Nenda kwa yaliyomo

Dua ya kumi na saba ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia

Dua ya kumi na saba ya Sahifa Sajjadiyya: ni tafakuri ya kina kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s.) juu ya dhana ya kujilinda kwa Mungu Muumba dhidi ya shari na uadui wa Shetani. Ndani ya dua hii, Imamu Sajjad anachanganua aina na mbinu mbali mbali za uadui anazotumia Shetani katika kupotosha nafsi za wanadamu, huku akionesha njia za kujkinga na kuulinda moyo wa mwanadamu dhidi ya uvamizi huo. Masuala msingi yanayozungumziwa ndani ya dua hii, ni pamoja na kudhalilika kwa utu wa mwanadamu kunakosababishwa na kutojali wajibu wake wa kiibada mbele ya Mola wake, haja ya kutafuta cheo na hadhi ya utakaso kamili (draja ya Mukhlasin), ili kujiepusha na ushawishi wa kishetani, pamoja na umuhimu wa kuwa na huruma na nia njema kwa wengine.

Ufafanuzi wa kifalsafa na ki-irfani wa dua hii ya kumi na saba unapatikana katika maandiko yalioandikwa kwa lugha mbalimbali. Kwa upande wa lugha ya Kifarsi, ufafanuzi huu unapatikana katika kitabu kiitwacho Diyare Asheqan, cha Hossein Ansarian na Shuhud wa Shenakht cha Hassan Mamdouhi Kermanshahi. Pia kuna vitabu vya lugha ya Kiarabu vilivyochambua dua hii, miongoni mwavyo ni Riyadhu al-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.


Dhamira na Mafunzo ya Dua Hii

Dhamira kuu ya dua ya kumi na saba ya Sahifa Sajjadiya inahusiana na dhana ya kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shari za wasiwasi wa Shetani. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s.) anachanganua na kuangaza aina mbalimbali za uhasama na vitimbi vya Shetani dhadi ya wanadamu, huku akibainisha mbinu za kuzuia uingiaji wake ndani ya hifadhi ya moyo wa mwanadamu, pamoja na uingiliaji wake kati ndani ya michakato mbali mbali ya maamuzi ya mwanadamu. [1] Mafunzo ya kina ya dua hii ya kumi na saba yamefafanuliwa katika ibara kumi na sita katika kitabu Sahifa Sajjadiyya. [2] mafunzo yaliomo katika dua hii kama inavyoainishwa hapa chini:

·        Kutafuta hifadhi ya Mungu dhidi ya uadui na hila za Shetani.

·        Hali ya kudhalilika kwa mwanadamu pale anapotengana na ibada kutokana na vishawishi vya Shetani.

·        Shetani huyafanya maovu yapendeze mbele ya macho ya wanadamu, na kuyafanya mazuri na mema yaonekane yachukize, ili kuathiri maamuzi ya mwanadamu.

·        Kumomba Mungu daraja ya walio safi (mukhlisina), ili kuokoka na vishawishi vya Shetani.

·        Kufunga milango ya Shetani kupitia kufuli ya ibada ya dhati na ya kweli.

·        Kuomba dua mbele ya Mungu ili Shetani akate tamaa za kuwadanganya waja.

·        Kuomba dua ili Shetani adhalilike na sisi tuwe na ujasiri wa kupingana naye.

·        Madhara ya urafiki na Shetani na hatima ya kukubaliana na ushawishi wake.

·        Kutawaliwa na Shetani ni ishara ya adha ya Mwenye Ezi Mungu.


·        Nafsi ya mwanadamu ndiyo mlango wa Shetani, na diyo mahali anapaopatumia katika kuanzisha ushawishi wake.

·        Kuomba dua ya kupata uoni wa kiroho, na kuzinduka kutoka katika usingizi wa kiroho (mghafala).

·        Dua na kutaka msaada wa Mungu ndiyo kinga dhidi ya mashambulizi ya Shetani.

