Hilyat al-Muttaqin (kitabu)
Hilyat al-Muttaqin (Kiarabu: حلية المتقين) ni kitabu cha Kifarsi kuhusu akhlaq (maadili), adabu, desturi na ada za Kiislamu kilichoandikwa na Allama Majlisi (1110-1037 H). Kama Allama Majlisi alivyosema, kitabu hiki ni tarjumi nyepesi ya hadithi sahihi za Shia. Kitabu cha Hilyat al-Muttaqin kimepangwa katika faslu au milango 14 na hitimisho moja, na miongoni mwa yaliyomo ndani ya kitabu hiki ni pamoja na adabu za uvaaji nguo, adabu za kula na kunywa, ndoa na maingiliano na wanawake, watoto na watu, adabu za kufanya biashara na kusafiri.
Allama Majlisi aliandika kitabu cha Hilyat al-Muttaqin mwaka 1081 Hijria akiwa na umri wa miaka 44. Kitabu hiki kimechapishwa mara nyingi na kutafsiriwa katika lugha za Kiarabu na Kiurdu. Mohammad Taqi Bahar amekitambua kitabu hiki kuwa moja ya kazi muhimu zaidi ya Allama Majlisi baada ya kuandika Bihar al-Anwar katika lugha ya Kiajemi.
Mwandishi
- Makala kuu: Muhammad Baqir Majlisi
Muhammad Baqir Isfahani (1037-1110 Hijria), mashuhuri kwa jina la Allama Majlisi na Majlisi wa Pili, ni mtoto wa Muhammad Taqi Majlisi, mashuhuri kwa jina la Majlisi wa Kwanza. [1] Allama Majlisi alizaliwa mwaka 1037 Hijria katika mji wa Isfahan, Iran. [2] Mjumuiko mkubwa wa hadithi wa kitabu cha Bihar al-Anwar na kadhalika kitabu cha Mir’at al-Uqul katika sherh na ufafanuzi wa Usul al-Kafi zimetambuliwa kuwa athari muhimu zaidi. [3]
Katika zama za Shah Suleyman Safavi, Allama Majlisi alikuwa na jukumu la Sheikh al-Islam na alishikilia wadhifa na jukumu hilo hadi mwishoni mwa umri wake. [4] Sheikh Hurr Amili alikuwa katika zama moja na Allama Majlisi. Yeye ni mhakiki, fakihi, mwanateolojia na mtaalamu wa elimu ya hadithi wa kuaminika ambaye ana vitabu vingi alivyaondika. [5] Majlisi wa Pili, alikuwa miongoni mwa wanazuoni wachache ambao waliandika vitabu vya lugha ya Kifarsi ambavyo vinaweza kutumiwa na umma ambapo miongoni mwavyo ni Hayat al-Qulub, Hilyat al-Muttaqin na Jalau al-Uyun. [6] Kuna athari na vitabu zaidi ya 50 ambavyo vinanasibishwa na yeye. [7] Muhammad Taqi Bahar, mshairi na mwanafasihi mahiri wa Iran, amekitambua kitabu cha Hilyat al-Muttaqin cha Allama Majlisi kuwa kitabu na athari muhimu zaidi ya mwanazuoni huyo kwa lugha ya Kifarsi baada ya kitabu cha Bihar al-Anwar. Kwa mujibu wa mshairi huyo ni kwamba, kabla yake hakuna mwanazuoni na msomi ambaye alikuwa amefanya kazi hiyo. [8]
Msukumo na zama za kuandikwa kitabu hiki
Kama Allama Majlisi alivyosema katika utangulizi wa kitabu cha Hilyat al-Muttaqin ni kuwa, aliandika kitabu hiki kwa ombi la baadhi ya watu ambao walimwomba aandike risala fupi na ya kueleweka na wote kuhusiana na maadili ambayo imesimuliwa kutoka kwa Maimamu kwa sanadi na mapokezi sahihi. [9]
Allama Majlisi aliandika kitabu hiki tarehe Rajab 5, 1079 Hijria [10] na Agha Bozorg Tehrani pia ameandika kwamba utunzi na uandishi wa Hilyat al-Muttaqin ulikamilika tarehe 26 Dhu al-Hijja 1081 Hijria;[11] yaani, wakati Allama Majlisi alipokuwa na umri wa miaka 44. [12]
Maudhui
Hilyat al-Muttaqin (pambo la wacha-Mungu) ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kifarsi kuhusiana na akhlaq, adabu na ada (mila) za Kiislamu kama alivyosema Allama Majlisi ni tarjumi nyepesi ya hadithi za Shia. [13] Miongoni mwa maudhui zilizoko katika kitabu hiki ni:
- Adabu za mavazi na uvaaji.
- Adabu za mapambo ya wanawaume na wanawake, kupaka wanja na hina.
- Adabu za kula na kunywa.
- Kubainisha fadhila za ndoa, adabu za kuingiliana na kuamiliana na wanawake na namna ya kuwalea watoto.
- Adabu za kupiga mswaki, kuchana nywele, kucha, sharubu, kunyoa na kadhalika.
- Adabu za kutumia manukato, kupaka mafuta na kadhalika.
- Adabu za kuoga na adabu za baadhi ya majosho.
- Adabu za kulala na kuamka.
- Adabu za hijamat, kutaja baadhi ya dhikri na sifa zake maalumu na kutibu baadhi ya maradhi na kusoma baadhi ya dua.
- Adabu za kuamiliana na kuingiliana na watu.
- Adabu za baadhi ya mambo kama kutoa salamu, kupeana mikono, kukumbatiana, kubusiana na kadhalika.
- Adabu za kuingia ndani na kutoa ndani kwenda nje.
- Adabu za kutembea kwa miguu, kupanda kipando, sokoni, biashara, kilimo na kufuga wanyama.
- Adabu za safari.
- Hitimisho: Katika kubainisha baadhi ya adabu mbalimbali na faida zake. [15]
Tarjumi na Mukhtasari
Kitabu cha Hilyat al-Muttaqin cha Allama Majlisi kimetarjumiwa na kufanyiwa mukhtasari tofauti tofauti; miongoni mwazo ni:
- Mukhtasari, kupanga faslu: Athari ya Muhammad Baqir Fesharaki (aliaga dunia 1315 Hijria) kikiwa na anuani ya «Adaab al-Shariah». [16]
- Mukhtasari uliofanywa na Sheikh Abbas Qumi kwa jina la Mukhtasari al-Abwab fi al-Sunan Wal-adab. [17]
- Tarjumi kwa lugha ya Kiarabu, athari ya Abdul-Hussein Shabestari. [18]
- Tarjumi kwa lugha ya Kiarabu iliyofanywa na Khalil Razaq Amili. [19]
- Tarjumi ya lugha ya Kiurdu iliyofanywa na Sayyid Maqbul Ahmad Dehlavi kwa jina la Tahdhib Islam. [20]