Dua ya Kumi ya Sahifa Sajjadiyya
![]() Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH. | |
Mtoaji / Mwandishi | Imamu Sajjad (a.s) |
---|---|
Lugha | Kiarabu |
Msimulizi / Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
Mada | Kutafuta hifadhi chini ya kivuli cha rehema za Mwenye Ezi Mungu na kuomba msaada wake. |
Chanzo | Sahifa Sajjadiyah |
Tafsiri kwa Lugha ya | Kifarsi |
Dua ya kumi katika kitabu Sahifatu Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الحادي عشر من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua zilizorithishwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Ndani ya dua hii Imamu Sajjad (a.s) anamuomba Mwenye Ezi Mungu aamiliane na viumbe vyake kwa misingi ya fadhila Yake, badala ya kuamiliana nao kwa kipimo cha uadilifu Wake. Hii ni kwa sababu matokeo ya kuamiliana nao kwa fadhila Zake, kunafungamana moja kwa moja na msamaha Wake Subhanahu Wataala, hali ya kwamba, iwapo Yeye ataamiliana na waja Wake kwa msingi wa uadilifu Wake, basi matokeo yake yatakuwa ni kula hasara kwa waja hao, na hatima yake ni kukumbana na adhabu ya Mwenye Ezi Mungu, na bila shaka viumbe hawana uwezo wa kuhimili adhabu ya Kiungu. Aidha, maombi haya yanaashiria juu ya utegemezi asili walio nao wanadamu katika kumtegemea Mola wao, na namna ya furaha ya Ibilisi inavyoshamiri kutokana na ukaidi wa kibinadamu dhidi ya Mola wao. kupokea Pia miongoni mwa madhumuni yaliomo katika dua hii, ni ile ahadi ya Mwenye Ezi ya kujibu dua za waja wake.
Dua hii ya kumi ya Sahifatu Sajjadiyya, imechambuliwa kwa kina katika vitabu mbali mbali vilivyofasiri dua za kitabu Sahifatu Sajjadiyya. Miongoni tafsiri za kitabu hichi ni pamoja na; Diyare Asheqan (Maskani ya Wapenzi) cha Hussein Ansarian na Shuhud wa Shenakht (Ushuhuda na Maarifa) cha Hassan Mamduhi Kermanshahi. Vitabu viwili hivi vimefasiri dua za kitabu hichi kwa lugha ya Kifursi. Pia kuna vitabu vilivyokuja kwa lugha ya Kiarabu katika kufasiri kitabu cha Sahifatu Sajjadiyya, miongoni mwavyo ni; kitabu kiitwacho Riyadhu as-Salikin (Bustani za Washikaji Njia) cha Sayyid Ali Khan Madani kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu.
Mafundisho ya Dua ya Kumi ya Sahifa Sajadiya
Mada kuu ya dua hii ni kutafuta hifadhi chini ya kivuli cha rehema za Mwenye Ezi Mungu na kuomba msaada wake. Mafunzo yaliyotolewa katika vipengele sita[1] vya dua hii ya Imamu Sajjad (a.s) ni kama ifuatavyo:
- Kumwomba Mungu awaamili waja Wake kwa rehema zake na kuto amiliana nao kulingana na uadilifu wake (kulingana na matendo yao).
- Matokeo ya Mungu kuamiliana na waja Wake kwa njia ya uadilifu wake, ni kukhasirika kwa waja hao, na matokeo ya kuamiliana nao kulingana na rehema zake ni kuwapa msamaha waja Wake.
- Njia pekee ya wokovu wa wanadamu ni kupitia msamaha wa Mungu.
- Katu waja hawawezi kuhimili adhabu ya Mwenye Ezi Mungu.
- Uhitaji usio na mipaka wa binadamu kwa Mola wao, na kujitosheleza kwa Mungu bila ya kuwa na aina yoyote ile ya uhitaji.
- Kuangamia kwa aliye mbali na rehema za Mwenye Ezi Mungu.
- Kukiri uhitaji wa mwanadamu na dharura aliyokuwa nayo katika kumhitaji Mola wake.[2]
- Ahadi ya Mwenye Ezi Mungu katika kujibu maombi ya waja Wake.
