Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Kumi na Mbili ya kitabu cha Sahifatu Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Kumi na Mbili ya Kitabu cha Sahifatu Sajjadiyyah
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH.

Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaUngamo la dhambi lililofungama na ombi la toba na kurejea kwa Mwenye Ezi Mungu.
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Du'a ya Kumi na Mbili ya kitabu cha Sahifatu Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الثاني عشر من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), nayo ni dua inayohusiana na ungamo la makosa lililofungamana na ombi la msamaha wa toba mbele ya Mwenye Ezi Mungu. Katika du'a hii, Imamu Sajjad (a.s) alichukua hatua ya kuchambua mambo kadhaa kuhusiana na maisha haya ya dunianai. Miongoni mwayo ni Pamoja na; vigezo vinavyoweza kupelekea kunyimwa taufiki ya kupata wasaa wa kuomba dua, waja wapendwao na Mwenye Ezi Mungu, kutokuwepo kwa kizuizi katika njia ya kurejea kwa Mola wetu, pamoja na hali au sifa za ndani (za kiroho) na nje za waja wanaotubia kwa Mola wao.

Du'a hii ya kumi na mbili imefafanuliwa na kutafsiriwa katika maandiko kadhaa fafanuzi yaliokuja kuchambua Dua za Kitabu Sahifa Sajjadijya. Miongoni mwa tafsiri chambuzi zilizoandikwa kwa lugha ya Kifursi (Kiajemi au Kipashia), kama vile; Diyare Asheghan kilichoandikwa na Hussein Ansarian na Shuhud wa Shenakht kilichoandikwa na Hassan Mamduhi Kermanshahi. Ama kwa upande wa lugha ya Kiarabu, ni; kitabu kiitwacho Riyadhu al-Salikin kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.

Dhana Msingi ya Mafunzo Dua ya Kumi na Mbili

Dhana kuu ya dua ya kumi na mbili ilioko katika Sahifa Sajjadiyya imejikita katika ungamo la makosa lililofungama na ombi la toba na kurejea kwa Mwenye Ezi Mungu. Ukiachana na mada kuu hiyo, pia dua hii imegusia baadhi ya mambo msingi kuhusiana na maisha ya mwanadamu ulimwenguni humu. Miongono mambo hayo ni pamoja na; vigezo vinavyozuia ufanisi wa maombi, sifa bainifu za waja watubiao kwa Mola wao, pamoja na hulka za waja walio bora mbele ya Mwenye Ezi Mungu.[1] Dhana hizi, zilimewasilishwa na Imam Sajjad (a.s) kupitia vipengele 16.[2] Vipengele hivyo zimefafanuliwa kama ifuatavyo:

  • Mambo yanayozuia taufiki ya kupata nafasi ya kuomba dua: Ulegevu na uvivu katika utekelezaji wa maagizo ya Mwenye Ezi Mungu na kughafilika na majukumu ya wajibu, kuelekea kwa haraka kwenye yale yaliyoharamishwa na Mweye Ezi Mungu, na kuto kuwa na shukurani juu ya neema mbali mbali.
  • Ukarimu wa Mungu (au taufiki ya Mungu) ni kichocheo muhimu kinachompelekea mja kuwa na dhana njema na Mwenye Ezi Mungu, na kumtia hamu ya kuelekeza mombi yake kwa Mola wake.
  • Ihisani na neema zote za Mwenye Ezi Mungu zinatokana na ukarimu na fadhila Zake juu ya waja wake.
  • Utegemezi wa viumbe kwa Mola wao.
  • Kuomba taufiki ya Mungu katika kuepukana na dhambi.
  • Hofu kuhusu athari za dhambi na uasi wa amri za Mwenye Ezi Mungu.
  • Uwezekano wa toba usio na mipaka kwa wale waliotenda dhambi.
  • Kuthamini fursa ya toba na kuihisabu kuwa ngawira muhimu.
  • Katazo la kukata tamaa juu rehema za Mungu kwa kuwa mlango wa toba upo wazi.
  • Hali za mja mtubiaji: Kujidhililisha kwa unyenyekevu, kugubikwa na woga (kutetemeka), pamoja na kutiririkwa na machozi, n.k.
  • Matarajio ya msamaha wa Kimungu (rehema za Mungu kuizidi ghadhabu Yake kwa toba ya waja).
  • Kuwa na Juhudi katika kutafuta rehema na msamaha wa Mwenye Ezi mungu.
  • Kukiri udhaifu (uasi) binafsi mbele ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Sifa za waja bora na wapendwao na Mwenye Ezi Mungu: Kuachana na majivuno, kuepukana na kung'ang'ania dhambi, na kulihisabu ombi la kutaka msamaha (istighfar) kuwa ni miongoni mwa mambo ya wajibu.
  • Kumtegemea Mwenye Ezi Mungu na kumuomba msamaha kutokana na kiburi pamoja na kudumu katika dhambi.
  • Kukimbilia hifadhi ya Mwenye Ezi Mungu kutokana na khofu ya madhara ya dhambi na kutaraji msaada Wake.
  • Kutawakali kwa Mwenye Ezi Mungu, kutafuta hifadhi Yake, pamoja na kudhihirisha unyenyekevu mbele ya Yake.
  • Kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu katika kutekeleza maamrisho Yake.
  • Kumuogopa Mwenye Ezi Mungu pekee yake, kwani Yeye ndiye Mwingi wa Msamaha.
  • Kutafuta hifadhi mbele ya Mwenye Ezi Mungu, ndiyo njia pekee ya kufikia ufanisi.
  • Hakikisho la ahadi ya Mungu ya kujibu maombi ya waja Wake.
  • Uhuru na wezekano wa kila mmoja kutumia neema za Mwenye Ezi Mungu, hata kwa wale wanaomuasi Mola wao.
  • Dhulma za waja dhidi ya nafsi zao, kutokana na matendo yao maovu.
  • Hali ya Mungu ya kuridhishwa na amali chache za waja wake, na namna na wingi wa malipo Yake kwa waja hapo.[3]

Tafsiri na Ufafanuzi Chambuzi Kuhusiana na Dua yaKumi na Mbili

Kuna tafsiri kadhaa chambuzi zilizokuja kufafanua dua hii ya kumi na mbili ilioko katika kitabu cha As-Sahifa as-Sajjadi yya. Miongoni mwa tafsiri zilizoandikwa kwa lugha ya Kiajemi katika kuichambua dua hii, ni pamoja na; Diyare Asheghan kazi ya Hussein Ansarian,[4] Shuhud wa Shenakht kazi ya Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi,[5] na Sharhe wa Tarjome Sahifeh Sajjadiyyeh kazi ya Sayyid Ahmad Fahri.[6]

Kadhalika, kuna chambuzi za Kiarabu zilizochambua dua hii ya kumi na mbili kwa lugha ya Kiarabu, miongoni mwazo ni pamoja na; Riyadhu al-Salikin kazi ya Sayyid Ali Khan Madani,[7] Fi Dhilali al-Sahifati al-Sajjadiya kazi ya Muhammad Jawad Mughniyya,[8] Riyad al-Arifin kazi ya Muhammad bin Muhammad Darabi,[9] na Afaq al-Ruh kazi ya Sayid Muhammad Hussein Fadhlullah.[10] Aidha, maneno ya kiistilahi yaliyotumika katika dua hii yamefafanuliwa kiisimu katika kitabu kiitwacho Ta'liqat 'ala al-Sahifa al-Sajjadiya kilichoandikwa na Faidhu Kashani.[11]

Matini ya Dua na Tafsiri Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الاِعْتِرَافِ وَ طَلَبِ التَّوْبَةِ إِلَي اللهِ تَعَالَي

