Ibara ya Kun Fayakun

Kutoka wikishia

Ibara isemayo: “Kun Fayakun کُنْ فَیَکونُ” inamaanisha kauli ya amri ya kukiamrisha kitu fulani kwa kiambia: “Kuwa! Nacho kikawepo”. Ibara iirejelea matakwa ya Mwene Ezi Mungu katika uumbaji wake wa vitu mbali mbali kwa mapenzi Yake. Kauli hii imetajwa mara kadhaa katika Quran, hadithi, na mashairi ya Kifarsi. Wafasiri wa madhehebu ya Imamiyyah (Shia Ithnaashariyyah) wanaijengea kauli hii taswira ya kwamba; Matakw ya Mwenye Ezi Mungu, ni sawa na uumbaji wake wa kuumba vitu mbali mbali, yaani matakwa yeke tu hua ni tosha katika kuumbika kwa vitu avitakavyo, bila haja halisi ya kutumi amri ya neno “Kun” lenye maana ya kukiamrishwa kitu fulani kumbike. Hata hivyo, wengi miongoni mwa wanazuoni wa Kisunni hawakubaliani na tafsiri hii. Ibara ya “Kun Fayakun کُنْ فَیَکونُ” Katika Qur’ani, Riwaya na Mashairi ya Kifarsi

Tungo au ibara hii ya “Kun Fayakun کُنْ فَیَکونُ” yanapatikana katika Aya nane za Qurani, Aya ambazo kiuhalisia zinahusiana uwepo wa matukio mbali mbali, ikiwemo mada ya kuzaliwa kwa nabii Isa (a.s) kwa njia isiyo ya kawaida (kimiujiza), masuala ya uumbaji pamoja na tukio la Siku ya Kiyama. [2] Aya mojawapo iliyotumia maneno haya ni ile Aya isemayo: “إِذا قَضی أَمْراً فَإِنَّما یقُولُ لَهُ کنْ فَیکونُ” [2] ambayo maana yake ni kwamba: “[Mwenyezi Mungu] anapolipitisha jambo (anapo amua), basi hukiambia tu kitu hicho kwa kusema: kuwa! Nacho huwepo.” Hii inaonyesha kwamba Mwenye Ezi Mungu anapotaka kitu fulani kiwepo, basi hukiambia tu: Ewe kitu fulani kuwa! Nacho huwepo papo hapo bila ya kuchelewa. [3]

Pia kuna Hadithi moja fulani iliyo nukuliwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kwamba: Mwenye Ezi Mungu anawaambia watu wa Peponi: “Nikitoa kauli ya kukiambia kitu fulani: ‘Kuwa’ basi kitu hicho hutokea; sasa mimi natoa mamlaka nakukupeni nyinyi, ili mkiseme kukiambia kitu fulani ‘Kuwa’, basi kitu hicho kifanyike na kiwepo kupitia amri yenu hiyo. [4]

Washairi wa lugha ya Kifarsi kama wakiwe; Attar, [5] Jalalau al-ddin Rumi, [6] Saadi, [7] na Nidhami, [8] pia nao wameitumia sentensi hiyo katika mashairi yao, wakionyesha muktadha wa Qur’ani kuhusiana na uwezo wa Mwenye Ezi Mungu. [9] Maana na Tafsiri ya “Kun Fayakun کُنْ فَیَکونُ” “Wafasiri wengi wa upande wa madhehebu ya Shia Ithna Ashari, wanaichukulia Aya hii kama mfano wa ukweli kwamba; Mwenye Ezi Mungu anapotaka kitu fulani kiwepo, basi kitu hicho huwepo; bila haja ya kutumia amri ya neno ya “Kun” katika kukiamrisha kitu hicho. [10] Wao wanaamini ya kwamba; Matumizi ya neno “Kun” kwa ajili kuumba kitu fulani, yanahitaji mfululizo wa amri nyengine kadhaa na hayana maana yoyote ile katika suala hilo. Hii inamaanisha ya kwamba; hata hilo neno “Kun” pia nalo litahitaji mfululizo wa “Kun” nyingine kwa ajili ya kuiumba hiyo “Kun” ya mwanzo. Na kila “Kun” itahitaji “Kun” nyengine hadi milele. Kutokuwa na maana juu ya kuwepo “Kun” ya kimatamshi, ni kwa sababu haiwezekani kukiambia kitu hicho “Kun”, kwani kitu hichio bado hakijawepo, kiasi ya kwamba kipewe amri ya “Kun”, na ikiwa kitu hicho kipo, basi hakuna haja tena ya kukiamrisha kiwepo kwa kutumia amri hiyo ya “Kun.” [11] Wafasiri wa upande wa madhehebu ya Shia Ithna Ashari, wanategemea sana maneno ya Imam Ali (a.s), katika kufasiri ibara hii ya “Kun Fayakun کُنْ فَیَکونُ”.

Katika mojawapo ya maneno yake, Imamu Ali (a.s) anasema: “Pale Mwenye Ezi Mungu anapotaka kitu kifanyike, husema tu: kuwa! Na papo hapo kitu hicho hutokea; hii si kwa maana ya kwamba sauti yake inasikika masikioni au kuna ukelele unaosikika kutoka kwake, bali neno la Mwenye Ezi Mungu ni sawa sawa na uwepo au uumbikaji wa kitu hicho, ambacho hakikuwepo kabla ya hapo.” [12] Nivyema kelewa kuwa, katika tafsiri za kiirfani (Kisufi); ibaya ya “کُنْ فَیکونُ” inaashiria uwepo na wa jambo fulani au kwamaana nyengine, ni dhihiriko la vitu na viumbe mbali mbali. [13] Wafasiri wengi wa Kisunni hawatafsiri wala kuifahamu Aya hii kwa mfumo wa lugha za kitamthilia (kimifano), na badala yake wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu anapotaka kuumba kitu fulani, hutumia neno la kimatamshi la ‘Kun’; au hata akitaka kitu fulani kibadilike, basi hutumia kauli hiyo ya ‘Kun’ kwa ajili ya kubadilisha hali ya mwanzo ya kitu hicho; [14] au pale Mwenye Ezi anapotaka kukitoa kitu fulani kilichopo ndani ya elimu na ulimwengu wa Kiungu, hutumia neno hilo ili kitu hicho kiweze kuumbwa na kudhihirika katika ulimwengu wa kimaumbile. [15]