Nenda kwa yaliyomo

Alayhi al-Salam

Kutoka wikishia
Picha yenye ibara ya Alayhi al-salam

Alayhi al-Salam (Kiarabu: عليه‌ السلام) ni ibara ya kidua na ya kiheshima ambayo ina maana ya “amani iwe juu yake”. Ibara hii huja baada ya kutajwa majina ya Maimamu, Mitume, baadhi ya watoto wa Maimamu na baadhi ya Malaika.

Ili kuidhinisha kuwatumia salamu na kuwaombea amani Maimamu na waumini, zinatumiwa Aya za 157 katika Surat al-Baqara, 143 katika Surat al-Ah’zab na 54 katika Surat al-An’am kama hoja ya hilo ambazo ndani yake waumini wote wametumiwa salama na dhikri ya kumsalia Mtume. Shahidi Thani aliamuru kuandikwa Alayhi al-Salaam (amani iwe juu yake) baada ya jina la Maimamu katika adabu za uandishi wa elimu za Kiislamu.

Waislamu wa madhehebu ya Ahlu-Sunna, wao baada ya jina la Maimamu wa Kishia hutumia ibara kama wanayotumia kwa masahaba yaani "Radhiallah Anhu" (Radhi za Allah ziwe juu yake) au Mungu awe radhi naye”. Hata hivyo kuhusiana na Imamu Ali (a.s) wametumia ibara ya (Alayhi al-Salam) na hawajaitumia ibara hiyo kwa makhalifa wengine. Pamoja na hayo, Ibn Kathir, mmoja wa wanafunzi wa Ibn Taymiyyah, anaamini kwamba, haistahiki kulijaalia hilo kuwa maalumu kwa Imamu Ali na kutolitaja kwa makhalifa wengine.

Waislamu wa madhehebu ya Shia wakiwa na nia ya kuonyesha heshima kwa wanawake kama Fatima al-Zahra (a.s), Zainab (a.s) na Bibi Khadijah (a.s), badala ya kutumia “Alayhi al-Salam” wanatumia ibara ya “Alayha al-Salam” au “Salamullahi Alayha” na kwa ajili ya Mtume wanatumia ibara ya “swalallah alayhi waalih (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake pamoja na aali zake). Ibara ya “Alayhi al-Salam” inatumika pia kwa sura ya ufupisho ambayo ni (a) au (a.s) na ufupisho wa ibara ya salamullah Alayha ni (s) au (s.a) na ufupisho wa ibara ya Swalallah alayhi waalih ni (s.a.w) au (s.a.w.w).

Matumizi na ibara inayoshabihiana

Alayhi al-Salam ni ibara ya kidua na ya kiheshima ambayo ina maana ya “amani iwe juu yake”. Ibara hii huja baada ya kutajwa majina ya Maimamu, Mitume, [1] baadhi ya watoto wa Maimamu kama Abul Fadhl al-Abbas (a.s), [2] Ali Akbar (a.s), [3] na Ali Asghar (a.s) [4] na baadhi ya Malaika kama Jibril (a.s). [5]

Wakati inapokuwa kwamba, idadi ya Maimamu au Mitume waliotajwa ni wawili, hutumika ibara ya "Alayhima-as-salam"; Amani iwe juu ya hao wawili" [6] na wanapokuwa ni zaidi ya watu wawili hutumika ibara ya "Alayhimu al-Salam; amani iwe juu yao". [7] Hii ni kutokana na muundo wa lugha ya Kiarabu. Waislamu wa madhehebu ya Shia baada ya kutajwa jina la mmoja wa Maimamu (a.s) hutumia pia ibara zingine zisizokuwa Alayhi al-Salaam kama vile: Salamullahi Alayh, swalawatu-Allah alayh, [8] alayih-e-swalata-wa-salam, [9] na ibara kama “Alayih-e-afdhal-lu-swalat was-salaam” na Alayh Aalaf al-Tahhiyyah wa Al-Thanna. [10]

Baada ya kutaja majina ya wanawake na mabinti wa Ahlul-Bayt (a.s) [11] kama: Fatima (a.s), [12] Zaynab (a.s), [13] Maasuma (a.s) [14] na baada ya jina la Bibi Khadija, mke wa Mtume (s.a.w.w), [15] Maryam, mama yake Nabii Issa [16] na Asia mke wa Firauni [17] hutumika ibara za Salamullahi alayha au Alayha al-Salam. "Amani ya Mungu iwe juu yake" au "Alayha al-Salam". Kwa Mtume inatumika ibara ya ibara ya Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam Amani ya Mungu iwe juu yake na familia yake” badala ya Alayhi al-Salam.[18]

