Nenda kwa yaliyomo

Aya ya Istirja’a

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Aya ya "Istirja’a")

Aya ya Istirja’a (Kiarabu: آية الاسترجاع): Ni Aya 156 ya Surat al-Baqara ambayo inaashiria kurudi kwa watu mbele ya Mwenyezi Mungu. Aya hii inatajwa kuwa ni sunna iliyopendekezwa kusomwa wakati wa kufikwa na msiba na taabu fulani. Katika tafsiri za Kishia, kama vile Tafsir Tibiani na Majma’a al-Bayani, Aya hii imetajwa kuwa ni moja ya ishara mwanadamu kukiri utumwa na utiifu wake mbele ya Mwenye Ezi Mungu na kuamini Siku ya Kiyama.

Ayatullahi Tabatabai katika kitabu chake Tafsir al-Mizan pia amezungumza juu ya maana ya Aya hii, ambapo amesema kuwa; ikiwa mtu anajua kuwa umiliki halisi ni wa Mwenye Ezi Mungu, na kuelewa kwamba umiliki wa mwanadamu ni umiliki wa sura nje tu, basi kule yeye kuwa na kipato au kumilki kitu fulani, hakutasababisha yeye kuwa na furaha na kiburi, wala kupoteza kitu fulani hakutasababisha yeye kuwa na majuto na huzuni.

Kulingana na Hadithi zilizonakiliwa na Allama Hilli na Ibn Shahrashub katika vitabu vyao, Aya ya Istirja’a iliteremshwa baada ya Imam Ali (a.s) kuitamka ibara ya «إنا لله و إنا الیه راجعون ; Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji'un» ambayo maana yake ni: (Hakika sisi ni wa Mwenye Ezi Mungu na bila shaka tutarejea kwake). Baada ya yeye kusema maneno hayo, Mwenye Ezi Mungu akateremsha Aya hiyo.

Kulingana na Riwaya kutoka Imamu Swadiq (a.s), mtu atakaye soma Aya ya Istirja’a wakati wa kufikwa na msiba, atakuwa ni miongoni mwa watu watakaoingia Peponi. Fadhlu bin Hassan Tabarsi katika kuifasiri Aya ya Istirja’a ameashiria moja ya Riwaya ambapo kulingana nayo, Mwenyezi Mungu hulipa fidia juu ya maafa ya wale ambao wanafanya Istirja’a pale wafikwapo na misiba. Kufanya kwao hivyo kunaashiria kuwa; pale wao wafikwapo na misiba wanakumbuka ya kwamba, wao wanatoka kwa Mwenye Ezi Mungu na pia wanarejea kwake.

Matini ya Aya na Tafsiri Yake

Aya ya 156 ya Surat al-baqara ni Aya inayo mtambulisha mwanadamu kuwa ni kiumbe atokaye kwa Mwenye Ezi Mungu na hatima yake ni kurejea kwa Mola wake ambayo kiumaarufu inajulikana kwa jina la Aya ya Istirja’a.

Matini ya Aya hii pamoja na tafsiri yake ni kama ifuatavyo:

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

Wale ambao pale wafikwapo na msiba fulani, husema: Hakika sisi ni wa Mwenye Ezi Mungu, na bila shaka hatima yetu itakuwa ni kurejea kwake yeye.



Maana na Uchambuzi wa Aya

Faidhu al-Kashani, mfasiri wa karne ya kumi na moja Hijiria, katika tafsiri yake ya Safi, akitegemea moja ya Hadithi ameelezea maana ya neno “msiba” lililoko katika Aya ya Istirja’a, akisema kwamba; makusudio yaliokususiwa kupitia neno hilo, ni jambo lolote lile linalomdhuru Muumini. [2] Sheikh Tusi, mfasiri wa karne ya tano Hijiria katika tafsiri ya Tibyan na Fadhilu bin Hassan Tabari, miongoni mwa wafasiri wa upande wa madhehebu ya Shia wa karne ya sita Hijiria, katika tafsiri ya Majma'ul Bayan, wameeleza Aya ya Istirja’a wakisema kuwa; Aya hii ina maana kadhaa, ikiwa ni pamoja na kukiri utumwa mbele ya Mwenye Ezi Mungu na kuamini siku ya hukumu, na kuisoma Aaya hii katika wakati wa msiba na taabu fulani, huwa na maana ya kukubali na kuridhika na maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu. [3]

