Nenda kwa yaliyomo

Dua ya ishirini na nane ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia

Dua ya ishirini na nane ya Sahifa Sajjadiyya: ni miongoni mwa dua zilizopokelewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), na ni dua maalumu inayosomwa wakati wa kuomba jambo fulani kwa njia ya unyenyekevu na wakati wa kutafuta hifadhi ya Mwenye Ezi Mungu. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s.) anaona kuwa; suala la kuomba mahitaji kwa asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu, linatokana na matokeo ya upotofu wa akili, na anasisitiza kujifunza kutokana na makosa ya wengine. Aidha, kwa kutaja sifa mahsusi za Mwenye Ezi Mungu, ikiwemo sifa upweke Wake, anaona kuwa; Miongoni mwa masharti ya kumfikia Mungu, ni kujitenga na vyote vile visivyokuwa Mwenye Ezi Mungu, na anamwelezea Mwenye Ezi Mungu, kuwa ndiye mtimizaji pekee wa haja za waja wake. Dua ya ishirini na nane ya Sahifa Sajjadiyya imefasiriwa na kufafanuliwa katika vita kadhaa vilivyofanya kazi ya kufasiri dua zilizomo ndani ya kitabucha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu hivyo ni pamoja na; Shuhud wa Shenakht kiilichoandikwa kwa lugha ya Kiajemi na Hasan Mamdouhi Kermanshahi, na Riadhu al-Salikin kilichandikwa na Sayyid Ali Khan Madani kwa lugha yaKiarabu.

Mafundisho Yaliomo Ndani ya Dua ya 28 Muktadha mkuu wa dua ya 28 ya Sahifa Sajjadiyya ni munājāt (maombi ya faragha) na taʿawwudh (kutafuta hifadhi) mbele ya Mwenye Ezi Mungu. [1] Matini hii hutazamwa kama kielelezo cha kilele cha unyenyekevu kinachoakisi hisia dhalili za mja mbele ya Mungu, ianotokana na hisisa za uduni wa nafsi yake mbele ya ukuu wa Mola Wake. Pia dua hii inaakisi na kudhihirisha maarifa ya kina kitheolojia aliyonayo Imamu al‑Sajjad (a.s) kuhusiana na Mola wake pamoja na uwepo Wake. Na kwa namna isiyo ya moja kwa moja, Imamu Sajjad (a.s), anatoa mwongozo kamili wa kimaadili na kiutambuzi juu ya sifa za mwombaji anazopaswa kuzijivisha nazo katika safari yake ya kuyaelekea uwanja wa maarifa ya kumtambua Mwenye Ezi Mungu. Mafundisho ya dua hii yamekua kama yafuatayo: • Kusafika na kuufikia unyofu wa nafsi (ikhlasi) kunapatikana kwa kuachana na mategemezi ya kutegemea chochote kile kisicho Mungu ili tumfikie Mungu. • Kumgeukia Mwenye Ezi Mungu kupitia mfumo mzima maisha yetu ya kiroho na kimwili. • Kutomtumainia yeyote yule ambaye yeye mwenyewe ni mhitaji kama wengine. • Usitarajie wema kutoka kwa asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu. • Kumhitaji mhitaji, ni dalili ya kupotoka kwa akili na maoni finyu. • Kudhalilika ndiyo hatima ya wale wanaotafuta heshima na utukufu kwa asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu. • Natija ya kuomba utajiri kutoka kwa asiye Mwenye Ezi Mungu, ni kugubikwa na umaskini na uhitaji. • Hatima ya kutafuta ukuu kwa asiyekuwa Mwenuye Ezi Mungu, ni aibu na uduni. • Ulazima wa mja kujifunze kutokana na makosa ya wengine. • Kuchagua njia sahihi hutokana na kujifunza kutoka kwa wanaomgeukia asiyekuwa Mungu. • Mungu peke yake ndiye anayekidhi mahitaji ya wahitaji. • Hakuna tumaini lenye matunda isipokuwa tumaini la kumtumainia Mwenye Ezi Mungu peke yake. • Baadhi ya sifa maalum za Menye Ezi Mungu kama vile: Upweke Wake, Aliyesimama kwa uweza Wake bila ya utegemezi wa wengine, Mwenye kujitosheleza. • Kivuli cha rehema za Mwenye Ezi Mungu, kimewafunika viumbe wote. • Tofauti kati ya Mungu na viumbe wake. • Mungu ametakasika na ufananikaji wa ya aina yoyote ya mifano. [3]

