Nenda kwa yaliyomo

Baqiyatullah

Kutoka wikishia

Baqiyatullah ( بَقیّةُاللّه) ni moja ya lakabu za Imamu Mahdi (a.t.f.s), Imamu wa mwisho katika mlolongo wa Maimamu 12 wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia ambaye kwa sasa yupo ghaiba (haonekani katika upeo wa macho ya watu). Neno Baqiyatullah limetumika katika Qur’ani na katika baadhi ya hadithi za tafsiri limefanyiwa taawili ya Maimamu wa Shia na katika baadhi ya hadithi hizo limetambuliwa kuwa lakabu ya Imamu Mahdi (a.t.f.s).

Neno "Baqiyatullah" katika msamiati na tafsiri lina maana ya kile ambacho Mungu anaweka kwa ajili ya mwanadamu, na neno hili limeelezwa pia kuwa lina maana ya fadhila na neema. Namna ya kuifasiri kwa Maimamu ni kwamba wao ni neema na baraka za Mungu juu ya watu.

Matumizi kwa Ahlu-Bayt (a.s)

Neno Baqiyatullah katika hadithi zilizopokewa na Mashia limefasiriwa kwa maana ya Maimamu Maasumina. Kwa mfano, Ibn Shahrashub amesema kwamba Aya ya :«بَقیّةُ اللّهِ خَیرٌ لکُم اِن کُنتم مُؤمِنین»[1] Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Iliteremka kuhusu Maimamu (a.s).[2] Allama Majlisi amesema kuwa, Baqiyatullah imechukuliwa kutoka katika «من ابقاه الله» yaani mtu ambaye Mwenyezi Mungu amembakisha na akasema kuwa, makusudio ya Baqiyatullah ni kuanzia Manabii, mawasii wao ambao Mwenyezi Mungu amewabakisha katika mgongo wa ardhi ili waongoze watu au Maimamu ambao ni mabaki ya Mitume miongoni mwa umma wao.[3] Pia, kwa kuzingatia hadithi, Imam Baqir (a.s), aliwahutubia watu waliofunga lango la mji wao dhidi yake, ambapo alijiita na kujitaja kwa jina la Baqiyatullah.[4]. Katika Ziyarat Jamiat Kabirah pia Maimamu wa Shia wametajwa kwa jina la Baqiyatullah.[5]

Lakabu ya Imamu Mahdi (a.t.f.s)

Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, kinachomaanishwa katika neno Baqiyatullah ni Imamu wa Zama yaani Imamu Mahdi (a.t.f.s). Miongoni mwa walioonukuliwa wakielezea maana hiyo ni pamoja na Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) ambaye amesema: Baqiyatullah maana yake ni Imam Mahdi.[6] Pia, kwa kuzingatia hadithi, Imam Sadiq, katika kujibu swali ambalo watu walikuwa wakimwita Imamu Mahdi kwa lakabu ya Amir al-Muuminin, alisema kuwa, Amir al-Mu'minina lakabu hii ni maalumu kwa Ali bin Abi Talib (a.s) na akawataka watu wamuite Imam wa Zama kwa lakabu ya Baqiyatullah.[7]

Katika Dua Nudba Imamu Mahdi anatajwa kwa jina la Baqiyatullah [8] na katika Ziyarat Aal Yassin pia anasalimiwa kwa ibara ya: «السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا بَقِيَّةَ اللَّهِ فِي أَرْضِه‏»[9]

Imekuja katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia kwamba, wakati wa kudhihiri Imamu Mahdi atasoma Aya hii:بَقیّةُ اللّهِ خَیرٌ لکُم اِن کُنتم مُؤمِنین» Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Na atajitambulisha kwamba, yeye ni Baqaiyatullah na Waislamu watamsalimia kwa ibara ya: «السلام عَلَیْکَ یا بَقِیَّةَ اللّهِ فی اَرْضِه»[10] Kadhalika inasimuliwa katika hadithi ya kwamba, Imamu Mahdi amejitambulisha kwa anuani ya: «بَقیَّةُ اللّهِ فی اَرضِه»[11]

