Aya ya Upanga
Jina la Aya | Upanga |
---|---|
Sura Husika | Tawba |
Namba ya Aya | 5 |
Juzuu | 10 |
Mahali pa Kushuka | Madina |
Maudhui | Itikadi |
Mada Yake | Kukabiliana na Washirikina |
Aya Zinazofungamana Nayo | Aya ya 5 ya Surat al-Hajj, Aya 29 ya Surat Tawba, Aya 190, 191 na 193 ya Surat al-Baqara |
Aya ya Upanga au Aya ya Vita (Kiarabu:آية السّيف أو آية القِتال) Ni Aya ya 5 ya Surat At-Tawba. Aya hii inawaamrisha Waislamu baada ya kumalizika kipindi cha miezi mine, kuwaua washirikina au kuwateka na kuzingira, isipokuwa kama watakubali kuingia katika dini ya Kiislamu. Kulingana na wafasiri wa Kishia na Kisunni, ni kwamba; Washirikina wanaokusudiwa katika Aya hii ni wale washirikina waliovunja mikataba yao walio wekeana na Waislamu wakati wa zama za bwana Mtume (s.a.w.w); hata hivyo, makundi ya Jihadi ya Wasalafia yanatumia Aya hii kwa ajili ya kuanzisha vita dhidi ya wengine.
Baadhi wanaihisabu Aya hii ya Upanga kuwa imekuja kufuta baadhi ya Aya zinazohusiana na; amani, jizya (gharama za fedha walipazo washirikina) na fidia. Kinyume chake, wengine wanaamini kwamba; Aya hii haikuja kufuta Aya yoyote ile; bali Aya hii kiasili ni yenye sabilio huru (Aammun au haikubanwa wala kufinywa kisheria), ila Aya inayofuatia ndiyo iliyokuja kuibana na kuifinya hukumu ya Aya hiyo, ambapo katika Aya iliyofuata Mwenyezi Mungu anamwamuru Mtume wake kuwapa amani baadhi ya washirikina kwa kumwambia: "Kama mmoja wa washirikina akikuomba hifadhi ili aje kusikiliza maneno ya Mwenye Enzi Mungu, mpe ruhusa na kisha umfikishe mahali penye amani naye (makazini mwake)".
Pia Aya 29 ya Surat At-Tawba na Aya 39 ya Surat Al-Hajj zimepewa jila la Aya za Upanga au Vita.
Utambuzi wa Dhana ya Aya
Aya ya Upanga au Vita ni Aya ya tano ya Surat At-Tawba. Kulingana na Aya hii, wachambuzi na wahakiki wa Qur’ani wamesema kwamba; Mnamo mwaka wa tisa wa Hijria, Waislamu waliamriwa ya kwamba, baada ya muda wa miezi mine kumalizika, wawe na msimamo mkali dhidi ya washirikina, nao msimamo wa ima kuwaua, kuwateka pamoja na kuwazingira.[1]
Kulingana na Aya hii, kama washirikina wataingia katika Uislamu kabla ya kumalizika muda uliowekwa, na kusimamisha (kutekeleza na kuziadhimu) ibada za Kiislamu ambazo muhimu zaidi kati yake ni sala na zaka, hilo litapelekea kuwa salama na hakutakuwa na tofauti ya kimiamala kati yao na Waislamu, na watapata haki zote wanazopata Waislamu wengine.[2] Maelezo ya kusimamisha sala na kutoa zaka katika Aya, yamechukuliwa kuwa ishara ya toba na kuwa na imani ya dini ya Kiislamu.[3] Makarim Shirazi, ambaye ni mfasiri wa Qur'an wa upande wa madhehebu ya Kishia, amesema kuwa; Dhahiri ya Aya hii ni kwamba, mambo manne haya yaluiotajwa katika Aya hii ambayo ni: "kufunga njia, kuzingira, kuwateka na kuwaua" si mambo ya hiari; bali ni mambo yanayo takiwa kutelezwa kwa mujibu hali, wakati, mahali, na watu husika, kwa hiyo kila moja kati ya mambo haya yatafaa kutekelezwa kwa kadri ya hali ilivyo.[4]
