Usul al-Arba'ami-a
Usul al-Arba'ami-a: ni jina liinarejelea mjumuiko maandishi mia nne juu ya Hadithi za Kishia. Huo ndio mjumuiko wa kwanza kabisa uliokuwa umekesanywa kwa mfumo ufafanao na vitabu kupitia wapokezi wa kwanza kabisa wa Kishia, ambao waliandika Hadithi hizi ima kwa njia moja kwa moja au kwa njia ya wapokezi wa wanao nukuu moja kwa moja kutoka kwa Maimamu wa Kishia. Umaalumu, upambanukaji na utofautikaji wa vitabu hivi, ni kwamba; hivi sio vile vitabu vyenye kutegemea vitabu vingine vya Hadithi, jambo ambalo ni lenye linapelekea kuaminika zaidi Hadithi zilizomo ndani yake, kwa kutokana na uwezekano mno wa kutokea makosa na mabadiliko katika Hadithi zake. Mjumuiko wa “Usul al-Arba'ami-a” umekuwa na umuhimu mkubwa mno mbele ya wanazuoni wa Kishia, na umekuwa mojawapo ya vigezo vya kutambua na kuthibitisha usahihi wa Hadithi mbali mbali.
Kwa mujibu wa wanazuoni wa Kishia, vitabu vingi vya Usul al-Arba'mi'ah viliandikwa wakati wa uhai wa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s), au muda mfupi kabla au baada ya zama zake. Imamu al-Sadiq (a.s) alikuwa na mchango mkubwa katika kueneza na kutoa mafunzo ya Kiislamu kwa njia ya Hadithi, na ni katika kipindi chake yeye ndicho kilichotoa sehemu kubwa ya Hadithi zilizomo kwenye mjumuiko wa Usul al-Arba'ami-a, zilirekodiwa kupitia wapokezi kutoka kwa wapokezi waliopokea waliopokuea moja kwa moja kutoka kwake. Wanazuoni wengi wa Kishia wanakubaliana kwamba idadi ya vitabu au mjumuiko wa Usul al-Arba'ami-a ulikuwa ulikuwa na idadi vitabu mia nne, ingawa kuna maoni tofauti miongoni mwa wanazuoni, kwani wengine wanaamini kwamba idadi yake ilikuwa ni ndogo zaidi. Hii inaonesha utofauti wa maoni kuhusu ukubwa wa hazina hii ya Hadithi, lakini pia haipunguzi umuhimu wake katika historia ya mafundisho ya Kiislamu ya Kishia. Katika jamii ya Kishia, kulikuwa na shauku kubwa ya kuhifadhi na kulinda vitabu vya Usul al-Arba'ami-a kutokana na thamani yake ya kipekee. Hata hivyo, kutokana na maendeleo ya uchapishaji na kuongezeka kwa vitabu vipya ambavyo vilijumuisha Hadithi zilizomo ndani ya Usul al-Arba'ami-a, umuhimu wa maandiko ya asili ulidumaa na kuyeyuka polepole. Hii ilisababisha upotevu wa sehemu kubwa ya maandishi haya ya awali. Leo hii, ni vitabu kumi na sita tu vya Usul al-Arba'ami-a vilivyobaki, ambavyo vimehifadhiwa na kuchapishwa kwa pamoja katika kitabu kiitwacho “Usulu Al-Sittatu ‘Ashar”
Maana ya Asl Makala Asili: Asl Neno “Asl” ni jina lipewalo kitabu cha Hadithi, ambacho mwandishi wake aliandika Hadithi hizo moja kwa moja au kwa kupitia mpokezi anaye nukuuu moja kwa moja kutoka kwa Maimamu Mwenyewe. [1] Yaani baina ya mwandishi na Imamu ni ngazi moja tu (mtu mmoja), kwa hiyo Hadithi zake huwa hazipiti katika matabaka mbali mbali. Hadithi zilizomo katika kitabu cha “Asl” , huwa hazikutokana na kitabu chengine; bali, zinajumuisha