Nenda kwa yaliyomo

Udhu wa Jabira

Kutoka wikishia

Udhu wa Jabira (Kiarabu: الوضوء الجبيرة) Ni mojawapo ya aina za udhu. Udhu huu ni kwa ajili ya mtu mwenye jeraha au mvunjiko kwenye sehemu ya viungo vya mwili ambavo ni viungo vipaswavo kutiwa udhu wakati wa kutenda ibada maalumu. Udhu huu hufanyika iwapo mtu atashidwa kuosha viungo hivyo, au kupangusa juu yake kwa maji. Katika hali kama hiyo yabidi mtu atie udhu kama kawaida, na pale afikapo kwenye eneo la jeraha au mvunjiko huo, itabidi aweke kitambaa au plastiki juu yake, kisha apanguse juu ya kitambaa hicho kwa umaji maji au uchaba wa maji ya mkononi mwake. Si lazima mtu kutumia kitambaa, bali anaweza kutumia chochote kile ambacho hutumika kufungia jeraha.

Uchambuzi wa dhana

Neno jabira lina maana ya kipande cha kitambaa au chochote ambacho hutumika kufungia jeraha. [1] Ikiwa kuna jeraha au mvunjiko kwenye moja ya viungo vya udhu, na ikawa haiwezekani kusafisha au kulikosha jeraha hilo kwa maji, basi hapo ni lazima atie udhu wa jabira. Katika udhu huu, mtu hutakiwa atie udhu kama kama kawaida yake, ila badala ya kusafisha na kuosha sehemu iliyovunjika au yenye jeraha, yeye hupaswa kupitisha mkono ulio na maji juu ya kitambaa ambacho kimewekwa juu ya sehemu hiyo. [2] Udhu huu umepewa jina la udhu wa jabira (wa kitambaa), kutokana na kule mwenye kutia udhu kupitisha mkono wake ulio na maji maji juu ya kitambaa.

Sheria na hukumu

Ikiwa kuna jeraha au mvunjiko kwenye sehemu moja ya mwili ambayo inapaswa kuoshwa au kufutwa wakati wa udhu, na ikawa haiwezekani kuoshwa au kufuta sehemu hiyo kutokana na jaraha au mvunjiko bhuo, basi mtu hupaswa kutia udhu kama kawaida, ila badala ya kuosha au kufuta sehemu iliyopata jeraha au mvunjiko, hupaswa kupitisha mkono wenye umaji maji juu ya kitambaa kilichoko juu ya jeraha au mvunjiko huo. [3] Udhu wa jabira (kupitisha mkono wenye maji juu ya kitambaa) ni halali tu iwapo itakuwa ni vigumu kufungua kitambaa kilichofungwa juu ya kiungo hicho, au kutasababisha madhara, au haiwezekani kumimina maji moja kwa moja kwenye jeraha au mvunjiko huo. [4]

Katika baadhi ya hali fulani, tayammum hutumika na hushika nafasi ya wa udhu wa wajibu; kwa mfano, ikiwa kuna wakati mdogo kumalizika wakati wa sala, kiasi ya kwamba kuchukua kutia udhu kutapelekea sala yote au sehemu ya sala kuswaliwa nje ya wakati wake [5]. Pia, katika hali ambayo maji hayapatikani au maji yanaweza kusababisha madhara kwa mwili. Katika hali kama hizo hutumika tayammum badala ya udhu [6]. Mtu aliye koga josho la janaba hawa hana haja ya kutia udhu kabla ya kuswali, kwani kuoga janaba hutosheleza na hukamata nafasi ya udhu, yaani aliye koga janaba ni sawa na aliyetia udhu, ila ni lazima ieleweke ya kwama kutia udhu hakuchukui nafasi ya kukoga janaba. [7] Madhui na tafiti zinazo husiana: Udhu, Viungo vya Udhu, Jabira, Udhu wa Irtimasi (Kuchovya)