Ukoloni
Ukoloni: Ukoloni ni hali ya ukaliwaji wa kimabavu wa taifa moja kupitia taifa jengine bila ya mamlaka halali, bali ni kwa njia ya kulazimisha na kulifanya taifa hilo, na hatimae kuwa ni taifa tegemezi, duni na lisiloendelea. Ukoloni wa Wazungu ulianza kwa kukalia kimabavu nchi za Waislamu kaskazini mwa Afrika, kisha kusambaa kwenye mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na mataifa ya Kishia ikiwemo; Iran, Iraq, na India. Kwa mujibu wa maelezo ya watafiti mbali mbali, Iran haikuwahi kuwa ni koloni rasmi la nchi fulani; hata hivyo, kupitia mikataba ya biashara iendayo kinyume na haki, nchi hii ilionekena kuathiriwa na nguvu za kikoloni. Wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, wanajeshi wa Uingereza waliikalia Iraq kimabavu na kuweka serikali ya kupitia vibaraka wake walioko nchini humo. Nchini India, serikali ya Kishia ya Awadh ilipinduliwa kupitia kampuni ya Uingereza ya India ya Mashariki. Ukaliaji wa Palestina kimabavu na kuanzishwa kwa Israeli pia ni matokeo ya njama za ukoloni.
Moja ya mbinu muhimu za wakoloni ni kuleta mfarakano ndani ya nchi walizokalia kimabavu na hatimae kunyakua rasilimali zao za kiuchumi zilizomo ndani ya nchi hizo. Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, Utawa wa Ottoman ilifarakanishwa na kugawanywa kupitia nguvu za kikoloni, na hatimae kukatengenezwa vijinchi vidogo vidogo kama vile Iraq, Syria, na Lebanon. Kuteka rasilimali asili, mikataba ya ukandamizaji wa kikoloni, mabadiliko ya kitamaduni na lugha, na kudhoofisha utambulisho wa ndani, ni miongoni mwa mbinu za kikoloni zilizotumiwa na wakoloni hao.
Waislamu walisimama na kulipingana na ukoloni kwa njia mbalimbali. Miongoni mwa njia hizi ni fatwa za wanazuoni wa Kishia nchini Iraq na Iran, kuanzishwa kwa mashirika ya kupinga ukoloni, kujitete kwa njia ya kutumia silaha, mapinduzi, au harakati za kupigania uhuru zisizo kwa njia ya amani.
Uchambuzi wa Dhana ya Ukoloni na Nafasi Yake
Katika istilahi ya kisiasa, ukoloni unamaanisha udhibiti wa kitamaduni, kisiasa, na kiuchumi unaofanywa na taifa lenye nguvu dhidi ya taifa dhaifu na kuendelea kulifanya taifa hilo kuwa tegemezi, duni, na lililo baki nyuma kimaendeleo. [1] Ukoloni unahusiana kwa karibu sana na dhana ya unyonyaji (exploitation). [2] Kuimarika kwa utawala wa Ottoman na kukatika kwa njia za ardhini kati ya Ulaya na Asia [3], pamoja na tamaa ya kurimbika mali katika makanisa ya Ulaya na tamaa ya kunyakua utajiri wa nchi za mashariki, ndizo sababu kuu zilizowafanya Wazungu kuingia katika mfumo wa ukoloni wa kuwatawala wengine. [4]
Inasemekana kuwa pale Wazungu wa karne ya kumi na tano na kumi na sita walipoanza kuyakalia maeneo ya Waislamu ya kaskazini mwa Afrika, mbali na malengo ya kiuchumi, pia walikuwa na nia ya kupambana na kuenea kwa Uislamu uliokuwa ukienea katika maeneo hayo. [5] Kulingana na kumbukumbu za kihistoria, nchi nyingi za Kiislamu na jamii za Kishia ziliathariwa na ukoloni wa Wazungu. [6] Kwa mujibu wa maoni ya watafiti wa kihistoria, ni kwamba; kutokana na vitendo vya wakoloni katika nyanja za kisiasa, kijamii na kitamaduni vilivyofanywa na wakoloni hao katika nchi walizozikaliwa kimabavu, nchi hizo zilipata mabadiliko makubwa katika nyanja za kijiografia, ikiwa ni pamoja na kutekwa na kugawanya kwa ardhi za nchi hizo. [7] Mabadiliko mengine yaliojiri kupitia ukoloni huo wa Wazungu ni mabadiliko ya kitamaduni, na kijamii pamoja na kudhoofishwa maadili ya kitaifa na kidini na kubadilisha mitindo na mifumo ya maisha ya nchi hizo. [8] Wakoloni wa kizungu walizdhoofisha nchi mbali mbali kiuchumi kwa kunyakua rasilimali zao na kuanzisha mifumo ya kuzalisha bidhaa mmaalumu [9] katika nchi hizo kulingana na matakwa yao.
