Dhu al-Thudayya
Dhū al-Thudayya (Kiarabu: ذُو الثُّدَیَّة) ni jina lenye maana ya mwenye ziwa au mwenye kinundu cha ziada. Nalo ni jima walilipowe watu maalumu wenye alama fulani vifuani mwao ifananayo na ziwa. Jina hili limehusishwa na watu kadhaa walio shiriki katika kundi la Khawarij, hususan katika vita vya Nahrawan dhidi ya Imam Ali (a.s). Watu hawa walikuwa ni miongoni mwa watu wa kundi lililopinga na kusimama dhidi ya uongozi wa Imam Ali (a.s), ambao ni maarufu kwa itikadi zao kali. Miongoni mwa watu waliotajwa kuwa na sifa hii ni Naafi’ al-Mukhdajiy’'u Mukhaddaj, Hurqus ibn Zuhair na Dhu al-Khuwaisira al-Tamimi. Watu hawa walishiriki katika vita vya Nahrawan, vita ambavyo vilitokea kati ya Imam Ali (a.s) na Khawarij. Baada ya kuuawa kwa mmoja wa watu hawa, ambaye alikuwa na alama ya mwili inayolingana na maelezo ya Dhū al-Thudayya, Imam Ali (a.s) alisujudu sijda ya shukrani akimshukuru Mola wake kutokana na neema ya kuuawa kwa mtu huyo. Katika Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kuna marejeo ya mtu mwenye alama kama hizo, ambaye alitabiriwa kuwa ni mmoja wa kundi la watu walio potea, na kulingana na Hadithi hiyo, bwana Mtume alimlaani mtu huyo. Kwa hiyo, jina Dhū al-Thudayya limekuwa na umuhimu maalumu katika historia ya Uislamu, likihusishwa na watu waliopinga uongozi wa Imam Ali (a.s) na kusababisha mfarakano mkubwa ndani ya jamii ya Waislamu.
Maelezo Kusiana na Lakabu ya Jina Dhū al-Thudayya
Lakabu au jina la Dhū al-Thudayy (ذوالثُدَیَة), linalomaanisha "mwenye ziwa," limetumika kihistoria kurejelea watu waliokuwa na alama maalum ya vifuani mwao inayofanana na ziwa la mwanamke. Ingawa kuna tofauti katika vyanzo vya Hadithi na historia kuhusu ni nani hasa anaye husika na jina hili, ila inabakia wazi kwamba; wote waliotajwa kwa jina hili ni wafwasi wa kundi la Khawarij ambao ni wapinzani wa Imam Ali (a.s) walio shiriki katika vita vya Nahrawan dhidi yake.
Kulingana na ripoti ya Sheikh Mufidu, aliyefariki mwaka 413 Hijria, ni kwamba; Imam Ali (a.s) akieleleza sifa za Makhawariji alisema kuwa: Makhawarij walikuwa na tabia ya kipekee kabisa, walikuwa wakifunga mchana na kusali usiku, lakini hatimae walipinga na uongozi wa Imam Ali (a.s). Katika muktadha huu, Imam Ali (a.s.) alitaja mmoja wa wafuasi wa kundi hili kwa jina la Dhū al-Thudayya.[1] Pia, Salman al-Farsi amenukuu kutoka kwa Imamu Ali (a.s) kwamba; Mtume (s.a.w.w) aliwalaani wafuasi wa Dhū al-Thudayya ambao ni Makhawarij.[2]
Ibn Abi Jumhur (aliyefariki mwaka 880 Hijria) amepokea kutoka kwa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s) kwamba; Nawruz, au Siku ya Nawruz, ni siku ya ushindi wa Imamu Ali (a.s) dhidi ya watu wa Nahrawan na ni siku ya kuuawa kwa Dhū al-Thudayya.[3] Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya kihistoria, baada ya kumalizika kwa vita vya Nahrawan na kupatikana kwa mwili wa Dhū al-Thudayya, Imam Ali (a.s.) alisujudu akionesha na kumshukuru Mungu,[4] furaha akionesha furaha kutokana na tokeo hilo.[5] Imamu Ali (a.s.) alieleza hisia zake kwa kusema: "Sifa zote ni za Mwenye Ezi Mungu ambaye amekufikisha mapema kwenye moto wa Jahannam." [6]