·        Moyo wa huruma kwa wengine: Dua ya kuwaombea ulinzi waumini, dhidi ya njama za Shetani.

·        Uhusiano yaliopo baina ya hali ya mtu binafsi na matukio ya ustawi au uharibifu wa jamii kwa ujumla.

·        Pupa kali ya Shetani katika kuwapoteza na kuwaangamiza watu.

·        Kumwomba Mwenye Ezi Mungu atuweke upande wa wapinzani wa Shetani, badala ya kusimama upande wa marafiki zake.

·        Dua ya kumwomba Allah avunje na afutilie mbali mipango ya Shetani dhidi yetu.

·        Kuomba ushindi dhidi ya majeshi ya Shetani, ambayo ni majeshi ya ujinga yanayopingana na majeshi ya hekima. [3]


Tafsiri Chambuzi za Dua ya Kumi na Saba

Kuna tafsiri kadhaa chambuzi zilizochambua ya Dua ya Kumi na Saba ya Sahifa Sajjadiyya, miongo mwa tafsiri zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; Diyare Asheqan, cha mwandishi ajulikanaye kwa jina la Hussein Ansarian, [4] Shohud wa Shenakht, cha Mohammad Hassan Mamduhi Kermanshahi, [5] na Sharh wa Tarjomeh Sahifeh Sajjadiyyeh, kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri. [6]

Kadhalika, kuna wanazuoni kadhaa waliotoa tafsiri ya dua hii kwa lugha ya Kiarabu, miongoni mwa tafsiri hizo ni pamoja na; Riyadhu al-Salikina, cha Sayyid Ali Khan Madani, [7] Fi Dhilali al-Sahifah al-Sajjadiyyah, cha Muhammad Jawad Mughniyyah, [8] Riyadhu al-'Arifina, cha Muhammad bin Muhammad Darabi, [9] na Afaqu al-Ruh, cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [10] Zaidi ya hayo, pia kua kazi chambuzi za kimsamiati za istilahi zilizotumika katika zilizofanywa na wanazuoni mbali mbali, miongoni mwa kazi hizi ni; Ta'liqat 'ala al-Sahifah al-Sajjadiyyah, cha Faidhu Kashani [11] na Sharhu al-Sahifah al-Sajjadiyyah, cha Izzu al-Din al-Jaza'iri. [12]


Dua na Tafsiri Yake

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا ذُكِرَ الشَّيْطَانُ فَاسْتَعَاذَ مِنْهُ وَ مِنْ عَدَاوَتِهِ وَ كَيْدِهِ

Na moja ya dua zake (rehema na amani zimshukie), ni ile dua aliyokuwa akiitumia wakati wa kutajwa Shetani, ambayo alikuwa akiitumia kwa ajili ya kuomba ulinzi dhidi yake na dhidi ya uadui wake pamoja na hila zake. Dua hii imekuja kama ifuatavyo:

اللَّهُمَّ إِنَّا نَعُوذُ بِكَ مِنْ نَزَغَاتِ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ وَ كَيْدِهِ وَ مَكَايِدِهِ، وَ مِنَ الثِّقَةِ بِأَمَانِيِّهِ وَ مَوَاعِيدِهِ وَ غُرُورِهِ وَ مَصَايِدِهِ.

Ee Mola wetu, hakika sisi tunajilinda Nawe kutokana na uchochezi wa Shaytani aliyefukuzwa (kutoka katika rehema za Allah), na (tunajilinda Nawe) kutokana na vitimbi vyake na njama zake; na (tunajilinda Nawe) kutokana na imani za kuamini poropaganda zake, ahadi zake, udanganyifu wake, pamoja na mitego yake.

وَ أَنْ يُطْمِعَ نَفْسَهُ فِي إِضْلَالِنَا عَنْ طَاعَتِكَ، وَ امْتِهَانِنَا بِمَعْصِيَتِكَ، أَوْ أَنْ يَحْسُنَ عِنْدَنَا مَا حَسَّنَ لَنَا، أَوْ أَنْ يَثْقُلَ عَلَيْنَا مَا كَرَّهَ إِلَيْنَا.