Uenezi wa Ukoloni katika Jamii za Kiislamu
Watafiti wanaamini kuwa Sebta au “Ceuta” (ulio kaskazini mwa Moroko ya leo) ni eneo la kwanza la Waislamu kukaliwa kimabavu na Wazungu. [10] Nchi kama vile; Algeria, Libya, Misri, na Tunisia ni miongoni mwa nchi za Waislamu zilizokuwa zikikaliwa kimabavu na kugeuzwa kuwa ni makoloni ya Wazungu. [11] Miongoni mwa mataifa ya Kishia, ni; Iran, Iraq, na Awadh (katika India) ndio miongoni mwa mataifa na jamii ziliathiriwa na ukoloni. [12]
Iran na Mikataba ya Kikoloni
Iran haijawahi kuwa koloni rasmi la nchi nchi yoyote ile ya Ulaya; hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa tangu kuwasili kwa kundi la kwanza la wakoloni katika karne ya 16 [13] hadi kufikia kipindi cha mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, [14] nchi hii ilikuwa chini ya taathira na ukandamizwaji wa nchi za kikoloni. Baadhi ya nyaraka na maandishi ya kihistoria yanayohuisiana na mawasiliano mbali mbali, yanaonyesha kuwa; baadhi ya mikataba ya kibiashara ya Iran na mawakala wa kigeni ni miongoni mwa mifano ya udhibiti wa nguvu za kikoloni dhidi ya Iran. [15] Katika karne ya ishirini, Mohammad Mossadegh na Abul-Qasim Kashani, kupitia msaada wa wananchi nchii hii, waliweza kuondoa mpango wa mafuta ya Iran kutoka miokononi mwa udhibiti wa mawakala wa Kiingereza, na kuyarudisha kwenye sekta ya kitaifa. [16] Hata hivyo, mnamo tarehe 28 Mordad 1332 (Agosti 19, 1953), serikali ya Mossadegh (waziri kiongozi), iliangushwa kupitia mapinduzi yaliosababiswa na shinikizo na usaliti wa Uingereza pamoja na Marekani. [17]
Ukaliaji wa Iraq na Wanajeshi wa Kiingereza
Wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia vya 1914, Uingereza ilitangaza vita dhidi ya utawala wa Ottoman. [18] Kulingana na ripoti mbali mbali, Waingereza walidhani kuwa Waislamu wa Kishia wangewaunga mkono Waingereza na kuwafukuza mawakala wa utawala wa Ottoman kutoka nchini Iraq. [19] Kinyume na dhana hii, na licha ya kuwa wanazuoni wa Kishia wa Iraq walikuwa na malalamiko dhidi ya utawala wa Ottoman, ila katu hawakuungana na njama za Waingereza, na badala yake walitoa fatwa ya jihad dhidi ya uvamizi wa Uingereza; hii ni kwa sababu ya yao ya kwamba, ni haramu kwa Wakristo kuzikalia na kuzitawala ardhi za Kiislamu. [20] Hata hivyo, wanajeshi wa Kiingereza waliweza kufanikisha njama zao kwa kwa kutumia silaha nzito, nguvu za anga, [21] na nguvu za binadamu zilizotumwa kutoka India, [22] kwa ajili ya kuidhibiti Iraq.
