Aalu Llahi
Aalu-Allahi (Kiarabu: آل الله): Kiswahili hufasirika kwa maana ya familia ya Mungu, neno hili ni neno la Kiarabu ambalo lina nia ya kuashiria familia ya bwana Mtume (s.a.w.w). Washairi na wahadhiri wa Shia pia katika Hadithi jina au sifa hii hutumika kurejelea Ahlul Bayt (a.s). Matumizi ya sifa hii yanatokana na heshima walio nayo Ahlul Bayt (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu, na hamaanishi kwamba wao ni familia na jamaa wa Mwenye Ezi Mungu. Pia, Quraish nao waliitwa Alu Allahi kwa sababu ya wao kuwa ni walinzi wa Kaaba.
Utafiti wa Kilugha
Katika Uislamu, neno Aalu-Allahi «آل الله» linamaanisha familia inayohusishwa na Mwenye Ezi Mungu.[1] Aalu «آل» kiasilia linatokana na neno Ahlu «اهل», ambalo linamaanisha familia, ukoo, wafuasi, na jamaa.[2] Pia neno hili limetumika mara kadhaa katika Qur'ani; kama vile kwenye Aya zilizowazungumzia watu wa Imran «آل عمران»[3] kwa maana ya familia ya Imran, ambayo inajumuisha ndani yake bibi Mariamu (a.s) na nabi Isa (a.s),[4] Aalu Luti «آل لوط»,[5] kwa maana ya familia ya nabi Lut (a.s)[6] na Aalu Firaun «آل فرعون»,[7] kwa maana ya wafuasi na jeshi la Firauni..[8] Hata hivyo, kuliegesha neno «آل» kwenye neno «الله» ni uegeshaji wa kuongeza heshima, kwa hiyo hii ya uegeshaji huashiria taadhima na utukufu wa kitu kilicho engezwa kwa (Mungu) «الله» sio uhusiano wa kifamilia baina yake na Mungu.[9]
Mifano Hai
Kulingana na maelezo msingi ya baadhi ya hadithi ni kwamba; Maimamu (a.s) wanamiliki elimu maalum kwa sababu wao ni watu wa siri za Mwenye Ezi Mungu, wao pia ni Aalu Llahi «آل الله» na ni warithi wa manabii. .[10] Kwa msingi huo huo, wahadhiri wamekuwa na kawaida kwawataja Aalu Llahi «آل الله» katika utangulizi wa mihadhara yao.[11] Pia ibara hii imetumika katika utangulizi wa ziara (sala na salamu) ya Imamu Hussein (a.s) isomwayo katikati ya mwezi wa Rajab, ambapo ndani yake imetajwa ibara isemayo: (السَّلامُ عَلَیْکُمْ یَا آلَ اللهِ السَّلامُ عَلَیْکُمْ یَا صَفْوَةَ اللهِ) Pia, ibara hii inapatikana katika vitabu kadhaa vilivyo jumuisha ndani yake sala na salamu za Maimamu (a.s) na watuku mbali mbali.[12] Pia ndani ya Ziaratu al-Arbain mmetumika aina hii ya ibara.[13]
Katika kutoa ufafanuzi juu ya husiana na uhusiano uliopo kati ya Maimamu Shia (a.s) na Mungu, imezezwa kwamba; matumizi haya yanaashiria taadhima na utukufu wao mbele ya Mola wao, na sio uhusiano wa kijamaa na Mwenye Ezi Mungu.[14] Wao wamehusishwa Naye kutokana na kule wao kuwa katika viwango vya juu zaidi katika kukaribiana na Mwenye Ezi Mungu..[15] Vivyo hivyo, kabila la Quraishi nalo liliitwa «Ahlu Llah» kutokana na wao kuwa ni walinzi wa Kaaba. Zaidi ya hilo, pia kabila hilo la Maquraishi liliitwa “Sukkaanu Llahi” kwa maana ya wakazi wa Mungu, na «Jiiranu Llahi» kwa maana ya majirani wa Mungu.[16] Kulingana na maelezo ya mwanazuoni wa Shia wa karne ya tano, Mansur ibn Hussein Aabi, ni kwamba; tukio la Watu wa Tembo liliwapa Maquraishi ukuu na taadhima na kusababisha wao kuitwa Ahlu Llah.[17]
Maudhui Zinazo Husiana
- Ahlu al-Bait
- Maimamu wa Shia
- Watukufu 14 (Maasumina 14)
- Dhawil Qurba
Rejea
- ↑ Kwanini Ahlul-Bayt (a.s) wanaitwa Ahlu-llah? (Kifarsi)
- ↑ Rāghib al-Iṣfahānī, al-Mufradāt, uk. 98.
