Nenda kwa yaliyomo

Al-Hiyazat

Kutoka wikishia

Al-Hiyazat / Hiyazat al-Mubahaat (Kiarabu: الحيازة أو حيازة المباحات) ni kumiliki na kutumia mali ambazo ni mubaha zinazohamishika (mali ambazo inawezekana kuihamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine) ambayo kimsingi haina mmiliki maalumu na watu wote wana haki ya pamoja katika mali hiyo. Mfano wa hilo ni kama vile sehemu ya kuvulia samaki, kuchota maji kutoka mtoni, kutumia miinuko, milima, sehemu za kuwindia, sehemu za kukata kuni na malisho ambayo hayana mmiliki na kimsingi ni ya umma na watu wote wanaweza kutumia.

Kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi na kwa mujibu wa kanuni ya Hiyazat, mtu ambaye amepata kitu katika mali mubaha huwa ndiye mmiliki wake. Ili kuhalalisha hukumu na kanuni hiyo kumetumiwa Qur’an, hadithi na sira na mwenendo wa wenye akili (Sirat al-Uqalaa) na lililozoeleka katika ada. Kwa mujibu wa mtazamo wa baadhi ya mafakihi, mtu ambaye anapata mali hiyo iliyotangulia maelezo yake anapaswa kuwa amebaleghe, mwenye akili timamu na anayejua baya na zuri (rashid) ili aweze kumiliki mali iliyopatikana na mali ambayo imepatikana inapaswa kuwa ni katika mali zinazohamishika kwani Hiyazat haijuzu katika mali ambazo hazihamishiki.

Kuna tofauti za kimitazamo baina ya mafakihi kuhusu kusihi Hiyazat katika kukodisha, ushirika na uwakala au uwakishi. Kitabu cha “Qaidat Hiyazat ba ruikard Eghtesadi” mwandishi Hassan Nazari, kinajadili na kuchunguza kanuni ya “(مَن حازَ مَلِکَ”, mwenye kupata amemiliki).


Fasili (maana) na ufafanuzi

Al-Hiyazat au Hiyazat al-Mubahaat maana yake ni kumiliki na kutumia mali ambazo ni mubaha. [1] Makusudio ya mali zinazohamishika (mali ambazo inawezekana kuihamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine) ni kuhusiana mali asili (rasilimali asili) ambazo hazina mmiliki maalumu na watu wote wana haki ya pamoja katika mali hizo na hakuna marufuku au katazo la kisheria la kutumia au kumiliki kwa sura na ada ya kawaida. Mfano wa hilo ni kama vile sehemu ya kuvulia samaki, kuchota maji kutoka mtoni, kutumia miinuko, milima, sehemu za kuwindia za nchi kavu na baharini, kuni na malisho ambayo hayana mmiliki na kimsingi ni ya umma na watu wote wanaweza kutumia. [2]

Katika maandiko ya fikihi, maudhui ya hiyazat haijajadiliwa peke yake na kwa sura ya kujitegemea, lakini imejadiliwa sambamba na anuani kama kukodisha, ushirika na uwakala. [3]


Hukumu

Hiyazat (kuchukua na kutia mkono) katika mali za mubaha (zinazohamishika) hupelekea kumiliki; kwa mfano mtu ambaye anavua samaki mtoni au baharini, huwa mmiliki wa samaki aliyemvua. [4] Lakini kuna hitilafu za kimitazamo baina ya mafakihi kuhusiana na namna ya kupatikana umiliki. [5] Baadhi yao wanaamini kwamba, kupatikana hali ya umiliki kunashuritishwa na nia na kusudio la kumiliki na baadhi ya wengine wanaamini kwamba, kuchukua na kutia mkono (hiyazat) katika mali ya mubaha isiyo na mmiliki maalumu ni jambo ambalo halihitaji nia na kusudio la kumiliki bali kitendo cha kuchukua na kutumia mali na kitu hicho kisicho na mwenyewe ni jambo linalotosha kuhesabiwa kuwa ni mmiliki wake. [6]

Kutia mkono na kutumia vilivyomo katika milima, miinuko, misitu, ukataji kuni, wanyama wa porini, chemchemi, vyanzo vya maji na kadhalika, kunafanyika kwa mujibu wa ada na mazoea. [7] Kwa mfano ardhi ya malisho inayotumiwa kwa ajili ya malisho ya wanyama na kustafidi na wanyama wa porini kwa kuwawinda na kuwafanya kitoweo na kadhalika. [8]