Kulingana na maelezo ya Ibn Shadhan katika kitabu chake “al-Iidhaah”, ni kwamba; Pale Aisha alipo fikishiwa habari za kuuawa kwa Dhū al-Thudayya kutoka kwa Imamu Ali (a.s), Aisha alimlaani Amr ibn al-As. Hii ilitokana na ukweli kwamba Amr ibn al-As alikuwa amemdanganya [7]Aisha kwa kumwambia kuwa Dhū al-Thudayya aliuawa akiwa Alexandria,[8] nchini Misri.[9] Aisha alihusisha tokeo hili na Hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), akisema: "Wao (Makahwarij) ndio viumbe wabaya zaidi wa Mwenye Ezi Mungu, watakaouawa na viumbe bora zaidi wa Mwenye Ezi Mungu."[10] Hata hivyo, baadhi ya wanahistoria wameeleza kuwa Dhū al-Thudayya aliuawa nchini Misri, jambo ambalo linaonyesha tofauti ya mitazamo kuhusu mahali pa kifo chake.[11]
Ni Nani Hasa Mlengwa wa Jina la Dhū al-Thudayya
Dhū al-Thudayya ni jina lililotumiwa likiashiria watu tofauti katika historia, likijumuisha watu kadhaa kama vile Naafi’ al-Mukhdajiy’' Mukhaddaj, Hurqus ibn Zuhair, Dhu al-Khuwaisira al-Tamimi,[12] pamoja na Amru ibn Abd al-Wudd aliye kuwa akiishi wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).[13] Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria,[14] katika vita vya Nahrawan, kulikuwa na watu watatu walioshikilia jina la Dhū al-Thudayya. Mmoja wao alikiwa ni Hurqus ibn Zuhair,[15]akifuatiwa na Dhu al-Khuwaisira al-Tamimi,[16] aliye kuwa kiongozi wa kundi la Khawarij,[17] na wa mwisho wao ni Naafi’ al-Mukhdajiy’',[18] ambaye aliuawa katika vita hivyo.[19] Ibn Abdulbar ameandika akisema kwamba; baadhi ya watu wengine humhisabu Dhu al-Khuwaisira kama mtu tofauti na Dhū al-Thudayya, jambo linalo ashiria kuwepo kwa tofauti za mitazamo kuhusiana na jina hili katika historia.[20]
Naafi’ Al-Mukhdajiy
Mmoja wa watu waliotambuliwa kwa jina la Dhū al-Thudayya ni Naafi’[21] au Tharmala,[22] ambaye kunia yale ilikuwa ni Mukhdaji,[23] naye alikuwa mtu wa kutoka nchi ya Habasha.[24] Kwa mujibu wa ripoti za kihistoria Naafi al- Mukhdaji,[25] alikuwa na kitu kinachofanana na matiti ya wanawake kifuani mwake, hiyo ndiyo sababu ya kupewa jina la Dhū al-Thudayya.[26] Muhammad Taqi Shushtari, mtafiti wa nasaba za wapokezi wa Hadithi wa Kishiia, alifanya utafiti na hatimaye akakubali kwamba Dhū al-Thudayya ni jina makhususi alilopewa Naafi’. [27]