Kupinduliwa kwa Serikali ya Kishia ya Awadh huko India
Mnamo karne ya kumi na nane (1757 hadi 1764), Kampuni ya Kiingereza ya India ya Mashariki, ilianzisha vita dhidi ya serikali za mitaa za India, ikiwa ni pamoja na serikali ya Kishia ya Awadh, na hatimae kuziangusha serikali hizo. [23] Kuanzia wakati huo na kuendelea, Kampuni hiyo ya Kiingereza, ilianza ukandamizaji kupitia nyenzo tofautu ikiwa ni pamoja na; kutumia ushawishi ulionao katika eneo hilo, usaliti wa kuvunja mikataba, pamoja na ukusanyaji wa kodi zilizokiuka viwango kutoka kwa wamiliki wa ardhi wa eneo hilo. Hatimae ukandamizaji huo ulisababisha kuvuruga uhusiano na uwiano uliopo kati ya watawala wa Awadh na wamiliki wa ardhi wa eneo hilo, jambo lilisababisha machafuko ndani ya jamii. [24] Aidha, Uingereza ilitoa mikopo mikubwa kwa serikali ya Awadh na badala ya madai yake ya kutaka kurudishiwa fedha zake, Serikali ya Uingereza iliamua kuchukua sehemu ya ardhi za Waislamu na kudhibiti mahusiano kigeni ya India na kuifanya serikali ya Awadh kuwa serikali ya vibaraka. [25] Mnamo mwaka 1858, kwa kisingizio cha kukomesha machafuko ya Awadh, Uingereza iliipindua serikali ya Kishia ilioko katika eneo hilo, na kuligeuza eneo hilo kuwa ni sehemu ya milki ya Uingereza. [26]
Ukaliwaji wa Palestina Kimabavu
Wanafikira wengi wanaamini kwamba; suala la ukaliwaji wa Palestina kimabavu ni moja ya matokeo ya ukoloni wa Kimagharibi. [27] Kulingana na wanafikra hawa, kushindi kwa Dola la Ottoman katika Vita vya Kwanza vya Dunia na mamlaka ya Uingereza juu ya Palestina ndiko kulikopelekea kuibuka kwa Israeli. [28] Mbali na jinsi Israeli ilivyoundwa, wachambuzi wengine wanaamini kwamba; mchakato wa ujenzi wa makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina ni miongoni mwa mifano halisi ya a ukaliaji wa nchi za wengine kikoloni. [29] Aidha, juhudi za utawala huu wa Kizayuni katika kudhibiti Ukanda wa Gaza na kujenga maeneo ya makazi ya Wayahudi katika eneo hili zinahisabiwa kuwa ni moja wapo ya matunda ya ukoloni wa Kimagharibi. [29]
Fatwa ya Jihad ya Muhammad Taqi Shirazi
"Ni wajibu kwa watu wa Iraq kudai haki zao, na ni juu yao kuhakikisha utulivu na usalama wakati wa kupigania madai yao. Ikiwa Waingereza watakataa kukubali madai ya watu, hapo kila mmoja ataruhusiwa kutumia nguvu na uwezo wake katika harakati za kujihami." [31] |
Mbinu za Kupambana na Ukoloni
Fatwa za Wanazuoni Dhidi ya Wavamizi
Miongoni mwa nyaraka zilizobaki mikononi mwa tarehe, kuna mifano kadhaa ya upinzani dhahiri wa wanazuoni wa Iraq dhidi ya ukoloni wa Uingereza. Kwa mfano, zama za utawala wa Qajar, Sayyid Muhammad Kadhim Yazdi alitangaza fatwa ya wajibu kupambana dhidi ya ukoloni wa Muingereza. [32] Wengine walitoa aina kama hiyo ya fatwa ni Muhammad Taqi Shirazi [33] na aliyekataza na kuharamisha kwa Waislamu kuajiriwa ndani ya mashirika ya Kiingereza. [34] Kwa mujibu wa maelezo ya wanahistoria, ni kwamba; baadhi ya wanazuoni walikuwa mstari wa mbele katika kuongoza mapambano dhidi ya Uingereza, miongoni mwa wanazuoni hao ni pamoja na; Akhund Khorasani [35] na Sheikh al-Shari'a Isfahani. [36] Mbali na Iraq, uwepo wa majeshi ya kigeni nchini Iran pia ulikabiliwa na vikwazo kutoka Kwa mfano mnamo mwaka 1329 H (1911 BK), baada ya mashambulizi ya majeshi ya Urusi kaskazini mwa Iran, wanazuoni mbali mbali akiwemo; Muhammad Taqi Shirazi, walitoa fatwa ya kupambana na wavamizi hao. [37] Fatwa hizi hazikuhusu tu utetezi wa ardhi za Kishia bali zilijumuisha ardhi zote za Waislamu ulumwenguni humu. Kwa mfano, katika tukio la ukaliwaji wa nchi ya Libya kimabavu lilikofanywa na wanajeshi wa Italia, au pia katika uvamizi wa majeshi ya Urusi na Uingereza nchini Iran, Sayyid Muhammad Kazim Yazdi alijitokeza na kutangaza fatwa ya jihadi kwa ajili ya kupambana na wavamizi wa nchi hizo, huku akisema kwamba; ni amali hiyo ya jihadi ni jukumu la kila Muislamu ulimwenguni. [38]