اللَّهُمَّ إِنَّهُ يَحْجُبُنِي عَنْ مَسْأَلَتِكَ خِلَالٌ ثَلَاثٌ ، وَ تَحْدُونِي عَلَيْهَا خَلَّةٌ وَاحِدَةٌ

يَحْجُبُنِي أَمْرٌ أَمَرْتَ بِهِ فَأَبْطَأْتُ عَنْهُ ، وَ نَهْيٌ نَهَيْتَنِي عَنْهُ فَأَسْرَعْتُ إِلَيْهِ ، وَ نِعْمَةٌ أَنْعَمْتَ بِهَا عَلَيَّ فَقَصَّرْتُ فِي شُكْرِهَا.

وَ يَحْدُونِي عَلَى مَسْأَلَتِكَ تَفَضُّلُكَ عَلَى مَنْ أَقْبَلَ بِوَجْهِهِ إِلَيْكَ ، وَ وَفَدَ بِحُسْنِ ظَنِّهِ إِلَيْكَ ، إِذْ جَمِيعُ إِحْسَانِكَ تَفَضُّلٌ ، وَ إِذْ كُلُّ نِعَمِكَ ابْتِدَاءٌ

فَهَا أَنَا ذَا ، يَا إِلَهِي ، وَاقِفٌ بِبَابِ عِزِّكَ وُقُوفَ الْمُسْتَسْلِمِ الذَّلِيلِ ، وَ سَائِلُكَ عَلَى الْحَيَاءِ مِنِّي سُؤَالَ الْبَائِسِ الْمُعيِلِ

مُقِرٌّ لَكَ بِأَنِّي لَمْ أَسْتَسْلِمْ وَقْتَ إِحْسَانِكَ إِلَّا بِالْإِقْلَاعِ عَنْ عِصْيَانِكَ ، وَ لَمْ أَخْلُ فِي الْحَالَاتِ كُلِّهَا مِنِ امْتِنَانِكَ.

فَهَلْ يَنْفَعُنِي ، يَا إِلَهِي ، إِقْرَارِي عِنْدَكَ بِسُوءِ مَا اكْتَسَبْتُ وَ هَلْ يُنْجِينِي مِنْكَ اعْتِرَافِي لَكَ بِقَبِيحِ مَا ارْتَكَبْتُ أَمْ أَوْجَبْتَ لِي فِي مَقَامِي هَذَا سُخْطَكَ أَمْ لَزِمَنِي فِي وَقْتِ دُعَايَ مَقْتُكَ.

سُبْحَانَكَ ، لَا أَيْأَسُ مِنْكَ وَ قَدْ فَتَحْتَ لِي بَابَ التَّوْبَةِ إِلَيْكَ ، بَلْ أَقُولُ مَقَالَ الْعَبْدِ الذَّلِيلِ الظَّالِمِ لِنَفْسِهِ الْمُسْتَخِفِّ بِحُرْمَةِ رَبِّهِ.

الَّذِي عَظُمَتْ ذُنُوبُهُ فَجَلَّتْ ، وَ أَدْبَرَتْ أَيَّامُهُ فَوَلَّتْ حَتَّى إِذَا رَأَى مُدَّةَ الْعَمَلِ قَدِ انْقَضَتْ وَ غَايَةَ الْعُمُرِ قَدِ انْتَهَتْ ، وَ أَيْقَنَ أَنَّهُ لَا مَحِيصَ لَهُ مِنْكَ ، وَ لَا مَهْرَبَ لَهُ عَنْكَ ، تَلَقَّاكَ بِالْإِنَابَةِ ، وَ أَخْلَصَ لَكَ التَّوْبَةَ ، فَقَامَ إِلَيْكَ بِقَلْبٍ طَاهِرٍ نَقِيٍّ ، ثُمَّ دَعَاكَ بِصَوْتٍ حَائِلٍ خَفِيٍّ.