- Kumtambua Shetani na nyezo anazozitumia katika kuwahadaa wanadamu.
- Furaha ya Shetani kutokana na dhambi za wanadamu.
- Lawama za Shetani dhidi ya wale walioachana na wito wa Mola wao na kushikamana na wito wa Shetani.[3]
Tafsiri ya Dua ya Kumi ya Sahifatu Sajjadiyya
Dua ya kumi ya Sahifatu Sajjadiyya ni tamathali ya kina ya fikra za kiroho inayounganisha mja na asili ya uwepo wake (Mola wake). Kuna tafsiri kadhaa za kitaaluma zilizifanyia kazi dua hii kwa lugha tofauti. Miongoni mwa tafsiri za dua ya kumi ya Sahifa Sajjadiyya zilizofafanua dua hii lugha ya Kifarsi, ni ile inayopatikana katika juzuu ya tano ya kitabu Diyare-Asheqan cha Hussein Ansarian.[4] Pia kuna tafsiri na maelezo yenye yaliotolewa kuhusiana na dua hii yanayopatikana katika kitabu kiitwacho Shuhud wa Shenakht kilichoandikwa na Muhammad Hasan Mamduhi Kermanshahi.[5] Kitabu chengine kilichochambua dua hii ni Sharh wa Tarjumah Sahife Sajjadiyya kitabu kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri.[6] Hivyo si vitabu pekee vilivyotoa tafsiri ya kitabu Sahifatu Al-Sajjadiyya kilichokusanya dua za Imamu Zainu Al-Abidina, bali pia kuna vitabu vyengine kadhaa vilivyojikita katika kazi hiyo.
Kwa upande wa Kiarabu, pia kuana vitabu vingi vilivyoshughulikia kazi ya uchambuzi wa dua hii, miongoni mwavyo ni kitabu Riyaḍhu al-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani,[7] Fi Dhilali al-Sahifa Al-Sajjadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyya,[8] Riyaḍhu al-‘Arifina, cha Muhammad bin Muhammad Darabi,[9] na Afaq al-Ruh cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah[10]. Kazi ya tafsiri ya kisemantiki ya maneno ya dua imefanywa na Faydh Kashani katika kitabu chake alichokiita Ta‘liqat ala al-Sahifa al-Sajjadiyya.[11]
Matini ya Dua na Tafsiri Yake
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي اللَّجَإِ إِلَي اللَّهِ تَعَالَي
اللَّهُمَّ إِنْ تَشَأْ تَعْفُ عَنَّا فَبِفَضْلِكَ، وَ إِنْ تَشَأْ تُعَذِّبْنَا فَبِعَدْلِكَ
فَسَهِّلْ لَنَا عَفْوَكَ بِمَنِّكَ، وَ أَجِرْنَا مِنْ عَذَابِكَ بِتَجَاوُزِكَ، فَإِنَّهُ لَا طَاقَةَ لَنَا بِعَدْلِكَ، وَ لَا نَجَاةَ لِأَحَدٍ مِنَّا دُونَ عَفْوِكَ
يَا غَنِيَّ الْأَغْنِيَاءِ، هَا، نَحْنُ عِبَادُكَ بَيْنَ يَدَيْكَ، وَ أَنَا أَفْقَرُ الْفُقَرَاءِ إِلَيْكَ، فَاجْبُرْ فَاقَتَنَا بِوُسْعِكَ، وَ لَا تَقْطَعْ رَجَاءَنَا بِمَنْعِكَ، فَتَكُونَ قَدْ أَشْقَيْتَ مَنِ اسْتَسْعَدَ بِكَ، وَ حَرَمْتَ مَنِ اسْتَرْفَدَ فَضْلَكَ
فَإِلَى مَنْ حِينَئِذٍ مُنْقَلَبُنَا عَنْكَ، وَ إِلَى أَيْنَ مَذْهَبُنَا عَنْ بَابِكَ، سُبْحَانَكَ نَحْنُ الْمُضْطَرُّونَ الَّذِينَ أَوْجَبْتَ إِجَابَتَهُمْ، وَ أَهْلُ السُّوءِ الَّذِينَ وَعَدْتَ الْكَشْفَ عَنْهُمْ
وَ أَشْبَهُ الْأَشْيَاءِ بِمَشِيَّتِكَ، وَ أَوْلَى الْأُمُورِ بِكَ فِي عَظَمَتِكَ رَحْمَةُ مَنِ اسْتَرْحَمَكَ، وَ غَوْثُ مَنِ اسْتَغَاثَ بِكَ، فَارْحَمْ تَضَرُّعَنَا إِلَيْكَ، وَ أَغْنِنَا إِذْ طَرَحْنَا أَنْفُسَنَا بَيْنَ يَدَيْكَ
اللَّهُمَّ إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ شَمِتَ بِنَا إِذْ شَايَعْنَاهُ عَلَى مَعْصِيَتِكَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ لَا تُشْمِتْهُ بِنَا بَعْدَ تَرْكِنَا إِيَّاهُ لَكَ، وَ رَغْبَتِنَا عَنْهُ إِلَيْكَ.