Wafasiri wa Qur’ani wana maoni tofauti kuhusiana na kwamba; ni miezi gani hasa mine inayokusudiwa kwenye Aya ya 5 ya Surat Al-Tawba. Baadhi yao wamesema miezi hiyo ni ile miezi mitakatifu.[5] Kinyume chake, wafasiri wengi wamedhania kuwa; Miezi hiyo mine ni miezi mingine kabisa, ambayo inaanzia tarehe tisa Dhul-Hijjah mwaka wa tisa Hijria hadi tarehe kumi Rabi' al-Thani mwaka wa kumi Hijria.[6]
Baadhi ya wanazuoni wa fiqhi, wakitegemea Aya ya Upanga (Aya ya Vita), wamemuhisabu apuzaye sala kuwa ni murtadi, na wakadai kuwa; ni wajib kuuawa. Hii ni kwa sababu ya kwamba; sala katika Aya hii, ni moja ya masharti yaliotajwa ambayo yanayozuia kuuawa kwa mshirikina.[7] Baadhi ya wafasiri, wameihisabu Aya ya 29 ya Surat At-Tawba,[8] [Maelezo 1] pamoja na Aya ya 39 ya Surat Al-Hajj [Maelezo 2] kuwa ni miongoni mwa Aya za Upanga na Vita.[9]
فَإِذَا انْسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدْتُمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ فَإِنْ تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ
Basi, itakapomalizika miezi mitukufu, waueni washirikina popote muwaonapo, na wakamateni, na wazungukeni, na waoteeni kila mahali pa kuvizia. Lakini wakitubu, wakasimamisha Sala na wakatoa Zaka, basi waacheni huru njia zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.
(Surat Tawba: Aya ya 5)
Vita na Washirikina Waliovunja Mkataba
Wafasiri wanaihisabu Aya hii kuwa ni Aya ianyo husiana na wale washirikina waliovunja mkataba yao katika zama za bwana Mtume (s.a.w.w), ambao walitiliana mikataba na Waislamu, kisha wakafanya khiana na walivunja ahadi zao.[10] Baadhi ya wafasiri wanasema kwamba washirikina walio kusudiwa hapa, ni wale wapangao njama na wale makafiri wenye kiu ya damu za Waislamu (Kafiru Harbiyyun).[11]
Imeelezwa ya kwamba; Rashid Ridha (aliyefariki: mwaka 1935 Miladia), ambaye ni mfasiri wa upande wa madhehebu ya Ahlus-Sunna, akielezea tafsiri ya Aya hii pamoja na Aya nyingine zinazohusiana na vita, ameihisabu Aya hii kuwa ni maalumu kwa ajili ya washirikina wa Makkah tu, ambao Mwenye Ezi Mungu amesisitiza juu ya uvunjaji wao wa ahadi zao mara kwa mara katika Aya za vita.[12] Muhammad 'Izzat Darwaza (aliyefariki: mwaka 1984 Miladia), ambaye ni mfasiri na mfafanuzi wa Qur'ani, anaamini kwamba; Walengwa wa hukumu za Aya za mwanzo za Surat At-Tawba, ni wale washirikina waliovunja mikataba yao, ambao pia wakati bwana Mtume alipokuwa akishiriki katika vita vya Tabuk, walikuwa wakipanga njama dhidi ya Waislamu.[13] Kwa mtazamo wa baadhi ya wafasiri, ni kwamba; Aya hii ya upanga imekuja kufuta idadi ya Aya 124 zinazorejelea suala la msamaha, amani na fidia zilipwazo na washirikina. Kwa imani yake; Kusema kwamba Aya hizi zinahusiana na washirikina wote duniani, huwa ni kulazimisha maana ambayo muktadha wa Aya hizi haziwezi kubeba maana ya dhana hizo.[14]
