Dua ya Kumi na Nane ya Sahifa Sajjadiya
Dua ya Kumi na Nane ya Sahifa Sajjadiya: ni dua iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s.), aliyokuwa akiisoma baada ya kuondokewa na dhiki au kujibiwa kwa haja zake. Ndani ya dua hii Imamu Zainu al-Abidin (a.s), anachambua falsafa ya mwanadamu kushukiawa na mitihani, kisha anaendelea kwa kutoa shukrani kwa Mwenye Ezi Mungu kwa majaaliwa mema aliyojaaliwa na Mola wake, pamoja na neema ya kwa kuondokewa na matatizo mbali mbali.
Aidha, kuna tafsiri kadhaa zinazopatikana ndani ya vitabu mbali mbali vya tafsiri ya kitabu Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa tafrisi ya dua hii kwa lugha ya Kifarsi ni pamona na; Diyare Asheqan, cha Hussein Ansarian na Shohud wa Shenakht, cha Hassan Mamduhi Kermanshahi. Kwa upande wa lugha ya Kiarabu, kitabu Riyad al-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani ndiyo moja ya vitabu maarufu vilivyochambu dua hii kwa lugha ya Kiarabu.
Mafundisho ya Dua ya Kumi na Nane
Dua ya kumi na nane ya Sahifa Sajadiya ni dua aliyokuwa ikisoma na Imamu Sajad (a.s) baada ya kupambazukiwa na kupata suluhisho la shida zake, au baada ya kufanikiwa alipofanikiwa haja zake. Mamhudahi Kermanshahi, mujtahidi na mwanafalsafa chuo kikuu cha kidini kilichopo Qom Iran, anaeleza akisema kwamba; dua hii inadhihirisha ya kwamba, katika kila hali, iwe ya shida au ya faraja, Imam Sajad (a.s) alionekana kuhifadhi uhusiano wa karibu uliopo baina yake na Mola wake, na wala hakuwa ni mwenye kuisahau Akhera yake katika hali yoyote ile. [1]
Mafundisho ya dua hii ya kumi na nane ya Sahifa Sajadiya yaliokuja katika vipengele vitau, [2] yanajumuisha mafunzo yafuatavyo:
· Kumshukuru Mungu kutokana na majaaliwa mema.
· Kuomba huruma ya Mungu, ni bora kuliko kuliko kuwa na afya njema tu.
· Maisha ya duniani ndiyo utangulizi au msingi wa maisha halisi yajayo (maisha ya Akhera).
· Kuwa na Shukurani mbele ya Mungu, kutokana na kuondokewa na majanga.
· Kumjua Mungu na pamoja na kuutambua ulimwengu, ndiyo njia msingi ya kufaulu.
· Falsafa na hekima ya kukumbwa na majanga.
· Kila kisichodumu (cha kidunia) hakiwezi kuingia katika jopo la vite vyenye thamani.
· Chenye thamani hasa ni kile chenye kudumu na kubaki milele (neema za Akhera).
· Usalama wa Akhera ni bora zaidi kuliko amani na usalama wa kidunia. [3]
Kuna tafsiri kadhaa chambuzi za Dua ya kumi na nane zinazopatikana kwa vitabu chambuzi vya kitabu Sahifa Sajjadiya. Mionmgoni mwa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiajemi vilivyochambua dua hii ni pamoja na; Diyare Asheqan, kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [4] Shuhud wa Shenakht, [5] cha Mohammad Hassan Mamduhi Kermanshahi, na Sharh wa Tarjome Sahifeh Sajjadiyeh, [6] cha Sayyid Ahmad Fahri.
Pia tafisiri chambuzi za hii zinapatiokana ndani tafsiri mbali mbali zilizondikwa kuhusiana na kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu hivyo ni kama vile; Riyadhu al-Salikin, cha Sayyid Ali-Khan Madani, [7] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya, [8] cha Mohammad Jawad Mughniyyah, Riyadhu al-Arifin, [9] cha Muhammad bin Muhammad Darabi, na Afaqi al-Ruh, [10] kilichoandikwa na Sayyid Mohammad Hussein Fadhlullah. Pia kuna vitabu maalumu vilivyokuja kuchambua msamiati uliotumika ndani ya dua hii. Miongoni mwavyo ni kama vile; Ta'liqati 'ala al-Sahifa al-Sajjadiyya, [11] cha Faidhu Kashani na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, [12] kilichoandikwa na Izzu al-Din al-Jazairi.
Matini ya Dua na Tafsiri yake
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا دُفِعَ عَنْهُ مَا يَحْذَرُ، أَوْ عُجِّلَ لَهُ مَطْلَبُهُ
Na miongoni mwa dua zake (amani iwe juu yake), ni ile dua aliyokuwa akiiomba baada ya Mola wake kumwepusha na shari aliyokuwa akiikhofu, au baaya ya kuharakishiwa matlabu yake. Nayo ni kama ifuatavyo:
اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ عَلَى حُسْنِ قَضَائِكَ، وَ بِمَا صَرَفْتَ عَنِّي مِنْ بَلَائِكَ، فَلَا تَجْعَلْ حَظِّي مِنْ رَحْمَتِكَ مَا عَجَّلْتَ لِي مِنْ عَافِيَتِكَ فَأَكُونَ قَدْ شَقِيتُ بِمَا أَحْبَبْتُ وَ سَعِدَ غَيْرِي بِمَا كَرِهْتُ.
Ewe Mwenye Ezi Mungu, himdi zote ni Zako Wewe kwa uzuri (hekima) katika gadari Zako (maamuzi Yako), na kwa yale uliyonikinga nayo dhidi ya mitihani Yako. Hivyo basi, usiujalie mgao wa huruma Zako kwangu ukwa ni kwa ajili ya kupata nafuu ya kidunia tu, kwani hilo litapelekea kukhasirika (na kukosa kile) nilichokitumainia, huku mwingine akafuzu kwa kile nilichokidharau.
وَ إِنْ يَكُنْ مَا ظَلِلْتُ فِيهِ أَوْ بِتُّ فِيهِ مِنْ هَذِهِ الْعَافِيَةِ بَيْنَ يَدَيْ بَلَاءٍ لَا يَنْقَطِعُ وَ وِزْرٍ لاَ يَرْتَفِعُ فَقَدِّمْ لِي مَا أَخَّرْتَ، وَ أَخِّرْ عَنّي مَا قَدَّمْتَ.
Na ikiwa ustawi huu wa afya njema ninaoishi nayo mchana na usiku, ni utangulizi wa janga lisilokoma na mzigo mzito usioondoka, basi niharakishie kile ulichoniakhirishia (yaani misukosuko ya duniani), na uniakhirishie kile ulichoniharakishia (yaani niondolee kheri hizi za duniani, ili nije kupata malipo ya kheri za Akhera).
فَغَيْرُ كَثِيرٍ مَا عَاقِبَتُهُ الْفَنَاءُ، وَ غَيْرُ قَلِيلٍ مَا عَاقِبَتُهُ الْبَقَاءُ، وَ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ.
Kwani hakina thamni kile kiishacho (kikomacho), na si kichache kile chenye kinachoendelea (kinachodumu). Na (ninakuomba) umshushie amani na rehema zako Muhammad pamoja na Aali zake.