Hadithu I’itilaa

Kutoka wikishia

Hadithu I’itilaa (Kiarabu:حديث الاعتلاء): Ni Hadithi iliyo nukuliwa kutoka Mtume Muhammad (s.a.w.w), inayo ashiria ubora wa dini ya Kiislamu juu ya dini nyingine na ukafiri kutokuwa na mamlaka ya utawala juu ya Mwislamu. Watu kama vile Sayyid Hassan Baqer al-Bajuni (aliyezaliwa mwaka 1936 Hijiria) wanaamini kuwa; udhaifu wa mlolongo wa wapokezi wa Hadithi ya Hadithu I’itilaa, unaweza kufidiwa kuzibwa pengo lake, kwa kuwa wanazuoni wengi maarufu wameifanyia kazi na kuiamini Hadithi hii.

Wataalamu wengine wa Hadithi wamekataa uhusiano uliopo kati ya Hadithu I’itilaa na kukataliwa kwa utawala wa kafiri juu ya Muislamu, wakiamini kuwa Hadithi hii inahusu tu ukamilifu wa dini ya Kiislamu juu ya dini nyingine. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba dini ya Kiislamu imeundwa na mkusanyiko wa sheria na kanuni, hivyo basi, kila wakati isemwapo kwamba; Uislamu una ukamilifu na ukuu wa kuzipiku dini nyengine, hii humaanisha kwamba, Mwenye Ezi Mungu ametunga sheria kwa njia ambayo katika hali zote zile, kafiri hawezi kuwa na aina yoyote ile ya mamlaka juu ya Muislamu. Ili kuthibitisha maudhui ya Hadithi, wanazuoni wamerejelea Aya ya 141 ya Surat al-Nisaa ijulikanayo kwa jina la Aya ya Nafy al-Sabil.

Maelezo Mukhtasari na Umuhimu wa Hadithi

Hadithu I’itilaa (Hadithi ya Ubora wa Dini ya Uislamu Juu ya Dini Nyengine): Ni Hadithi kutoka kwa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambayo imenukuliwa katika kitabu Man laa Yahdhuruhu al-Faqih, ambacho ni miongoni mwa vitabu vine mashuhuri vya Shia. [1] Pia Hadithi hii imenukuliwa ndani ndani kitabu cha Kisunni kiitwacho “Sunni al-Daruqutniy”. [2] Pia Hadithi hii iweza kuaamsha hisia wanazuoni kadhaa, akiwemo Sheikh Mufid na Sayyid Murtadha. [3] Kwa mujibu wa maelezo ya Murtadha Mutahhari (aliye fariki mwaka 1358 shamsia), ni kwamba; Hadithi hii ni yenye ufahamu tata, ambapo kila mmoja miongoni mwa watafiti mbali mbali, wameifahamu kwa namna tofauti na wengine. [4]

Hadithu I’itilaa, kulingana na nukuu za Sheikh Saduqu ni kama ifuatavyo: (اَلأِسلامُ يَعْلُو وَ لا يُعلي عَليْهِ وَ الْكُفّارُ بِمَنْزِلَةِ الْمَوْتي لا يَحْجُبونَ وَ لا يَرِثُونَ) Yaani: Uislamu siku zote iko juu na wala hauwezi kukaliwa juu yake, na makafiri wako kama wafu, hawana uwezo wa kuzuia mali yao kuto rithiwa na wala hawana mamlaka ya kurithi kitu (katika mali ya urithi). [5]

Hadithi hii inazingatiwa na wanazuoni kama ni uthibitisho wa kanuni ya kutowezekana kwa asiyekuwa Mwislamu kuwa na mamlaka juu ya Waislamu umilki. [6] Kulingana na maoni ya Musa al-Bajuni ni kwamba; Hadithi hii si kwamba inahusu tu makafiri kuto kuwa na haki ya mamlaka ya kuwatawala Waislamu, bali pia inathibitisha ubora na uadhimu wa dini ya Kiislamu juu ya dini nyinginezo. [7]

Hadithu I’itilaa inachukuliwa kuwa ni kielelezo kinachoelezea sheria na kanuni [8] ambazo kwa mujibu wake zinakataza aina yoyote ya mamlaka ya makafiri juu ya Waislamu katika nyanja zote, kama vile mikataba, upitishaji (ukataji wa kauli katika utekelezaji wa miamala fulani ambayo hupitisha kwa kauli ya upande mmoja tu), madaraka, makubaliano pamoja na ndoa. [9] Hadithi hii inajumuisha ndani yake sentensi mbili za uthibitisho na ukunushaji (ukataaji); ambazo zote mbili zinaonyesha kutowezekana kwa makafiri kuwa na mamlaka juu ya Waislamu: [10]

  1. Sentensi ya uthibitisho isemayo: (يعلو و لایعلی علیه) “Uislamu upo juu na wala haiwezekani kukaliwa juu yake”。 Inahusiana na sheria na kanuni zilizotungwa katika Uislamu, ambazo zinazingatia uadhimu na ubora wa Waislamu katika nyanja zote. [11]
  2. Sentensi ya ukanushaji isemayo: (لا يَحْجُبونَ وَ لا يَرِثُونَ) “Makafiri ni kama hawana uwezo wa kuzuia mali yao kuto rithiwa na wala hawana mamlaka ya kurithi kitu (katika mali ya urithi”。 Inahusiana na ukanushaji na ukataaji wa kule makafiri kuwa na mamlaka juu ya Waislamu katika sheria na kanuni zilizotungwa katika Uislamu. [12]