Baadhi ya watafiti wamesema kuwa; Aya ya 5 ya Surat At-Tawba inatumiwa na vikundi vya Jihadi vya Wasalafia kwa ajili ya kuanzisha jihad (Jihadi ibtida-i).[15] Wao wanaona kuwa; Aya hii imekuja kumefuta Aya zote zile zinazo husiana na masuala ya amani pamoja na msamaha, na kwamba maana ya washirikina katika Aya hii, ni makafiri wote, wapiganaji (wenye kiu ya damu za Waislamu), ambao kiistilahi huitwa “Kaafiru Harbiyyun” na wasiopiganaji (wasio na kiu ya damu za Waislamu), ambao huitwa “Kaafiru Ghairi Harbiyyun”.[16] Kinyume chake, wafasiri wa madhehebu mengine wamesema kwamba; Hiyo si tafsiri sahihi na ufasiri wa aina hiyo wa kuwalazimisha watu waikubali dini kwa mabavu kupitia Aya hii, kunapelekea kuharibu sura ya Uislamu, jambo ambalo limeacha athari mbaya katika kuzielewa itikadi za Waislamu.[17]
Kufuta au Kufutwa kwa Aya
Kwa mtazamo wa baadhi ya wafasiri wa Qur’ani, ni kwamba; Aya ya upanga imekuja kufuta Aya zipatazo 124 zinazorejelea masuala ya msamaha, amani na fidia watoazo washirikina.[18] Wengine wameona kuwa Aya hii imefutwa kupitia Aya za msamaha na amani.[19] Kwa mtazamo wa wafasiri wengine, ni kwamba; Aya ya Upanga pamoja na Aya ya 4 ya Surat Muhammad ambazo inahusiana na masuala ya kuchukua fidia kutoka kwa washirikina, hazifutani bali Aya zote mbili ni Aya thabiti ziendeleazo kufanya kazi; kwa sababu pale bwana Mtume alipokuwa akikabiliana na washirikina maishani mwake, baadhi ya wakati alikuwa akiamrisha vita, na pia baadhi ya wakati alikuwa akitoa amri ya msamaha na kupokea fidia kutoka kwa washirikina hao.[20]
Baadhi ya wafasiri wamehusisha Aya hii na Aya inayofuata baadha yake.[21] Katika Aya inayofuata, Mwenye Ezi Mungu anamwamuru Mtume wake kwa kumwambia kwamba; “Ikiwa mmoja wa washirikina ataomba hifadhi kutoka kwako (ili asikie neno la Mwenyezi Mungu), basi mpe ruhusa na kisha umfikishe mahali penye amani naye”.[22] [Maelezo 3] Rashid Ridha (aliyefariki: mwaka 1935 Miladia), ambaye ni mfasiri kutoka upande wa madhehebu ya Ahlu-Sunna, anaamini kwamba; Aya hii imekuja kuifinya Aya ya iliopita ya Suratu Al-Tawba, hii ni kwa sababu ya kwamba; baadhi ya washirikina hawajalisikia neno la Mwenye Ezi Mungu, na bado hawajafikiwa na wa dini ya Allah kikamilifu. Hiyo ndiyo iliyo mfanya Mwenye Ezi Mungu kuacha njia ili haki na ukweli uweze kuwafikia, ambapo Mwenye Ezi Mungu amewavua washirikina wa hii kutoka katika ile hukumu iliokuja mwanzo.[23]
Wengine wamesema kuwa kufutwa kwa Aya ya Apanga hakuwezi kukubalika; kwa sababu Aya ya 29 ya Surat At-Tawba, ilishuka baada ya Aya hii ambayo inadaiwa kuwa ni yenye kufuta huku ya Aya ya Surat Al-Tawba.[24]
Maelezo
- ↑ قَاتِلُوا الَّذِینَ لَا یُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْیَوْمِ الْآخِرِ وَلَا یُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَلَا یَدِینُونَ دِینَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِینَ أُوتُوا الْکِتَابَ حَتَّیٰ یُعْطُوا الْجِزْیَةَ عَنْ یَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ ; Piganeni na wale wasio mwamini Mwenye Ezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharamishi aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaifuati Dini ya Haki, miongoni mwa Watu wa Kitabu mpaka watoe jizya (walipe gharama) kwa mkono na hali ya unyonge.