Kulingana na ripoti za waandishi wa historia kama vile Ibn Kathir na Ibn Ash'ath al-Sijistani, Naafi’ al- Mukhdaji alikuwa ni maskini, ambaye mara zote alikuwa akiishi msikitini na akila chakula pamoja na maskini wengine kwenye jamvi la Imamu Ali (a.s).[28] Jina lake maarufu miongoni mwa watu ni Harqus.[29] Baladhuri (aliye fariki mwaka 279 Hijiria), ameandika akisema kwamba; baada ya vita vya Nahrawan, Imamu Ali (a.s) alichukua juhudi binafsi za kuutafuta mwili wa Dhū al-Thudayya, hatimae akampata kwenye shimo. Aliye patikana shimoni humo alikuwa ni al- Mukhdaji, aliye kuwa akiitwa kwa jina la Naafi. [30] Ibn Abi 'Aasim (aliyeaga dunia mnamo mwaka 287 Hijiria), baada ya kunukuu Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) inayo rejelea kundi la watakao toka nje ya dini, ambapo aliashiria kuwepo kwa mtu mwenye zaaida kifuani mwake kama matiti ya wanawake miongoni mwa watu wa kundi hilo, aliendelea kuripoti suala la kupatikana kwa mwili wa al- Mukhdaji na Takbir ya Imam Ali (a.s), inayo ashiria furaha ya tokeo hilo. [31]
Hurqus ibn Zuhair
- Makala asili: Hurqus ibn Zuhair
Kuna mtu mwengine aitwaye Hurqus ibn Zuhair[32] aliye shiriki katika vita vya Nahrawan dhidi ya Imamu Ali (a.s), ambaye pia naye ametajwa kwa jina la Dhū al-Thudayya.[33] Kulingana na ripoti za Allama Hilli, hapo mwanzo Hurqus alikuwa ni miongoni mwa wapiganaji wa upande wa Imamu Ali (a.s).[34] Ila baada ya tokeo la Hakimiyyat (la makubaliano ya kusimamisha vita bina ya Muawia na Imamu Ali), Hurqus alibadili msimamo wake na kusimama dhidi ya Imamu Ali (a.s).[35] Baada ya kumaliza kwa vita vya Nahrawan, Imamu Ali (a.s), aliwataka wafwasi wake kuutafuta mwili wa Hurqus miongoni mwa maiti zilizotawanyika vitani humo. Baada ya kupatika na kwa mwili wa Hurqus, Imamu Ali (a.s) alionekana akisujudu sijda ya kushukuru Mungu, kisha akawaelekea wafweasi wake akiwaambia kuuambia: «Nyinyi mmefanikiwa kumuua mtu aliye bobea shari kisawa sawa».[36]
Rejea
- ↑ Sheikh Mufid, al-Ikhtisas, uk. 179, 1414 H.
- ↑ Khatib Baghdadi, Tarikh Baghdad, juz. 13, uk. 284, 1417 H;Tazama Tabrani, al-Mu'jam al-Ausat, juz. 4, uk. 34, 1415 H; Tabrani, al-Mu'jam al-Saghir, Dar al-Kutub al-Ilmiah, juz. 1, uk. 155
- ↑ Ibnu Abi Jumhur, 'Awali al-La'ali, juz. 3, uk. 41, 1404 H.
- ↑ Ibnu Abi Shaibah Kufi, al-Musannaf, juz. 2, uk. 368, 1409 H.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, Dar Sadir, juz. 6, uk. 230; Muhaqqiq Hilli, al-Mu'tabar, Muasasah Sayidu al-Shuhada, juz. 2, uk. 270; Allamah Hilli, Nihayat al-Ahkam, juz. 1, uk. 498, 1410 H; Shahid Awal, Dhikra al-Shiah, juz. 3, uk. 463, 1419 H.
- ↑ Rawandi, al-Kharaij wa al-jaraih, juz. 1, uk. 227, 1409 H.
- ↑ Ibnu Shadhan, al-Idhah, uk. 86, 1363 S.
- ↑ Ibnu Abi al-Hadid, Sharh Nahj al-Balaghah, juz. 2, uk. 268, 1378 H.
- ↑ Ibnu Shadhan, al-Idhah, uk. 86, 1363 S.
- ↑ Ibnu Abi al-Hadid, Sharh Nahj al-Balaghah, juz. 2, uk. 268, 1378 H; Qomi, al-'Aqd al-Nadhid, uk. 131, 1423 H.
- ↑ Ibnu Shahr Ashub, Manaqib, juz. 1, uk. 5, 1376 H.
- ↑ Ibnu Abd al-Bar, al-Tamhid, juz. 23, uk. 332, 1387 H.
- ↑ Baladhuri, Insab al-Ashraf, juz. 2, uk. 375, 1394 H.