قَدْ تَطَأْطَأَ لَكَ فَانْحَنَى ، وَ نَكَّسَ رَأْسَهُ فَانْثَنَى ، قَدْ أَرْعَشَتْ خَشْيَتُهُ رِجْلَيْهِ ، وَ غَرَّقَتْ دُمُوعُهُ خَدَّيْهِ ، يَدْعُوكَ بِيَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ ، وَ يَا أَرْحَمَ مَنِ انْتَابَهُ الْمُسْتَرْحِمُونَ ، وَ يَا أَعْطَفَ مَنْ أَطَافَ بِهِ الْمُسْتَغْفِرُونَ ، وَ يَا مَنْ عَفْوُهُ أَكْثَرُ مِنْ نَقِمَتِهِ ، وَ يَا مَنْ رِضَاهُ أَوْفَرُ مِنْ سَخَطِهِ.

وَ يَا مَنْ تَحَمَّدَ إِلَى خَلْقِهِ بِحُسْنِ التَّجَاوُزِ ، وَ يَا مَنْ عَوَّدَ عِبَادَهُ قَبُولَ الْإِنَابَةِ ، وَ يَا مَنِ اسْتَصْلَحَ فَاسِدَهُمْ بِالتَّوْبَةِ وَ يَا مَنْ رَضِيَ مِنْ فِعْلِهِمْ بِالْيَسِيرِ ، وَ يَا مَنْ كَافَى قَلِيلَهُمْ بِالْكَثِيرِ ، وَ يَا مَنْ ضَمِنَ لَهُمْ إِجَابَةَ الدُّعَاءِ ، وَ يَا مَنْ وَعَدَهُمْ عَلَى نَفْسِهِ بِتَفَضُّلِهِ حُسْنَ الْجَزَاءِ.

مَا أَنَا بِأَعْصَى مَنْ عَصَاكَ فَغَفَرْتَ لَهُ ، وَ مَا أَنَا بِأَلْوَمِ مَنِ اعْتَذَرَ إِلَيْكَ فَقَبِلْتَ مِنْهُ ، وَ مَا أَنَا بِأَظْلَمِ مَنْ تَابَ إِلَيْكَ فَعُدْتَ عَلَيْهِ.

أَتُوبُ إِلَيْكَ فِي مَقَامِي هَذَا تَوْبَةَ نَادِمٍ عَلَى مَا فَرَطَ مِنْهُ ، مُشْفِقٍ مِمَّا اجْتَمَعَ عَلَيْهِ ، خَالِصِ الْحَيَاءِ مِمَّا وَقَعَ فيِهِ.

عَالِمٍ لَيْكَ، بِأَنَّ الْعَفْوَ عَنِ الذَّنْبِ الْعَظِيمِ لَا يَتَعَاظَمُكَ ، وَ أَنَّ التَّجَاوُزَ عَنِ الْإِثْمِ الْجَلِيلِ لَا يَسْتَصْعِبُكَ ، وَ أَنَّ احْتِمالَ الْجِنَايَاتِ الْفَاحِشَةِ لَا يَتَكَأَّدُكَ ، وَ أَنَّ أَحَبَّ عِبَادِكَ إِلَيْكَ مَنْ تَرَكَ الاِسْتِكْبَارَ عَلَيْكَ ، وَ جَانَبَ الْاِصْرَارَ ، وَ لَزِمَ الاِسْتِغْفَارَ.