Fadhlu bin Hassan Tabari katika kutoa tafsiri Aya ya “Istirja’a” aliashiria moja Hadithi, ambayo kulingana nayo, Mwenye Ezi Mungu atafia misiba ya wale wanaofanya Istirja’a, (wasemao innaa lillahi wa innaa ilaihi raajiuna), yaani yeye huwafidia kwa kwapa maisha bora ya Akhera, wale ambao pale wafikwapo na msiba fulani, huwa wanakumbuka ya kwamba: wao ni wa Mwenye Ezi Mungu na hatima yao ni kurudi kwake. [4] Pia amenukuu Hadithi kutoka kwa Imamu Ja'afar al-Sadiq (a.s) ambayo kwa mujibu wake ni kwamba; wale wanaofanya “Istirja’a” wakati wanapo fikwa na msiba, ni moja miongoni mwa makundi manne yatakayo ingia peponi. [5] Katika Hadithi fulani Imamu Ali (a.s), ameieleza Aya ya Istirja’a akisema kwamba: Pale tunaposema Inna lillahi tunamaanisha kuwa sisi tumekiri ya kwamba; sisi ni mali ya Mwenye Ezi Mungu na yeye ndiye mmiliki wetu, na tunaposema Inna ilayhi raaji'una, tunamaanisha kuwa sisi tumekiri ya kwamba; sisi si wa kudumu duniani hapa na hatima yetu ni kio. [6] Sababu ya sentensi hii kuitwa Istirja’a inatoka na kule sentensi kuwa ndio sentesi ilioko katika kipengele cha pili ambayo husomeka: Inna ilayhi raaji'una yenye maana ya kukiri kurudi kwa Mwenye Ezi Mungu.

Allama Tabatabai katika tafsiri ya al-Mizan akieleza kuhusiana na maana ya Aya ya Istirja’a amesema kwamba; ikiwa mwanadamu atajua ya kwamba umiliki halisi na wa kweli ni wa Mwenye Ezi Mungu peke yake, na kwamba ule umiliki wa mwanadamu ni umiliki bandia na dhahiri tu, basi hata kama yeye atakuwa kipato cha kumiliki kitu fulani, hilo halitamfanya yeye kuwa na furaha na kiburi, wala iwapo yeye atapoteza kitu fulani, hilo halitapelekea yeye kuwa nahuzuni katika hisia zake. [7] Tabatabai amenukuu kutoka kwa mwalimu wake Sayyid Ali Qadhi ya kwamba; mwalimu wake huyo ili kuondoa hisia ya matamanio ya nafsi, alipendekeza njia ya kujiunguza ili kuondoa matamani hayo na nia za ubinafsi zilizoko ndani ya nafsi ya mwanadamu, na akasema kwamba; ubunifu aliupata kutoka kwenye Aya za Qur'an Tukufu, kama vile Aya ya Istirja’a. Katika njia hii, mja ambaye ni msafiri aelekeaye kwa Mola wake, hushikamana na fikra zinazo msindikiza katika kuelewa ya kwamba; kila kitu ni mali kamili ya Mwenye Ezi Mungu na yeye kiuhalisia ni kiumbe mwenye umaskini asilia, na fikra hizi hupelekea kuungua kwa sifa zake zote za matamanio zilizoko nafsi mwake, na hii ndiyo sababu ya fikra hizo kuitwa za kuunguza. [8]

Istihbabu (Mapendekezo) ya Kisheria

Kulingana na Shahid Thani, mwanachuoni wa Kishia katika karne ya nane Hijri, kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kusema: Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji'un wakati wa msiba ni Mustahabb (amali inayopendekezwa)[9] na kuna riwaya nyingi zinazosisitiza kwamba Mtume (s.a.w.w) na Maasumina wametuhimiza kusema istirja wakati wa msiba.[10] Kulingana na Sahib al-Jawahir, mwanachuoni wa Kishia katika karne ya kumi na tatu Hijri, kusema istirja wakati wa mazishi pia ni Mustahabb.[11]

Asili ya Kuteremka kwa Aya ya Istirja’a

Kulingana na Hadithi iliyo nukuliwa na Allama Hilli katika kitabu chake Nahju al-Haqqi na Kashf al-Sidqi kuhusiana na asili ya kuteremka kwa Aya ya Istirja’a, ni kwamba; Imam Ali (a.s) ndiye mtu wa kwanza aliye fanya Istirja’a hata kabla ya kuteremka kwa Aya ya Istirja’a. Kwa mujibu wa Hadithi yeye alifanya hivyo baada ya kupata habari ya kuuawa kwa ami yake Hamza, na baada ya kitendo chake hicho, Mwenye Ezi Mungu ndipo alipo ishusha Aya ya Istirja’a. [12] Pia kulingana na Riwaya nyingine iliyo nukuliwa na Ibn Shahrasub, mwanahadithi na mfasiri wa Kishia katika karne ya sita Hijri katika kitabu chake Manaqib Aal Abi Talibi ni kwamba; baada ya bwana Mtume (s.a.w.w) kumfikishia Imamu Ali (a.s) habari za kuuawa kwa Ja'far bin Abi Talib katika Vita vya Muutah, Imamu Ali (a.s) alisema: «Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji'un» na baada ya hapo Aya ya Istirja’a ikashuka. [13]

Vyanzo

  • Faiḍh al-Kāshānī, Muḥammad b. al-Murtaḍā al-. Tafsīr al-Ṣāfī. Edited by Ḥusayn Aʿlamī. Second edition. Tehran: Maktabat al-Ṣadr, 1415 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Nahj al-ḥaq wa Kashf al-ṣidq. Beirut: Dār al-Kitāb al-Lubnānī, 1982.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: ʿAllāma, 1379 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Edited by ʿAbbās Qūchānī & ʿAlī Ākhūndī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Shahīd al-Awwal, Muḥammad b. Makkī. Al-Dhikrā al-shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa. Qom: 1419 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1390 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1408 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Aḥmad Qaṣīr al-ʿĀmilī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].