Baadhi ya waliotoa ufafanuzi wa kitabu cha Nahaj al-Balagha wamezungumzia ibara ya: «بَقیَّةُ مِنْ بَقایا حُجَّتِه» Alivyokubaikisheini Mwenyezi Mungu ni katika mabaki ya Huja wa Mwenyezi Mungu” iliyokuja katika kitabu hicho[12] na kuifasiri kwa maana ya Imamu wa 12.[13] Ibn Abil Hadid Mu’tazili amesema: Mashia wanalifasiri neno hili kuwa ni Mahdi, Masufi wanaona kuwa linalokusudiwa ni Maurafaa na Ahlul-Sunna wanalifasiri kwa maana ya Maulamaa ambao ni Huja wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake.[14]

Mitazamo ya Wafasiri

Makala kuu: Aya ya 86 ya Surat Hud

Mwenyezi Mungu anasema: «بَقیّةُ اللّهِ خَیرٌ لکُم اِن کُنتم مُؤمِنین» Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. [15] Chini ya Aya hii, wafasiri wa Qur’ani mbali na nasaha za Nabii Shuaib kwa kaumu yake, wametoa tafsiri na maana mbalimbali. Baadhi yao wamesema kuwa, Baqiyatullah katika Aya hii maana yake ni faida ya halali inayotokana na muamala na biashara ambayo inabakia kwa ajili ya mwanadamu.[16] Baadhi wamesema kuwa, maana yake katika Aya hii ni kipimo na mizani yaani wenzo unaotomika kupimia vitu kama ilivyotangulia katika Aya ya 85 ya Surat Hud.[17] Zamakhshari mfasiri mashuhuri wa Kisuni wa karne ya tano na sita Hijria amezungumzia uwezekano huu kwamba, makusudio ya Baqiyatullah ni ibada ambazo zinabakia kwa Mwenyezi Mungu.[18] Allama Majlisi amesema, wafasiri wa Qur’ani wamefasiri pia neno Baqiyatullah kwa maana ya neema na thawabu zinazobakia kwa ajili ya Akhera.[19]

«Baqiyya» Kwa Maana ya Fadhila na Kheri

Baadhi ya wafasiri wamefasiri neno «Baqiyya» kwa maana ya fadhila, kheri na baraka pia; Zamakhshari ameandika chini ya Aya ya 116 ya Surat Hud ambapo ndani yake limekuja neno «Ulu Baqiyyah» ya kwamba, Baqiyyah imechukuliwa kwa maana ya fadhila na kheri.[20] Neno Baqiyatullah katika Aya ya 248 Surat al-Baqarah limetumika pia kwa maana ya «fadhila» na «kheri».[21] Neno hili limeelezwa pia kuwa lina maana ya neema na fadhila. Namna ya kuifasiri kwamba, inahusiana na Maimamu ni kwamba wao ni neema na baraka za Mwenyezi Mungu kwa watu.[22]

