikuu mbalimbali ulimwenguni, hasa katika masomo ya uchumi wa Kiislamu. kitabu Iqtisaduna hakijapewa kipaumbele tu katika nchi za Waislamu wa madhehebu ya Shia, bali pia kinafundishwa katika baadhi ya vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu zinazokaliwa na wafwasi wa madhehebu ya Sunni, ikiwemo Misri.[9] Dk. Muhammad Mubarak ameandika akisema kwamba; kitabu “Iqtisaduna” kiimewasilisha nadharia ya uchumi wa Kiislamu kwa kuchunguza kwa kina hukumu za Kiislamu na kuwasilisha nadharia zake kwa kutumia dhana za kisasa za elimu ya uchumi, huku kikihifadhi asili ya kifiq-hi juu ya masuala hayo.[10]

Muundo wa Kitabu

Muundo wa jumla wa Iqtisaduna unajumuisha vipande vifuatavyo:

  1. Utangulizi na Upembuzi wa Ujamaa (Marxism): Utambulisha na ukosoaji wa nadharia za uchumi wa Ujamaa.
  2. Utangulizi na Upembuzi wa Ubepari (Capitalism): Kutambulisha na kukosoa nadharia za uchumi wa Ubepari.
  3. Vigezo Muhimu vya Uchumi wa Kiislamu: Kuainisha na kueleza vipimo vya msingi vya mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu.
  4. Mchakato wa Kufikia Madhebu (Nadharia) ya Uchumi: Ufafanuzi wa hatua na michakato inayohitajika ili kufikia na kutekeleza mfumo wa uchumi wa Kiislamu.
  5. Nadharia ya Usawa Kabla ya Uzalishaji (Usawa Katika Mgao wa Mali Asili au Ghafi): Maelezo kuhusu jinsi rasilimali zinavyogawiwa kabla ya hatua ya uzalishaji.
  6. Nadharia ya Usawa Baada ya Uzalishaji: Ufafanuzi wa jinsi rasilimali zinavyogawiwa baada ya hatua ya uzalishaji.
  7. Nadharia ya Uzalishaji: Ufafanuzi wa mchakato na kanuni za uzalishaji katika uchumi wa Kiislamu.
  8. Majukumu ya Serikali katika Uchumi wa Kiislamu: Maelezo kuhusu majukumu na wajibu wa serikali katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu.

Mambo ya Msingi

Katika kitabu cha “Iqtisaduna”, kimetafautisha kati ya dhana mbili za "madhehebu (mifumo) ya kiuchumi" na "sayansi ya uchumi". Kitabu hichi kinaeleza ya kwamba; Sayansi ya uchumi ni ile sayansi inayo lenga kugundua matokeo na nyenendo za kiuchumi katika jamii pamoja na sababu na mafungamano yaliopo kati ya nyenendo hizo. Kwa upande mwingine, mfumo wa kiuchumi ni mtoaji wa njia ya adilifu katika kupanga maisha ya kiuchumi ya watu fulani. [11]

Kwa mtazamo wa Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr, ni kwamba; Uislamu umekuja kubainisha "mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu" na siyo "sayansi ya uchumi wa Kiislamu". Kwa hiyo, uchumi wa Kiislamu unatoa mbinu za haki za kupanga maisha ya kiuchumi, bila ya kutafuta au kugundua mambo mapya katika nyanja za uchumi. Kwa mfano, Uislamu haukuwa na lengo la kugundua sababu za riba katika eneo la Hijaz; badala yake, ulipiga marufuku riba na kuanzisha mfumo mpya unaotumia njia ya mudharabah (mpango wa uwekezaji kwa ushirikiano).[12]

Mantiqatu Al-Faragh

Makala Asili: Mantiqatu Al-Faragh

Nadharia ya Mantiqatu Al-Faragh (Eneo lenye ukosefu wa sheria za kidini) ni moja ya nadharia muhimu iliyowasilishwa katika kitabu “Iqtisaduna” na ni miongoni mwa uvumbuzi wa Shahidi Sadr. Kulingana na nadharia hii, Uislamu unaruhusu serikali ya Kiislamu kutoa hukumu na sheria katika baadhi nyanja na maeneo fulani, kulingana na mahitaji ya nyakati zilivyo. Shahidi Sadr aliliita eneo hilo kwa jina la Mantiqatu Al-Faragh. Katika mtazamo wake, baadhi ya sheria zilizowekwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) ziliwekwa zinaendana sawa na nadharia yake yeye. Hii si kwa sababu ya kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa Nabii, bali kwa sababu alikua ni kiongozi na msimamizi wa jamii.[13] Kwa hiyo uongozi wake ulikuwa ukienda sambamba na mahitaji ya jamii yalivyo.