- ↑ Ibnu Sa'ad, al-Tabaqat al-Kubra, Dar Sadir, juz. 3, uk. 33; Zey 'Ali, Nasb al-Rayat, juz. 2, uk. 372, 1415 H.
- ↑ Hairi Tehrani, Tafsir Muqtanayat al-Durar, juz. 11, uk. 268, 1337 S.
- ↑ Sheikh Tusi, al-Khilaf, juz. 6, uk. 462, 1417 H; Ibnu Hamdun, al-Tadhkirat al-Hamduniah, juz. 8, uk. 295, 1996 M; Ibnu Abi al-Fida, al-Mukhtasar fi Akhbar al-Bashar, Dar al-Ma'rifah, juz. 1, uk. 148; Sheikh Tusi, al-Khilaf, juz. 1, 1407 H; Pawaraqi, uk. 436; Halabi, al-Sirah al-Halabi, juz. 3, uk. 89, 1400 H; Namazi, Mustadrakat Ilm Rijal al-Hadith, juz. 8, uk. 533, 1415 H.
- ↑ Nahj al-Balaghah, Subhi Salihi uk. 579; Namazi, Mustadrak Safinat al-Bihar, juz. 2, uk. 260, 1418 H.
- ↑ Al-'Aini, Umdat al-Qari, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 16, uk. 143 & juz. 18, uk. 8.
- ↑ Baladhuri, Insab al-Ashraf, juz. 2, uk. 362, 1394 H; Mas'udi, Muruj al-Dhahab, juz. 2, uk. 406, 1404 H; Amili, Tafsir al-Muhit, juz. 4, uk. 331, 1428 H.
- ↑ Ibnu Abd al-Bar, al-Tamhid, juz. 23, uk. 332, 1387 H.
- ↑ Ibnu Ash'ath Sajistani, Sunan Abi Dawud, juz. 2, uk. 430, 1410 H; Baladhuri, Insab al-Ashraf, juz. 2, uk. 375, 1394 H; Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 7, uk. 325, 1408 H; Al-'Aini, Umdat al-Qari, Dar al-Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 15, uk. 230; Shaukani, Nail al-Autar, juz. 7, uk. 343, 1973 M; Tustari, Qamus al-Rijal, juz. 11, uk. 509, 1422 H.
- ↑ Ibnu Qutaibah Dinuri, al-Ma'arif, uk. 421, 1969 M; Rawandi, al-Kharaij wa al-Jaraih, juz. 1, 1409 H; pawaraqi, uk. 227.
- ↑ Al-'Aini, Umdat al-Qari, Dar al-Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 15, uk. 230.
- ↑ Mas'udi, Muruj al-Dhahab, juz. 2, uk. 406, 1404 H.
- ↑ Badri, Nuzhat al-Nadhar, uk. 221, 1421 H.
- ↑ Ibnu Ash'ath Sajistani, Sunan Abi Dawud, juz. 2, uk. 430, 1410 H; Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 7, uk. 325, 1408 H; Ibnu Hajar, Fat-hu al-bari, Dar al-Ma'rifah, juz. 12, uk. 265; Tustari, Qamus al-Rijal, juz. 11, uk. 509, 1422 H.
- ↑ Tustari, Qamus al-Rijal, juz. 12, uk. 107, 1422 H
- ↑ Ibnu Ash'ath Sajistani, Sunan Abi Dawud, juz. 2, uk. 430, 1410 H; Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 7, uk. 325, 1408 H; Ibnu Hajar, Fat-hu al-bari, Dar al-Ma'rifah, juz. 12, uk. 265; Shaukani, nil al-Autar, juz 7, uk 343, 1973 M.
- ↑ Ibnu Ash'ath Sajistani, Sunan Abi Dawud, juz. 2, uk. 430, 1410 H;Tustari, Qamus al-Rijal, juz. 11, uk. 509, 1422 H.
- ↑ Baladhuri, Insab al-Ashraf, juz. 2, uk. 375, 1394 H
- ↑ Baladhuri, Insab al-Ashraf, juz. 2, uk. 375, 1394 H; Ibnu Abi 'Asim, al-Sunnah, uk. 432, 1413 H.