masimulizi ambayo mwandishi mwenyewe aliyapata kutoka kwa Ma'sum au kwa mtu ambaye alizipokea moja kwa moja kutoka kwa Ma'asum na kuzirekodi kitabuni mwake. [2] Kulingana na mwandishi wa kitabu Dirasatu Hawla al-Usuli al-Arba'ami-a, istilahi ya kutumia neno "Asl" kwa mara ya kwanza kabisa, ilianza kutumika katika fasihi za wanazuoni wa Kishia baada ya karne ya tano Hijria. [3] Istilahi hii ilijitokeza zaidi katika maandiko ya Sheikh Mufid, Najashi, na Sheikh Tusi. [4]
Nafasi na Uaminifu wa Usul al-Arba'mi'ah Kwa mujibu wa maelezo ya Feidh Kashani, Usul al-Arba'ami-a, ilikuwa ni mojawapo ya vigezo na nyenzo muhimu ya kupima usahihi wa Hadithi. Wanazuoni wa Kishia wa mwanzo walikuwa na desturi ya kuziamini kuzipa hukumu ya usahihi zile Hadithi zilirekodiwa ndani ya vitabu tofauti vya Usul al-Arba'ami-a, zile zinazopatikana katika angalau katika kitabu kimoja au viwili vya Usul al-Arba'ami-a, pamoja na zile zilizonukuliwa kupitia mfululizo wa wapokezi wa kuaminika kutoka katika matabaka tofauti ya wapokezi wa Hadithi, [5] ua zilizo andikwa na mmoja wa wandishi (mmiliki) wa Usul al-Arba'ami-a, ambaye ni mmoja wa wapokezi wanaokubalika mbele ya wanazuoni wa Kishia. [5] Yasemekana kwamba; wanazuoni wa Kishia wanawafikiana ya kwamba; vitabu hivi vilikuwa ndiyo msingi wa uandishi wa mikusanyo (ensaiklopidia) muhimu zaidi za Hadithi za Kishia, na kwamba hadithi nyingi zilizomo ndani ya vitabu vinne vikuu vya Hadithi za Kishia (Kutub al-Arba’a) zilichukuliwa kutoka kwenye Usul al-Arba'ami-a. Hii inathibitisha umuhimu mkubwa wa vitabu hivi katika historia ya elimu ya Hadithi na fiqhi ya Kishia. [6] Agha Bozorge Tehrani, mtaalamu mashuhuri wa Kishia wa fani ya utafiti wa vitabu, ametoa maelezo ya kina kuhusu umuhimu wa Usul al-Arba'ami-a , akibainisha mtazamo wake kwa njia ya maandishi, amesisitiza ya kwamba; uwezekano wa kutokea makosa na hali ya kusahau katika vitabu hivi, ni mdogo mno ikilinganishwa na vitabu vyengine vya Hadithi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba; Hadithi zilizo kusanywa ndani ya vitabu hivi, ima zilitokana moja kwa moja kutoka kwa Ma'asum (a.s), au kupitia mpokezi anaye nukuu moja kwa moja kutoka kwa Imamu. Hili ndilo lililo pelekea vitabu hivi kuaminika zaidi kuliko vitabu vyengine vya Hadithi. Hadithi zitokazo kwenye Usul al-Arba'ami-a hupewa tahamani zaidi, hasa ianpokuwa mwandishi wa Usul al-Arba'ami-a, alikuwa ni miongoni mwa mpokezi mwenye sifa za kuaminika na aliyetimiza vigezo vya kisheria vya upokezi wa Hadithi, hali ambayo hupelekea kunathibitishwa kwa usahihi wa Hadithi zilizomo ndani yake. [7] Kwa msingi huo basi, wanazuoni wa elimu ya rijal (wasifu wa wapokezi wa hadithi) wanaposema kuwa mpokezi fulani alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa “Asl”, hilo huchukuliwa kuwa ni sifa ya kipekee kwa mpokezi huyo. Hii ni kwa sababu ya