Na (tunakuomba Ee Mola wetu) usimjaalie kuwa na hima (usimpe hima) ya kutupotosha na kutuweka mbali utiifu wako, na (wala uismpe uwezo wa) kutudunisha kwa kukuasi Wewe; au kwa kuvutika na kile alichotupambia (kwa udanganyifu), au kwa kuchoshwa na kile (chema) alichokifanya kichukize mbele yetu (alichokifanya tukichukie).


اللَّهُمَّ اخْسَأْهُ عَنَّا بِعِبَادَتِكَ، وَ اكْبِتْهُ بِدُؤُوبِنَا فِي مَحَبَّتِكَ، وَ اجْعَلْ بَيْنَنَا وَ بَيْنَهُ سِتْراً لَا يَهْتِكُهُ، وَ رَدْماً مُصْمِتاً لَا يَفْتُقُهُ.

Ewe Mola wetu!  Mdhalilishe (Shetani huyu) na umweke mbali nasi kupitia ibada zetu Kwako, na umdhoofishe kwa kudumu kwetu katika mapenzi Yako. Weka baina yetu na baina yake pazia asiloweza kulichana, na kinga (ngao) madhubuti asiyoweza kuipasua.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اشْغَلْهُ عَنَّا بِبَعْضِ أَعْدَائِكَ، وَ اعْصِمْنَا مِنْهُ بِحُسْنِ رِعَايَتِكَ، وَ اكْفِنَا خَتْرَهُ، وَ وَلِّنَا ظَهْرَهُ، وَ اقْطَعْ عَنَّا إِثْرَهُ.

Ewe Mola wetu!  Mshushie rehema Zako Muhammad na Aali zake, na umshughulishe (Shetani huyu) na baadhi ya maadui zako badala yetu, na utulinde naye kwa wema Wako, na utuepushe na shari zake, na utugeuze tuwe kisogo chake, na uzikate athari zake dhidi yetu.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَمْتِعْنَا مِنَ الْهُدَى بِمِثْلِ ضَلَالَتِهِ، وَ زَوِّدْنَا مِنَ الْتَّقْوَى ضِدَّ غَوَايَتِهِ، وَ اسْلُكْ بِنَا مِنَ التُّقَى خِلَافَ سَبِيلِهِ مِنَ الرَّدَى.

Ewe Mola wetu!  mrehema Muhammad na Aali zake, na utujaalie uwongofu imara na uthabiti kama yeye (Shetani) alivyo iimara na thabiti katika upotovu wake, na utuzidishie uchamungu dhidi ya upotovu wake, na utuongoze kwenye njia ya uchamungu, kinyume na njia yake ya maangamizi.

اللَّهُمَّ لَا تَجْعَلْ لَهُ فِي قُلُوبِنَا مَدْخَلًا وَ لَا تُوطِنَنَّ لَهُ فِيما لَدَيْنَا مَنْزِلاً.

Ewe Mola Wetu! Usimfungulie njia ndani ya nyoyo zetu, na wala usimpe nafasi ya makaazi ndani ya yale tuliyonayo nafsini mwetu.

اللَّهُمَّ وَ مَا سَوَّلَ لَنَا مِنْ بَاطِلٍ فَعَرِّفْنَاهُ، وَ إِذَا عَرَّفْتَنَاهُ فَقِنَاهُ، وَ بَصِّرْنَا مَا نُكَايِدُهُ بِهِ، وَ أَلْهِمْنَا مَا نُعِدُّهُ لَهُ، وَ أَيْقِظْنَا عَنْ سِنَةِ الْغَفْلَةِ بِالرُّكُونِ إِلَيْهِ، وَ أَحْسِنْ بِتَوْفِيقِكَ عَوْنَنَا عَلَيْهِ.

