Nenda kwa yaliyomo

Aba Abdillah (Lakabu)

Kutoka wikishia

Aba Abdullah (Kiarabu: أبو عبد الله) (ni lakabu tukufu alilopewa Imamu Hussein (a.s). lakabu hilo linaonyesha sifa na utukufu wa Imamu huyo. Vile vile, Aba Abdullah ni miongoni mwa lakabu za Imamu Hussein (a.s) na Imamu Swadiq (a.s). Lakabu hutumiwa katika utamaduni wa Kiarabu yakimaanisha kuheshimu watu. Katika hadithi tofauti, maimamu wa Shia wametajwa kwa lakabu zao, Katika vitabu vya Hadithi, neno "Aba Abdullah" linapotumika bila kutaja jina asili, maana yake linakusudiwa ni Imamu Swadiq (a.s.).

Lakabu Katika Utamaduni wa Kiarabu

Kuhusiana na neno lakabu zingatia ibara hii ifuatayo:

Katika utamaduni wa Kiarabu, lakabu ni nomino au jina la kwanza la mtu lisilokuwa asili, ambalo hutumika kwa ajili ya kuonyesha heshima kwa watu .[1] Majina ya lakabu mara nyingi huanza na "Abu", "Aba" na "Abi" yakimaanisha (maana ya baba) kama vile Abul Hasan, Abul Qasim, Abi Bakr na "Umm". (likimaanisha mama) Ummu Kulthum.[2]

Lakabu za Pamoja Zinazo washirikisha Maimamu

Katika hadithi nyingi, maimamu wa Shia wametajwa kwa lakabu zao[3] Majina mengi ya lakabu ya maimamu yanatumika Pamoja miongoni mwao[4] Kwa mfano, lakabu ya Abu Ja'far linatumiwa pamoja kati ya Imam Baqir (a.s.) na Imam Jawad (a.s.). Pia, kuna Maimamu watano ambao wamepewa lakabu la Pamoja la Abul Hasan: maimamu hao watano ni hawa wafuatao: Imam Ali (a.s.), Imam Sajjad (a.s.), Imamu Kadhim (a.s), Imam Ridha (a.s) na Imamu Hadi (a.s).[5]

Lakabu la Aba Abdullah

Lakabu la Abu Abdullah, ambalo katika lugha ya kiarabu pia linatumika kama Abu Abdullah na Abi Abdullah, linatumiwa Pamoja baina ya Imamu Hussein (a.s) na Imamu Swadiq (a.s)[6] kwa mujibu wa kitabu kijulikanacho kwa jina la Tadhalum Az-Zahra imeashiriwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akimuita mjukuu wake Imam Hussein (a.s) kwa lakabu la Aba Abdullah.[7] Imamu Swadiq (a.s) pia alikuwa akijulikana kwa lakabu la Aba Abdullah kwa sababu alikuwa mwana wa pili wa Abdullah Aftah.[8]

Katika vitabu vya hadithi, sio hadithi nyingi za Imamu Hussein (a.s) ambazo zimesimuliwa kuhusiana na lakabu la Aba Abdullah,[9] Kwa upande mwingine, hadithi nyingi za Shia zimesimuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s),[10] kwa hiyo, katika vyanzo vya hadithi, lakabu ya "Aba Abdullah" inapotumiwa peke yake, bila ya kutajwa kielezi chengine kando yake, Ina maana kwamba, anakusudiwa Imamu Swadiq (a.s).[11]

Rejea

  1. Majmuat minal mualifiin, Al-muujamu al-wasiit, juz. 2, uk. 802.
  2. Ibnu Mandhur, Lisanu al-arabia, juz. 15,uk. 233
  3. Mudir Shanejii, Ilmu al-hadith, uk. 192
  4. Mudir Shanejii, Ilmu al-hadith, uk. 192
  5. Mudir Shanejii, Ilmu al-hadith, uk. 192
  6. Mudir Shanejii, Ilmu al-hadith, uk. 192
  7. Maahadi tahqiq baqir al-ulumi, Muasasat kalimat al-Imamu al-Hussein, uk. 39.
  8. Bakitajii, Jaafar Swadiq (a.s), Imamu, uk. 181.
  9. Mudir Shanejii, Ilmu al-hadith, uk. 192
  10. Shahidi, Zandekani Imamu Swadq, 1384 HS, uk. 61.
  11. Sayfi, Miqyas al-ruwaat, Muasasat al-nashri al-islamy, 1422 H, uk. 275.

Vyanzo

  • Ibn Mandhur, Muhammad, Lisanu al-Arab, Al-Muhaqq: Ahmad Faris Sahib al-Jawaib, Beirut-Lebanon, Al-Nashru: Dar al-Aswadir, Toleo la 3, 1414 AH.
  • Bakitajii, Ahmed, Ja'far Swadiq (a.s.), Imamu, Tehran, Markaz dairat al-maarif, 1389 AH.
  • Sayfi, Ali Akbar, Miqyas al-ruwaat fi kuliyaat ilmu alrijal, Muasasat al-nashr al-islamy, Qom, 1422 AH.
  • Shahidi, Ja'far, Zindagii Imamu Swadiq Ja'far bin Muhammad (a.s), Tehran, Daftar nashr farhang islamy, 1384 HS.
  • Majmuat min mualifiin(Majmau al-lughat al-arabiyah bil-Qahira: Ibrahim Mostafa, Ahmad Al-Zayat wa Hamid Abdul-Qadir wa Muhammad Al-Najjar), Al-Mu'jam al-Wasit, D.M, Al-nashir: Dar Da'awa, D.T.
  • Mudir Shanejii, Kadhim, Ilmu al-Hadith, Qom, Al-Nashir: Daftar intisharat islamy, Toleo la 16, 1381 SH.
  • Maahadi tahqiq Baqir al-ulumi, Muasasat kalimat al-Imam al-Hussein, Qom, Danesh, Toleo la 2, 1415 AH.