Nenda kwa yaliyomo

Dhana ya mrengo wa Batiniyya

Kutoka wikishia

Dhana ya mrengo wa Batiniyya (Kiarabu: الباطنيّة) ni dhana na itikadi inayodai kwamba; dini ina maana nyengine ya ndani zaidi, ambayo muqtadha wake unatofautiana na muqtadha wa maana yake dhahiri, ambayo ni muhimu zaidi kuliko ile maana yake ya dhahiri inayoeleweka na kila mtu. Wafuasi wa mrengo wa Batiniyya, hufasiri Aya za Qur’ani kwa njia ya ta’wil (maana mbadala halisi), wakijaribu kufikia maana ya ndani iliyofichika ndani ya Aya hizo. Miongoni mwa madhehebu na vikundi vya Kiislamu, wafuasi wa madhehebu ya Sufiyya na Ismailiyya ndio wanaojulikana zaidi katika kufuata mrengo wa Batiniyya.

Wafuasi wa Tasawwuf wanaamini kuwa; Sheria ni gamba la nje tu la dini ya Kiislamu, na lengo kuu ni kufikia haqiqa (roho ya dini), ambayo ndiyo kiini chake. Wao wanasisitiza kwamba; Mtu yuapaswa kupiga hatua na kuondoka kwenye dhahiri ya sheria na kufikia kwenye ukweli wa kiroho. Kwa upande wa madhehebu ya Ismailiyya, wao wanaamini kuwa; Maana halisi ya Aya za Qur'ani inaweza kupatikana tu kupitia ta’awil (ufasiri wa maana mbadala). Nao Wanamini kuwa jukumu hili ni la Imamu wao, ambaye ndiye kiongozi wao wa kiroho.

Ama kuhusana na madhehebu ya Shia Ithna Ashariyya, pia kuna baadhi ya watu wamewatambulisha wafuasi wa madhehebu haya, kama ni miongoni mwa wale wenye mwelekeo wa Kibatiniyya, hii ni kwa sababu ya msisitizo wao juu ya nafasi ya Imamu katika mafunzo ya ndani kidini. Hata hivyo, wapo wale wanaopinga madai haya, wakisema kwamba madhehebu ya Imamiyya si miongoni mwa wale wanaofwata mrengo wa itikadi ya Kibatiniyya.

Katika hadithi za Kishia, kuna Riwaya kadhaa zinazoeleza kwamba; Aya za Qur’ani zina maana mbili tofauti ambazo ni maana ya nje (dhahir) na maana ya ndani (batin). Vilevile, Riwaya nyingine zimekuja zikitoa maana ya kita’awil ya Aya ya baadhi ya Aya za Qur’ani, ambo zimekuja kuelezea maana za kiroho au za ndani ya Aya hizo. Wanazuoni wa Kishia, wakitegemea Riwaya hizi, wanakubaliana na dhana ya kufasiri Qur’ani kwa mtindo wa ta’awil. Hata hivyo, mtazamo wao hutofautiana na ule wa wafuasi wa madhehebu ya Tasawwuf na Ismailiyya. Kwani mara nyingi watu wa Tasawwuf na wafuasi wa madhehebu ya Ismailiyya, hutoa maelezo ya ndani yaliyo huru au yanayolenga maana za kiroho pekee bila kujali maana dhahiri, hali ya kwamba wanazuoni wa Kishia huweka vigezo maalum kwa katika tafsiri zao za kita’awil, ili kuhakikisha kuwa tafsiri zao zinalingana na miongozo ya Qur’ani pamoja na Hadithi sahihi.