وَ أَنَا أَبْرَأُ إِلَيْكَ مِنْ أَنْ أَسْتَكْبِرَ ، وَ أَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُصِرَّ ، وَ أَسْتَغْفِرُكَ لِمَا قَصَّرْتُ فِيهِ ، وَ أَسْتَعِينُ بِكَ عَلَى مَا عَجَزْتُ عَنْهُ.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ هَبْ لِي مَا يَجِبُ عَلَيَّ لَكَ ، وَ عَافِنِي مِمَّا أَسْتَوْجِبُهُ مِنْكَ ، وَ أَجِرْنِي مِمَّا يَخَافُهُ أَهْلُ الْإِسَاءَةِ ، فَإِنَّكَ مَلِي‌ءٌ بِالْعَفْوِ ، مَرْجُوٌّ لِلْمَغْفِرَةِ ، مَعْرُوفٌ بِالتَّجَاوُزِ ، لَيْسَ لِحَاجَتِي مَطْلَبٌ سِوَاكَ ، وَ لَا لِذَنْبِي غَافِرٌ غَيْرُكَ ، حَاشَاكَ وَ لَا أَخَافُ عَلَى نَفْسِي إِلَّا إِيَّاكَ ، إِنَّكَ أَهْلُ التَّقْوَى وَ أَهْلُ الْمَغْفِرَةِ ،

صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ ، وَ اقْضِ حَاجَتِي ، وَ أَنْجِحْ طَلِبَتِي ، وَ اغْفِرْ ذَنْبِي ، وَ آمِنْ خَوْفَ نَفْسِي ، إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْ‌ءٍ قَدِيرٌ ، وَ ذَلِكَ عَلَيْكَ يَسِيرٌ ، آمِينَ رَبَّ الْعَالَمِينَ.

Na mojawapo ya dua zake (Imamu Sajjad) amani iwe juu yake, ilihusu ni ile dua yake juu ya kuungama na kukiri makosa, pamoja na kuomba toba kwa Mwenye Ezi Mungu Mtukufu. Dua ambayo imekuja kwa ibara zifuatazo:

Ewe Mola wangu ! Kwa yakini, kuna sifa (khulka) tatu ambazo hunizuia mimi kuwasilisha maombi yangu Kwako; na ni sifa (khulka) moja tu ndiyo inayonielekeza katika kukuomba Wewe. Zile sifa (hulka) tatu ambazo ni kizuizi katika kuwasilisha maombi yangu Kwako ni kama ifuatavyo:

(Kizuizi cha kwanza kabisa) Ni ile pazia, inayotokana agizo uliloliamuru, nami nikasuasua katika kulitekeleza. (Kizuizi cha pili), ni lile katazo ulilonikataza, nami nikaliharakia katika kulikwaa katazo hilo. (Ama kizuizi cha tatu) ni ile neema uliyonijaalia, nami nikawa ni mchache wa shukurani katika kukishukuru kile ulichonijaalia shukrani.

Na kinachonivuta (kinachonisukuma na kunipa shauku ya) kukuelekea Wewe katika ombi yangu, ni ile hisani Yako tukufu ulikuwa nayo kwa yule anayekuja Kwako kwa moyo msafi na kuingia katika Ufalme Wako wa Kiroho, hali akiwa na matarajio yaliyojaa imani katika kutaraji ukarimu Wako; kwani hisani Zako zote ni tunuko unayotutunukia hali ya kwamba kiuhalisia sisi hatustahili hisani adhimu kama hizo (kutokana na mapungufu yetu), na kila neema Yako tokea mwanzo ni wa ukarimu Wako usio na kikomo (kwa viumbe Wako).

Ewe Maabudu (Mwabudiwa) wangu! Hivi mimi (kama unavyoniona nipo) hapa nimesimama mbele ya adhama Yako; (hali nikiwa nimesimama kwa) kisimamo cha mtumishi mnyenyekevu aliye dhalili. Na (Nipo hapa) nikiwa ni muombaji aliyegubikwa na haya usoni mwake, ninafikisha ombi hili la mhitaji aliyelemewa na shida (na mahitaji).

Ninakiri wazi kwamba; pale nilipopokea ihsani Yako, sikudhihirisha utiifu wowote ule wala sikujisalimisha mbele Yako, zaidi ya kujizuia tu na uasi dhidi Yako; na katika vipindi vyote (hivyo), sikuwahi (hata mara moja) kunyimwa mgao wa wema na fadhila Zako.

