Barua ya Ayatullahi Khamenei

Kutoka wikishia

Barua ya Ayatullah Khamenei kwa Wanafunzi Wanaowaunga Mkono Watu wa Palestina Nchini Marekani: Ni barua nyenzo yenye ujumbe wa mshikamano wa nyoyo na umoja kutoka kwa Ayatullah Khamenei, ambaye ni kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa wanafunzi wanaounga mkono Palestina nchini Marekani ambao walikusanyika katika vyuo vikuu vya Marekani kupinga mashambulizi ya Israeli dhidi ya Ukanda wa Gaza baada ya Operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa.

Katika barua hii, Ayatullah Khamenei amewataja vijana wanaounga mkono Palestina nchini Marekani kama ni sehemu ya wapambanaji wilio mapambanoni, ambao kiitikadi ni tofauti na kinyume na serikali yao. Wao wameanzisha mapambano ya heshima dhidi ya Israeli, na wanasimama mstari sahihi kabisa katika historia. Yeye baruani humo ameeleza nafsi ya Uingereza katika kuanzisha utawala haramu wa Kizayuni. Pia amezitaja Uingereza na Marekani kama ndio wafuasi wakubwa wanaoiunga mkono Israeli, huku kisisitiza haki ya Wapalestina ya kujitetea na kulihami taifa lao. Ayatullah Khamenei katika barua hii, amebainisha kwamba; Kusimama imara na kuwa katika mstari wa haki, ni moja ya mafunzo muhimu ya Qur’ani kwa Waislamu pamoja na wanadamu wote duniani. Pia alikumbusha kuwa; Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umepanua na kuengeza nguvu fikra na msimamo wa kusimama kwenye mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya dhulma. Mwishoni mwa barua hiyo aliwasihi vijana waliolengwa baruani humo kukaribiana na Qur'ani ili kuelewa ujumbe uliomo ndani yake;[1] kuhusiana na hili imeelezwa kuwa, Ayatullah Khamenei katika barua hii kama ilivyo kwa barua zake nyingine mbili zilizotangulia katika kipindi kilichopita, amewataka vijana wa Magharibi kutafuta welewa dini ya Kiislamu kwa kurejelea maandiko na vyanzo halisi vya Kiislamu na kuto kubali kuathiriwa na tafsiri za Mashariki na Magharibi pamoja na mitazamo ya fikra mbalimbali.[2]

Uchapishaji wa barua hii imeakisika kwa namna tofauti duniani, jambo ambalo limeripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari ulimwenguni.[3] Baadhi ya mashirika ya habari yaliripoti habari za kutembelewa mara milioni 15 kwa tweet ya akaunti inayodaiwa kuwa ni ya Ayatullahi Khamenei, tembeleo ambalo lilihusiana hasa na barua hiyo kwa vijana wa Marekani. Hadi hiyo ni baina ya tarehe 11 Juni na 31 Mei (siku moja baada ya kuchapishwa).[4]

Barua hii ilitolewa mnamo tarehe 5 mwezi wa Khordad mwaka 1403 Shamsia sawa na tarehe 25 Mei 2024, na kuchapishwa tarehe 10 Khordad mwaka 1403 Shamsia.[5] Kutoa na kuchapisha barua hii kulifuatia baada ya tukio la kusimama kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani katika kupinga mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza yaliokuwa yakifanywa na Israeli, wanafunzi ambao wakabiliwa na ukandamizaji wa polisi wa Marekani waliokuwa na nia ya kuzima mwamko wa wanafuzi hao.[6] Mwamko wa amani wa wanafunzi wa kuunga mkono watu wa Gaza ulianza mnamo tarehe 17 Aprili mwaka 2024 kutoka vyuo vikuu vya Marekani na polepole kuenea hadi vyuo vikuu vya nchi nyingine za Magharibi.[7] Ukandamizaji, kukamatwa na kufukuzwa kwa wanafunzi waliokuwa wakiandamana, kutoka vyuo vikuu vya Marekani na nchi nyingine, kulikabiliwa na mwakisiko wa maoni mbalimbali duniani.[8]


Matini ya barua ya Ayatollah Khamenei kwa Wanafunzi Wanaounga Mkono Palestina Nchini Marekani


Bismillah ar-Rahman ar-Rahim

Naiandika barua hii kwa vijana ambao dhamiri zao zenye ufahamu zimewasukuma kutetea watoto na wanawake wanyonge wa Gaza. Wanafunzi wapendwa nchini Marekani! Huu ni ujumbe wetu wa mshikamano wa kinyoyo na umoja kwenu. Sasa mnasimama upande mstari sahihi wa historia -ianzayo kurasa zake mpya za mabadiliko-.