- ↑ Ibnu Abi al-Bar, al-tamhid, juz. 23, uk. 332, 1387 H.
- ↑ Hairi Tehrani, Tafsir al-Muqtanayat al-Durar, juz. 11, uk. 268, 1337 S.
- ↑ Ba'alami, Tarikh Nameh Tabari, juz. 5, uk. 1537, 1378 S.
- ↑ Allamah Hilli, Kashf al-Yaqin, uk. 165, 1411 H.
- ↑ Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 41, uk. 283, 1403 H.
Vyanzo
- Ibnu Abi al-Hadid, Abdu al-Hamid. Sharh Nahju al-Balaghah. Tahqiq: Muhammad Abu al-Fadhl Ibrahim, bita. Dar Ihya al-Kutub al-Arabia, 1378 S.
- Ibnu Abi Jumhuri Askafi. 'Awali al-La'ali al-'Azizi fi al-Ahadith al-Ilmiah. Tahqiq: Mujtaba Araqi, Qom: Sayid al-Shuhada, 1404 H.
- Ibnu Abi Shaibah, Abdullah. al-Musanif fi al-Ahadith wa al-Athar. Tahqiq: Sayyid al-Liham. Beirut: Dar al-Fikr, 1409 H.
- Ibnu Abi 'Asim, Umar. al-Sunnah. Tahqiq: Muhammad Nasiru al-Din. Beirut: al-Maktab al-Islami, 1413 H.
- Ibnu Ash'ath Abi Dawud Sulaiman. Sunan Abi Dawud. Tahqiq: Said Ahmad Liham, Bita. Dar al-Fikr, 1410 H.
- Ibnu Hajar Asqalani, Ahmad. Al-asabah, Tahqiq: 'Adil Ahmad wa 'Ali Muhammad, Beirut, Dar al-kutub al-'alamiah, 1415 H.
- Ibnu Hajar Asqalani, Ahmad. Fat-hu al-Bari Sharh Sahih al-Bukhari. Beirut: Dar al-Ma'rifah Li Tiba'ah wa al-Nashr, Bita.
- Ibnu Hamdun, Muhammad bin Hasan. al-Tadhkirah al-Hamduniah. Tahqiq: Ihsan Abbas va Bakar Abbas. Beirut: Dar Sadir, 1996 M
- Ibnu Sa'ad, Muhammad. al-Tabaqat al-Kubra. Dar Sadir, Bita.
- Ibnu Shadhan, Fadhl. al-Idhah. Tahqiq: Jalaluddin Husseini. Tehran: Muasasah Intisharat, 1363 S.
- Ibnu Shahr Ashub, Muhammad. Manaqib Ali Abi Talib. Tahqiq: lijannat Asatidhat al-najaf al-Ashraf. Najaf al-Ashraf al-Haidariah, 1376 H.
- Ibnu Abdu al-Bar. al-Tamhid. Tahqiq: Mustafa bin Ahmad. al-maghrib: Wizarat 'Umum al-Auqaf wa al-Shu'un al-Islamiah, 1378 H.
- Ibnu Qutaibah, Abdullah. al-Ma'arif. Qom: Manshurat al-Sharif al-Ridha, 1969 M.
- Ibnu Kathir, Ismail. al-Bidayah wa al-Nihayah. Tahqiq: Ali Shiri. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, 1408 H.
- Al-'Ain, Mahmud bin Ahmad. Umdah al-Qari. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, Bita.
- Amili, Haidar. Tafsir al-Muhit al-A'dham. Tahqiq: Muhsin Musawi. Bita. Muasasah Farhang va Nashr Nur Ali Nur, 1428 H.
- Badri, Adil Abdu al-Rahman. Nuzhat al-Nadhar fi Gharib al-Nahj wa al-Athar. Qom: Muasasah al-Ma'rifah al-Islamiah, 1421 H.
- Baladhuri, Ahmad bin Yahya. Insab al-Ashraf. Tahqiq: Muhammad Baqir Mahmudi. Beirut: Muasasah al-A'lami, 1394 H.
- Tustari, Muhammad Taqi. Qamus al-Rijal. Tahqiq: Muasasah al-Nashr al-Islami. Qom: Al-Nashr al-Islami, 1422 H.
