Hadith Qurb al-Nawafil

Kutoka wikishia

Hadith Qurb al-Nawafil (Kiarabu: حديث قرب النوافل) ni hadithi Quds ambayo Mwenyezi Mungu alimhutubu Mtume (s.a.w.w) akiwa katika safari ya Miraji. Hadithi hii inaeleza nafasi na daraja ya muumini mbele ya Mwenyezi Mungu na kujikurubisha mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu (SWT) kupitia kutekeleza faradhi na mambo ya wajibu na nafila (mambo ya sunna na mustahabu).

Katika hadithi hii, kumvunjia heshima Walii wa Mwenyezi Mungu kumetambuliwa kuwa ni mithili ya kupigana vita na Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu amezungumzia kuliko kitu kingine suala la huharakisha kwa ajili ya kumsaidia walii wake. Kwa mujibu wa kipengee kingine cha hadithi hii, mja muumini hujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia kutekeleza mambo ya mustahabu na hivyo Mwenyezi Mungu huwa masikio na macho yake.

Wataalamu wa elimu ya irfan wa Kiislamu wanaiona ibara hii kuwa ni ya ukweli na kiuhalisia na kwamba, ni ushahidi juu ya nadharia ya uwepo wa Mungu mmoja. Hata hivyo wataalamu wa elimu ya hadithi na mafakihi wanaamini kuwa, ibara iliyoitajwa ni ya kimajazi (sio ya kiuhalisia) na inaashiria juu ya msaada wa Mwenyezi Mungu kwa muumini au ukuruba wa Mwenyezi Mungu kwa muumini au maana zingine.

Hadithi ya Qurb al-Nawafil imenukuliwa katika vyanzo vya Kishia na Kisunni kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ikiwa na tofauti ndogo.

Kuitwa Kwa Jina Hilo

Hadithi ya Qurb Nawafil ni hadith Qudsi ambayo Mwenyezi Mungu alisema alipomhutubu Mtume (s.a.w.w) alipokuwa katika safari ya Miraj. Hadithi hii ilikuwa jibu la swali la Mtume alilomuuliza Mwenyezi Mungu kuhusiana na nafasi na daraja ya muumini Kwake. [1] Sababu ya kuwa mashuhuri hadithi hii ni kwamba, katika sehemu ya mwisho ya hadithi hii kumetajwa maudhui ya kuwa, kutekeleza sunna kunamfanya muumini kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na kuwa miongoni mwa watu maalumu mbele ya Allah Mola Muumba na maurafaa wa Kiislamu wakitegemea kipande hiki cha hadithi kwa ajili ya kuashiria daraja ya muumini wametumia ibara ya Qurb Nawafil. [2] Nafila maana yake ni kila kitu cha ziada, [3] zawadi au kazi ya ziada. [4]

Maudhui ya Hadithi

Katika hadithi ya Qurb Nawafil inaelezwa kuwa, kumvunjia heshima walii wa Mwenyezi Mungu kumetambuliwa kuwa ni mithili ya kupigana vita na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amezungumzia suala la huharakisha kwa ajili ya kumsaidia Walii wake kuliko kitu kingine na amesema: Mimi sina shaka katika kazi yoyote kabla ya kuaga dunia Muumini; kwani yeye anachukia kifo chake na mimi ninachukia yeye kuchukia na kuhuzunika. Kadhalika katika hadithi hii imekuja kwamba, kama mtu atataka kujikurubisha kwangu kupitia Nafila (Mustahabu), ninampenda na nitakuwa masikio, macho, ulimi na mkono wake na kupitia kwavyo atasikia, ataona na kama ataniita nitamuitikia na nitatekeleza maombi na matakwa yake. [5]