Vyanzo vya Kitabu

Vyanzo vilivyotumika Katika uandishi wa kitabu “Iqtisaduna”, vinashirikisha mchanganyiko wa aina mbalimbali za vitabu ndani yake, ikiwa ni pamoja na; vyanzo vya hadithi, fiqhi, historia, tafsiri, falsafa na vyanzo vya nje ya Uislamu.[14] Shahidi Sadr, katika utangulizi wa chapa ya kwanza ya kitabu “Iqtisaduna”, alieleza akisema kwamba; lengo lake halikuwa ni kutoa maoni yake pekee katika ya kifiq-hi. Kwa hivyo, mbali na maoni yake mwenyewe, pia yeye aliongeza maoni ya wanazuoni wengine wa fiq-hi katika uandishi wa kitabu hicho.[15]

Vyanzo vya Kiislamu vilivyotumika katika Kitabu:

Vyanzo vya Kigeni vilivyotumika:

  • Das Kapital: kilichoandikwa na Karl Marx
  • Karl Marx kilichoandikwa na Henry Leffmann
  • La Philosophie et les Sciences: kilichoandikwa na Roger Garaudy
  • Al-Ishtrakiyyah: kilichoandikwa na Ahmad Shibli
  • The Communist Manifesto kilichoandikwa na Karl Marx na Friedrich Engels
  • Histoire du Développement de la Philosophie: kilichoandikwa na Andrei Zhdanov
  • On the Application: kilichoandikwa na Mao Zedong [16]

Maoni Kuhusu Kitabu

Kulingana na maoni ya baadhi ya watafiti, “Iqtisaduna” ni kitabu cha kipekee ikilinganishwa na vitabu vingine vya Muhammad Baqir Sadr. Hii ni kwa sababu ya kwamba; kitabu hicho kilitungwa katika kipindi ambapo mawazo ya Kibepari na ya Kijamaa yalikuwa yakienea kwa nguvu katika nchi mbali mbali za Kiarabu na Kiislamu. Wakati huo, kulikuwa na maswali, kama je, Uislamu ulikuwa na mpango wowote ule wa kutatua matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii?[17] Kwa upande mwingine, kitabu hichi kinatambuliwa kwa hadhi ya kiwango chake, mada, pamoja na mbinu zake, na kimejulikana kuwa ni miongoni mwa vitabu vyenye mwelekeo mpya wa kina na madhubuti katika uwanja wa masuala ya Kiislamu na elimu ya kidini.[18]

Vilevile, kumekuwa na baadhi ya maoni yaliojitokeza katika kukosoa kitabu hichi. Miongoni mwa maoni ya ukosoaji huo yanasema kwamba; kitabu “Iqtisaduna” hakikujali wala kuweka mikakati na mipango maalumu ya kimatendo, ya usimamizi wa taasisi za kiuchumi za jamii. [19] Pia wengine wameka vizingiti dadisi kuhusiana juu ya nadharia yake ya “Matiqatu al-Faragh” aliyo iwasilishwa katika kitabu chake hicho.[20]

Chapa na Tafsiri

Baadhi ya machapisho na tafsiri za kitabu cha Iqtisaduna ni kama ifuatavyo:

  • Iqtisaduna, chapa ya Pujuhishgahe Ilmiy-Takhassusiy Shahid Sadr, Qom.
  • Iqtisaduna, chapa ya Dar al-Fikr, Beirut.
  • Iqtisad Maa, tafsiri ya Muhammad Mahdi Fooladwand, chapa ya Bunyade Ulume Islamiy.
  • Iqtisad Maa, tafsiri ya Sayyid Muhammad Mahdi Barahani na Sayyid Abul-Qasim Hosseini Jorfaa, chapa ya Pujuhishgahe Ilmiy-Takhassusiy Shahid Sadr, Qom.
  • Iqtisad Maa, tafsiri ya Muhammad Kadhim Musawi na Abdul ‘Aali Esphandi, chapa ya Jumiatu-al-Madarisin Hawze Ilmiyye Qom.
  • Baresiy Sistemhaye Iqtisad (Mukhtasari wa kitabu Iqtisaduna), kilicotayarishwa na Gholamreza Misbahi, chapa ya Naassir, Qom.