- Hairi, Tehrani, Ali. Muqtanayat al-Durar. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiah, 1337 S.
- Halabi, Ali bin Ibrahim. al-Sirat al-Halabiah. Beirut: Dar al-Ma'rifah, 1400 H.
- Khatib Baghdadi, Ahmad. Tarikh Baghdad aw Madinah al-Islam. Tahqiq: Mustafa Abdu al-Qadir. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, 1417 H.
- Rawandi, Qutub al-Din. al-Kharaij wa al-Jaraih. Tahqiq: Muasasah al-Imam al-Mahdi. Qom: Muasasah al-Imam al-Mahdi, 1409 H.
- Zeyn Ali, Jamalu al-Din. Nasbu al-Rayat. Tahqiq: Eiman Salih Sha'ban. Kairo: Dar al-Hadith 1415 H.
- Shahid Awal, Muhammad bin Makki. Dhikri al-Shiah fi Ahkam al-Shariah. Tahqiq: Muasasah Ali al-Beit. Qom: Muasasah Ali al-Bait, 1419 H.
- Sheikh Tusi, Muhammad. al-Khilaf. Tahqiq: Ali Khurasani, Jawad Shahrestani & Muhammad Mahdi Najaf. Qom: al-Nashr al-Islami, 1417 H.
- Sheikh Mufid, Muhammad. al-Ikhtisas. Tahqiq: Ali Akbar Ghafari va Mahmud Zarandi. Beirut: Dar al-Mufid, juz. 2, 1414 H.
- Tabrani, Sulaiman bin Ahmad. al-Mu'jam al-Saghir. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, Bita.
- Tabrani, Sulaiman bin Ahmad. al-Mu'jam al-Ausat. Tahqiq: Ibrahim Husseini. Bita. Dar al-Haramain, 1415 H.
- Allamah Hilli, Husain bin Yusuf. Kashf al-Yaqin fi Fadhail Amir al-Mu'minin (a.s). Tas-hih: Hussein Dargahi, Tehran: Vezarat Ershad, juz. 1, 1411 H.
- Allamah Hilli, Hasan bin Yusuf. Nihayah al-Ahkam. Tahqiq: Mahdi Reja-i. Qom: Muasasah Ismailiyan, 1410 H.
- Qomi, Muhammad bin Hasan. al-'Aqd wa al-Nadhid wa al-Dar al-Farid. Tahqiq: Ali Ausat al-Natiq, al-Musaid Hashim Shahrestani & Latif Faradi. Qom: Dar al-Hadith Li Tiba'ah wa al-Nashr, 1423 H.
- Mubarakfuri, Muhammad Abdu al-Rahman. Tuhfah al-Ahwadhi. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, 1410 H
- Muttaqi Hindi, Ali. Kanz al-'Amal fi Sunan al-Aqwal wa al-Af'al. Tahqiq: Bakri Hayani. Beirut: Muasasah al-Risalah, 1409 H.
- Majlisi, Muhammad Baqir. Bihar al-Anwar. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 2, 1403 H.
- Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hasan. al-Mu'tabar. Qom: Muasasah Sayidu al-Shuhada, Bita.
- Mas'udi, Ali bin Hussein. Muruj al-Dhahab wa Ma'adin al-Jauhar. Qom. Dar al-Hijrat, juz. 2, 1404 H.
- Nu'man Maghribi. Sharh al-Akhbar. Tahqiq: Muhammad Husseini. Qom: Muasasah al-Nahsr al-Islami, 1414 H.
- Namazi, Ali. Mustadrak Safinah al-Bihar. Tahqiq: Hassan bin Ali Namazi. Qom: Muasasah al-Nashr al-Islami, 1418 H.
- Namazi, Ali. Mustadrakat Ilm Rijal al-Hadith. Tehran: Ibnu Mualif, 1415 H.
- Nahj al-Balaghah. Tahqiq: Subhi Salih. Beirut: Bita, 1387 H.
- Haithami, Ali. Majma' al-Zawaid wa Manba' al-Fawaid. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, 1408 H.