Ewe Mola wetu! Na utujulishe kila batili aliyoiandaa dhidi yetu, na utulinde nayo baada ya kuibainishia batili hiyo, na tuoneshe njia ya kuepukana na tujuze kila linalostahiki kuandaliwa dhidi yake, na utuzindue kutokana na usingizi maghafiliko yanayopelekea (yanayosababisha) utegemezi wa Shetani, na tuboreshee taufiki Yako itakayotupa msaada wa kupambana naye.

اللَّهُمَّ وَ أَشْرِبْ قُلُوبَنَا إِنْكَارَ عَمَلِهِ، وَ الْطُفْ لَنَا فِي نَقْضِ حِيَلِهِ.

Ewe Mola wetu! Zijaze (zinyishe) nyoyo zetu makanusho ya kukanusha matendo yake, na uturahisishie njia ya kuharibu mipango yake.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ حَوِّلْ سُلْطَانَهُ عَنَّا، وَ اقْطَعْ رَجَاءَهُ مِنَّا، وَ ادْرَأْهُ عَنِ الْوُلُوعِ بِنَا.

Ewe Mola wetu! Mbariki Muhammad na Aali zake, na atuepushe na utawala wake (nguvu zake) dhidi yetu, na ukakatilie mbali matumaini yake juu yetu, na umzuie na tamaa ya kutupotoa.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ آبَاءَنَا وَ أُمَّهَاتِنَا وَ أَوْلَادَنَا وَ أَهَالِيَنَا وَ ذَوِي أَرْحَامِنَا وَ قَرَابَاتِنَا وَ جِيرَانَنَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَ الْمُؤْمِنَاتِ مِنْهُ فِي حِرْزٍ حَارِزٍ، وَ حِصْنٍ حَافِظٍ، وَ كَهْفٍ مَانِعٍ، وَ أَلْبِسْهُمْ مِنْهُ جُنَناً وَاقِيَةً، وَ أَعْطِهِِمْ عَلَيْهِ أَسْلِحَةً مَاضِيَةً.

Ewe Mola wetu! Mshushie rehema baraka zako Muhammad na Aali zake. Na uwajaalie baba zetu, mama zetu, watoto wetu, ahli zetu, wenye nasaba nasi, jamaa zetu, na majirani zetu miongoni mwa Waumini wa kiume na wa kike; wawe ndani ya kinga (Yako) madhubuti, na (uwaeke kweny) boma la hifadhi (Yako), na (uwaingize kweny) pango lenye kuzuia (madhara). Na uwavishe mavazi yenye kinga dhidi ya Shetani, na uwapatie silaha dhidi dhidi yake, silaha ambazo zinatakuwa na uwezo wa kupenya (na kumfika popote pale alipo).

اللَّهُمَّ وَ اعْمُمْ بِذَلِكَ مَنْ شَهِدَ لَكَ بِالرُّبُوبِيَّةِ، وَ أَخْلَصَ لَكَ بِالْوَحْدَانِيَّةِ، وَ عَادَاهُ لَكَ بِحَقِيقَةِ الْعُبُودِيَّةِ، وَ اسْتَظْهَرَ بِكَ عَلَيْهِ فِي مَعْرِفَةِ الْعُلُومِ الرَّبَّانِيَّةِ.

Ewe Mola wetu! Na uwashirikishe katika neema hii wote wale wanaokiri Ufalme wako (Ulezi Wako), na wanaojitakasa Kwako wewe peke Yako katika kukiri upweke Wako, na wanaojenga uadui dhidi yake (dhidi ya Shetani) kupitia ibada zao za kweli mbele Yako, na wanaotafuta msaada wako dhidi yake kupitia njia ya kutafuta elimu Yako.

اللَّهُمَّ احْلُلْ مَا عَقَدَ، وَ افْتُقْ مَا رَتَقَ، وَ افْسَخْ مَا دَبَّرَ، وَ ثَبِّطْهُ إِذَا عَزَمَ، وَ انْقُضْ مَا أَبْرَمَ.