Masharti ya Hiyazat

  • Mtu ambaye anapata kitu au mali mubaha na ya halali ambayo haina mmiliki maalumu na ambayo inahamshika anapaswa kutimiza masharti ambayo ni kuwa amebaleghe, akili timamu na anayejua baya na zuri (rashid) [9] ili aweze kumiliki mali iliyopatikana na mali ambayo imepatikana inapaswa kuwa ni katika mali zinazohamishika, kwani Hiyazat haijuzu katika mali ambazo hazihamishiki. Hata hivyo baadhi ya mafakihi wanaamini kwamba, Hiyazat kutokana na kuwa haipo ndani ya uqud (mikataba ya pande mbili) na iqaat (mkataba wa upande mmoja ambao unatimia tu kwa kauli ya “kukubali”) haina haja ya nia na kusudio na kwa msingi huo watoto pia wanaweza kuwa ni wamiliki wa mali isiyo na mmiliki maalumu na ambayo inahamishika. [10)
  • Mali ambayo haina mmiliki maalumu na ambayo inaweza kuchukuliwa na mtu yeyote inapaswa kuwa ni katika mali mubaha zinazohamishika; kwani Hiyazat haijuzu katika mali ambazo hazihamishiki. [11]


Hiyazat kwa uwakala

Baadhi ya mafakihi wa Kishia kama Sheikh Tusi na Ibn Idiris Hilli anaamini kuwa, haijuzu umiliki kwa uwakala au uwakilishi mali ambayo haina mmiliki maalumu na ambayo inahamishika. [12] Mkabala na yeye Ayatullah Khui mmoja wa mafakihi wa Kishia anasema, hilo linajuzu na anaamini kwamba, katika uwakala (kuwakilishwa) katika kupata na kumiliki mali isiyo na mmiliki maalumu na ambayo inahamishika, aliyewakilishwa huwa mmiliki wa kitu na mali hiyo iliyopatikana. [13]


Kukodisha katika Hiyazat

Kuna tofauti za kimitazamo baina ya mafakihi kuhusuhu kusihi Hiyazat katika kukodisha. Baadhi kama Sheikh Tusi na Muhaqqiq Hili wanasema inajuzu. [14]. Allama Hilli anasema haijuzu kwa sababu haifahamiki na haiko wazi kwamba, mali iliyopatikana (ambayo haina mmiliki maalumu na ambayo inahamishika) ni ya mwenye kukodisha au mwenye kukodiwa. [15]

Baadhi ya mafakihi wengine wamesema, kama kupata tu hiyazat (kitu na mali isiyo na mmiliki maalumu na ambayo inahamishika) kunapelekea kupatikana umiliki, katika hali hii mtu ambaye amekodishwa kwa ajili ya kupata kitu na mali isiyo na mmiliki maalumu na ambayo inahamshika, atakuwa mmiliki wa mali hiyo. Kwa muktadha huo, haijuzu kukodisha mtu katika hali kama hii; lakini kama ni kinyume na hivyo, yaani hali ya umiliki haipatikani na kuna haja ya nia na kusudio la kumiliki, katika hali hii inajuzu kukodisha mtu. [16]


Ushirika katika Hiyazat

Hiyazat inafanyika pia kwa sura ya ushirika. [17] Hili hutumia kwa kuweko ushirika baina ya watu kadhaa kwa ajili ya kuchota maji kwa chombo kimoja au kung’oa mti au kuvua samaki kwa nyavu moja na mfano wa hayo. [18] Hata hivyo kuna mitazamo tofauti kuhusiana na kwamba, hisa ya kila mmoja kati ya pande shirika ni nusu kwa nusu kama hisa haikuainishwa hapo kabla au kwa kiwango cha juhudi na mchango wa mtu. [19]


Kanuni ya Hiyataz

Kuna kanuni katika fiq’h inayosema: (مَن حازَ مَلِکَ ; Mwenye kupata amemiliki). Kwa mujibu wa kanuni hii ni kuwa, kila ambaye atapata kitu cha mubaha ambacho hakuna mmiliki maalumu na kinahamishika basi amekimiliki. Kwa maana kwamba, amekuwa mmiliki wa kitu hicho. [20] Kwa mujibu wa mtazamo wa Ayatullah Makarim Shirazi mmoja wa Marajii Taqlidi ni kwamba, hakuna andiko au hadithi maalumu yenye anuani ya: (مَن حازَ مَلِکَ ; mwenye kupata amemiliki); bali anuani na kanuni hii imepatikana kupitia mafuhumu na maana ya hadithi mbalimbali. [22]


Hoja na nyaraka za kanuni ya Hiyazat

Kwa mujibu wa mafakihi hoja za kanuni ya Hiyazat ni:

  • Qur’an

Mafakihi mashuhuri wanaitumia Aya ya 29 ya Surat al-Baqara (Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi). [23] Kwa mujibu wa Aya hii, vitu vyote ambavyo ni mubaha vilivyoko ardhini, vimeumbwa ili mwanadamu avimiliki na kila ambaye atapata kitu miongoni mwa vitu hivyo basi huwa mmiliki wake. [24]

