Murtadd al-Milli

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Al-Murtadd al-Milli)

Murtadd Milli (Kiarabu: المرتد الملي) ni mkabala wa al-Murtadd al-Fitri naye ni mtu ambaye hakuzaliwa na baba na mama mwislamu, lakini yeye mwenyewe baada ya kubaleghe akasilimu na kisha baadaye akaritadi na kutoka katika Uislamu. Murtadd Milli huzuiwa kutumia mali yake kama ambavyo akiwa ameoa ndoa yake huvunjwa. Kama Murtadd Milli hatotubia adhabu yake ni kuuliwa, lakini kama ni mwanamke basi hukamatwa na kufungwa jela mpaka atubu au aage dunia.

Utambuzi wa Maana

Makala Asili: Al-Irtidâd (Kuritadi)

Murtadd Milli ni mtu ambaye wakati wa kutunga mimba yake, baba na mama yake hawakuwa waislamu, isipokuwa yeye baada ya kubaleghe akasimu na kuingia katika Uislamu kisha baadaye akaritadi na kutoka katika Uislamu na kuwa kafiri.[1] Murtadd Milli ni mkabala wa al-Murtadd Fitri ambaye huyu yeye amezaliwa katika Uislamu yaani baba na mama yake au mmoja wao alikuwa muislamu, lakini baada ya kubaleghe akaritadi na kuwa kafiri.[2]

Adhabu

Kuna adhabu maalumu imeainisha na Uislamu kwa Murtadd Milli: Mtu wa namna hii hupatiwa fursa ya kutubu na kama hatatubia basi adhabu yake ni kuuawa.[3] Lakini kama akiwa ni mwanamke adhabu yake ni kufungwa jela na nyakati za Swala anaadhibiwa mpaka atubu au aage dunia.[4] Mwanamke ambaye ni Murtadd Mili kama atakariri kuritadi kwake kwa mujibu wa fat'wa ya baadhi ya mafakihi mara ya tatu au ya nne ananyongwa,[5] lakini kwa mujibu wa fat'wa ya Sayyied Abul-Qassim Khui, mwanamke wa namna hii hata kama atakariri kuritadi kwake hanyongwi.[6]

Hukumu

Hukumu na matokeo ya kuritadi mtu ambaye hakuzaliwa katika Uislamu lakini baadaye baada ya kubaleghe akisilimu kisha baadaye akaritadi ni kama ifuatavyo:

  • Kuzuiwa kutumia mali: Kwa mujibu wa fat'wa ya baadhi ya mafakihi, Murtadd Milli madhali hajatubu, hana ruhusa ya kutumia mali yake.[7] Pamoja na hayo Sayyied Abul-Qassim Khui yeye anaamini kwamba, haijuzu kumzuia Murtadd Milli kutotumia mali yake.[8]
  • Kutosihi ndoa: Kwa mujibu wa kauli mashuhurii ya mafakihi wa Kishia, haisihi kwa murtadi kufunga ndoa na muislamu na kafiri.[10] pamoja na hayo, Sayyied Abul-Qassim Khui yeye anasema kuwa, ndoa ya mwanaume murtadi na mwanamke kafiri inasihi.[11]
  • Kunyimwa urithi: Murtadi hamrithi muislamu, lakini muislamu anamrithi yeye.[12]

Kwa mujibu wa mafakihi wa Kishia, toba ya Murtadd Milli inapelekea kuondoka adhabu dhidi yake pamoja na mambo mengine ambayo kama asingetubu angefanyiwa.[14]

Rejea

  1. Shahid Thani, al-Raudhah al-Bahiyah, 1410 H, juz. 8, uk. 30
  2. Muhaqiq Hilli, Syarai' al-Islam, 1408 H, juz. 4, uk. 170
  3. Muhaqiq Hilli, Sharai' al-Islam, 1408 H, juz. 4, uk. 170 ; Khui, Mabani Taqmilah al-Manhaj, 1422 H,juz1, uk. 396
  4. Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 H, juz. 41, uk. 610-616; Imam Khomeini, Tahrir al-Wasilah, 1379 S, juz. 2, uk. 365-368; Khui, Mabani Takmilah al-Manhaj, 1422 H, juz. 1, uk. 399-401 H
  5. Tazama: Muhaqqia Hilli, SHarai' al-Islam,1408 H, juz. 4, uk. 172, ; Shahid Thani, 1413 H, Maslik al-Afham, juz. 15, uk. 31
  6. Khui, Mabani Takmilah al-Minhaj, 1422 H, juz. 1, uk. 401
  7. Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 S, juz. 41, uk. 620
  8. Khui, Mabani Takmilah al-Minhaj, 1422 H, juz. 1, uk. 396
  9. Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 41, uk. 615; Khui, Mabani Takmilah al-Minhaj, 1422 H, juz. 1, uk. 396
  10. Tazama: Shekh Tusi, al-Mabsuth, 1351 S, juz. 7, uk. 289; Muhaqqiq Karaki, Jami' al-Maqasid, 1429 H, juz. 12, uk. 423; Muhaqqiq Hilli, Sharai' Hilli, 1408 H, juz. 4, uk. 172 ; Allamah Hilli, Tahrir al-Ahkam, juz. 2, uk. 21; Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 H, juz. 41, uk. 602
  11. Khui, Mabani Takmilah al-Minhaj, 1422 H, juz. 1, uk. 405
  12. Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 S, juz. 39, uk. 17
  13. Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 6, uk. 293
  14. Shahid Thani, 'al-Raudhah al-Bahiyah, 1410 H, juz. 8, uk. 30

Vyanzo

  • Alamah Hilli, Hassan bin Yusuf. Tahrir al-Ahkam. Qom: Muasasah Ali al-Bait, li al-Ihya' al-Turath.
  • Imam Khomeini, Sayyied Ruhullah. Tahrir al-Wasilah. Qom: Dar al-'Ilm, 1379 H.
  • Khui, Sayyied Abu al-Qasim. Mabani Takmilah al-Minhaj. Qom: Muasasah Ihya' Athar al-Imam al-Khui, 1422 H.
  • Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hassan. Sharai' al-Islam fi Masail al-Halal wa al-Haram. Mhakiki: Abdul Hussein Muhammad Ali Baqal. Qom: Ismailiyan, 1408 H.
  • Muhaqqiq Karaki, Ali bin Hussein, Jami' al-Maqasid fi Sharh al-Qawaid. Qom: Muasasah Ali al-Bait li al-Ihya' al-Turath, 1429 H.
  • Musawi Ardibili, Sayyied Abdul Karim. Fiqh al-Hudud wa al-Ta'zirat. Qom: Muasasah Intisharat Daneshgah Mufid, 1427 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan. Jawahir al-Kalam. Mhakiki: Ibrahim Suthani. Beirut: Dar Ihya' al-Turath al-Arabi, 1362 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan. Al-Mabsuth fi al-Fiqh al-Imamiyah. Teheran: Maktabah al-Radhawiyah, 1351 S.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Al-Raudhah al-Bahiyah fi Sharh al-Lum'ah al-Dimishqiyah. Sherh: Sayyied Muhammad Kalantar. Qom: Kitab Furushi Davari, 1410 H.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Masalik al-Afham ila Tanqih Syarai' al-Islam. Qom: Muasasah al-Ma'arif al-Islamiyah, 1413 H.