kwamba; jambo hilo laashiria kuwa mpokezi huyo alikuwa na jitihada kubwa katika kuhifadhi na kurekodi Hadithi kwa usahihi, huku akihakikisha kuwa maneno ya Ma'asum yamenukuliwa bila mabadiliko yoyote. Tendo ambalo hupelekea Hadithi hizo kubakia na uthabiti wake wa asili, na kuongeza uaminifu wa Usul al-Arba'ami-a, katika tafiti za kielimu na za kihistoria. [8] Historia • Wanazuoni wa Kishia wanakubaliana kwamba; Mjumuiko wa vitabu vya Usul al-Arba'ami-a, ulikusanywa na kuandikwa katika mnamo za Maimamu (a.s), nazo ni kuanzia zama za Imamu Ali (a.s) hadi kipindi cha Imamu Hassan al-Askari (a.s). [9] Hata hivyo, kuna mitazamo tofauti kuhusu wakati halisi wa kuanza kwa uandishi wa vitabu hivyo. Katika suala hili, kuna maoni mawili makuu yafuatayo: [10] Kulingana na mtazamo wa kwanza, uandishi wa vitabu hivi ulianza tangu wakati wa Imamu Ali (a.s) na ukaendelea hadi kipindi cha Imamu Hassan al-Askari (a.s). Wanazuoni wakubwa kama Sayyid Muhsin Amin na Sheikh Mufid ni miongoni mwa wanaounga mkono mtazamo huu, wakiona kwamba; uandishi wa mijumuiko hii ya “Usul” ulianza mapema na uliendelea katika nyakati zote za Maimamu, ukikusanya mafundisho ya moja kwa moja kutoka kwao.
• Mtazamo wa pili unaamini ya kwamba; vitabu vya “Asl au Usul ”, viliandikwa katika kipindi cha Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s) kwa muda mfupi tu kabla au baada ya kipindi chake. Kuna wanazuoni kadhaa wanaounga mkono mtazamo huu, akiwemo Shahidu al-Awwal, Muhaqqiq al-Hilli, na Mir Damad, ambao wanashikilia mtazamo huu [11] wakisisitiza ya kwamba; hali ya kisiasa na kijamii ya wakati wa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s) ilikuwa ni yenye utulivu zaidi, hivyo kutoa nafasi na fursa nono kwa wafuasi wake kukusanya na kuandika Hadithi kwa mpangilio na kwa wingi zaidi. Mitazamo miwili hii inaonesha jinsi Usul al-Arba'ami-a inavyothaminiwa katika historia ya elimu ya Kishia, ikiwa ni hazina muhimu ya maarifa na mafundisho yaliyo pokewa moja kwa moja kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s). Muhammad Hussein Husseiniy Jalaliy, katika kitabu chake “Dirasah Hawla al- Usul al-Arba'ami-a”, ameunga mkono kwa nguvu zote mtazamo wa pili kuhusiana na uandishi wa vitabu hivi. [12] Yeye anaeleza kwamba; vitabu vingi vya “Asl” vilikusanywa katika kipindi cha Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s) au muda mfupi kabla au baada ya kipindi chake, hii ni kutokana na mazingira mazuri yaliyo kuwepo wakati huo kwa ajili ya kuandika na kuhifadhi Hadithi. Mtazamo huu umepata msisitizo mkubwa zaidi kwa sababu ya mazingira ya kiutulivu ya zama hizo yaliyowezesha uandishi wa vitabu hivi muhimu kukamilika. Kwa mujibu wa maelezo ya Agha Bozorge Tehrani, katika kitabu chake “al-Dhari'a”, ni kwamba; haijulikani kwa uhakika kamili ni lini hasa uandishi wa Usul al-Arba'ami-a ulianza. Akifafanua