Hamida mke wa Imamu Sadiq (as)
Humaidah au Hamida al-Musaffa (Kiarabu: حميدة زوجة الإمام الصادق) alikuwa mke wa Imamu Swadiq (a.s) na mama wa Imamu Kadhim (a.s). Kwa mujibu wa hadithi, Imamu wa Sita wa Waislamu wa Kishia (Imamu Swadiq) alimtaka mmoja wa masahaba zake akachukue kwa Hamida jibu la swali lake alilomuuliza. Kwa maana kwamba, baada ya yeye kuulizwa na sahaba wake, hakujibu na badala yake alimtaka akajibiwe swali lake hilo na Bi Hamida. Hamida alikuwa pia mmoja wa mawasii watano wa Imamu Swadiq (a.s).
Imamu Muhammad Baqir (a.s) katika kumsifu Hamida anasema: Hamida ni mwenye kupendwa duniani na mwenye kusifiwa akhera. Imamu Swadiq (a.s) alimtambua Bi Hamida kuwa mwanamke msafi, mtakasifu kunako mambo machafu.
Historia
Humaidah ni mama wa Imamu Kadhim (a.s) [1]. Katika nyaraka za historia hakuna taarifa za tarehe ya kuzaliwa kwake. [2]
Baba yake Hamida ni Sa’id Berber au Salih. [3] Kuhusiana na mbari na kizazi cha Hamida kuna hitilafu za kimitazamo [4]. Imekuja katika vyanzo vya historia kwamba, Hamida alikuwa na asili ya Berbariyyah, Andalusia [5] na Maghribiyah. [6]
Kwa mujibu wa hadithi Imam Baqir (a.s) alimnunua akiwa mtumwa na akampa zawadi mwanawe Imamu Swadiq (a.s). [7] Kwa mujibu wa nukuu ya Allama Majlisi ni kuwa, yeye ni mama wa Mussa bin Ja’far, Is’haq na Fatma ambao ni watoto wa Imamu Swadiq (a.s). [8]
Inaelezwa kuwa, kaburi la Hamida lipo Mashraba Umm Ibrahim katika eneo la al-Waali mashariki mwa makaburi ya Baqi’i jirani na kaburi la Najma mama wa Imamu Ridha (a.s). [9]
Daraja
Kwa mujibu wa vyanzo vya hadithi, Imamu wa Sita wa Waislamu wa Kishia (Imamu Swadiq) alimtaka mmoja wa masahaba zake akachukue jibu la swali lake alilomuuliza kwa mkewe Hamida. Hivyo alimtaka amtume kijakazi wake kwa Hamida ili akachukue jibu la swali lake. Kwa maana kwamba, baada ya yeye kuulizwa na sahaba wake, hakujibu na badala yake alimtaka akajibiwe swali lake hilo na Bi Hamida. Imamu Swadiq (a.s) alikuwa akimtuma Hamida na Umm Farwa binti yake kwa ajili ya kutekeleza haki za watu wa Madina. [11] Kadhalika Hamida ni mmoja wa watu watano ambao Imamu Swadiq (a.s) aliwatambulisha kuwa ni mawasii wake. [12]
Imamu Muhammad Baqir (a.s) amemtaja bi Hamida kuwa: Mwenye kupendwa duniani na mwenye kusifiwa akhera. [13] Imamu Swadiq (a.s) amemtaja Hamida kuwa ni msafi na mtakasifu kunako machafu na akamsifia kuwa ni mkuo wa dhahabu na ambaye daima malaika wanamlinda. [14] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana akapewa lakabu ya Hamida al-Musaffa. [15] Lakabu zake zingine ni Lu’ulu’ah [16] na Muhadhabah [17].
Kumenukuliwa hadithi kutokana kwa Hamida kuhusiana na hija ya watoto [18] na vilevile hadithi kuhusiana na kuuawa shahidi Imamu Ja’afar Swadiq (a.s) katika vyanzo vya hadithi. [19] Kwa mujibu wa hadithi, Najma mama wa Imam Ridha (a.s) alikuwa kijakazi ambaye baada ya Hamida kuota ndoto ya kweli [20] ali mpatia mwanawe Imam Kadhim (a.s) kama zawadi. [21]
Rejea
Vyanzo
- Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-Ṭālibīyyīn. Beirut: Dār al-Maʿrifa, n.d.
- Baḥrānī, Sayyid Hāshim al-. ʿAwālim. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Mahdī, 1409 AH.
- Gharawī Nāʾīnī, Nahlā. Muḥaddithāt al-Shīʿa. Tehran: Dānishgāh-i Tarbīyat Mudarris, 1375 Sh.
- Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1421 AH.
- Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1363 Sh.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Muʾassisat al-Wafāʾ, 1403 AH.
- Māmaqānī, ʿAbd Allāh al-. Tanqīḥ al-maqāl. Najaf: Maṭbaʿat al-Murtaḍawīyya, 1352 AH.
- Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Ithbāt al-waṣīyya. Qom: Anṣārīyān, 1417 AH.
- Qarashī, Baqir Sharīf al-. Ḥayāt al-Imām Mūsa ibn Jāʿfar. N.p: Dār al-Balāgha, 1413 AH.
- Qummī, Shaykh ʿAbbās. Muntahī l-āmāl. Qom: Hijrat, 1412 AH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. Qom: Muʾassisat al-Biʿtha, 1417 AH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Ḥusayn Aʿlamī. Beirut: Muʾassiat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1404 AH.
- Ṭabarī al-Shīʿī, Muḥammad b. Jarīr al-. Dalāʾil al-Imāma. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1408 AH.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi-aʿlām al-hudā. Qom: Āl al-Bayt, 1417 AH.