- ↑ أُذِنَ لِلَّذِینَ یُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ عَلَیٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِیرٌ ; Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa, na hakika Mwenye Ezi Mungu ni Mwenye nguvu ya kuwapa ushindi.
- ↑ وَإِنْ أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِکِینَ اسْتَجَارَکَ فَأَجِرْهُ حَتَّیٰ یَسْمَعَ کَلَامَ اللَّهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذٰلِکَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا یَعْلَمُونَ ; Na kama mmoja wa washirikina akikuomba hifadhi, basi mpe hifadhi ili asikie neno la Mwenye Ezi Mungu; kisha umfikishe mahali penye amani naye. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiofahamu.
Rejea
- ↑ Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 152.
- ↑ Mughnīya, Tafsīr al-Kāshif, juz. 4, uk. 12.
- ↑ Bayḍhāwi, Anwār al-tanzīl, juz. 3, uk. 71.
- ↑ Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nemūne, juz. 7, uk. 292.
- ↑ Ḥāshimī Rafsanjānī, Tafsīr-i Rāhnamā, juz. 7, uk. 16; Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 21, uk. 33.
- ↑ Ṭabrasī, Majmaʿ al-bayān, juz. 5, uk. 12; Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 151.
- ↑ Istrambadi, Ayat al-Ahkam, Maktabat al-Maarij, juz. 1, uk. 249.
- ↑ Khuī, al-Bayān, uk. 286.
- ↑ Markaz-i Iṭṭilāʿāt wa Madārik-i Islāmī, Farhangnāme ʿulūmi Qurʾānī, juz. 1, uk. 415.
- ↑ Kāshifī, Tafsīr Ḥusseinī, uk. 398; Fayḍh al-Kāshānī, Tafsīr al-Ṣāfī, juz. 2, uk. 322; Sharīf Lahījī, Tafsīr Sharīf lahījī, juz. 2, uk. 227; Bayḍhāwi, Anwār al-tanzīl, juz. 3, uk. 71.
- ↑ Qurashī, Tafsīr-i aḥsan al-ḥadīth, juz. 4, uk. 188.
- ↑ Ārmīn, Jaryān-hā-yi tafsīrī-yi muʿāṣir, uk. 140.
- ↑ Ārmīn, Jaryān-hā-yi tafsīrī-yi muʿāṣir, uk. 395.
- ↑ Ārmīn, Jaryān-hā-yi tafsīrī-yi muʿāṣir, uk. 395.
- ↑ Luṭfī, «Naqd-i dīdgāh-i Salafīyya-yi jahādī darbāra-yi jahād-i ibtidāʾī bā tikya bar āya-yi 5 sūra-yi Tawba», uk. 35.
- ↑ Luṭfī, «Naqd-i dīdgāh-i Salafīyya-yi jahādī darbāra-yi jahād-i ibtidāʾī bā tikya bar āya-yi 5 sūra-yi Tawba», uk. 35.
- ↑ Shāyiq, «Ḥalli taʿāruḍhi dhāhirī bayna āyāti Sayf wa Nafyi ikrāh wa taʾthīri ān dar masʾala-yi āzādī dar intikhāb-i dīn, uk. 82.
- ↑ Suyūṭī, al-Itqān, juz. 2, uk. 51; Jazāʾirī, ʿUqūd al-marjān, juz. 2, uk. 288.
- ↑ Naḥḥās, al-Nāsikh wa al-mansūkh, uk. 493.
- ↑ Shāh ʿAbd al-ʿAdhīmī, Tafsīr ithnā asharī, juz. 5, uk. 22.
- ↑ Rashīd Riḍhā, Tafsīr al-manār, juz. 10, uk. 159.
- ↑ Surat Tawba: Aya ya 6.
- ↑ Rashīd Riḍhā, Tafsīr al-manār, juz. 10, uk. 159.
- ↑ Shāyiq, «Ḥalli taʿāruḍhi dhāhirī bayna āyāti Sayf wa Nafyi ikrāh wa taʾthīri ān dar masʾala-yi āzādī dar intikhāb-i dīn, uk. 81.