  • Hadithi

Hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) inasema: Kila ambaye atapata mali au mnyama jangwani ambaye mwenyewe amemuacha naye akaihuisha, atakuwa mmiliki wake na ni kwa namna hii ambapo vitu huhesabiwa kama vitu vya mubaha.” [25] Katika hadithi nyingine kutoka kwa Imam Swadiq pia amenukuliwa akisema: Mtu ambaye anatia mkono katika kitu mubaha (anapokidhibiti kitu hicho) huwa mmiliki wake. [26] Kwa kuzingatia hadithi hizi na nyinginezo, zilizotoa hukumu ya umiliki wa vitu kama ndege, wanyama waliowindwa na samaki waliovuliwa, wanazuoni wa fikihi wamehukumu pia kwamba, kila mali au kitu mubaha ambacho kimepatikana kwa njia ya hiyazat huwa ni milki ya aliyekipata. [27].

  • Sira ya wenye akili

Kumiliki mali mubaha kupitia hiyazat (kupata mali ambayo haina mmiliki maalumu na yenye kuhamishika) ni katika mambo yanayokubaliwa na akili [28] na sheria imepasisha hili. [29] Imam Khomeini anasema: Sira isiyo na shaka kuanzia mwanzoni mwa ustaarabu wa mwanadamu ilikuwa kwamba, umiliki unapatikana kupitia kuhuisha na hiyazat (kupata mali mubaha isiyo na mmiliki maalumu na ambayo inahamshika) na hakuna Nabii, Walii wala muumini aliyekana hili. [30]


Monografia

Kitabu cha “Qaidat Hiyazat ba ruikard Eghtesadi” kimeandikwa na Hassan Nazari, Kitabu hiki kinajadili na kuchunguza pande tofauti za kifikihi, kisheria na kiuchumi. Kitabu hiki kilichapishwa 1385 Hijria Shamsia na Bustan Ketab.


Rejea

Vyanzo

  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf, Qawa'id al-Ahkam, Qom, Muassasah al-Nashr al-Islami, 1413 H
  • Ibn Idris al-Hilli, Muhammad bin Manshur, al-Sarair, Qom, Daftar Intisyarat Islami, 1410 H
  • Imam Khumaini, Sayyied Ruhullah, Kitab al-Bai', Qom, Muassasah Ismailiyan, 1407 H/1987
  • Isfahani, Sayyied Abu al-Hassan, Wasilah al-Najah, Tehran, Muassasah Tanzhim wa Nashr Athar Imam Khomaini, cet. I, 1434 H
  • Khui, Sayyied Abul Qasim, Minhaj al-Shalihin, Qom, Nashr Madinah al-'Ilm, 1368 HS/1410 H
  • Makarim Shirazi, Nashr, al-Qawa'id al-Fiqhiyah, Qom, Madrasah Imam Ali bin Abi Talib, 1383 HS
  • Makarim Shirazi, Nashr, Khuthuth al-Iqtishad Islami, Qom, Madrasah al-Imam Ali bin Abi Talib, cet. I, 1360 HS
  • Muassasah Dairah al-Ma'arif al-Fiqh al-Islami, al-Mausu'ah al-Fiqhiyah, Qom, Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, 1423 H
  • Muassasah Dairah al-Ma'arif al-Fiqh al-Islami, Farhang-e Fiqh Farsi, Qom, Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islam, 1387 HS
  • Muhaqqiq Damad, Sayyied Mustafawi, Qawa'id Fiqh, jld. 1, Teheran, Nashr Ulum Islami, 1406 H
  • Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hassan, Sharai' al-Islam fi Masail al-Halal wa al-Haram, Qom, Muassasah Ismailiyan, cet. II, 1408 H
  • Mustafawi, Sayyied Muhammad Kazhim, al-Qawa'id al-Fiqhiyah, Qom, Muassasah al-Nashr al-Islami, cet. IV, 1421 H
  • Najafi, Muhammad Muhsin, Jawahir al-Kalam, Beirut, Dar Ahya al-Turath al-'Arabi, 1430 H
  • Razmi, Muhsin dan Khalid Nabiniya, Barresi Qa'edah Man Haza Milk dar Fiqh wa Huquq Maudhu'ah Iran, Pezuhesyihai Fiqh wa Huquq Islami, no. 31, 1392 HS
  • Sabziwari, Sayyied Abd al-A'la, Madzhab al-Ahkam, Qom, Dar al-Tafsir Shahid Thani, Zain al-Din bin Ali, Masalik al-Afham, Qom, Muassasah al-Ma'arif al-Islamiyah, 1413 H
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, al-Mabsuth, Tehran, cet. Murtadhawi, 1387 H