Dhana ya Kuharakisha Faraja
Dhana ya Kuharakisha Faraja (تَعجیل الفَرَج): Ni dhana yenye lengo la kutatua changamoto na kusubiri tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f). Dhana hii ya Ta'ajil al-Faraj (تَعجیل الفَرَج) -yenye maana ya kuharakisha faraja- kiuhalisia katika teolojia ya Kiimamu (madhehebu ya Shia Ithna Asharia), huwa inahusishwa na dhana ya kusubiri tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f). [1] Kwa mujibu wa maelezo ya mwanazuoni wa Kiislamu na mtafiti wa elimu ya Hadithi aitwaye Muhammad Muhaddith Ri-Shahri (aliyefariki mwaka 2023), ni kwamba; Riwaya nyingi zitkazo kwa bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na Maimamu (a.s), zimekuja zikihimiza waumini kuomba dua mara kwa mara, ili kuharakisha kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s). Pia Hadithi hizo zinaeleza kwamba; amali ya kuomba dua katika kuharakisha tukio hili, ni moja ya majukumu makuu ya waumini waishiwo katika wakati wa kipindi cha ghaiba (kutoweka kwa Imamu Mahdi). [2] Hadithi nazo haikuacha kutaja dua maalumu juu ya suala hili, kwa hiyo tukirudi katika Hadithi mbali mbali tukuta maandiko ya dua maalumu na muhimu zenye lengo la kuharakisha kufikia faraja za waumini kupitia tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f) [3]
Umuhimu na Nafasi ya Dua
Mwanazuoni maarufu wa Kishia, Sayyid Muhammad Taqi Isfahani (aliyefariki mwaka 1347 Hijiria), katika kitabu chake Mikyal al-Makarim fi Fawa'id al-Du’a lil-Qa’im, alitaja aina 18 za dua kutoka katika Hadithi mbali mbali, ambazo zinalenga kuharakisha tukio muhimu la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f). [4] Imeelezwa kwamba; zaidi ya kwamba dua hizo ni zina uzito maalumu katika kutimizwa kwa ahadi ya kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.f), pia dua za mara kwa mara kwa ajili ya kuomba Faraja ya kudhihiri kwa Imamu, huimarisha uhusiano wa kiroho kati yam ja na Imamu wake, na husaidia waumini kuepukana na kukata tamaa wakati wa kipindi kirefu cha ghaiba (kutoweka kwa Imamu). [5]
Kuepuka Uhimizaji na Uharakishaji
Licha ya ya kuwepo himizo la kuomba dua za kuharakisha tukio la kudhihiri kwa Imamu (a.f), pia kuna Riwaya nyengine zinye kuonya suala la kuharakisha au kutaka kuyasogeza mbele matukio ambayo Mwenye Ezi Mungu ameamua kuyachelewesha kwa maslahi yake maalumu. [6] Pia kuna Riwaya makhususi zinazokemea na kukataza suala la uharakishaji wa tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f). [7] Katika moja ya Riwaya ilipokewa kutoka kwa Imamu al-Sadiq (a.s), itoayo majibu kwa waulizao nyakati hasa za kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f); Imamu aliwaarifisha wanaotabiri muda wa kudhihiri kwa Imamu, kuwa watu waongo, huku akiwasifu wale wenye haraka juu ya tukio hilo, kuwa ni watu waliopotea. Ama kwa upande wa wale wanaosubiri kwa utulivu na kuyaweka mambo yao mikononi mwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, Imamu al-Sadiq (a.s) aliwatambulisha watu hawa kuwa ni miongoni mwa wale walionusurika. [8]
Sifa za Uharakishaji Isiyopendekezwa
Sayyid Muhammad Taqi Musawi Isfahani, (aliyeishi kati ya mwaka 1301 na 1348 Hijiria), alitayarisha orodha maalumu ya sifa za uharakishaji usiyopendekezwa katika kitabu chake kiitwacho Mikyal al-Makarim. miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na:
1. Kufuata madai ya uongo ya unajipa sifa za Umahdiyya (Mahdi wa uongo).
2. Kukata tamaa juu ya kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f).
3. Kukanusha uwepo wa Imamu Mahdi (a.f).
4. Kumkosoa Mwenye Ezi Mungu au Imamu kwa kuchelewesha tukio la kudhihiri kwake.
5. Kutojali na kupinga hekima ya ghaiba (kutoweka kwa Imamu).
6. Kudharau Riwaya zinazohusu kusubiri faraja ya kudhihiri kwa Imamu.
7. Kukanusha au kupotosha Riwaya zinazohusu kudhihiri kwa Imamu.
8. Kuwadhihaki waumini wa kweli wanaosubiri tukio la kudhihiri.
9. Kuacha kuomba dua kwa sababu ya kukata tamaa juu ya tukio la kudhihiri. [9]
Mizani Katika Dua
Kulingama na maoni ya mwandishi huyu ni kwamba; ni muhimu kufahamu kuwa kuepuka haraka au uharakishaji wa tukio hili, hakuendani kinyume na suala la kuomba kwa ajili ya kuharakisha tukio hili muhimu la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f). katika maandishi yake, Isfahani alisisitiza kwamba; dua ya namna hii, kama zilivyo dua nyingine zote, huwa inahitaji masharti maalumu ili kufanikisha athari na natija inayotarajiwa kupitia dua hiyo. Hivyo basi, ni vyema kutambua kwamba; dua kama dua ni jambo la kupendeza, na yapaswa kufanyika kwa nia njema bila ya kusahau au kukanisha hekima ya Mwenye Ezi Mungu juu ya tukio hilo. Hivyo basi dua ya kuomba tukio la kudhihiri kwa Imamu (a.f) yapaswa kufuata masharti maalumu ya, na kama itaombwa bila kuchunga masharti hayo, dua hii inaweza kupoteza sifa yake. Hivyo basi iwapo dua hii itaombwa bila ya kufuata masharti ya dua, dua hii itakuwa ni sawa na ibada ya Sala isiyoambatana na masharti maalumu yaliyowekwa na Mwenye Ezi Mungu. Hali ambayo itaifanya dua hiyo kutokuwa na athari yoyote ile ndani yake. [10]
Imam Mahdi (a.f)
Imamu Mahdi (a.f) amesema: "Ongezeni dua kwa ajili ya kuharakisha tukio la kudhihiri, kwani hakika ya amali hiyo, yenyewe ni faraja kwenu." [11] |
Ali-Asghar Ridhwani (aliyezaliwa mwaka 1341 Hijria Shamsia), ambaye ni mtafiti wa masuala ya Mahdiyya (tafiti juu ya Imamu Mahdi), akitoa mtazamo wake kuhusiana na suala hili anasema kwamba; Suala la kuomba dua ya kuharakisha tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f) halipingani na Riwaya zinazokataza uharakishaji wa tukio hilo. Ridhwani katika maelezo yake anasisitiza kwamba; kumuomba Mwenye Ezi Mungu kuharakishwa tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f), hakumaanishi kupuuza masharti na kuwa na maandalizi yanayohitajika juu ya tukio hilo muhimu. Aidha, Ridhwani anaamini kwamba; dua inaweza kuwa ni moja ya sababu muhimu za kufanikisha tukio la kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a). [12]
Maudhui zinazofungamana: ‘Ajjil Farahum (Harakisha Faraja Zao), Intidhare Faraj (Kusubiri Faraja), Dhuhur Imam Mahdi (Kudhihiri kwa Imamu), Du’a’u al-Faraj (Dua ya Kuomba Faraja)