Zuleikha

Kutoka wikishia

Zuleikha (Kiarabu: زليخا أو زليخاء أو زليخة) alikuwa mke wa mheshimiwa/azizi wa Misri (kiongozi wa kijadi). Baadaye Zuleikha alikuja kuolewa na Nabii Yusuf (a.s) na kisa chache na Nabii Yusuf kimekuja katika Qur'ani Tukufu. [1] Jina la Zuleikha halijatajwa katika Qur'an bali ameelezwa kwa ibara kama; yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani (الَّتِی هُوَ فِی بَيْتِهَا) na mke wa mheshimiwa wa Misri (امْرَأَتُ الْعَزِیز) [3] [4] Pamoja na hayo katika baadhi ya vyanzo vya tafsiri, [5] historia [6] na hadithi [7] jina lake limetajwa kuwa ni Zuleikha. Fakhru Razi mfasiri wa Qur'an anaamini kwamba, hakuna vyanzo vyenye itibari kuhusiana na jina hili. [8] Katika baadhi ya vyanzo pia jina la mke wa mheshimiwa wa Misri liimetambuliwa kuwa ni Zuleikha. [9]

Katika sehemu za Qur'an na Torati, kisa cha Yusuf na Zuleikha kimesimuliwa na kubainishwa. [10] Kwa mujibu wa baadhi ya watafiti, Quran na Torati zina tofautiana katika kubainisha na kusimuliia kisa hiki. [11] Kulingana na Quran, Zuleikha alimtaka kimapenzi Yusuf; Lakini Yusuf alikimbia kuelekea mlangoni baada ya “kuona hoja za Mola wake Mlezi.” [12] Nasser Makarem Shirazi, mmoja wa wafasiri wa Kishia, anaamini kwamba Nabii Yusuf aliokolewa kutoka katika mazingira hayo ya dhambi kwa msaada wa ghaib. [13] Zuleikha alimfikia Yusuf na kumchania kanzu yake. [14] Mbele ya mlango Yusuf na Zuleikha walikkutana na mheshimiwa wa Misri. [15] Zuleikha na Yusuf kila mmoja alimtuhumu mwenziwe kwa khiyana na usaliti. [16] Katika hali hiyo mtu mmoja wa ndugu wa Zuleikha alisema: Tunagalie, ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma, basi mwanamke amesema uwongo, naye Yusuf ni katika wakweli. [17] Basi yule mtu alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Bila ya shaka vitimbi vyenu ni vikuu. Kwa muktadha huo, Yusuf akawa ameondolewa tuhuma ya khiyana. [18]

Kulingana na baadhi ya ripoti, shahidi aliyemtetea Yusuf alikuwa mpwa wa Zuleikha miezi mitatu [19] ambaye alizungumza kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. [20] Hata hivyo, katika ripoti nyingine, shahidi huyo ametambulishwa kama mtu mwenye hekima. [21 ] Kulingana na baadhi ya wafasiri, Yusuf alitupwa gerezani kwa ombi la Zuleikha; [22] lakini baada ya muda Zuleikha alikiri hatia yake na ukweli wa Yusuf. [23]

Zuleikha alikuwa mwanamke mrembo, tajiri [24] na mwabudu sanamu. [25] Hakufanikiwa kupata watoto kutoka kwa mumewe. [26] Kulingana na baadhi ya vyanzo, baada ya Zuleikha kutubu katika uzee wake na kuwa mwabudu Mungu mmoja, alibadilika na kurudi katika ujana baada ya Yusuf (a.s) kumuombea dua na akaolewa na Yusuf. [27] Inasemekana kuwa, walifanikiwa kuzaa watoto wawili katika ndoa yao. [28] Hata hivyo, baadhi ya watafiti wanaamini kwamba hadithi hizi haziwezi kutegemewa kutokana na sababu mbalimbali, kama vile kuwepo matatizo na ishkali katika sanadi, mapokezi na andiko lake na muhtawa na maudhui yake imechukuliwa kutoka katika Torati. [29]

Kulingana na tafiti zilizofanywa, Zuleikha amekuwa na ushawishi mkubwa kwa mawazo na fikra za Kisufi. [30] Inasemekana kwamba, Masufi walisifu hali na muamala wa Zuleikha na wakitumia hali na miamala yake hiyo walibainisha mitazamo yao ya Kiirfani. [31] Kisa cha mapenzi cha Zuleikha kwa Nabii Yusuf (as) kimeakisiwa sana katika fasihi ya lugha mbalimbali ikiwemo fasihi ya Kifarsi, Kiituruki na lugha za Ulaya. [32].