- ↑ Qur'an 3:33.
- ↑ Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nimūna, juz. 2, uk. 518.
- ↑ Qur'an 27:56; Qur'an 15:61.
- ↑ Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān, juz. 15, uk. 376.
- ↑ Qur'an 2:50; Qur'an 8:54.
- ↑ Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nimūna, vol. 1, p. 251; Qurashī, Tafsīr-i aḥsan al-ḥadīth, vol. 1, p. 120.
- ↑ Kwanini Ahlul-Bayt (a.s) wanaitwa Ahlu-llah? (Kifarsi)
- ↑ Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 31, uk. 592; juz. 44, uk. 184.
- ↑ Jibu la Ayatollah Wahid: kwanin Ahlul-Bayt (a.s) wanaitwa Ahlu-llah? (Persian)
- ↑ Majlisi, Biharul anwar, juz. 99, uk. 202
- ↑ Majlisi, Biharul anwar, juz. 98, uk. 329
- ↑ Kwanini Ahlul-Bayt (a.s) wanaitwa Ahlu-llah? (Kifarsi)
- ↑ Jibu la Ayatollah Wahid: kwanin Ahlul-Bayt (a.s) wanaitwa Ahlu-llah? (Persian)
- ↑ Ibn ʿAbd Rabbih, al-ʿIqd al-farīd, juz. 3, uk. 226; Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 15, uk. 258; Ṣadūq, al-Amālī, uk. 317.
- ↑ Aabi. Nathr dar, 1424 H. uk. 273
Vyanzo
- Ābī, Manṣūr b. Ḥusayn. Nathr al-durr fī al-muḥāḍirāt. Edited by Maḥfūz Khālid ʿAbd al-Ghanī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1424 AH.
- Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Luhūf manzūm. Translated to Farsi by ʿAlī Maḥallātī. [n.p], Daftar-i Nashr-i Nawīd-i Islām, 1377 Sh.
- Ibn ʿAbd Rabbih, Aḥmad Muḥammad. Al-ʿIqd al-farīd. Edited by ʿAbd al-Majīd al-Tarḥīnī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, [n.d].
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Intishārāt-i Muʾassisat al-Wafāʾ, 1403 AH.
- Qurashī, Sayyid ʿAlī Akbar. Tafsīr-i aḥsan al-ḥadīth. [n.p], Daftar-i Nashr-i Nawīd-i Islām, 1391 Sh.
- Rāghib al-Iṣfahānī, Ḥusayn b. Muḥammad al-. Al-Mufradāt fī qarīb al-Qurʾān. [n.p]: Dār al-Qalam, 1412 AH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. Qom: Muʾassisat al-Biʿtha, 1417 AH.
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1417 AH.
- چرا به اهل بیت علیهم السلام، آل الله می گویند؟ (Persian) (Why the Ahl al-Bayt (a) are called Al Allah?) The Website of Hawza.net. Accessed: 2022/05/21.
- پاسخ آیتالله العظمی وحید؛ چرا به اهلبیت پیامبر «آل الله» می گویند (Persian). (The answer of Ayatollah Wahid: why the Ahl al-Bayt (a) are called Al Allah?) Accessed: 2022/05/21.