Na miongoni mwa dua zake, (amani iwe juu yake), ilikuwa ni kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu Mtukufu
Ee Mwenye Ezi Mungu, iwapo utasmus kutusamehe, basi ni kwa ukarimu Wako, na iwapo utaamua kutuadhibu, basi ni kwa uadilifu Wako.
Basi, turahisishie msamaha Wako kwa fadhila Zako, na utukinge na adhabu Yako kwa msamaha Wako (kwa kufumbia macho mapungufu yetu). Hakika sisi hatuna uwezo mbele ya uadilifu Wako, na hakuna uokovu kwa yeyote yule kati yetu bila msamaha Wako.
Ewe Tajiri wa matajiri (Ewe Tajiri kuliko matajiri wote), tazama (tuangalie), sisi waja Wako kwenye (baina ya) mikono Yako, na mimi ndiye maskini (fakiri) zaidi Kwako (au mhitaji zaidi Kwako Wewe kuliko wahitaji wote). Basi ziba pengo la uhitaji wetu kwa mtando wa utajiri Wako, na usikate matumaini yetu kwa kutunyima (fadhila Zako). (Na ukifanya hivyo) utakawa umemwangamiza (umemwingiza hasarani) yule anayetafuta kufuzu kupitia Kwako Wewe, na kumnyima yule anayetafuta msaada wa fadhila Zako.
Sasa, tutamgeukia nani tukikuacha wewe, na tutakwenda wapi (tutauelekea mlango gani) tukiachana na mlango Wako? Umetukuka (ewe Mola wetu)! Sisi ndio wenye shida (tusio na mashiko) ambao umejiwajibishia kuwajibu (maombi yao), nasi ni (wale) wenye matatizo ambao umeahidi kuwaondolea shida zao.
Na jambo linalokubaliana zaidi na takdiri Yako, na linalonasibiana zaidi Nawe katika utukufu Wako, ni kumrehema yule anayetafuta rehema Zako, na kumpa nusura yule anayekuomba msaada Wako. Hivyo basi, irehemu hali ya unyenyekevu wetu Kwako, na utukidhie haja zetu kwa kule kujisalimisha kwetu kikamilifu mbele Yako (tukiwa baina mikono yako).
Ewe Allah, hakika Ibilisi amefurahishwa na anguko letu tuliloanguka katika kumuunga mkono yeye kwa uasi dhidi Yako. Hivyo basi, mteremshie rehema na amani Muhammad na Aali zake watoharifu, na usimruhusu tena (Ibilisi huyu) kupata furaha (kwa mara nyengine tena kutokana na uasi wetu), baada ya sisi kumkana yeye kwa ajili Yako, na hamu yetu ya dhati ya kujitenga naye na kukuelekea Wewe.
Rejea
- ↑ Tarjume wa Sherh Duaye Dahome Sahife Sajjadiye, Tovuti ya Erfan.
- ↑ Matini ya Dua
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 5, uk. 75-96; Mamduhi, Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 465-482.
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 5, uk. 75-96.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388, juz. 1, uk. 465-482.
- ↑ Fihri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadiyah, 1388, juz. 1, uk. 519-525.
- ↑ Madani Shirazi, Riadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 425-441.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 159-165.
- ↑ Darabi, Riadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 137-140.
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 275-284.
- ↑ Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 34-35.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.