Waislamu wa Kisunni pia wakiwa na lengo la kuonyesha heshima na taadhima kwa Mitume [19] na baadhi ya malaika [20] hutumia neno au ibara ya Alayhi al-Salam; lakini kwa Maimamu wa Shia, kama ilivyo kwa masahaba wengine hutumia “Radhiallah Anhu (r.a); [21] isipokuwa kwa Imam Ali (a.s), ambaye kwake wanatumia ibara ya Karamma Allahu Wajha (Mwenyezi Mungu ameutukuza uso wake). [22] Pia, katika vitabu vya Kisunni, mara nyingi baada ya jina la Imam Ali (a.s), neno ``Alayhis Salam limetajwa. [23] Ibn Kathir mwandishi wa historia na mfasiri wa Ahlu-Sunna [24] na Muhammad Saleh al-Munajjid msomi na mwanazuoni wa Kisalafi, [25] wanaamini kwamba, kutumiwa ibara ya Alayhi Salam baada ya jina la Imam Ali (a.s) katika vitabu vya Ahlu-Sunna kulifanywa na waandishi na kwamba, hilo halikufanywa na wasomi na wanazuoni.

Baada ya jina la Mtume (s.a.w.w), Masunni hutaja ibara ya swalallah alayh wasallam [26] na wakati mwingine hutumia “Swallallah alayhi waalih wasallam” [27] na wakati mwingine hutumia ibara ya “Alayhi Salam”. [28]

Kwa mujibu wa nakala iliyoandikwa kwa mkono ya Kitab al-Irshad, kilichoandikwa mwaka wa 566 Hijiria, ibara ya Alayhi al-Salam ilikuwa ikitumika kwa Maimamu (a.s). [29]

Hukumu na falsafa yake

Shahidi Thani fakihi na mwanazuoni wa Kishia wa karne ya 10 Hijiria aliamuru kuandikwa Alayhi al-Salaam (amani iwe juu yake) baada ya jina la Maimamu katika adabu za uandishi wa elimu za Kiislamu. [30] Kwa mujibu wa Fakhr al-Muhaqqin ni kwamba, Maulamaa wa Kishia wanasema kuwa inajuzu kuwatumia salamu za amani waumini wote; [31] hata hivyo kwa mtazamo wake ni kwamba, ni bora na ni karibu zaidi na adabu kutuma salamu na kumtakia amani Mtume na Maimamu na kulifanya hilo kuwa maalumu kwao na lisitumike hilo kwa ajili ya waumini wengine. [32]

Kwa upande mwingine, Ibn Kathir, mmoja wa wanafunzi wa Ibn Taymiyyah [33] na Abdul Aziz bin Baz, mufti wa Kiwahabi, [34] wanaona haifai na haistahiki kulifanya hilo kuwa maalumu na mahususi kwa Imam Ali na kutolitaja kwa Makhalifa wengine (kama ambavyo imeenea katika baadhi ya vitabu vya Ahlu-Sunna).

Ili kuidhinisha na kujuzisha kuwatumia salamu na kuwaombea amani Maimamu na waumini, zinatumiwa Aya za 103 katika Surat al-Tawba, [35] 157 al-Baqarah, 143 katika Surat al-Ah’zab na 54 katika Surat al-An’am kama hoja ya hilo ambazo ndani yake waumini wote wametumiwa salama na dhikri ya kumsalia Mtume. [36] Kadhalika Aya ya “سَلَامٌ عَلیٰ اِلْ یاسِینَ” [37] kwa mujibu wa tafsiri [38] na hadithi [39] ni kuwa, makusudio ya Aal Yasin ni Aal Muhammad. [40]

Kuhusu kuruhusiwa kutuma salamu na kuwaombea amani Mitume, zimetumiwa Aya za Qur’an kama hoja kwamba, salamu zimetumwa kwa Mitume wote kwa sura jumla [41] na kwa baadhi ya Mitume kwa majina [42] [43]. Hata hivyo katika kitabu cha Amali cha Sheikh Swaduq [44] na Amali cha Sheikh Tusi [45] imekokotezwa kwamba, baada ya kutajwa jina la mmoja wa Mitume, awali salamu na amani zitumwe kwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) na kisha juu ya Mtume huyo. Katika hadithi inayofanana na hiyo, katika kitabu cha Wasail al-Shia imekokotezwa kwamba, awali salamu na amani zitumwe kwa Mtume (s.a.w.w) na aali zake kisha kwa Mtume huyo. [46] Baadhi ya Maulamaa wa Kishia baada ya kutajwa majina ya Mitume wanatumia ibara ya Ala Nabiyyina waalih Waalayh Salam. [47]

