Abul Qassim (Kuniya)

Kutoka wikishia

Abul Qassim (Kiarabu: ابوالقاسم) ni kuniya ya mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). [1] Baada ya kuzaliwa Qassim mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), mtukufu huyo akaondokea kuwa mashuhuri kwa kuniya ya Abul-Qassim. [2] Sheikh Saduq (aliyeaga dunia: 381 H) sambamba na kubainisha hadithi anasema kuwa, kuniya hii imechukuliwa kutoka katika sifa ya al-Qassim (mgawaji) kiasi kwamba, kumuamini na kumkufurisha Mtume (s.a.w.w) ndiko kutakakowagawa watu katika makundi mawili ya watu wa peponi na motoni. [3] Kadhalika akitegemea hadithi hii hii anasema kuwa, kwa kuwa Imamu Ali ni mgawaji wa pepo na moto, Mtume (s.a.w.w) ameitwa kwa lakabu ya Abul-Qassim kwa sababu Mtume anahesabiwa kuwa ni baba wa Imamu Ali na baba wa Waislamu wengine. [4]

Kadhalika angalia: Hadithi ya Qasim al-Naar wa al-Jannah

Kwa mujibu wa Muhammad Ali Ardebili katika kitabu cha Jamiu al-Ruwat ni kuwa, kuniya hii imenasibishwa pia na Imamu Sajjad (a.s). [5] Kadhalika kuniya hii imetumiwa kwa Imamu Mahdi (a.t.f.s). [6] Inayatullah Qohpai, mtambuzi wa wapokezi wa hadithi wa Kishia wa karne ya 11 Hijria anasema, matumizi ya kuniya ya Abul-Qassim yalitumiwa zaidi kwa Imam Mahdi (a.s) kuliko kwa Mtume (s.a.w.w). [7]

Sheikh Hurr al-Amil katika kitabu cha Wasail al-Shiah anaamini kuwa, kama mtu jina lake ni Muhammad, ni makuruhu kupewa lakabu ya Abul-Qassim. [8] Kwa mujibu wa ripoti ambayo imesajili majina katika Idara ya Kusajili Hali (za watu) nchini Iran (vifo, uzazi, ndoa na kadhalika) ni kwamba, Abul Qassim ni miongoni mwa majina 100 yaliyoongoza kuitwa wanaume nchini Iran kati ya mwaka 1297 hadi 1380 Hijria Shamsia. [9]

Rejea

Vyanzo