Dua ya ishirini na nane ya Sahifa Sajjadiyya imefafanuliwa kupitia vitabu mbalimbali vilivyofasiri kitabu cha Sahifa Sajjadiyya kwa ligha ya Kifarsi. Miongoni mwa vitabu ni pamoja na; Shuhud wa Shenakht, ambayo ni kazi ya Mohammad‑Hassan Mamduhi Kermanshahi, [4] na Sharh wa Tarjome Sahife Sajjadiyye, ambayo ni kazi ya Sayyid Ahmad Fahri. [5] Pia kuna wafasiri mbali mbali waliofasiri dua ya ishirini na nane ya Sahifa Sajjadiyya kwa Kiarabu katika kazi zao za kufasiri kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa tafsiri za za dua hii zinazopatikana kwa lugha ya Kiarabu ni kama vile; Riyad al‑Salikina kazi ya Sayyid Ali Khan Madani, [6] Fi Dhilali al‑Sahifa al‑Sajjadiyya, kazi ya Muhammad Jawad Mughniyya, [7] Riyadhu al‑‘Arifina, kazi ya Muhammad bin Muhammad Darabi, [8] na Afaqi al‑Ruh, kazi ya Sayyid Muhammad Husayn Fadhlullah. [9] Aidha, kuna baadhi ya wanazuoni waliofanya kazi ya kukusanya msamiati wa dua hii, na kuuchambua kiisimu katika vitabu maalumu kuhusiana na kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni kazi maridadi kabisa zilizochambua msamiati huo ni kama vile; Ta‘liqat ‘ala al‑Sahifa al‑Sajjadiyya, kitabu kilichoandikwa na Faidhu Kashani, [10] na Sharh al‑Sahifa al‑Sajjadiyya kazi ya Izzu al‑Din al‑Jaza’iri. [11]

Matn na tafsiri ya Dua ya 28 ya Sahifa Sajjadiyya وَکانَ مِنْ دُعَائِهِ علیه‌السلام مُتَفَزِّعاً إِلَی اللَّهِ عَزَّوَجَلَّ Na miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, ilikuwa ni ile dua aliyokuwa akiiomba huku akitafuta kimbilio mbele ya Mola wake na kuomba hifadhi kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu Mtukufu. Dua hii imekuja kama ifuatavyo: اللَّهُمَّ إِنِّی أَخْلَصْتُ بِانْقِطَاعِی إِلَیک Ewe Mola wangu! kwa yakini nimeitimiza ikhlasi yangu (na kuitakasa nafsi yangu) kwa kujitenga na mategemeo yote katika njia ya kuelekea Kwako. وَ أَقْبَلْتُ بِکلِّی عَلَیک Na nimeuelekeza uwepo wangu wote Kwako Wewe (bila kubakisha sehemu yoyote nje ya mwelekeo huo). وَ صَرَفْتُ وَجْهِی عَمَّنْ یحْتَاجُ إِلَی رِفْدِک Na nimejiepusha (kwa kugeuza uso wangu) kutoka kwa yeyote yule ambaye naye ni mhitaji wa msaada Wako. وَ قَلَبْتُ مَسْأَلَتِی عَمَّنْ لَمْ یسْتَغْنِ عَنْ فَضْلِک Na nimehamisha ombi langu kutoka kwa mhusika yeyote yule asiyekuwa na uwezo wa kujitosheleza pasi na fadhili zako. وَ رَأَیتُ أَنَّ طَلَبَ الْمُحْتَاجِ إِلَی الْمُحْتَاجِ سَفَهٌ مِنْ رَأْیهِ وَ ضَلَّةٌ مِنْ عَقْلِهِ. Na nimebaini kwamba; suala la mhitaji kuomba ombi lake kwa mhitaji mwingine (kama yeye), ni ujinga unayotokana na mpungufu rai yake na upotovu unaotokana na (welewa dhaifu wa) akili yake. فَکمْ قَدْ رَأَیتُ -یا إِلَهِی- مِنْ أُنَاسٍ طَلَبُوا الْعِزَّ بِغَیرِک فَذَلُّوا، وَ رَامُوا الثَّرْوَةَ مِنْ سِوَاک فَافْتَقَرُوا، وَ حَاوَلُوا الارْتِفَاعَ فَاتَّضَعُوا، Ni mara ngapi! Ee Mungu wangu, nimewaona (nimeshuhudia) kudhalilika, wale waliotafuta heshima kutoka kwa mwingine badala Yako Wewe. Pia nimeshuhusia namna walivyoingia ufukara, pale waliotafuta utajiri kwa asiye Wewe. Aidha namna walivyoporomoka (na kubweteka) pale walipojaribu kuinuka (kwa msaada wa asiyekuwa Wewe). فَصَحَّ بِمُعَاینَةِ أَمْثَالِهِمْ حَازِمٌ وَفَّقَهُ اعْتِبَارُهُ، وَ أَرْشَدَهُ إِلَی طَرِیقِ صَوَابِهِ اخْتِیارُهُ. Basi mifano ya watu hao ikamsahihisha yule mwenye azma, kisha welewe wa kuelewa hatima yao (hasara yao) ikawa ni ndiyo nyenzo ya kmpatia tawfiki, na hatimae chaguo lake likamuongoza kwenye njia iliyo sahihi. فَأَنْتَ یا مَوْلَای دُونَ کلِّ مَسْئُولٍ مَوْضِعُ مَسْأَلَتِی، وَ دُونَ کلِّ مَطْلُوبٍ إِلَیهِ وَلِی حَاجَتِی