Rejea

  1. Husseini Hairi, Sayid Kadhim, Zendegi wa Afkar Shahid Sadr, uk. 35.
  2. Fadhlullah, Shahid Sadr Dar Bastar Andisheh wa Amal, uk. 13 va 14.
  3. Islami, Maktab Usuli Shahid Ayatullah Sadr, uk. 153; Larijani, Nadhariyyah Haq al-Tha'ah, uk. 12.
  4. Husseini Hairi, Iqtisad Islami wa Rawesh An az Didgah Shahid Sadr Rahimahullah,uk. 29.
  5. Khasrupanah, Manteqe Esteqra' az Didgahe Shahid Sadr, uk. 29
  6. Sadr, Mabahith al-Usul, Muqaddimah Husseini Hairi, 1407 H, juz. 1, uk. 67-69.
  7. Sadr, Iqtisaduna, 1424 H, uk. 43-44.
  8. Sadr, Iqtisaduna, Muqaddame uk. 34.
  9. «Ta'amili Bar Iqtisad Islami Dar Andishe Shahid Muhammad Baaqir Sadr», Pegah Hawze, 1 Ardibehesht 1386 S, 205.
  10. Sadr, Iqtisad Ma, Muqaddame Nashir, juz. 1, 1393 S, uk. 10.
  11. Husseini Hairi, Iqtisad Islami wa Rawesh An az Didgah Shahid Sadr Rahimahullah,uk. 22-24.
  12. Husseini Hairi, Iqtisad Islami wa Rawesh An az Didgah Shahid Sadr Rahimahullah,uk. 22 va 23.
  13. Sadr, Iqtisaduna, 1424 H, uk. 443, 444 Sadr, Iqtisad Ma, tarjumah. Sayid Abul Qasim Zarfa, 1393 S, juz. 2, uk. 41-42.
  14. Sadr, Iqtisad Ma, 1393, juz. 2, uk. 489-499
  15. Sadr, Iqtisaduna, uk. 31, 1411 H.
  16. Sadr, Iqtisad Ma, 1393, juz. 2, uk. 489-499
  17. Salman, Iqtisaduna (Muhammad Baqir Sadr), uk. 253
  18. Salman, Iqtisaduna (Muhammad Baqir Sadr), uk. 254.
  19. Jidari Ali, Naqde Kitabe Iqtisaduna, uk. 167.
  20. Husseini, Bazshenasi, Tahlil va Naqd Nazariye Manteqah al-Faragh, uk. 96

Vyanzo

  • Islami, Ridha. Maktab Usul Shahid Ayatullah Sadr. Majalah Pajuhesh wa Hauzeh. uk. 28 va 29, 1385 S (2006).
  • «Ta'ammuli Bar Iqtisad Islami Dar Andishe Shahid Muhammad Baaqir Sadr», Pegah Hawze, 1 Ardibehesht 1386 S, 205.
  • Jidari Ali, Muhammad Naqde Kitabe Iqtisaduna, Iqtisad Islami, juz. 1, 1380 S.
  • Husseini, Sayid Ali, Bazshenasi, Tahlil va Naqde Nazariye Manteqah al-Faragh, majalah Andeshe Sadeq, juz. 6 va 7, 1381 S.
  • Husseini Ha'iri, Sayid Kadhim. Iqtisad Islami va Rawesh Kashf An az Didgah Shahid Sadr Rahimahullah. Tarjumeh Ahmad Ali Yusufi, Iqtisad Islami. juz. 1, 1380 S (2001).
  • Husseini Ha’iri, Sayid Kadhim. Zendegi va Afkar Shahid Sadr. Tarjumeh Hassan Tarimi. Tehran: Wezarat Farhang wa Arshad Islami, juz. 1, 1375 S (1996).
  • Khusrupanah, Abdul Husain. Mantiq Istiqra' az Didgah Shahid Sadr. Dhihn. juz. 1, 1383 S (2004).
  • Salman, Hasan. Iqtisaduna (Muhammad Baqir Sadr). al-Ijtihad. juz. 37, 1418 H.
  • Fadhlullah, Sayid Muhammad Hussain. Shahid Sadr dar Bastar Andishe va Amal: U be Shekle Tabi'i dar Jaigahe Marja'iyat Qarar gerift, majalah Shahid Yaran, juz. 18, 1386 S.
  • Sadr, Sayid Muhammad Baqir. Iqtisaduna. Markaz al-Abhath wa ad-Dirasat at-Takhassusiyyah li al-Imam Shahid Sadr, Qom: juz. 1, 1424 H.
  • Sadr, Sayyid Muhammad Baqir. Iqtisad Ma. Juz. 2. Tarjumeh Sayid Abul Qasim Husseini Zarfa. Qom: Pajuheshgah 'Ilmi Takhassusi Shahid Sadr, 1393 S (2014).
  • Larijani, Sadiq. Nadhariye Haqq at-Ta'ah. Pajuheshha-ye Usuli. juz. 1, 1381 S(2002).