Ewe Mungu wangu! Je, hivi kukiri (kuungama) kwangu mbele Yako juu uovu wa matendo yangu kutaniletea faida yoyote? Na je hivi kuungama kwangu Kwako kwa makosa niliyoyafanya, kutaniondoa katika adhabu Yako? Au katika hali hii niliyo nayo, tayari hasira na ghadhabu Zako vimenilazimu (zimeshalazimiana nami)? Au wakati huu ninapokuomba, maangamizi Yako yamesha ambatana nami?"

Umetukuka kwa utukufu ulioje! Katu sitakata tamaa Kwako, ilhali (ninatambua kwamba) umenifungulia mlango wa toba mbale hadhara Yako; badala yake, nanena kwa kutumia kauli za mja dhalili, mja aliyejidhulumu nafsi yake, mja aliyedharau hadhi ya Mola wake Mlezi.

(Ewe Mola wangu mimi ni) mja ambaye madhambi yake yamekithiri na kurundikana (kurimbikana), na tayari siku zake zimemeshamwacha mkono na kumpa mgongo, (mpaka imefikia hali ya kwamba), yeye mwenye ameshajua ya kuwa; wakati wa kutenda 'amali njema umeshapita na tayari ajali yake imeshawadia; na anapata yakini kuwa; hana hifadhi itakayomlinda na adhabu Yako, wala kimbilio la kukimbilia na kuepukana Nawe. (Hivyo basi) amekuelekea Wewe kwa inaba (kujiegemeza) na kilio, akiikhilisisha Kwako tawba yake. Basi, amesimama mbele ya Hadhrati Yako kwa moyo msafi, uliotwaharika, na anakunadi (anakuita au anakuomba) kwa kilio kilchojaa huzuni (chenye kutakata na kubadilika) na (kwa) sauti ya chini.

(Mja huyu anakuomba) hali akiwa ameinamisha kichwa chake katika kilele cha unyenyekevu mbele Yako, akapindisha kichwa chake hadi umbo lake likapindana. Hakika khofu yake imetetemesha miguu yake, na machozi yake yamefurika juu ya mashavu yake. Anakuita akisema: "Ewe Mwingi wa Rehema kupita wote wenye kurehemu! Na Ewe Mrehemevu mkuu anayekimbiliwa na watafutao rehema! Na Ewe Mwenye huruma kuu anayezungukwa na watafutao maghufira! Na Ewe ambaye msamaha Wake ni umepindukia adhabu Yake, na Ewe ambaye ridhaa Zake zimeforika zaidi ya ghadhabu Zake.

Na Ewe Ambaye Umeonesha upendo Wako kwa viumbe wake kupitia hisani ya uvumilivu (juu ya upungufu wao!) Na Ewe Ambaye Umewazoeza waja Wako kukubali (kushikamana na) fursa ya kurejea Kwako! Na Ewe Unayerekebisha uharibifu wa (nafsi za waja) kupitia njia ya utakaso wa toba! Na Ewe Ambaye Unaridhika hata na chembe ndogo za waja Wako! Na Ewe Ambaye Unazidisha thamani ya mchango wao mdogo kwa malipo makubwa yasiyo na kifani! Na Ewe Uliehakikishia (Uliyedhamini) kujibu maombi yao (ya waja Wako)! Na Ewe Ambaye, kwa ukarimu Wako wa asili, Umewaahidi (waja Wako) malipo mema yasiyopimika!

Mimi si muasi aliyepindukia mipaka zaidi miongoni mwa waliokuasi Nawe Ukawaghufiria; wala mimi si mwenye kulaumika zaidi miongoni mwa walioomba radhi Kwako na Ukawakubalia; wala mimi si dhalimu mkubwa zaidi miongoni mwa waliotubu Kwako Nawe Ukawarejeshea fadhila Zako (Ukawaridhia).