Tafsiri ya Hadithi

Mtazamo wa Maurafaa

Maurafaa wa Kiislamu wanaichukulia hadithi hii kama hoja kwa ajili ya maudhui zao za Kiirifani. [6] Ibn Arabi, amezitambua lafudhi za hadithi ya Qurb al-Nawafil kuwa zina uhalisia na kwamba, ni ushahidi kwa ajili ya nadharia ya umoja wa uwepo. [7] Kwa mtazanmo wake ni kuwa, Mwenyezi Mungu huwa macho na masikio ya muumini na hivyo mwanadamu kuzama na kupotelea katika sifa za Mwenyezi Mungu. [8]

Sayyid Haidar Amuli analiona hilo kuwa ni ushahidi wa kuzama katika sifa za Mwenyezi Mungu na kuwa kitu kimoja muhibu na mahabubu. [9] Kwa mtazamo wa maurafaa (wataalamu wa elimu ya irfani) ni kuwa, harakati ya kibatini kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu inafanyika katika hatua mbili, Qurb Faraidh (kujikurubisha kwa mambo ya faradhi) na Qurb Nawafil (kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia mambo ya sunna). Imamu Khomeini anasema, Qurb Nawafil ni jambo linalosimamia kuzama katika matendo, sifa na dhati na Qurb Faraidh imetabikishwa juu ya kubakia baada ya kuzama. [10]Murtadha Mutahhari (1298-1358 Hijria Shamsia) mwandishi wa Kishia anasema kuwa, madhumuni ya hadithi inaendana na hatua za kufanya ibada na kwa njia hiyo mtu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu ambapo katika hatua hizi mtu hufikia katika kiwango ambacho huba na mapenzi ya Mwenyezi Mungu humjumuisha na huyavuta mapenzi na huba ya Mwenyezi Mungu kuelekea kwake na katika hatua hii hakubakii tena kitu kuhusiana na utambulisho wake na hufanya mambo yote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. [11]

Baadhi ya maurafaa wanaona kuwa, hatua ya Qurb Faraidh ni ya juu zaidi kuliko Qurb Nawafil. Kwa mtazamo wao ni kuwa, natija ya Qurb Faraidh ni kuzama katika dhati ya Mwenyezi Mungu na natija ya Qurb Nawafil ni kuzama katika sifa za Mwenyezi Mungu. Kadhalika wanaamini kuwa, katika hatua ya Qurb Faraidh, mwanadamu hupanda na kukwea, lakini katika hatua ya Qurb Nawafil Mwenyezi Mungu hushuka. [12]

Mtazamo wa Mafakihi na Wataalamu wa Hadithi

Baadhi ya mafakihi na wataalamu wa hadithi wanaona kuwa, lafudhi za hadithi hii ni kinaya na majazi na wanaamini kuwa, lafudhi za hadithi zinapaswa kufasiriwa kwa namna ambayo hazipelekei kupatikana Wahdat al-Ujud (nadharia ya Mungu mmoja) na kuangamia na kusambaratika. [13] Kundi hili limebainisha pande mbalimbali kwa ajili ya ibadara jadiliwa; [14] miongoni mwao ni Sheikh Hurr Amili ambaye ametaja pande zifuatazo kuwa zina maana sahihi:

  • Msaada wa Mwenyezi Mungu kwa muumini kwa ajili ya kutekeleza mambo kwa ajili tu ya kumridhisha Mwenyezi Mungu.
  • Msaada wea Mwenyezi Mungu kwa muumini kama msaada kwa viungo vyake vya mwili.
  • Mwenyezi Mungu kuwa azizi na mwenye thamani kwa muuninu kama viungo vyake vya mwili.
  • Muumini kumtegemea Mwenyezi Mungu tu.
  • Mwenyezi Mungu kuwa karibu na muumini. [15]