Vyanzo

  • Asadī, ʿAlī. Zuleikha dar Dāʾirat al-maʿārif-i Qurān-i Karīm. Qom: Būstān-i Kitāb, 1395 Sh.
  • Bayḍāwi, ʿAbd Allāh b. ʿUmar. Anwār al-tanzīl wa asrār al-taʾwīl. 1st edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1418 AH.
  • Daylamī, Ḥasan b. Muḥammad. Aʿlām al-dīn fī ṣifāt al-muʾminīn. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt(a), 1408 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Fayḍ al-Kāshānī, Muḥammad b. al-Murtaḍā al-. Tafsīr al-Ṣāfī. Edited by Ḥusayn Aʿlamī. Second edition. Tehran: Maktabat al-Ṣadr, 1415 AH.
  • Kāshānī, Mullā Fatḥ Allāh. Manhaj al-ṣādiqīn fī ilzām al-mukhālifīn. Kitābfurūshī-yi Muḥammad Ḥasan ʿIlmī. Tehran: 1336 Sh.
  • Khazzāz al-Qummī, ʿAlī b. Muḥammad b. ʿAlī al-. Kifāyat al-athar fī l-naṣṣ ʿalā l-aʾimmat al-ithnā ʿashar. Qom: Bīdār, 1401 AH.
  • Khusrawī, Zahrāʾ. Pajūhish-i taṭbīqī-yi dāstān-i Yūsuf wa Zuleikhā dar adabiyyāt-i Islāmī. Majalla-yi Dānishnāma 2 (Waḥīd-i ʿUlūm wa taḥqīqāt) (1388 Sh).
  • Ibn al-Jawzī, ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Al-Muntaẓam fī tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1412 AH.
  • Ibn Khaldūn, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Diwān al-mubtadaʾ wa l-khabar fī tārīkh al-ʿarab wa l-barbar wa man ʿaṣarahum min dhawi l-shaʾn al-akbar. Beirut: Dār al-Fikr, 1408 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
  • Maʿārif, Majīd and others. Barrasī-yi riwāyāt-i tafsīrī-yi farīqayn dar masʾala-yi izdiwāj-i Ḥaḍrat-i Yūsuf bā Zuleikhā. Dū faṣlnāma-yi ḥadīth pajūhī 13 (1394 Sh).
  • Maqātil, Ibn Sulaymān. Tafsīr Maqātil b. Sulaymān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth, 1423 Sh.
  • Muqaddasī, Muṭahhar b. Ṭāhir. Al-Badʾ wa al-tārīkh. Egypt: Maktabat al-Thiqāfa al-Dīnīyya, [nd].
  • Pākmihr, ʿAlī. Zuleikha dar andīsha-yi Shāʿirān wa ʿĀrifān-i qarn-i panjum tā haftum. Faslnamā-yi takhassusī adabiyyāt-i Fārsī 46 (1394 Sh).
  • Qurtubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Tehran: Nāṣir Khusraw, 1364 Sh.
  • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Mūsawī Jazāʾirī. Third edition. Qom: Dār al-Kitab, 1404 AH.
  • Rāwandī, Saʿīd b. Hibat Allāh. Qiṣaṣ al-anbīyāʾ. Mashhad: Markaz-i Pazhūhish-hā-yi Islāmī, 1409 AH.
  • Saʿdī, Muṣliḥ b. ʿAbd Allāh. Būstān-i Saʿdī. Edited by: Muḥammad ʿAlī Furūghī. Tehran: Quqnūs, 1372 Sh.
  • Saʿdī, Muṣliḥ b. ʿAbd Allāh. Ghazalīyyāt -i Saʿdī. Edited by: Muḥammad ʿAlī Furūghī. Tehran: Quqnūs, 1342 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Mahdī Lājiwardī. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿIlal al-sharāʾiʿ. Qom: Dāwarī, 1385 Sh.
  • Ṣādiqī, Sayyid Muḥammad. Nigāh-i taṭbīqī bi dāstān-i Yūsuf wa Zuleikhā dar Qurʾān-i majīd wa Tūrāt. Majalla-yi adabiyyāt-i taṭbīqī 4 ( 1368 Sh).
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.