Pia, kwa mujibu wa maelezo ya wanahistoria ni kwamba; baadhi ya wanazuoni wa Iran na Iraq walitengeneza makundi maalumu ya kupambana na ukoloni, ambayo baadhi yake ni kama vile; “Jam’iyyate Nahdhate Islami” (Jumuiya ya Harakati ya Kiislamu), “Hizb Sirriy Najaf” (Chama cha Siri cha Najaf) na “Hizb Sirriy Kaadhimain” Chama cha Siri cha Kadhimain. [39]
Upinzani Dhidi ya Mikataba ya Kikoloni
Kama inavyoonekana katika ripoti za kihistoria za enzi za Qajar, baadhi ya wasomi wa wakati huo, walikuwa na ufahamu wa kutosha juu ya dhana ya ukoloni na athari zake, hasa kuhusiana na zile athari za ukolono zilizokuwa zikijitokeza nchini India. [40] Kwa kuzingatia masuala haya, wanazuoni wa Kishia walipinga kwa sauti moja mikataba kadhaa ya kikoloni, ikiwa ni pamoja na; Mkataba wa Reuter unaohusiana na ujenzi wa barabara, reli, mabwawa, uchimbaji wa madini, misitu pamoja na mradi wa forodha za Iran). Mkaba mwengine muhimu uliopigwa vita na wasomi wa wakati huo, ni Mkataba wa Rigi (ukiritimba wa tumbaku na sigara). [41] Miongoni mwa juhudi zilioamsha harakati dhidi ya ukiritimba wa tumbaku, ni pamoja na mapambano ya Sayyid Jamal al-Din Asadabadi na fatwa ya Mirza Shirazi ilioharamisha sigara na matumizi yote ya tumbaku. [42]
Juhudi za Kupindua Serikali za Vibaraka
Mnamo mwaka 1932 BK (1340 H), wanazuoni kadhaa walisimama kupinga utawala wa Mfalme Faisal aliyekwa kama ni kibaraka kwa ajili ya ajenda za Uingereza, miongoni mwa waliosimama kupinga utawala huo ni pamoja na; Muhammad Hussein Na'ini, Sayyid Abul-Hasan Isfahani, Mahdi Khalisi, na Sayyid Hassan Sadr. [43] Pia, mnamo mwaka 1941 BK, baada ya Faisal kuingia madarakani, kuliibuka misimamo ya uasi dhidi yake, tokeo ambalo pia lilionekana kuungwa mkono na baadhi ya wanazuoni wa Kishia, akiwemo; Sayyid Abul-Hasan Isfahani, Muhammad Hussein Kashif al-Ghita, na Abdulkarim Jazairi. Wanazuoni hawa walisismama pamoja na jamii huku wakitangaza fatwa za jihad dhidi ya kiongozi huyo. [44]
Mapinduzi na Harakati za Kutafuta Uhuru Pasipo na Vurugu
Kwa mujibu wa maelezo ya wanahistoria, katika karne ya 19, juhudi za Wahindi za kupinga ukoloni wa Kiingereza, zilijikita zaidi kwenye mbinu za kutumia vurugu, lakini Waingereza walifanikiwa kuzima juhudi hizo za uasi wa kutumia nguvu dhidi yao. [45] Hata hivyo, kufikia karne ya 20, harakati za uhuru wa India zilianza kushika kasi chini ya uongozi wa Mahatma Gandhi, ambaye alifanikiwa kufikia malengo yake kwa kutumia mbinu za utulivu na usalama katika kugombea uhuru wa nchi yake. [46] Wakati huohuo, Waislamu wa India, waliinuka wakiwa na azma ya kujitenga na kujitawala wenyewe. Hatiame kwa kutumia njia ya kujishirikisha katika vyama vya kisiasa vya wakati huo, mwishowe walifanikiwa kujitenga na kuunda taifa lao wenyewe waliloliita “Pakistan”. [47]
Watafiti kadhaa wamejaribu kufananisha mbinu za kutotumia vurugu za Gandhi na mikakati iliyotumiwa na Imamu Khomeini nchini Iran, katika harakati za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [48] Imam Khomeini, katika maandishi yake pamoja na hotuba nyingi alizokuwa akizisambaza katika jamii, alionekana kuuelezea ukoloni kwa sifa mbali mbali, ikiwa ni pamoja na; kuutambua ukoloni kama ni chanzo cha uporaji wa rasilimali za kitaifa, chanzo cha utegemezi wa kiuchumi, uharibifu wa maadili na utamaduni wa ndani, kuvuruga dini pamoja na kuchochea mifarakano ya kidini na kimadhehebu. [49] Aliuona ukoo wa Pahlavi kama ni washirika msingi wa wakoloni. [50] Hata hivyo, watafiti wanaeleza kuwa; Imamu Khomeini hakuwa na imani na matumizi ya silaha katika kupambana na ukoloni wa zama zake. [51]
