Bab al-Sa’at
Bab al-Sa’at au Mlango wa Saa (Kiarabu: باب الساعات أو بوابة الساعات) ni eneo ambalo linapatikana huko Damascus Syria. Ni eneo ambalo mateka wa Karbala waliwekwa hapo kwa muda kabla ya kuingia katika kasri ya Yazid. Sahl Sa’idi sahaba wa Mtume (s.a.w.w) amesimulia namna msafara wa mateka wa Karbala ulivyoingia katika Mlango wa Saa (Bab al-Sa’at) huko Damascus na ni kutokana na sababu hiyo hilo linasimuliwa katika fasihi ya Ashura.
Sababu ya Kupewa Jina Hilo
Bab al-Sa’at ulikuwa mlango mkubwa kuingilia katika Msikiti wa Umawiya huko Damascus ambapo juu yake kulikuwa na saa kubwa. Mlango huo ulikuwa ukijulikana pia kwa jina la Bab al-Jayrun. [1] Sababu ya kuitwa kwa jina la Bab al-Sa’at imetajwa kuwa ni kutokana na kuweko saa juu ya mlango huo. [2] Kadhalika vitabu vinavyohusiana na ripoti na nukuu za tukio la mateka wa Karbala huko Sham vimetaja humo Bab al-Sa’at. [3] Inaelezwa kuwa, Bab al-Sa’at hii ni tofauti na Bab al-Sa’at ya msikiti wa Umawiya Damascus na kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kiliwekwa hapo kabla ya kuingizwa katika kasri ya Yazid. [4] Kutokana na kuwa, mwaka 61 Hijria, msafara wa mateka wa Karbala waliwekwa kwa masaa kadhaa hapo, eneo hilo likaondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Bab al-Sa’at. [5]
Hata hivyo kuna kundi linaloamini kwamba, mateka wa Karbala waliingia Sham kupitia Bab Tuma. [6] Kuna wanaoamini pia kwamba, Bab al-Sa’at ndio uleule mlango wa Tuma (Bab Tuma) ambao unapatikana katika kitongoji ambacho wakazi wake ni Wakristo mjini Damascus na athari zake zimebakia. [7]
Ripoti ya Sahl Sa’idi
Imepokewa na Sahel Sa'idi kwamba wakati msafara wa mateka wa Karbala ulipoletwa Damascus, watu wa Damascus walikuwa wamekusanyika kwenye Mlango wa Saa (Bab al-Sa’at) na walikuwa wakisherehekea kwa kurukaruka na kupigiza miguu chini. [8] Sheikh Abbas Qomi ameripoti kutoka Kamil Baha'i kwamba, watu wa nyumba ya Imamu Hussein (a.s.) walikaa na kubakia kwenye mlango wa Damascus kwa muda wa siku tatu. [9]
Sahl Sa’idi ameripoti jinsi mateka walivyoingia katika mji wa Damascus kupitia Mlango wa Saa. Kulingana na yeye, vichwa vilivyokatwa vilikuwa kwenye mikuki na vilikuwa vikitembea pamoja na mateka, na Sakina, bintiye Imam Hussein, alimwomba awape kitu waliokuwa na mikuki ili wasogeze vichwa vya mashahidi mbele kidogo ya mateka, ili wasio maharimu wasiwaangalie wanawake na mabinti. [10] Ni kutokana na sababu hii ndio maana, katika maombolezo yanayohusiana na tukio la Ashura yakiwemo maombolezo ya kikao cha Yazid, imetajwa kuhusu Bab al-Sa’at.
Katika Mlango wa Saa katika msikiti wa Umawiya Damascus kuna jiwe kubwa ambalo inasemekana na la Habil na Qabil waliweka vichinjwa vyao juu yake. [11]
Fasihi na Utamaduni wa Kifarsi
Mlango wa Sa’at umetumika katika fasihi na mashairi ya Kifarsi. Neno hili limeashiriwa katika fasihi ya Ashura kuwa ni Mlango wa Damascus kutoka Halab na Kufa ambapo mateka wa Karbala waliowekwa hapo. [12]
Filamu ya Mfululizo
Mlango wa Saa ni jina la filamu ya mfululizo ya televisheni ambayo ina sehemu nne. Filamu hii ya mfululizo iliandikwa na kuongozwa na Sayyid Javad Hashimi. Filamu hii ya mfululizo inaelezea matukio ya kando ya mlango huo katika siku za kuingia mateka wa Karbala huko Sham. Filamu hii ya mfululizo ilionyeshwa katika Kanali ya Qur'ani ya Sauti na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. [13]
Rejea
Vyanzo