mtazamo wake huu anasema kwamb; hata hivyo, sisi tunaelewa kuwa, mjumuiko mwingi wa vitabu hivyo uliandikwa na masahaba wa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s) isipokuwa vitabu vichache tu miongoni mwavyo, ambao ima walikuwa ni Masahaba wake maalumu, au wanafunzi wa Imamu Baqir na Imamu Kadhim (a.s). [13] Majiid Ma'arif, mwandishi wa kitabu “Tarekh Umuumi Hadith”, ana mtazamo mwingine kinyume na mitazo miwili iliyotangulia. Yeye anadhani kwamba; vitabu vya “Dirasah Hawla al- Usul al-Arba'ami-a” viliandikwa katika vipindi vya Maimamu watatu ambao ni; Imamu Baqir (a.s), Imamu Sadiq (a.s), na Imamu Kadhim (a.s). [14] Akitetea mtazamo wake, ametumia hoja na ushahidi usemao kwamba; Hadithi nyingi zilizomo ndani ya “Dirasah Hawla al- Usul al-Arba'ami-a” zinatokana na mafundisho ya moja kwa moja kutoka kwa Maimamu watatu hawa. [15]
Sababu ya Kuenea Desturi ya Uandishi wa Vitabu vya “Asl” Katika Kipindi cha Imamu al-Sadiq (a.s) Sababu ya kuenea kwa uandishi wa “Asl” miongoni mwa Waislamu wa Kishia katika kipindi cha Imamu al-Sadiq (a.s) inahusishwa na hali ya kisiasa na kijamii ya wakati huo. Kipindi cha uongozi wa Maimamu al-Baqir (a.s), al-Sadiq (a.s), pamoja na sehemu kipindi cha uongozi wa Imamu al-Kadhim (a.s) viliambatana na wakati wa udhaifu wa utawala wa Bani Umayyah na kisha kupata nguvu kwa Bani Abbas. Katika kipindi hichi cha mpito, watawala walikuwa wamejishughulisha zaidi na migogoro ya kisiasa ya wenyewe kwa wenyewe, kwa hiyo hawakuwa na muda wala uwezo wa kuwabana sana Maimamu na wafuasi wao.
Kutokana na hali hii, Maimamu walipata fursa ya kueneza mafundisho yao ya kidini kwa uhuru zaidi, bila kukabiliwa na vizuizi vikali kutoka kwa watawala. Kwa upande wao, wapokezi wa Hadithi wa Kishia walipata nafasi ya kuhudhuria darsa au mafunzo ya wazi na ya faragha ya Maimamu hao, ambapo walijifunza Hadithi na mafundisho mengine moja kwa moja kutoka kwao. Katika mazingira haya ya utulivu na uhuru wa kidini, wapokezi hawa walikuwa na uwezo wa kuandika na kurikodi Hadithi hizo bila hofu ya mateso au uingiliaji wa kisiasa. Hali hii ilitoa mchango mkubwa katika kuenea kwa uandishi wa vitabu vya “Asl” katika kipindi cha Maimamu watatu hawa (a.s). Uandishi wa vitabu hivi uliwezeshwa na mazingira haya mazuri, na hivyo ukawa ni sehemu muhimu ya kuhifadhi na kusambaza mafundisho ya Maimamu, ambayo yamekuwa na athari kubwa katika maendeleo ya Uishia. [16]
Kulinganishwa Kwake na Kitabu Musnad cha Ahlul-Sunna Mara nyingi Usul al-Arba'ami-a hulinganishwa na vitabu maarufu vya Ahlu al-Sunna, vyenye jina la Musnad au Masaaniid. Katika ulimwengu wa Kisunni, uandishi wa Masaaniid ulikuwa na umaarufu mkubwa katika zama mbali mbali. [17] Kuna mambo kadhaa yanayofanana kati ya vitabu vya “Usul” na Musnad au Masaaniid. Sifa kuu zinazo vikutanisha vitabu hivi ni kwamba; Msingi mkuu wa kukusanya na