Ewe Mola wetu! fungua kile alichokifunga, na fumua kile alichokiunganisha (alichokifuma), na ibomoe mipango yake, na mshinde pale anapoazimia kutekeleza uadui wake, na kitengue kila alichokidhatiti.

اللَّهُمَّ وَ اهْزِمْ جُنْدَهُ، وَ أَبْطِلْ كَيْدَهُ وَ اهْدِمْ كَهْفَهُ، وَ أَرْغِمْ أَنْفَهُ

Ewe Mola! Na ulisambaratishe jeshi lake, na utengue vitimbi vyake, na uporomoshe ngome yake, na umdhalilishe.

اللَّهُمَّ اجْعَلْنَا فِي نَظْمِ أَعْدَائِهِ، وَ اعْزِلْنَا عَنْ عِدَادِ أَوْلِيَائِهِ، لَا نُطِيعُ لَهُ إِذَا اسْتَهْوَانَا، وَ لَا نَسْتَجِيبُ لَهُ إِذَا دَعَانَا، نَأْمُرُ بِمُنَاوَاتِهِ، مَنْ أَطَاعَ أَمْرَنَا، وَ نَعِظُ عَنْ مُتَابَعَتِهِ مَنِ اتَّبَعَ زَجْرَنَا.

Allahumma (Ewe Mola)! Tujaalie tuwe katika jopo la maadui zake, na ututenge mbali na ile hesabu ya (kutuhisabu kuwa ni miongoni mwa) marafiki zake. Wala tusije mtii pale anapotupambia maovu, na wala tusimjibu katika wito wake pale atakapotuita. Tujaalie tuwe ni wenye kunaamrisha mapambano dhidi, kwa wale wenye kutii amri zetu, na tuwe ni wenye kunatoa waadhi wa kutomfuata, kwa wale wanaofuata makatazo yetu.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ خَاتِمِ النَّبِيِّينَ وَ سَيِّدِ الْمُرْسَلِينَ وَ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ الطَّيِّبِينَ الطَّاهِرِينَ، وَ أَعِذْنَا وَ أَهَالِيَنَا وَ إِخْوَانَنَا وَ جَمِيعَ الْمُؤْمِنِينَ وَ الْمُؤْمِنَاتِ مِمَّا اسْتَعَذْنَا مِنْهُ، وَ أَجِرْنَا مِمَّا اسْتَجَرْنَا بِكَ مِنْ خَوْفِهِ

Ewe Mola wet! Mshushie rehema Zako Muhammad, ambaye ni hitimisho (mhuri) la Manabii na bwana wa Wajumbe (Wako), (Mrehemu yeye) pamoja na watu wa nyumba yake walio wema na watoharifu. Na utuhifadhi sisi pamoja na jamaa zetu, ndugu zetu, na Waumini wote wa kiume na wa kike, dhidi ya yale yote tuliokuomba kinga kwayo. Na (tunakuomba) utunusuru kutokana na yale yote tuliokuomba ulinzi wako dhidi yake miongoni mwa vitisho vyake.

وَ اسْمَعْ لَنَا مَا دَعَوْنَا بِهِ، وَ أَعْطِنَا مَا أَغْفَلْنَاهُ، وَ احْفَظْ لَنَا مَا نَسِينَاهُ، وَ صَيِّرْنَا بِذَلِكَ فِي دَرَجَاتِ الصَّالِحِينَ وَ مَرَاتِبِ الْمُؤْمِنِينَ. آمِينَ رَبَّ الْعَالَمِينَ.

Na utuitikie kwa yale tuliyokuomba, na utupe yale tuliyoghafilika nayo (ambayo tumesahau kukuomba), na utuhifadhie yale tuliyo yasahau. Na (dua hii) iwe ndiyo sababu ya kutuinua na kutuweka katika daraja za wachamungu na viwango vya waumini (wa kweli), amina ewe Mungu wa walimwengu wote.