(Ewe Mola wangu) ninatubia Kwako nikiwa katika hali hii niliyokuwa nayo, kwa toba (au kupitia toba) ya mtu mwenye majuto ya kina (nadama) kutokana na yale aliyoyatenda, mwenye wasiwasi na hofu (mushfiq) kutokana na yale yaliyomkusanyikia juu yake (juu ya dhima yake), na mwenye ikhlasi katika hisia za haya aliyo nayo, (haya) inayotokana na yale aliyojitumbukiza ndani yake.

(Ewe Mola wangu) ninajua fika kwamba: suala la kusamehe dhambi kuu, si jambo zito mbele yako, na wala hakuna ugumu wowote ule mbele yako, juu ya kusamehe kosa lililopindukia mipaka, na wala hukukutii mashakani (wala hupati tabu yoyote ile) katika kuvumilia makosa ya watenda-uovu. Pia (ninatambua fika), kwamba; mja wako umpendaye zaidi, ni yule anayeacha jeuri na kutakabari dhidi yako, (ambaye) huepukana na kung'ang'ania dhambi, na anayeshikamana na maombi ya msamaha (Wako).

Na mimi (ninakuhakikishia) mbele Yako kamba nimejitenga (niko mbali mno) na hisia za kuwa na kiburi (na kujitapa mbele Yako), nami ninatafuta hifadhi Kwako, dhidi ya (uchu wa) kung’ang’ani makosa (matendo maovu), na ninakuomba msamaha kwa yale mapungufu yangu (kwa nilipoteleza), na ninakuomba msaada kwa yale niliyoshindwa (kupambana nayo).

Ewe Mola wangu, msalie (mshushie rehema zako) Muhammad na Aali zake. Na unipe hidaya (taufiki) ya kutekeleza yale yaliyo wajibu juu yangu Kwako wewe, na uniafi (unisamehe) kutokana na yale (adhabu) ninayostahiki kutoka Kwako, na unipe hifadhi dhidi ya yale wanayoyakhofia watenda maovu. Kwani hakika Wewe ni Mkwasi wa usamehevu, unayetarajiwa kwa maghufira, na unafahamika kwa upole (wa kufumbia macho maovu ya waja Wako katika mahakama Yako). Sina pengine pa kuielekeza haja yangu isipokuwa Kwako tu, na wala hakuna wa kuisamehe (kuifunika) dhambi yangu zaidi Yako. Hashaka (umetakasika hisia za Maangamizi dhidi ya waja Wako)! Wala sikhofu kitu chochote kile dhidi ya nafsi yangu isipokuwa Wewe tu. Hakika, Wewe ndiye chimbuko la taqwa na chimbuko la maghufira.

Mshushie rehema Zako (ikweze daraja dhati ya) Muhammad na Aali zake. Na unitimizie haja yangu, na zifanikishe jitihada zangu. Nifutie kosa langu, na unilinde na wasiwasi wa nafsi yangu (niondolee wasiwasi uliomo nafsini mjwangu). Hakika Wewe ni mwenye mamlaka kamili juu ya kila jambo, na utekelezaji wa hayo ni jambo rahisi mno Kwako. Itakabali (dua yangu hii) Ewe Mlezi wa walimwengu.

🌞
🔄

Rejea

  1. Mamduhi, Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 505.
  2. Tarjume wa Sherh Duaye Davozdahom Sahife Sajadiye, Touti ya Erfan.
  3. Ansarian, Diyar Asheqan, 1372 S, juz. 5, uk. 129-157; Mamduhi, Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 505-557.
  4. Ansarian, Diyar Asheqan, 1372, juz. 5, uk. 125-157.
  5. Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 505-557.
  6. Fihri, Sherh wa Tafsir Sahifa al-Sajjadiyah, 1388 S, juz. 2, uk. 15-62.
  7. Madani Shirazi, Riadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 465-523.
  8. Mughniyyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 171-181.
  9. Darabi, Riadh Al-Arifin, 1379 S, uk. 145-158.
  10. Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 299-316.
  11. Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 35-38.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.