Sanadi ya Hadithi

Shahidi Murtadha Mutahhari anasema, hadithi ya Qurb Nawafil ni hadithi mashuhuri na isiyo na shaka ambayo Mashia na vilevile Masuni wanaikubali na wameinukuu katika vitabu vyao. [16] Hadithi hii ameinukuu Aban bin Taghlib kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) na Hammad bin Bashir kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) na wawili hao wamenukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w). [17] Hadithi hiyo tajwa imenukuliwa katika vyanzo na vitabu vya Ahlu-Sunna kwa njia ya wapokezi kama Aisha, [18] Maymunah [19] na Abu Hurairah [20] kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). Hadithi hii imepokewa kwa mapokezi tofauti ambapo baadhi ya mapokezi hayo yametambuliwa kuwa sahihi na mengine yamehesabiwa kuwa dhaifu. [21]

Andiko na Tarjumi ya Hadith Qurb Nawafil

لَمَّاأُسْرِی‏ بِالنَّبِی ص‏ قَالَ يَا رَبِّ مَا حَالُ الْمُؤْمِنِ عِنْدَكَ؟ قَالَ يَا مُحَمَّدُ! مَنْ أَهَانَ لِي وَلِيّاً فَقَدْ بَارَزَنِي بِالْمُحَارَبَةِ، وَأَنَا أَسْرَعُ شَيْ‌ءٍ إِلَى نُصْرَةِ أَوْلِيَائِي، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْ‌ءٍ أَنَا فَاعِلُهُ كَتَرَدُّدِي عَنْ وَفَاةِ الْمُؤْمِنِ يَكْرَهُ الْمَوْتَ، وَأَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ، وَإِنَّ مِنْ عِبَادِيَ الْمُؤْمِنِينَ مَنْ لَا يُصْلِحُهُ إِلَّا الْغِنَى، وَلَوْ صَرَفْتُهُ إِلَى غَيْرِ ذَلِكَ لَهَلَكَ، وَإِنَّ مِنْ عِبَادِيَ الْمُؤْمِنِينَ مَنْ لَا يُصْلِحُهُ إِلَّا الْفَقْرُ، وَلَوْ صَرَفْتُهُ إِلَى غَيْرِ ذَلِكَ لَهَلَكَ، وَمَا يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ عَبْدٌ مِنْ عِبَادِي بِشَيْ‌ءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَإِنَّهُ لَيَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّافِلَةِ حَتَّى أُحِبَّهُ فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ إِذاً سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَلِسَانَهُ الَّذِي يَنْطِقُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، إِنْ دَعَانِي أَجَبْتُهُ، وَ‌إِنْ سَأَلَنِي أَعْطَيْتُهُ.


Wakati Mtume (s.a.w.w) alipokuwa katika safari ya Miraj alisema: Ewe Mola! hali ya Muumini ikoje kwako? Mwenyezi Mungu akasema: Ewe Muhammad, yeyote anayemtukana mmoja wa marafiki zangu, basi hakika ameingua kwenye vita na mimi, na mimi ni mwenye kuharakisha zaidi kuwasaidia marafiki zangu kuliko kitu chochote. Sina shaka na chochote kama ninavyo shaka juu ya kifo cha Muumini; kwa sababu anachukia kifo na ninachukia kuchukia kwake; na hakika wako baadhi ya Waumini ambao hawatengemai isipo kuwa kwa mali, na nikiwaweka katika hali nyingine, wataangamia, na kuna baadhi ya Waumini ambao hawatengenezwi ila kwa upungufu na ufukara, na nikiwaweka katika hali nyingine, wataangamia. Na asinikaribie hata mmoja katika waja wangu kwa kitendo ambacho ni kipenzi zaidi kwangu kuliko nilichomuwajibishia. Na ni kweli kwamba anataka kujikurubisha kwangu kwa njia ya nafilah (mustahbat) kwa kadiri ninavyompenda na kwa sababu ninampenda. Kisha nitakuwa sikio lake analosikia nalo, na nitakuwa macho yake aonayo nayo, na nitakuwa ulimi wake anaozungumza nao, na nitakuwa mkono wake anaogusa nao. Akiniita ninamuitikia na akiniomba ninampatia.


Rejea

Vyanzo