kuratibu Hadithi ni mpokezi wa Hadithi, badala ya mada za hadithi hizo. Hii ina maana kwamba katika vitabu vya “Usul” na Musnad, Hadithi za mpokezi mmoja hukusanya na kuratibiwa kulingana na mpokezi wake, bila kuzingatia mpangilio wa mada za Hadithi hzio. Sifa nyengine unganishi ziunganishazo vitabu viwili hivi, ni kwamba; vitabu vyote viwili hutegemea upokeaji na usikivu wa moja kwa moja wa Hadithi zake, na si kwamba Hadithi zake zinatokana na vitabu au vyanzo vyengine mbali mbali, jambo ambalo huleta uhalisia zaidi wa Hadithi zilizomo ndani yake. Mlingano mwingine muhimu ni kwamba: kama ilivyokuwa Usul al-Arba'ami-a ni msingi ndio msingi na chimbuko la uandishi wa vitabu muhimu mbali mbali vya hadithi za Kishia, vivyo hivyo kwa upande wa vitabu vya Hadithi za Kisunni, navyo pia viliandikwa kwa msingi wa Masaaniid. Hii inaonesha umuhimu wa vitabu hivi katika kuhifadhi na kusambaza mafundisho ya dini katika madhehebu yote mawili. [18] Hata hivyo, wanazuoni wa Kishia wanaona kuwa; si kwamba kuna mifanano tu baina ya makundi mawili ya vitabu hivyo, bali pia kuna tofauti muhimu kati ya vitabu vya Usul al-Arba'ami-a na vitabu vya Musaaniid. Moja ya tofauti hizo ni kwamba; vitabu vya Usul al-Arba'ami-a vilikusanya Hadithi zilizopokelewa moja kwa moja au kupitia mpokezi mmoja tu kutoka kwa Imamu wa Kishia, hali inayopunguza sana uwezekano wa makosa na mabadiliko katika hadithi hizo. hili linadhamini kuwepo kwa ukaribu mkubwa wa Hadithi hizi na chanzo chao cha awali, kwa kuwa mlolongo wa wapokezi ni mfupi mno. Ila kwa upande wa pili, mara nyingi Hadithi za Musnad huwa zina mfululizo wa wapokezi wanne, watano, au hata sita kabla ya kufikia kwa Mtume (s.a.w.w). Hivyo basi, kulingana na mtazamo wa Kishia, vitabu vya Masaaniid haviwezi kuhesabiwa kuwa vya daraja la kwanza kwa mujibu wa vigezo vya uhakika wa upokezi wake. Tofauti hii inaonesha jinsi ya vitabu Usul al-Arba'ami-a vilivyokuwa hadithi zenye hadhi ya ukaribu zaidi na vyanzo asili, huku Musnad zikichukuliwa kuwa na thamani ya chini kulingana na mnyororo mrefu zaidi wa wapokezi wake. [19]
Idadi ya Vitabu vya “Usul” Mtazamo maarufu miongoni mwa wanazuoni wa Kishia ni kwamba vitabu vya “Usul” mia nne [20] au kwa mujibu wa Agha Bozorge Tehrani, havikuwa chini ya vitabu mia nne, yaani vyaweza kuwa ni zaidi ya hapo. [21] Wanazuoni mashuhuri kama Sheikh Mufid (kulingana na simulizi zilizomo katika kitabu “Ma'alim al-Ulamaa” ingawa halipatikani katika maandiko yake ya moja kwa moja), pi Fadhlu bin Hassan Tabarsi, Sheikh Baha'i, Hur al-Amili, na Mir Damad, wote ni wanye kuthibitisha na kuunga mkono mtazamo huu. [22] Kwa mfano, katika kitabu “Ma'alim al-Ulama”, imesimuliwa ya kwamba, Sheikh Mufid akigusia suala hili alisema kuwa; waumini wa Kishia waliandika vitabu mia nne vinavyojulikana kwa jina la “Usul”, kazi ambayo ilianzia wakati wa Imamu Ali (a.s) hadi wakati wa Imamu Hassan al-Askari (a.s). Hii ni aina fulani ya ithibati muhimu juu ya uwepo wa idadi hiyo ya vitabu vya “Usul”. [23] Aidha, Sayyid Muhsin Amin, mwandishi wa “A'yan al-Shi'a”, nasema kuwa; Waislamu wa Kishia waliandika vitabu elfu sita kutoka wakati wa Imamu Ali hadi Imamu Hassan al-Askari (a.s), ambapo vitabu mia nne kati yake vilizingatiwa kuwa na umuhimu wa kipekee, ambavyo miongoni mwa wafuasi wa Kishia, vilijulikana kwa jina la Usul al-Arba'ami-a. [24] Mtazamo Ulio Kinyume na Maoni Maarufu Katika kitabu “Dirasah Hawla al-Usul Usul al-Arba'ami-a”, Jalaliy Hussainiy amekuja na uendao kinyume na mtazamo maarufu kuhusiana na idadi ya vitabu vya “Usul” katika historia ya Kishia. Hussaini anadai kwamba; idadi ya vitabu vya “Usul” haifiki vitabu mia nne kama ilivyodhaniwa na wanazuoni wengi wa Kishia, bali haizidi vitabu mia moja. [25] Sababu kuu anazozitaja katika usemi wake huo ni kwamba; katika utafiti wake, hakupata zaidi ya vitabu sabini na kitu, vilivyotajwa katika maandiko ya wanazuoni wakubwa wa Kishia kama Sheikh Tusi na Najashi, ambao walikuwa ni mashuhuri na mabingwa kwa kuorodhesha vitabu vya Kishia. Hussainiy anasisitiza kwamba Sheikh Tusi, ambaye alikuwa ameahidi kukusanya na kuorodhesha vitabu vyote vya Kishia, hakutaja na zaidi ya idadi hii, jambo linaloashiria kwamba vitabu vilivyostahili kuitwa “Usul” vilikuwa vichache kuliko inavyodhaniwa. [26] Hussainiy pia anasema kuwa; tofauti ya tafsiri iliopo katika kufasiri maana ya neno "Usul" miongoni mwa wanazuoni wa Kishia ilisababisha kutofautiana kwa maoni kuhusu idadi ya vitabu hivi. Wanazuoni wengine walikiita kila kitabu chenye kuaminika kwa jina la "Usul ", huku wengine wakikihisabu kila kitabu ambacho hakikutolewa kutoka katika kitabu chengine kuwa ni "Usul ". Kwa mujibu wa maoni ya Hussainiy, ni kwamba; kauli inayosema kuwa Waislamu wa Kishia waliandika vitabu elfu sita vya hadithi, na kwamba mia nne kati yavyo vilikuwa ni “Usul”, haimaanishi kwamba kulikuwa na vitabu mia nne vilivyokuwa maalum kama “Usul”, bali inaashiria kuwa vitabu hivyo mia nne vilichukuliwa kuwa ni miongoni mwa vitabu vinayo aminika zaidi na vilivyopata umuhimu wa kipekee kwa wanazuoni wa Kishia. Hii kwa maoni yake, inamaanisha kwamba idadi halisi ya vitabu vya “Usul” inaweza kuwa ni ndogo zaidi kuliko ilivyodhaniwa na wanazuoni mbali mbali. [27] Mtazamo Unaounga Mkono Majiid Ma'arif, mwandishi wa kitabu “Taarikh Umumiye Hadith”, anakubaliana na mtazamo maarufu juu ya idadi ya vitabu vya “Usul”, ambapo ameandika akisema ya kwamba; kuna ushahidi mwingi unathibitisha uhalali wa mtazamo huo. Ma'arif anasisitiza kuwa; katika vitabu vya Najashi na Sheikh Tusi, kuna zaidi ya wafuasi mia tano wa Imam Baqir hadi Imam Kadhim (a.s) waliotajwa kama ni waandishi wa vitabu vya Hadithi vilivyopokewa moja kwa moja kutoka kwa Maimamu hao (a.s). Hii