Nenda kwa yaliyomo

Aya ya Nafy al-Sabil

Kutoka wikishia
Aya ya Nafy al-Sabil
Jina la AyaAya ya Nafy al-Sabil
Sura HusikaNisa'a
Namba ya Aya141
Juzuu5
Sababu ya KushukaKujiondoa kwa Abdullah bin Ubayyah na Masahaba zake Kutoka katika Jeshi la Uislamu
Mahali pa KushukaMadina
MaudhuiItikadi
Mada YakeKukanusha Utawala wa Makafiri Juu ya Waumini
Aya Zinazofungamana NayoAya ya Hadhar


Aya ya Nafy al-Sabil (Kiarabu: آآية نفي السبيل) ni sehemu ya Aya ya 141 katika Surat al-Nisaa ambayo inakataa aina yoyote ile ya satwa na udhibiti wa makafiri kwa Waislamu. Kwa maana kwamba, Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waislamu. Aya hii ni katika hoja za kanuni ya kutowapa njia makafiri ya kuwa na udhibiti kwa Waislamu ambayo ina matumizi katika milango mbalimbali ya fikihi.

Baadhi ya wafasiri wakishikamana na hali ya ujumla ya Aya hii, wanatambua kuwa, hukumu ya kukataa kuwapa njia makafiri ya kuwa na udhibiti kwa makafiri, inahusiana na nyuga zote za kijeshi, kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na vilevile duniani na Akhera.

Aya hii imekuwa ni moja ya misingi ya fikihi ya baadhi ya Maulamaa wa Kishia. Kwa mfano Imamu Khomeini (r.a) wakati aliposimama na kupinga muswada wa sheria ya Capitulation (iliyomfanya Mmarekani yeyote yule awe na kinga ya kutoshtakiwa ndani ya Iran) alitumia Aya hii na kanuni iliyochukuliwa kutoka ndani yake.

Kupewa Jina na Sababu ya Kushushwa Kwake

Sehemu ya Aya 141 ya Surat al-Nisaa isemayo: (وَ لَنْ یجْعَلَ اللَّهُ لِلْکافِرِینَ عَلَی الْمُؤْمِنِینَ سَبِیلًا ; …wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini) [1] Inafahamika kwa jina la Aya ya Nafy al-Sabil. [2] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha Tafsir Qumi, Aya hii ilishuka ikimlaumu Abdallah bin Ubayy na masahaba zake. Watu hawa walijiondoa na kujitenda na jeshi la Waislamu katika Vita vya Uhud kwa lengo kwamba, kama makafiri watawashinda Waislamu wao waseme kwamba, sisi hatukuwa na wao na endapo Waislamu watawashinda makafiri waseme, sisi tulikuwa na nyinyi. [3]

وَ لَنْ یجْعَلَ اللَّهُ لِلْکافِرِینَ عَلَی الْمُؤْمِنِینَ سَبِیلًا


…wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.



(Quran: 4: 141)


Wigo Mpana wa Kukataa Makafiri Kuwa na Udhibiti kwa Waislamu

Kwa mujibu wa Allama Tabatabai, hukumu hii inajumuisha makafiri na wanafiki wote; [4] hata hivyo, baadhi wamechukulia duara la makafiri katika Aya hii kuwa linaishia kwa Wayahudi pekee. [5]

Pia, kwa mujibu wa baadhi ya wafasiri, ujumla wa Aya hii unajumuisha aina yoyote ya ubora wa Waumini juu ya makafiri, iwe ni kwa kwa dalili na hoja, [6] duniani na Akhera [7] na iwe ni kwa upande wa fikihi na sheria. [8] Hata hivyo baadhi wa waliichukulia hukumu ya Aya hii kuwa ni mahsusi kwa Siku ya Kiyama; [9] Yaqub Jafari, katika tafsiri yake ya Kawthar anasema kuwa, kujaalia Aya hii kwamba, ni makhsusi kwa jambo tu, ni kinyume dhahiri ya Aya na bila ya sababu. [10]

Kwa mujibu wa tafsiri ya Aya hiyo, kukataa kutawaliwa na kudhibitiwa kunajumuisha nyanja zote za kijeshi, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi. [11] Kwa msingi huo wamesema kuwa, mapatano au maelewano yoyote yanayofungua njia kwa makafiri kuwa na udhibiti kwa Waislamu ni haramu na waumini lazima wasimame na kukabiliana na hilo. [12]