Rejea

  1. Qur'an, 11:86.
  2. Ibn Shahrashub, Manaqib Al AbI Talib, juz. 3, uk. 102, 1379 H.
  3. Majlisi, Bihar al-anwar, juz. 24, uk. 211, 1403 H.
  4. Majlisi, Biḥar al-anwar, juz. 24, uk. 211, 1403 H.
  5. Ibn Mashhadi, al-Mazar al-kabir, uk. 526, 1419 H.
  6. Tabrisi, al-Ihtijaj, juz. 1, uk. 252, 1403 H.
  7. Kulayni, al-Kafi, juz. 1, uk. 411-412, 1407 H.
  8. Ibn Mashhad, al-Mazar al-kabir, uk. 578, 1419 H.
  9. Ibn Mashhad, al-Mazar al-kabir, uk. 569, 1419 H.
  10. Sheikh Saduq, Kamal al-din, juz. 1, uk. 331, 1395 H.
  11. Sheikh Saduq, Kamal al-din, juz. 1, uk. 384, 1395 H.
  12. Nahj al-balagha, khutba 182, uk. 262.
  13. Qutb al-Rawandi, Minhaj al-bara'a, juz. 2, uk. 722, 1404 H, Be Naql Az: Zaryob «Baqiyatullah» uk. 643, khui, Minhaj al-bara'a, juz. 10, uk. 355, 1400 H.
  14. Ibn Abi al-Hadid, Sharh nahj al-balagha, juz. 10, uk. 95-96, 1404 H.
  15. Qur'an, 11:86.
  16. Tabatabayi, al-Mizan, juz. 10, uk. 364, 1417 H.
  17. Zamakhshari, al-Kashaf, juz. 2, uk. 418, 1407 H.
  18. Zamakhshari, al-Kashaf, juz. 2, uk. 418, 1407 H.
  19. Majlisi, Bihar al-anwar, juz. 24, uk. 211, 1403 H.
  20. Zamakhshari, al-Kashaf, juz. 2, uk. 436, 1407 H.
  21. Zaryob «Baqiyatullah» uk. 643.
  22. Zaryob «Baqiyatullah» uk. 643.

Vyanzo

  • Qur'an al-Karim
  • Ibnu Abi al-Hadid, Abdulhamid bin Hibatullah. Sharh Nahj al-Balaghah. Ibrahim Muhammad Abu al-Fadhl, Qom: Maktabah Ayatullah Marashi Najafi, 1404 H.
  • Ibnu Shahr Ashub Mazandarani, Muhammad bin Ali. Manaqib Al AbiTalib. Qom: Allamah, 1379 H.
  • Ibnu Mashhadi, Muhammad bin Ja'far. Al-Mazar al-Kabir. Tas-hih: Jawad Quyyumi Isfahani, Qom: Daftar Intisharat Islami Vabaste be Jami'ah Mudarrisin Hauzah Ilmiah Qom, 1419 H.
  • Khui, Mirza Habibullah, Minhaj al-Bara'ah fi Sharh Nahj al-Balaghah, Tas-hih: Ibrahim Miyanji, tarjume: Hassan Hassan Zadeh Amuli Va Muhammad Baqir Kamrei, Tehran: Maktabah al-Islamiyah, 1400 H.
  • Zaryob, 'Abas «[Baqiyatullah]», Dar Danesh Nameh Jahan Islam, juz. 3, Tehran, Bunyad Dayer al-ma'arifa Islami, juz. 2, 1378 S.
  • Zamakhshari, Mahmud bin Umar. Al-Kashaf 'an Haqaiq Ghawamidh al-Tanzil, Beirut: Dar al-Kitab al-'Arabi, 1407 H.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali. Kamal al-Din wa Tamam al-Ni'mah, Tas-hih: Ali Akbar Ghaffari, Tehran: Islamiah, 1395 H.
  • Tabarsi, Ahmad bin Ali. Al-Ihtijaj 'ala Ahl al-Lijaj. Tahqiq: Muhammad Baqir Khurasan, Mashhad: Nashr Murtadha, 1403 H.
  • Allamah Tabatabai, Sayid Muhammad Hussain. Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an. Qom: Daftar Intisharat Islami Vabaste Be Jami'ah Mudarrisin Hauzah Ilmiah Qom, 1417 H.
  • Kulaini, Muhammad bin Ya'qub. Al-Kafi. Tas-hih: Ali Akbar Ghaffari Va Muhammad Akhundi, Tehran: Dar al-Kitab al-Islamiah, 1407 H.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar al-Anwar. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-'Arabi, 1403 H
  • Nahj al-Balaghah. Tahqiq: Shubhi Salih, Qom: Hijrat, 1414 H.