Basi ewe Mola wangu! Nikiachana na muombwa mwengine yeyote yule asiyekuwa wewe, (Basi) Wewe tu ndiye (unayebaki kuwa ndiyo) kituo cha kuwasilisha haja yangu. Na nimewatupilia mbali wauombwa msaada mwengine wote, kisha Wewe peke yako ndiye ukawa mlango wa kutafuta matilaba yagu. أَنْتَ الْمَخْصُوصُ قَبْلَ کلِّ مَدْعُوٍّ بِدَعْوَتِی، لَا یشْرَکک أَحَدٌ فِی رَجَائِی، وَ لَا یتَّفِقُ أَحَدٌ مَعَک فِی دُعَائِی، وَ لَا ینْظِمُهُ وَ إِیاک نِدَائِی

Wewe (peke yako) ndiye mkusudiwa (pekee) katika dua yangu kabla ya yeyote anayeweza kufikishiwa (kuombwa) ombi fulani; hakuna anayeshirikiana nawe katika tumaini langu; wala hakuna anayelingana (aliye sambamba) nawe katika maombi yangu; na wala mwito wangu haukuchanganyi Wewe na mwingine yeyote.

لَک- یا إِلَهِی- وَحْدَانِیةُ الْعَدَدِ، وَ مَلَکةُ الْقُدْرَةِ الصَّمَدِ، وَ فَضِیلَةُ الْحَوْلِ وَ الْقُوَّةِ، وَ دَرَجَةُ الْعُلُوِّ وَ الرِّفْعَةِ.

Ee Mongu wangu! ni Wewe peke Yako unayesifika kwa sifa upweke (Mmoja) usiokuwa na aina yoyote ile ya sifa za kiidadi; na Wewe ndiye mmilikiwa mamlaka ya uwezo wa As‑Samad (kujitosheleza); Nawe ndiye mwenye sifa ya uwezo pamoja na nguvu; na Wewe ndiye uliye na daraja ya juu na utukufu.

وَ مَنْ سِوَاک مَرْحُومٌ فِی عُمُرِهِ، مَغْلُوبٌ عَلَی أَمْرِهِ، مَقْهُورٌ عَلَی شَأْنِهِ، مُخْتَلِفُ الْحَالاتِ، مُتَنَقِّلٌ فِی الصِّفَاتِ

Na mwengine yeyote yule asiyekuwa Wewe, maisha yake ni maisha tegemezi yanayotegemea rehema zako, huku mambo yake yote yakiwa ndani ya mkondo hatamu yako, na jambo lake lolote lile huwa liko chini ya shinikizo la matakwa yako, naye hupitiwa na mabadiliko ya aina mbali mbali maishani mwake (yaani hana uwezo kuituliza nafsi yake wala mwili wake katika hali moja), pia daima huwa safarini akibadili vituo vya sifa mbai mbali.

فَتَعَالَیتَ عَنِ الْأَشْبَاهِ وَ الْأَضْدَادِ، وَ تَکبَّرْتَ عَنِ الْأَمْثَالِ وَ الْأَنْدَادِ، فَسُبْحَانَک لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ. Bila shaka, umetukuka na dhana ya sifa linganifu pamoja na dhana ya sifa pinzani, na umejipambanua kwa kuipindukia dhana mifano linganishi na viigizo mfanano. Basi, utukufu ni Wako (Wewe peke Yako); hakuna Mungu wa kweli ila ni Wewe tu.