Kwa mujibu wa Aya hiyo, baadhi wanaona kuwa, kukataa kuweko njia ya makafiri kuwadhibiti Waislamu, kuna pande mbili za chanya na hasi: Kipengele chake chanya kinaeleza wajibu wa jamii ya Kiislamu na watawala wake kudumisha mamlaka ya kujitawala na kuondoa mazingira ya utegemezi, na kipengele chake hasi kinahusu kukaa utawala wa wageni (ajinabi) kwa hatima na mustakabali wa kijamii na kisiasa wa Waislamu. [13]

Kuwa Sheria Hukumu ya Nafy al-Sabil

Hukumu katika Aya haiko kwa sura kwamba, Mwenyezi ametaka (kuwa na irada) kafiri yeyote asiwe na aina yoyote ya satwa na udhibiti wa makafiri kwa Waislamu, bali makusudio ni utashi wa kisheria ni kwamba, Mwenyezi Mungu hajaleta sheria ambayo inamfanya kafiri awe na satwa na udhibiti kwa muumini. Kwa hiyo, hukumu yoyote katika hali yake jumla (umumiyat) ambayo inaonyesha udhibiti wa kafiri kwa muumini inapaswa pamoja na Aya hii. [14]

Mifano ya satwa na udhibiti wa kidhahiri wa makafiri juu ya Waislamu ambao umeripotiwa katika historia unachukuliwa kuwa wa muda mfupi na ulitokana na uzembe na mapungufu ya waumini[15] au kutokana na majaribu na mitihani ya Mwenyezi Mungu. [16] Pia wamesema kwamba, ubora na kuwa juu waumini huja pale wanapojitolea na kufungamana na mambo muhimu ya imani [17] na kuepuka kushirikiana na kujumuika na wageni wasaliti [18] na kujiweka mbali na mifarakano. [19]

Hoja kwa Ajili ya Kanuni ya Nafy al-Sabil

Makala Asili: Kanuni ya Nafy al-Sabil

Aya ya Nafy al-Sabil ni hoja ya kanuni ya Nafy al-Sabil (kutowapa njia makafiri ya kuwa na udhibiti kwa Waislamu). Kanuni hii inatanguliza kila hukumu mbele ya hukumu ambayo inapelekea makafiri kuwa juu ya Waislamu. [20] Kanuni ya Nafy al-Sabil ina matumizi katika milango mbalimbali ya fikihi. [21] Kwa mujibu wa kanuni hii, kafiri hamrithi Mwislamu. Haijuzu kumuuza mtumwa wa Kiislamu kwa kafiri. Babu kafiri hana Wilaya (usimamizi) kwa mtoto Mwislamu na ndoa ya mwananmke Mwislamu na mwanaume kafiri ni batili. [22]

Kuakisiwa Aya na Kanuni ya Nafy al-Sabil katika Fikihi ya Kisiasa

Aya ya Nafy al-Sabil na kanuni iliyochukuliwa ndani yake imeakisiwa katika fikihi ya kisiasa. Kanuni ya Nafy Al-Sabil inatambuliwa kuwa moja ya misingi ya kifikihi ya fat’wa ya kuharamisha tumbaku iliyotolewa na Mirzaei Shirazi, hukumu ya jihadi dhidi ya warusi iliyotolewa na Maulamaa wa Kishia katika zama za mfalme wa wakati huo wa Iran Mozaffar al-Din Shah na kupinga Imamu Khomeini (r.a) muswada wa sheria ya Capitulation (iliyomfanya Mmarekani yeyote yule awe na kinga ya kutoshtakiwa ndani ya Iran). [23] Imamu Khomeini katika kupinga muswada wa sheria ya Capitulation aliashiria Aya hii. [24]

Aya na Hadithi Zinazofanana

Katika Aya zingine kama Aya ya 51 na 52 ya Surat al-Maida zinaashiria kupinga satwa na usimamizi wa makafiri. Kadhalika hadithi ya I’tilaa (ubora na kuwa juu Uislamu kwa dini zingine) iliyonukuliwa katika kitabu cha Man La Yahdhruh al-Faqih, moja ya Kutub al-Ar’ba’a (Vitabu Vinne vya Mashia vya hadithi) [25] inaashiria juu ya Uislamu kuwa juu ya dini zingine. [26]

Baadhi wakiwa na nia ya kuthibitisha Nafy al-Sabil wametumia hoja za kiakili; kwa maana kwamba, ushindi wa makafiri kwa Waislamu ni jambo baya na Mwenyezi Mungu hafanyi jambo baya; na ni kutokana na sababu hiyo, Mwenyezi Mungu hawezi kuruhusu makafiri wawe na satwa na udhibiti kwa Waislamu. [27]

Rejea

Vyanzo