Sasa tayari mmesha unda sehemu muhimu ya ngome ya mapambano, hali mkiwa chini shinikizo lisilo na huruma la serikali yenu — ambayo kwa wazi kabisa inatetea utawala dhalimu na usio na huruma wa Kizayuni — kwa kweli mmeanza mapambano adhimu yenye heshima.

Ngome kuu ya mapambano ilioko maeneo ya mbali, na yenye ufahamu na hisia kama zenu za leo, umekuwa ukipipambana kwa miaka kadhaa. Lengo la mapambano haya ni kusitisha ukandamizaji wa wazi ufanywao na mtandao wa kigaidi na usio na huruma unaoitwa "Wazayuni" matendo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka mingi dhidi ya Wapalestina. Baada ya Wazayuni hao kuvamia nchi yao, wamewaweka wenyeji wa nchi hiyo chini ya shinikizo na mateso makali kabisa. Mauaji ya halaiki ya ya hivi leo yafanyawo na utawala wa kibaguzi wa Wazayuni, ni mwendelezo wa tabia ya kikatili kwa miongo kadhaa iliyopita.

Palestina ni ardhi huru na yenye historia refu inayo jumuisha watu mbali mbali ndani yake, wakiwemo; Waislamu, Wakristo, na Wayahudi. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mtandao mabepari wa Kizayuni, kwa msaada wa serikali ya Uingereza, waliingiza maelfu ya magaidi kwa taratibu katika ardhi hii; walivamia miji na vijiji vyake; waliua maelfu kadhaa ya watu au kuwafukuza hadi nchi za jirani; walitwaa nyumba zao, masoko, pamoja na mashamba, na kushikilia ardhi za Palestina zilizo pokonya kimababu, na hatimae walianzisha serikali iitwayo Israeli.

Mfuasi mkubwa na muungaji mkono zaidi wa utawala huu wa kinyang'anyi, baada ya msaada wa awali wa Uingereza, ni serikali ya Marekani. Marekani ambayo ianonekana ikiendelea kutoa msaada wa kisiasa, kiuchumi, na kijeshi kwa utawala huo. Suala hili linaonekana kufanyika kwa uzembe usioweza kusameheka, imewafungulia njia Wazayuni na kuwasahilishia utengenezaji wa silaha hatari za nyuklia.

Tokea mwanzoni, utawala wa Kizayuni ulitumia sera ya "ngumi ya chuma" dhidi ya watu wa Palestina wasio na ulinzi, na bila kujali maadili yoyote yale ya kibinadamu, utu, na dini. Kila siku walionekana kuongeza ukatili, ugaidi, na ukandamizaji.

Utawala wa Marekani na washirika wake hata hawajatupa jicho na kuuangaza ugaidi wa serikali hii na dhuluma yake endelevu. Hata hivi leo, baadhi ya matamko ya serikali ya Marekani kuhusu jinai za Wazayuni huko Gaza yanaonekana kuwa ni ya kinafiki tu, na wala hayana ukweli wowote ndani yake.

Ngome ya mapambano ilijitokeza kutoka katika mazingira haya ya giza na kukata tamaa, na kuundwa kwa serikali ya "Jamhuri ya Kiislamu" nchini Iran kuliipa nguvu ngome hiyo na kuipa upeo mpana zaidi.

Viongozi wa Uzayuni wa kimataifa, ambao wanamiliki mashirika mengi zaidi ya habari nchini Marekani na Ulaya au wako chini ya ushawishi wa pesa na rushwa za Wazayuni, walielezea mapambano haya ya kibinadamu na ya kishujaa kama ugaidi! Je, taifa ambalo linajitetea dhidi ya jinai za wavamizi wa Kizayuni katika ardhi yao wenyewe ni magaidi? Na je, msaada wa kibinadamu kwa taifa hili na kuwapa msaada watu kama hawa ni ugaidi?

