Nenda kwa yaliyomo

Aya ya al-Shura

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na Aya ya al-Shura (kushauriana). Kama unataka kujua kuhusiana na maudhui ya kutaka ushauri au mashauriano angalia Aya ya al-Mushawarah.
Aya ya al-Shura
Jina la AyaAya ya al-Shura
Sura HusikaShura
Namba ya Aya38
Juzuu25
Sababu ya KushukaKusifu Ada za Ansari katika Mashauriano
Mahali pa KushukaMadina
MaudhuiItikadi - Maadili
Mada YakeUmuhimu wa Kufanya Kazi za Umma na za Kiserikali kwa Kuzingatia Mashauriano
Aya Zinazofungamana NayoAya ya 159 ya Surat al-Imran, Aya ya 233 ya Surat al-Baqara


Aya ya al-Shura (Kiarabu: آية الشورى) (Surat al-Shura: 38) inabainisha moja ya sifa maalumu za Waislamu kama vile kukubali wito wa Mwenyezi Mungu, kushikamana na Sala, kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu na kushauriana. Kwa mujibu wa wafasiri, katika Aya hii kutaja kushauriana kando ya mambo kama kumuamini Mwenyezi Mungu na Sala, ni jambo linalotilia mkazo umuhimu wa kushauriana.

Kadhalika wanasema kuwa, katika Aya ya al-Shura kumebainishwa sifa muhimu kabisa za waumini ambazo ni kuitikia au kukubali mwito wa Mwenyezi Mungu wao ambapo kila mema na mazuri yamekusanyika humo. Kwa mtazamo wa wafasiri ni kuwa: Kuitikia mwito wa Allah katika Aya hii kuna maana ya kutekeleza amali zote njema na matendo mema ambayo Mwenyezi Mungu amemtaka mwanadamu ayatekeleze na kwamba, asipinge jambo lolote lile ambalo limekatawazwa na Mwenyezi Mungu.

Utambulisho, Andiko na Tarjumi ya Aya

Aya ya 38 katika Surat Shura ni muendelezo wa Aya za kabla yake ambazo zinabainisha sifa za waumini ambapo Aya hii inabainisha sifa nyingine kadhaa za waumini; mingoni mwazo ni kuitikia mwito wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha Sala, na kutoa na kwamba, mambo yao yanafanyika kwa kushauriana baina yao. [1] Allama Tabatabai anasema kuwa, Aya hii ni hoja juu ya kuwa muhimu suala la mashauriano na kushauriana katika jamii ya Kiislamu na kushauriana ni ishara ya kukua kiupeo wanadamu. Kwa mujibu wake ni kuwa, waumini wanapotaka kufanya jambo lolote huunda baraza la mashauriano ili kufikia katika maoni na mtazamo sahihi huomba ushauri kutoka kwa watu wenye akili. [2]

Wanaamini watafiti wa masuala ya kidini kwamba, Aya ya 38 ya surat Shura pamoja na Aya ya 159 katika Surat al-Imran zimepelekea kuweko suala la mashaurinao katika jamii na watu wote wamekuwa na hisa na mchango katika mchakato wa maamuzi. [3] Tabarasi sambamba na kunukuu hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika Tafsiri yake ya Maj’maa al-Bayan kuhusiana na kupata njia sahihi kupitia kuomba na kutaka ushauri, anaitambua Aya hii kwamba, ni hoja na dalili ya kuwa na fadhila suala la mashauriano na kuomba ushauri. [4]

وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَ‌بِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُ‌هُمْ شُورَ‌ىٰ بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَ‌زَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ


Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa.



(Surat Shura: 38)


Sababu ya kushuka

Fadhl bin Hassan Tabarsi, mmoja wa wafasiri wa Qur'ani katika karne ya 5 na 6 Hijria anasema kuwa, Aya ya 38 ya Surat Shura ilishuka ikiwahusu Ansar, ambao hata kabla ya Uislamu na kabla ya kuwasili kwa Mtume (s.a.w.w) huko Madina, walikuwa wakifanya mambo yao kwa mashauriano. Anasema kwamba Mungu amewasifu katika Aya hii. Vile vile imenukuliwa kutoka kwa al-Dhahhak bin Muzahim Hilali (aliyefariki mwaka 102 au 105 Hijiria), ambaye alikuwa ni mfasiri na mmoja wa tabiin [5] kwamba, Aya hii inazungumzia kundi miongoni mwa Ansari ambalo liliposikia kwamba Mtume (s.a.w.w) amedhihiri, walikusanyika katika nyumba ya Abu Ayyub Ansari kwa ajili ya kushauriana ambapo walimuamini Mtume (s.a.w.w) kabla ya kuhama kwake Makka na kwenda Madina na walimpa kiapo cha utii huko Aqaba. [6] Ayatullah Makarim Shirazi anaamini kuwa, licha ya kuwa kuna sababu kadhaa kuhusiana na kushuka Aya hii, lakini Aya hii, sio makhsusi tu kwa sababu hii ya kushuka kwake bali inabainisha ratiba ya umma na ya wote. [7]

Kujibu mwito wa Mwenyezi Mungu kuna maana gani?

Kwa mujibu wa Makarim Shirazi, katika Aya ya Shura, kumebainishwa sifa muhimu zaidi ya waumini ambayo ni kukubali na kuitikia mwito wa Mola wao Mlezi, ambamo kheri zote zimekusanywa humo. [8] Kwa mujibu wa wafasiri ni kuwa, kuitikia mwito wa Allah katika Aya hii kuna maana ya kutekeleza amali zote njema na matendo mema ambayo Mwenyezi Mungu amemtaka mwanadamu ayatekeleze na kwamba, asipinge jambo lolote lile ambalo limekatawazwa na Mwenyezi Mungu. [9] Kwa mujibu wa Allama Tabatabai ni kuwa, kuashiriwa ibada ya Sala kuwa miongoni mwa amali njema ni kwa sababu ya fadhila na heshima yake [10].

Umuhimu wa kushauriana katika maisha

Kubainisha na kuelezwa mashauriano miongoni mwa sifa za waumini [11] na kuwekwa katika safu na daraja moja na kumuamni Mwenyezi Mungu na Sala ni ishara ya wazi ya kuwa na umuhimu usio na kawaida suala la kushauriana. Kwa maana kwamba, inaonyesha ni jinsi gani suala hili lina umuhimu mkubwa. [12] Kwa mujibu wa Makarim Shirazi ni kuwa, msisitizo wa Qur'ani juu ya kufanya mambo kwa mashauriano ni kutokana na ukweli kwamba binadamu yeyote hata kama ana akili imara kiasi, yeye hutazama tu mwelekeo mmoja au zaidi katika masuala fulani na kughafilika na upande mwingine.[13]

Wajibu wa kutaka ushauri

Sayyd Muhammad Taqi al-Mudarrisi amesema katika tafsiri yake ya Min Huda al-Qur'an chini ya Aya ya Shura kwamba: Baadhi ya wahakiki wanaona kushauriana kuwa ni wajibu na wanaamini kwamba, mtawala wa Sheria, hata kama ni faqihi muadilifu, hatakiwi kutenda kwa mujibu tu anavyoona yeye katika kusimamia mambo ya jamii. Bali, ni wajibu kwake kutumia ujuzi na weledi wa wengine katika kufanya na kuendeleza mambo. Pia, kulingana na yeye, kushauriwa na watu mtawala kutakuwa ni mfano na kigezo cha wazi za mashauriano. Ayatullah Mudarrisi anaamini kwamba, kushauriana kutadhamini uhuru wa maoni na haki ya kuchagua. [14]

Rejea

Vyanzo