ni moja ya hoja na vielelezo vinavyo tumika kuthibitisha kuwa; kulikuwa na idadi kubwa ya vitabu vya “Usul”. [28] Pia Ma'arif Katika kitabu chake hicho, amerejelea maneno ya Sheikh Tusi katika kitabu “Al-fihrist”, ambacho ni moja ya kazi mashuhuri katika kuorodhesha vitabu vya “Usul” na maandiko mengine ya Kishia. Akirejelea kitabu hicho alisema kwamba; Sheikh Tusi alisema kuwa; yeye (Sheikh Tusi) hakuwa na uhakika wenye kudhamini kuwa yeye aliweza kuwafahamu na kuwaorodhesha waandishi wote wa vitabu hivyo, jambo linalashiria kwamba; kuna uwezekano wa kuwepo kwa vitabu zaidi ya vile vilivyotambuliwa na kuorodheshwa kitabuni humo. Hali hii inaunga mkono wazo kwamba idadi ya vitabu vya “Usul” ilikuwa ni kubwa zaidi, ikiendana na kauli maarufu inayosema kwamba kulikuwa na vitabu vinne mia vya “Usul”. [29]
Hatima ya Vitabu vya Usul al-Arba'ami-a Inasemekana kwamba Waislamu wa madhehebu ya Kishia walitilia mkazo mkubwa umuhimu wa kuhifadhi na kulinda vitabu vya “Usul al-Arba'ami-a”, hata hivyo baada ya kuanzishwa kwa vitabu vya tofauti vya ensaiklopidia za Hadith, hitaji la kuhifadhi vitabu hivi lilipungua. Hii ndiyo sababu, iliyo pelekea kuwepo kwa vitabu vichache tu vya “Usul” vilivyo baki hadi leo, huku vingine vingi vikiwa vimepotea na kutoweka kabisa. [30] Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kwamba; wakati wa uandishi wa vitabu vikuu vinne, maarufu kwa jina la “Kutub al-Arba’a”, ambavyo ni miongoni mwa vitabu muhimu zaidi vya Hadithi za Kishia , bado vitabu vingi vya “Usul al-Arba'ami-a” vilikuwa vinapatikana. [31] Hadithi nyingi zilizomo ndani ya vitabu vya “Kutub al-Arba’a”, zilichukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye vitabu vya “Usul” ambavyo vilikuwepo hadi wakati huo. [32] Kwa sasa, vitabu vya “Usul” vilivyobakia, ni kumi na sita tu, ambavyo vinajulikana kwa jina la “Al-Usul al-Sitatu 'Ashar” ambavyo ukiachana na asili ya vitabu vyenyewe vya kale, pia vitabu hivi vimechapishwa na nutolewa kupitia matoleo mbali mbali. [33] Miongoni mwavyo ni:
1. Kitabu (Asl) cha Zaid Zarrad Kufi 2. Kitabu (Asl) cha Abu Said Abad Usfuri 3. Kitabu (Asl) cha ‘Asim bin Humayd Hannaat Kufi 4. Kitabu (Asl) cha Zaid Narsi Kufi 5. Kitabu (Asl) cha Ja'afar bin Muhammad bin Shuraih Hadhrami 6. Kitabu (Asl) cha Muhammad bin Mathna Hadhrami 7. Kitabu (Asl) cha Abdulmalik bin Hakim Khath-ami 8. Kitabu (Asl) cha Muthanna bin Waleed Hannat 9. Kitabu (Asl) cha Khallaad Sindiy 10. Kitabu (Asl) cha Hussein bin Othman ‘Aamiriy 11. Kitabu (Asl) cha Abdullah bin Yahya Kahili 12. Kitabu (Asl) cha Sallam bin Abi ‘Amra 13. Kitabu (Asl) cha Ali bin Asbat Kufi au Nawadir Ali bin Asbaat Kufi 14. Kitabu (Asl) cha Alaa bin Razin al-Qalaa (mukhtasari) 15. Kitabu (Asl) cha Darust bin Abi Mansur Muhammad Wasiti 16. Kitabu (Asl) cha Abdullah bin Jabri maarufu kama Diyat Dhuraif bin Nasih Kufi [34]