Mbinu za Ukoloni
Kufosi au Kuzigawanya Nchi
Moja ya mbinu msini za ukoloni ni kuteka mataifa ya watu na kuyakalia kimabavu. [52]. Kwa mfano, wakoloni wa Kireno wa karne ya 16 waliteka ardhi kazaa za mafia mbali mbali, ikiwa ni pamona na visiwa Hormuz pamoja na Bahrain. [53] Pia, imeripotiwa kuwa mwanzoni mwa karne ya 20, asilimia 90 ya ardhi ya Afrika ilikuwa juu ya mikono ya ukoloni. [54] Wakoloni wa Ulaya walikalia maeneo ya taifa la Ottoman kisha wakaligawanya kwa jinsi ya matakwa yao, na hivyo kuunda nchi mpya kabisa kama vile Iraq, Syria, na Lebanon. [55] Mchakato huu uliendelea na kushika kasi hata baada ya kumaliza kwa Vita vya Pili vya Dunia. Moja ya mifano ukaliaji wa nchi za watu kimabavu, ni kuanzishwa kwa Israeli, tukio lililotokea baada ya kumaliza kwa vita hivyo vya dunia. [56] Katika enzi za utawala wa Qajar nchini Iran, Uingereza ili iendelee kudumisha udhibiti wake juu ya India, pamoja na kueneleza ushindani wake dhidi ya Ufaransa na Urusi, iliamua kuvamia visiwa vya Ghuba ya Uajemi, kisha wakaamua kuitenganisha Afghanistan kutoka Iran, uamuzi ulioamuliwa kupitia Mkataba wa Paris. [57]
Kubadilisha Utamaduni wa Ndani
Kubadilisha utamaduni katika maeneo yaliyokaliwa ni moja ya mbinu za wakoloni za kumiliki udhibiti wa mataifa mbali mbali. [58] Hii inajumuisha kueneza dhana za uhuru usio na mipaka, kudhoofisha maadili ya ndani, pamoja na kubadilisha mfumo mzima wa nyenendo za kimaadili. [59] Kwa mfano, Waingereza walijaribu kuimarisha lugha ya Kihindi nchini India, dhidi ya Waislamu waliokuwa wakitaka kuimarisha lugha ya Kiurdu nchini humo; kutokana na hilo, Waislamu wa India walilazimika kuanzisha taasisi maalumu za kukuza lugha ya Kiurdu. [60] Vile vile, Ufaransa ilijaribu kueneza lugha ya Kifaransa nchini Lebanon na Syria, na pia kueneza mtindo wa maisha ya Kizungu katika mataifa hayo. [61]
Ukoloni wa Kiuchumi
Ukoloni wa kiuchumi unajumuisha njia tofauti, ikiwa ni pamoja ya na uporaji wa rasilimali na ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi mbali mbali. [62] Kwa mfano, lengo la wakoloni katika visiwa vya Ghuba ya Uajemi lilikuwa ni kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wa Ghuba ya Uajemi, kudhibiti usafiri wa baharini wa Bahari ya Hindi, na kudhibiti mapato ya uzamiaji wa lulu. [63] Pia, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, Urusi na Uingereza zilikalia maeneo ya kaskazini na kusini mwa Iran na kudhibiti faida za kiuchumi, kibiashara, na kijeshi za maeneo hayo. [64]
Miongoni mwa mbinu zisizo za moja kwa moja za ukoloni wa kiuchumi ni pamoja na kubadilisha mfumo wa kilimo na kuelekea kwenye zao moja maalumu, utegemezi wa mfumo wa uzalishaji wa koloni kwa nchi zilizotawaliwa kikoloni, na kulazimisha mifumo ya maendeleo kufuata matakwa ya mifumo yao. [65] Kwa mfano, watafiti wanasema kwamba; mikataba ya kigeni ya enzi za utawala wa Qajar nchini Iran, ilibadilisha Iran na kuifanya iwe na hali ya kikoloni, kwani mauzo ya malighafi yake kwa ajili ya nchi za nje, yalikuwa yakikua haraka, huku mauzo ya bidhaa zinazozalishwa nchini Iran yakididimia siku hadi siku. [66] Aidha, moja ya hatua za mwazo za wakoloni wa Kiingereza nchini India na Bangladesh, ilikuwa ni kuharibu viwanda na vilimo vya kienyeji na kuhakikisha wenyeji wa nchi hizo wanauza malighafi zao kwa wakoloni. [67] Inasemekana kuwa sera hii ilisababisha njaa kubwa, kwa mfano, kati ya mwaka 1880 na 1920, zaidi ya Wahindi milioni mia moja walikufa kutokana na njaa zilizotengenezwa na wakoloni hao. [68]