Vyanzo
- Ārmīn, Muḥsin.Jaryān-hā-yi tafsīrī-yi muʿāṣir. Tehran: Nashr-i Ney, 1396 Sh.
- Astarābādī, Mīrzā Muḥammad bin ʿAlī. Āyāt al-aḥkām. Tehran: Maktabat al-Miʿrājī, [n.d].
- Bayḍhāwi, ʿAbd Allāh bin ʿUmar. Anwār al-tanzīl wa asrār al-taʾwīl. Chapa ya kwanza. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1418 AH.
- Fayḍh al-Kāshānī, Muḥammad bin al-Murtaḍā al-. Tafsīr al-Ṣāfī. Mhakiki: Ḥussein Aʿlamī. Chapa ya pili. Tehran: Maktabat al-Ṣadr, 1415 AH.
- Ḥāshimī Rafsanjānī, Akbar. Tafsīr-i Rāhnamā. Qom: Būstān-i Kitāb, 1386 Sh.
- Jazāʾirī, Niʿmat Allāh bin Abd Allāh al-. ʿUqūd al-marjān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Nūr-i Waḥy, 1388 Sh.
- Kāshifī, Ḥussein bin ʿAlī. Tafsīr Ḥusseinī. Saravan: Kitābfurūshī-yi Nūr, [n.d].
- Khuī, Abū l-Qāsim. Al-Bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Muʾassisa-yi Iḥyā-yi Āthār-i Āyatullāh Khuī, 1430 AH.
- Luṭfī, ʿAlī Akbar. Naqd-i dīdgāh-i Salafīyya-yi jahādī darbāra-yi jahād-i ibtidāʾī bā tikya bar āya-yi 5 sūra-yi Tawba. In Sirāj-i Munīr 27 (1396 Sh).
- Markaz-i Iṭṭilāʿāt wa Madārik-i Islāmī. Farhangnāma-yi ʿulūm-i Qurʾānī. Qom: Pazhūhishgāh-i ʿUlūm wa Farhang Islāmī, 1394 SH.
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1371 Sh.
- Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Tafsīr al-Kāshif, Qom: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1424 AH.
- Naḥḥās, Abū Jaʿfar Aḥmad bin Muḥammad. Al-Nāsikh wa l-mansūkh. Kuweit: al-Falāḥ, 1408 AH.
- Najafī, Muḥammad al-Ḥassan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
- Qurashī, Sayyid ʿAlī Akbar. Tafsīr-i aḥsan al-ḥadīth. Chapa ya tatu. Tehran: Bunyād-i Biʿthat, 1375 Sh.
- Rashīd Riḍā, Muḥammad. Tafsīr al-manār. Egypt: al-Hayʾat al-Miṣrīyya al-ʿĀmma li l-Kitāb, 1990.
- Shāh ʿAbd al-ʿAẓīmī, Ḥussein. Tafsīr ithnā asharī. Tehran: Mīqāt, 1363 Sh.
- Sharīf Lahījī, Muḥammad b. ʿAlī. Tafsīr Sharīf lahījī. Mhakiki: Jalāl al-Dīn Ḥussein Armawī. Tehran: Intishārāt-i Dād, 1373 Sh.
- Shāyiq, Muḥammad Riḍhā. Ḥalli taʿāruḍ-i dhāhirī bayna āyāti Sayf wa Nafy-i ikrāh wa taʾthīr-i ān dar masʾala-yi āzādī dar intikhāb-i dīn. In Pazhūhishnāma-yi Tafsīr-i Kalāmī-yi Qurʾān 9 (1395 Sh).
- Suyūṭī, Jalāl al-Dīn al-. Al-Itqān fī ʿulūm al-Qurʾān. Egypt: al-Hayʾat al-Miṣrīyya al-ʿĀmma li l-Kitāb, 1415 AH.
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥussein al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
- Ṭabrasī, Faḍhl bin al-Ḥassan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Naṣir Khusruw, 1372 Sh.