Ufafanuzi wa Dhana ya Batiniyya

Dhana ya mrengo wa Batiniyya, ni fikra inayosisitiza juu ya maana ya ndani ambyo ndiyo roho ya dini, ikiamini kuwa dini ina sehemu mbili: sehemu ya nje (dhahiri) na sehemu ya ndani (batin). Katika mrengo wa Batiniyya, maana ya ndani ya dini huchukuliwa kuwa ndiyo sehemu muhimu zaidi kuliko ile ya nje, na lengo kuu lake ni kufikia kiini cha ndani na uhakika wa dini ya Kiislamu. [1]

Madhehebu na Vikundi vya Batiniyya Miongoni mwa Waislamu

René Guénon, mwanafalsafa wa Kiislamu kutoka Ufaransa (1886–1951), aliihusisha dhana ya mrengo wa Batiniyya miongoni mwa Waislamu na wafuasi wa mirengo ya Tasawwuf na wanazuoni wanaoshikamana na mafunzo ya kiroho ya Kiislamu ambao hujulikana kwa jina la Maurafaa. [2] Yeye anasema kuwa; vikundi hivi vilitofautisha kati ya gamba la nje la (dhahiri) ya kidini cha kiini cha ndani (batin) cha makusudio ya sheria, huku wafuasi wa vikundi hivi wakisisitiza kuwa ukweli na hakika ya dini hupatikana kupitia maana ya ndani ya sheria za kidini. [3]

Kwa mujibu wa maelezo ya Farhad Daftary, mtaalamu wa madhehebu ya Ismailiyya (aliyezaliwa mwaka 1317 Hijria Shamsia), ni kwamba; Kati ya madhehebu yote ya Kiislamu, kundi la madhehebu ya Ismailiyya ndilo linahusishwa zaidi na fikra ya nadharia ya Kiatiniyya. [4] Kwa mujibu wa imani ya Ismailiyya, manabii walikuja kuwafafanulia watu maana ya nje (dhahir) ya wahyi. Hata hivyo, jukumu la kufasiri wahyi kwa njia ya ta’awil, yaani kufikia maana yake ya ndani na ya dini (batin), lilikuwa ni jukumu la warithi wao wa kiroho wanaoitwa Mawasii au Maimamu. [5]

Ufwasi wa Nadharia ya Batiniyya Katika Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyya

Yasemekana kwamba; watafiti wa masuala ya Kiislamu kama vile Henry Corbin na Muhammad Ali Amir-Moezzi, wamewaweka wafuasi wa madhehebu ya Shia Imamiyya sambamba na madhehebu yenye mwelekeo wa Batiniyya na (ta’awil). Hata hivyo, si wote miongoni mwa watafiti wa mambo ya Kiislamu wanokubaliana na maoni haya. Wengine wamesisitiza wakisema kuwa; msimamo wa wastani wa Kishia una tofauti kubwa na wale mtazamo wa Batiniyya. Miongoni mwa mambo yanayowatofautisha ni pamoja na:

  1. Kuheshimu Dhahiri ya Aya na Maana Dhahiri ya Sheria: Shia Imamiyya wanatambua mamlaka ya sheria na kukubaliana na maana dhahiri ya Aya za Qur’ani na Hadithi, na wala haizikengeushi na kuziweka pembeni maana hizo.
  2. Kiini cha Dini ni Ucha-Mungu: Imamiyya wanasisitiza kuwa uokovu unapatikana kwa kufuata sheria dhahiri za kidini, na dini haijifungi tu na tafsiri za ndani (batini). [6]

Wanazuoni wa Shia wanakubaliana na dhana ya ta’awil kwa ujumla, lakini wanapinga tafsiri za Ismailiyya ambazo mara nyingi zinaonekana ni zenye kupindukia mipaka. Wao wanaweka masharti maalum katika kutasiri Aya za Qur’ani kwa njia ya ta’awil, ili kuhakikisha kuwa tafsiri hiyo inaendana na Qur’ani pamoja na Sunna. [7] Shia pia wanamenukuu Hadithi kadhaa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) zinazoeleza kwamba; Aya za Qur’ani zina maana mbili tofauti, nazo ni maana za nje (dhahir) na za ndani (batin). [8] Pia wamenukuu Hadithi zilizotumia tafsiri ya ndani katika kutoa ufafnuzi wa baadhi ya Aya za Qur’ani, [9] moja ya mfano ya Hadithi hizo ni ile Hadithi ya Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s), iliyofasiri Aya isemayo: (Na pimeneni (vipimo vya mizani) sawasawa kwa vipimo vya haki, wala msipunguze kipimo) [10] kwa maana ya Kufuata Imamu wa haki bila kumpunja haki yake. [11]

