Al-Mujtaba (Lakabu)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Al-Mujtaba (lakabu))
Makala hii inahusiana na moja ya lakabu za Imamu Hassan (as). Ili kujua kuhusiana na shakhsia na maisha ya mtukufu huyu, angalia makala ya Imamu Hassan Mujtaba (a.s).

Al-Mujtaba (Kiarabu: المجتبى) yenye maana ya mteuliwa au ni moja ya lakabu za Imamu Hassan (a.s). [1]Lakabu hii imetumika pia kwa Mtume (s.a.w.w) [2] na Maimamu [3] wengine. Katika hotuba iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) kuhusiana na sifa maalumu za Maimamu, lakabu hii imetajwa kuwa ni katika sifa ya Imamu [4], lakini imekuwa mashuhuri kama lakabu ya Imamu Hassan (a.s). [5] Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Maimamu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, Maimamu wamemtaja Imamu Hassan kwa lakabu ya Mujtaba. [6] Katika Dua Tawasul pia lakabu ya al-Mujtaba imetajwa [7] na katika hirizi ya Imamu Sajjad (a.s) pia ibara ya al-Hassan al-Mujtaba [8] imekuja.

Mujtaba ina maana ya mteule au aliyechaguliwa. [9] Chini ya Aya ya 121 ya Surat Nahl Allama Tabatabai anafasiri neno ijtaba kwamba, Mwenyezi Mungu amemteua Imamu Maasumu kwa ajili yake kwa namna ambayo anamuongoa kwenye njia iliyonyooka.[10]

Inaelezwa kuwa lakabu hii, licha ya kuwa ina maana maalumu ambayo inapatikana uhakika wake kuhusiana na Maimamu wote wa Kishia, lakini ni Imamu wa pili tu wa Mashia (yaani Imamu Hassan) ndiye aliyeondokea kuwa mashuhuri kwa lakabu hii.[11]

Rejea

  1. Ibnshahr Ashhoob, al-Manaqib, 1379 AH, juzuu ya 4, uk.29.
  2. Zarandi Hanafi, Nazm Derar al-Samatin, 1425 AH, uk. 27.
  3. Angalia Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 25, uk. 150.
  4. Angalia Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 25, uk. 150.
  5. Nizami Hamadani, Al-Maarif al-Rafa'a, 2009, uk 314.
  6. Paknia Tabrizi, "Tafakari juu ya hati na vyeo maarufu vya wasio na dosari, amani iwe juu yao", uk. 132.
  7. Qami, Mufatih al-Janan, 1415 AH, 185.
  8. Atardi Guchani, Masnad al-Imam al-Sajjad, 1379, juzuu ya 2, uk.32.
  9. Mantzari, Masomo kutoka kwa Nahj al-Balagha, 1395, uk.398.
  10. Tabatabaei, Al-Mizan, 1390 AH, juzuu ya 12, uk.368.
  11. Fattahi, Anwar Elahi, 1390, uk 274.

Vyanzo

  • Ibnshahrashob, Muhammad bin Ali, Manaqib Al Abi Talib, Qom, Allameh, 1379 AH.
  • Paknia Tabrizi, Abdul Karim, "Tafakari juu ya hati na vyeo maarufu zaidi vya wasio na hatia, amani iwe juu yao", Wamisionari wa Kila Mwezi, Na. 145, Oktoba na Novemba 2013.
  • Zarandi, Muhammad bin Youssef, Nazm Derar Al-Samatin, Beirut, Dar Ihya Al-Tarath Al-Arabi, 1425 AH.

Tabatabai, Seyyed Mohammad Hossein, Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an, Beirut, Al-Alami Foundation for Publications, chapa ya pili, 1390 AH.

  • Atardi Qochani, Azizullah, Musnad al-Imam al-Sajjad, Tehran, Atard, 1379.
  • Fatahi, Hamid, Anwar Elahi, Qom, Mirfatah, 1390.
  • Qami, Abbas, Mufatih al-Jinan, Beirut, Dar al-Malak, 1415 AH.
  • Majlesi, Mohammad Baqer, Bihar al-Anwar, mchapishaji: Al-Wafa Foundation, chapa ya pili, 1403 AH, imepotezwa.
  • Muntzari, Hossein Ali, Masomo kutoka kwa Nahj al-Balagha, Tehran, Saraei, 2015.
  • Nizami Hamdani, Ali, Al-Ma'arif Al-Rafa'a Fi Al-Ziyarah Al-Jama'a, Mashhad, Astan Quds Razavi, 2009.