Ufafanuzi juu ya Uhalali wa Hadithu I’itilaa

Wanazuoni wamesema kwamba; Kuna utata juu ya uhalali wa Hadithu I’itilaa. Baadhi ya wanazuoni wameona kwamba; mnyororo (mlolongo) wa wapokezi wa Hadithi hii una mashaka, jambo ambalo limewafanya baadhi yao kuiona kuwa ni Hadithi dhaifu. [13] Hata hivyo, kinyume chake, wanazuoni wengine wameona kuwa; Hadithi hii ni ya kweli na wametoa sababu kadhaa za kuunga mkono Hadithi hii. Mojawapo ya sababu hizo ni umaarufu wa kufanyiwa kazi hadithi Hadithi hii na wanazuoni maarufu waliopita, na sababu nyengine ni kwamba; kule Hadithi kutumiwa na kufanyiwa kazi na wanazuoni waliopita, kunapelekea kupatikana kwa uhakika kwamba Hadithii imenukuliwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w). [14] Pia wametoa Sababu nyingine nayo kwamba; Kule Hadithi kunukuliwa na Shaykh Saduqu katika kitabu chake Man La Yahdhuruhu al-Faqih, ambacho ni kimoja kati ya vitabu vinne vya madhehebu ya Shia, ni dalili ya usahihi wake, kwani yeye hanukuu kitabuni mwake isipokuwa Hadithi sahihi. [15] Abdul-Aali al-Sabzewari (aliyofariki mwaka 1973 Shamsia) pia katika kitabu chake cha tafsiri ya Qur’ani kiitwacho Tafsiru Mawaahibu al-Rahman kwa kuzingatia Aya ya Nafy al-Sabil, amekubaliana na usahihi wa Hadithu I’itilaa na kuihisabu kuwa ni sahihi na ya kweli. [16]

Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa; Hadithu I’itilaa inahusiana na suala la kuitangaza na kuiarifisha dini ya Kiislamu kama dini bora zaidi impwekeshayo Mwenye Ezi Mungu kuliko dini nyengine. Wao wanasema kwamba; Hadithi hii haina uhusiano wowote ule na suala la ukanushaji wa mamlaka ya makafiri juu ya Waislamu. [17] Katika kujibu utata wa wazo hili, imeelezwa kwamba; dini ya Kiislamu ni mkusanyiko wa sheria na kanuni, na kwamba pale isemwapo kuwa Uislamu una uadhimu, utukufu na ubora dhidi ya dini nyengine, maana yake ni kwamba; sheria zilizotungwa na Mwenye Ezi Mungu, zimetungwa kwa njia ambayo hakuna mtu asiyekuwa Muislamu katika hukumu hizo, atakaye kuwa na wa kuwa na mamlaka ya kuwalia Wailsamu juu ya vichwa vyao, kuwaendesha kwa matakwa yake. [18]

Matumizi ya Hadithi

Kulingana na maoni ya mwanazuoni maarufu marehemu Murtadha Mutahhari ni kwamba; Hadithu I’itilaa inatumiwa katika maeneo matatu maalumu; ambayo ni Fiqhi, Kalam (Theolojia), na Jamii:

  • Matumizi ya Fiqhi: Hadithu I’itilaa kifiqhi inaonyesha kwamba; hakuna sheria katika Uislamu ambayo inasababisha na kupelekea wasio Waislamu kuwa na mamlaka juu ya Waislamu.
  • Matumizi ya Kalam: Hadithu I’itilaa katika uwanja wa kitheolojia inaonyesha kwamba; dini ya Kiislamu katika kusimamisha hoja na kutoa ithibati ndio bingwa, ambayo iko juu ya dini nyinginezo katika suala hilo, na kwamba mantiki ya Kislamu iko juu zaidi ya mantiki nyenginezo katika usimamishaji wake wa hoja na uthibitishaji wa dhana zake.
  • Matumizi ya Jamii: Hadithu I’itilaa kijamii, inaonyesha kwamba; sheria za Kiislamu inaendana zaidi na mahitaji ya mwanadamu kuliko sheria nyingine yoyote ile. [19]

Uhusiano wake na Aya ya Naf'yu Sabil

Makala asili: Aya ya Nafy al-Sabil

Madhumuni ya kila moja kati ya Aya ya Nafy al-Sabil na Hadithu I’itilaa zinarejelea juu ya suala la makafiri kutowa na mamlaka ya kutawala Waislamu. [20] Hata hivyo kiuhalisia, kuna uhusiano maalumu wa kimantiki kati ya matini mbili Aya ya Naf'u Sabil na Hadithu I’itilaa.[21] Uhusiano huu wa kimantiki ni kwamba; Maudhui ya Hadithi yanaonyesha makafiri kutokuwa na mamlaka juu ya Muislamu, na Aya nayo inaashiria kafiri kutokuwa na mamlaka juu ya Muumini. Kulingana na ufafanuzi wa Qur'ani, maana ya Muislamu ni pana zaidi kuliko maana ya Muumini. [22] Kwa hivyo, dhana na maana ya Aya ya Naf'u Sabil pia ni pana zaidi kuliko dhana na maana ya Hadithi. [23]

Kwa hiyo natija inayopatikana kupitia ufafanuzi huu ni kwamba; Kafiri anaweza kuwa na mamlaka juu ya Muislamu, ila katu hawezi kuwa na mamlaka juu ya muumini. Hi ni kutokana na kwamba; muumini ni yule mtu aliyeshikamana na Uislamu kisawa sawa na katu hawezi kuliacha la Mungu na kufuata la kiumbe.