Rejea

Vyanzo

  • Anwarī, Ḥasan. Farhang-i buzurg-i sukhan. Tehran: Intishārāt-i Sukhan, 1390 Sh.
  • Dihkhudā, ʿAlī Akbar. Lughatnāma. Edited by Akram Sulṭānī and others. Tehran: Dānishgāh-i Tehrān, 1385 Sh.
  • Fakhr al-Muḥaqqiqīn, Muḥammad b. Ḥasan. Īḍāḥ al-fawāʾid fī sharḥ ishkālāt al-qawā'id. Edited by ʿAlīpanāh Ishtihārdī and others. Qom: Ismāʿīlīyān, 1387 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). 3rd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Furāt al-Kūfī, Abu l-Qāsim Furāt b. Ibrāhīm. Tafsīr furāt al-kūfī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tafṣīl wasāʾil al-Shīʿa ilā taḥṣīl masā'il al-sharī'a. 1st edition. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1409 AH.
  • Ibn Ḥajar al-Haytamī, Aḥmad b. Muḥammad. Al-fatāwā l-ḥadīthiyya. [n.p]. Dār al-Fikr, [n.d].
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Edited by Sāmī b. Muḥammad Salāma. 2nd edition. [n.p], 1420 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1380 Sh.
  • Mazāhirī, Ḥusayn. Mazhar-i ḥaqq. Qom: Muʾassisa-yi farhangī muṭāliʿī al-Zahrā (a), 1388 Sh.
  • Munajjid, Muḥammad Ṣāliḥ al-. Mawqiʿ al-Islām suʾāl wa jawāb. [n.p]. 1431 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Beirut: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1416 AH.
  • Muḥammadī Reyshahrī, Muḥammad. Dānishnāmah-yi Amīr al-Muʾminīn. Translated by Javād Muhaddithī and Mahdī Mihrīzī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1389 SH.
  • Muḥammadī Reyshahrī, Muḥammad. Guzīda-yi shahādatnāmah-yi Imām Ḥusayn (a) bar pāya-yi manābiʿ-i muʿtabar. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1391 Sh.
  • Mūjāhid b. Jabr, Abū l-Ḥajjāj Qurashī Makhzūmī. Tafsīr Mūjāhid. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Salām Abu l-nīl. Egypt: Dār al-Fikr al-Islāmī al-Ḥadītha, 1410 AH.
  • Nizām Aʿraj Neyshābūrī, Sharh al-nazzām ʿalā al-shāfiya. Edited by Muḥammad Zakī Jaʿfarī. Qom: Dār al-Ḥujja li-l-Thiqāfa, [n.d].
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. Tehran: Kitābchī, 1376 Sh.
  • Ṣāfī Gulpāyigānī, Luṭf Allāh. Muntakhab al-athar fī al-Imām al-thānī ʿashar. Qom: Maktabaṭ Āyat Allāh al-Ṣāfī al-Gulpāyigānī, 1422 AH.
  • Ṣāfī Gulpāyigānī, Luṭf Allāh. Silsila mabāḥith-i imāmat wa mahdawīyyat. Qom: Daftar-i Nashr-i āthār-i Āyat Allāh Ṣāfī Gulpāyigānī, 1391 Sh.
  • Sāniʿī, nayyīra sādāt. Pāsukh bih shubahāt dar shabhāy-i Pishāwar. Tehran: Mashʿar, 1385 Sh.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Munyat al-murīd fī adab al-mufīd wa l-mustafīd. Qom: Maktab al-Aʿlām al-Islāmī, 1415 AH.
  • Subḥānī Tabrīzī, Jaʿfar. Āʾīn-i wahhābiyat. Tehran: Mashʿar, 1386 Sh.
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Qom: Maktabaṭ Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1408 AH.
  • Thaʿlabī, Aḥmad b. Muḥammad al-. Al-Kashf wa l-bayān ʿan tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1422 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Edited by Muʾassisat al-Biʿtha. Qom: Dār al-Thiqāfa li-ṭibaʿat wa al-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1414 AH.
  • Zahīrī,ʿAlī Aṣghar. Qiṣaṣ al-Ḥusayn (a). Qom: Payām-i ḥujjat, 1386 Sh.
  • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Tafsīr al-kashshāf. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, 1407 AH.
  • دلیل استفاده از علایم اختصاری برای تعظیم و تکریم امامان (The reason for using abbreviations for honoring imams (Persian). Accessed: 2023/03/02.