Viongozi wa utawala wa kimabavu wa ulimwengu hawana huruma wala wajali dhana za kibinadamu. Taswira waitoayo juu ya ugaidi wa Kizayuni, ni taswira ya watu wanao jitetea na kujilinda, na kuyaita mapambano ya Wapalestina yenye nia ya kutetea uhuru, usalama, na haki ya kujitawala kuwa ni “ugaidi"!

Ninataka kukuhakikishieni kwamba; leo hali imeanza kubadilika. Hatima nyingine ipo njiani kuelekea eneo nyeti la Asia ya Magharibi. Dhamira nyingi duniani zimeamka na ukweli uko katika hatua za kujitokeza. Ngome ya mapambano imeimarika na itaendelea kuimarika zaidi. Pia historia nayo imeanza kufungua kuraza mpya kabisa.

Mbali na nyinyi wanafunzi wa vyuo vikuu kadhaa vya huko Marekani, pia watu na vyuo vikuu vilivyoko nchi nyingine vimeamka dhidi ya dhulma hii. Ushirikiano na msaada wa walimu wa vyuo vikuu kwa nyinyi wanafunzi ni tukio muhimu na lenye athari kubwa ulimwenguni. Hii inaweza kuwa na athari ya kutuliza na kupunguza hali ya ukandamizaji wa polisi wa serikali na shinikizo lililopo dhidi yenu. Mimi pia najihisi kuwa na huruma na nyinyi vijana na pia ninathamini msimamo wenu huu mlio nao.

Mafunzo ya Qur’ani kwetu sisi Waislamu na kwa watu wote duniani, ni kusimama imara katika njia ya kuhakikisha haki, kwani Qur’ani yatwambia: «فَاستَقِم کَما اُمِرتَ; Simama kidete (katika njia ya haki) kama ulivyo amrishwa». Pia Qur’ani inatupa funzo kuhusiana na mahusiano ya kibinadamu kwa kusema: «لا تَظلِمونَ وَ لا تُظلَمونَ ; msidhulumu na wala msidhulumiwe». Naamini kwamba; Kwa kujifunza na kutekeleza maagizo haya, pamoja na mamia ya maagizo mengine yanayofanana na haya, bila shaka ngome ya mapambano itasonga mbele na hatimae kufikia ushindi kwa idhini ya Mwenye Ezi Mungu.

Ninakuusieni kukaribiana na Qur'ani (ili kuelewa dhamira yake).

Sayyid Ali Khamenei

5/3/ 1403 Shamsia sawa na 25 Mei 2024[9]

Rejea

  1. «Name Hadharat Ayatullah Khamenei Be Daneshjuyan Hamiy Mardum Palestine Dar Daneshgahaye Wilayat Mutahide Amerika», Webgah Daftar Hafidh wa Nashr Athar Hadharat Ayatullah Khamenei.
  2. «Bayaban-Nurd Sarvistan, Fursat Dark Bidun Pishdovarii Az Islam Mahya-ast»
  3. «Baztab Namee Rahbar Inqilab Be Daneshjuyan Amerika Dar Fadhaye Baina al-Milali», Khabarigozari Mehr.
  4. «Bazdid 15 Milioni tweet Hesab Karbari Rahbar Inqilab», Mashriqnews.
  5. «Name Hadharat Ayatullah Khamenei Be Daneshjuyan Hamiy Mardum Palestine Dar Daneshgahaye Wilayat Mutahide Amerika», Vibgah Daftar Hafidh wa Nashr Athar Hadharat Ayatullah Khamenei.
  6. Tazama: Idhhari, «Shekaste Marpich Sukut Dar Del Amerika, Ruzname Farhkhtagan»
  7. «Baztab Namee Rahbar Inqilab Be Daneshjuyan Amerika Dar Shabake t.r.t Turkey», Khabarigozari Mehr.
  8. Tazama: «Vaknesh Sazman Milal Be Bazdosht Daneshjuyan Hamiy Palestine Dar Daneshgahaye Amerikaa», Khabarigozari Iran.
  9. «Name Hadharat Ayatullah Khamenei Be Daneshjuyan Hamiy Mardum Palestine Dar Daneshgahaye Wilayat Mutahide Amerika», Webgah Daftar Hafidh wa Nashr Athar Hadharat Ayatullah Khamenei.

Vyanzo