Al-Mujtaba (Lakabu)

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na moja ya lakabu za Imamu Hassan (as). Ili kujua kuhusiana na shakhsia na maisha ya mtukufu huyu, angalia makala ya Imamu Hassan Mujtaba (a.s).

Al-Mujtaba (Kiarabu: المجتبى) yenye maana ya mteuliwa au ni moja ya lakabu za Imamu Hassan (a.s). [1] Lakabu hii imetumika pia kwa Mtume (s.a.w.w) [2] na Maimamu [3] wengine. Katika hotuba iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) kuhusiana na sifa maalumu za Maimamu, lakabu hii imetajwa kuwa ni katika sifa ya Imamu [4], lakini imekuwa mashuhuri kama lakabu ya Imamu Hassan (a.s). [5] Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Maimamu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, Maimamu wamemtaja Imamu Hassan kwa lakabu ya Mujtaba. [6] Katika Dua Tawasul pia lakabu ya al-Mujtaba imetajwa [7] na katika hirizi ya Imamu Sajjad (a.s) pia ibara ya al-Hassan al-Mujtaba [8] imekuja.

Mujtaba ina maana ya mteule au aliyechaguliwa. [9] Chini ya Aya ya 121 ya Surat Nahl Allama Tabatabai anafasiri neno ijtaba kwamba, Mwenyezi Mungu amemteua Imamu Maasumu kwa ajili yake kwa namna ambayo anamuongoa kwenye njia iliyonyooka.

Inaelezwa kuwa lakabu hii, licha ya kuwa ina maana maalumu ambayo inapatikana uhakika wake kuhusiana na Maimamu wote wa Kishia, lakini ni Imamu wa pili tu wa Mashia (yaani Imamu Hassan) ndiye aliyeondokea kuwa mashuhuri kwa lakabu hii. [11]