Misingi ya Batiniyya Kutoka Upande wa Tasawwuf

Kwa mujibu wa maelezo ya René Guénon, ni kwamba; Misingi ya Batiniyya ya wafuasi wa Tasawwuf inasisitiza kwamba, sharia ni gamba au sura ya nje ya dini, inayojitokeza kupitia hukumu za kifiqhi. Hata hivyo, kiini hasa cha dini ni ile haqiqa yake (ukweli halisi), na njia ya mtu kufikia haqiqa hiyo, ni kupitia tariqa (njia ya kiroho au Kisufi), ambayo inahusisha mazoezi ya kiroho na kujitakasa. [12] Katika mtazamo huu, sharia huchukuliwa kuwa ni mwongozo tu wa kimatendo, ilhali haqiqa ni maarifa safi yanayofungua maana ya juu na ya kina zaidi ya sharia za dini. Maarifa haya hutoa au hujenga uelewa halisi wa maarifa ya kisharia, yakiipa umuhimu wa kiroho na mtazamo wa ndani kabisa. [13]

Misingi ya Batiniyya katika Madhehebu ya Ismailiyya

Mfumo wa Batiniyya katika madhehebu ya Ismailiyya unategemea dhana kuu tatu: dhahiri na batin, tanzil na ta’awil, na muqtadha wa sheria kwa watu makhususi na watu wote kwa jumla. [14] Dhana tatu hizi zinafafnuliwa na misingi mitatu ifwatayo:[15]

  • Kanuni ya Maana ya Batin dhidi ya Maana ya Dhahiri: Mafundisho ya dini yana pande mbili, yaani dhahiri (muonekano wa nje) na batin (kiini cha ndani). Ismailiyya wanasisitiza kuwa maana ya batini ni muhimu zaidi kuliko maana ya dhahiri. [16]
  • Kanuni ya Ta’awil dhidi ya Tanzil na Tafsiri: Ismailiyya pamoja na wanoshikamana na nadharia hii, hutumia ta’wil (tafsiri mbadala), ili kufikia maana ya batini na kuachana na maana dhahiri za Qur’ani na Hadithi. Lengo lao ni kufichua maana ya kiroho na ya siri iliyozikwa nyuma ya maelezo ya nje. [17]
  • Kanuni ya Kugawanya Watu Kundi Maalumu na la Jumla Jamala: Kwa msingi wa nadharia ya Batiniyya ya Ismailiyya, ta’wil ni jukumu la Maimamu, na ni wachache tu wanaoweza kufikia kiini cha dini kupitia ta’wil ya Maimamu. Hivyo, watu wanagawanywa katika makundi mawili khawas (wateule) na awam (jumla jamala). Khawas ni wale wanaofuata imani ya Ismailiyya na kukubali uongozi wa Maimamu wa Ismailiyya nao ndio wale wenye uwezo wa kuelewa maanda za ndani za sheria, na awam ni wale wasio Ismailiyya na wanaoweza tu kuelewa maana dhahiri ya dini. [18]

Ushikamanifu na Utekelezaji wa Hukumu za Kisheria kwa Wafuasi wa Batiniyya

Baadhi ya madhehebu na vikundi vinavyo fuata  nadharia ya Batiniyya havioni kuwepo ulazima wa kufuata hukumu za kisheria chini ya hali fulani. Kwa mfano, imeelezwa kwamba; Ismailiyya wa mwanzo, pamoja na vikundi vyengine kama vile Qarmatiyya na Nizariyya, waliona kuwa hakuna ulazima wa kushikanama na hukumu za kisheria za dini kwa wale walifikia maarifa juu ya kuwatambua Imamu na ambao tayari wameshaufikia ukweli wa kibatini. [19]

Mifano ya Ta’wil za Wafuasi wa Batiniyya

Ifuatayo ni mifano ya tafsiri za ndani (ta’wil) zilizotolewa na wafuasi wa Batiniyya juu ya baadhi ya Aya za Qur’an:

  • (يَوْمَ نَطْوِي السَّمَاءَ كَطَيِّ السِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ; Siku ambayo tutakiunja mbingu kama inavyofungwa kurasa ya kitabu (Qur’an, 21:104) [20] Ta’wil yake inasema kwamba: Siku ambayo sharia itakabatilishwa au kumalizika muda wa matumizi yake. [21]
  •  (فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا ۚ)

Kisha (Mungu) akaziumba mbingu saba kwa muda wa siku mbili, na kila mbingu akawekea amri yake (Qur’an, 41:12) [22] Ta’wil yake ni kwamba: Mungu aliwateua viongozi saba kwa ajili ya vipindi viwili vya mfululizo wa kidhahiri (sheria) na wa kibatini (kindani), huku kila mmoja akipewa jukumu lake maalum. [23]

  • (وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَٰلࣰا ; Basi Usiwaongezee madhalimu kitu chengine isipokuwa upotovu) (Qur’an, 71:24) [24] Ta’wil ya Ibn Arabi: Ewe Mola, usiwaongezee wale waliodhulumu nafsi zao -ambao wameufikia daraja la kujitakasa kabisa na kuyeyuka katika Zati Yako (fanaa fi’llah)- isipokua maarifa yazidishayo hali ya mshangao kwa mwanadamu kamili, ambayo humfanya mwanadamu kuyatafakari Maajabu ya Zati Yako. [25]

Asili ya Mafundisho ya Kibatini

Inadhaniwa kuwa mizizi ya fikra za kibatini, hasa katika madhehebu ya Ismailia, zinatokana na mawazo ya wapenda kupitiliza (Maghulati), ambao ni miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Shia walioishi katika karne ya pili Hijria. Wanazuoni wanahusisha msingi mawazo ya Kibatiniyya kwa watu wawili wafuatao: Mughara bin Said (aliyefariki mwaka 119 Hijria), kiongozi wa kikundi cha Mughairiyya, anadhaniwa kuwa ndiye Muislamu wa kwanza aliyekuwa na mielekeo ya Kibatini. Mughara ndiye wa kwanza kutuhumiwa kwa kutumia tafsiri za ndani (ta’wil) katika kutoa maana ya Aya za Qur'an kwa namna ya kipekee. Na Abu’l-Khattab (aliyefariki dunia mwaka 138 Hijria), mwanzilishi wa madhehebu ya Khattabiyya, anatambulika kuwa ndiye aliyeanzisha harakati za kwanza za kibatini zenye sifa za nadharia za Kibatiniyya miongoni mwa Waislamu. [26]

Hata Ufuasi wa Batini uliopo katika Tasawwuf pia nao unahusishwa na Karne ya Pili ya Hijria, ambacho ni kipindi cha kuibuka kwa Masufi (wanatasawwuf) wa mwanzo; yaani watu kama vile Hasan al-Basri, Abu Hashim al-Kufi (aliyefariki mwaka 150 Hijria), Sufyan al-Thawri (aliyefariki mwaka 161 Hijria), na Ibrahim bin Adham (aliyefariki mwaka 162 Hijria). [27]

Tuhuma za Ufuasi wa Nadharia za Kibatiniyya

Katika historia ya Uislamu, Ufuasi wa Batiniyya umetumika kama ni tuhuma ya kidini au kisiasa yenye lengo la kushutumu wapinzani wa kidini au kuwaondoa wapinzani fulani katika uwanja wa kisiasa. Kwa mfano, Ibn Taymiyyah aliwapachika Mashia, Masufi na wanafalsafa jina la Batiniyya. [28] Aidha, watu waliuawa kwa tuhuma za ufuasi wa nadharia za Batiniyya, ambao miongoni mwa walio maarufu katia yao ni; Hasanak Waziri, aliyekuwa waziri wa Sultan Mahmud wa Ghazni, ambaye alinyongwa kwa sababu za kisiasa. [29]

Rejea

Vyanzo