Udhayb al-Hijanat
Udhayb al-Hijanat (Kiarabu: عُذَیبُ الهِجانات) ni eneo lililopo karibu na mji wa Kufa na ni eneo ambalo Imam Hussein bin Ali (a.s) pamoja na masahaba zake walishukia hapo 28 Mfunguo Tatu Dhhul-Hija 60 Hijiria katika tukio la Karbala. Katika Udhayb al-Hijanat watu wanne wa mji wa Kufa walijiunga na Imam kwa muongozo wa Tirimmah ibn Adi. Walimfikishia Imam Hussein habari ya kuuawa shahidi Qays ibn Musahir Saidawi pamoja na ripoti ya hali ya mambo ya mji wa Kufa. Tirimmah alisikia habari ya kufa shahhidi Imam pamoja na masahaba zake akiwa katika eneo hilo.
Lilipo kijiografia na sababu ya kuitwa kwa jina hilo
Udhayb al-Hijanat ni eneo ambalo lipo umbali wa maili 4 kutoka Qadisiyyah na maili 32 kutoka Mughithah na katika njia ya Makka kuelekea Kufa. Eneo hili liliikuwa la watu wa ukoo wa Bani Tamim.[1] Udhayb imetokana na adhb yenye maana ya maji matamu.[2] na Hijanat ni wingi wa Hijan yenye maana ya ngamia mteule. Eneo hili lilikuwa sehemu ya malisho ya farasi wa Nu'man na liliondokea kuwa mashuhuri kwa jina hilo hilo. [3]
Matukio
Imam Hussein (a.s) akiwa pamoja na masahaba zake, 28 Dhul Hija 60 Hijiria aliwasili katika eneo hili la Udhayb al-Hijanat. Imam Hussein alipokuwa hapo alipata habari ya kuuawa shahidi Qays ibn Musahir Saidawi.[4] Njia ya baada ya Udhayb inaelekea Qadisiyyah na ilikuwa ikiishia Kufa. Hata hivyo Imam Hussein kwa ajili ya kuelekea Kufa alilazimika kubadilisha njia kwa kulazimishwa na Hurr bin Yazid al-Riyah na kuelekea upande wa Qasr Bani Muqatil.[5] Katika eneo la Udhayb al-Hijanat watu wa Kufa waliokuwa Nafi' ibn Hilla, Majma' ibn Abdallah Aidhi na Amr ibn Khalid Saydawi walijiunga na Imam Hussein kwa muongozo wa Tirimmah ibn Adi.[6] Hurr alikuwa na nia ya kuwatia mbaroni au kuwarejesha watu hao, lakini Imam alizuia hilo. Watu hao walimpa habari Imam Hussein kuhusiana na kuwa mbaya hali katika mji wa Kufa, kuuawa Qays ibn Musahir Saidawi na kujiandaa jeshi kubwa kwa ajili ya kupigana vita na Imam Hussein (a.s).[7] Maj'ma' ibn Abdallah Aidhi alisema:
- Mabwanyenye na shakhsia wakubwa wa mji wa Kufa kutokana na rushwa waliochukua wako dhidi yako, watu wengine waliobakia kiroho wako na wewe lakini panga zao ziko dhidi yako.[8]
Akiwa hapo, Imam Hussein alifanya mazungumzo na Tirimmah.[9] Tirimmah alimpatia Imam Hussein (a.s) baadhi ya mapendekezo ambayo hayakukubaliwa na Imam. Tirimmah alisikia habari ya kuuawa shahidi Imam Hussein akiwa katika eneo hilo hilo au jirani na hapo na alisikia hilo kutoka kwa Samma'ah ibn Badr.[10]
Sayyied ibn Tawus amesema, barua kutoka kwa Ibn Ziyad ilimfikia Hurr akiwa katika mafikio hayo ya Udhayb al-Hijanat ambayo ilikuwa ikitoa maagizo ya kutekeleza mbinyo.[11] Baadhi ya vyanzo vya historia vimeripoti kwamba, barua ya Ibn Ziyad ilimfikia Hurr akiwa katika eneo la Nainawa.[12]
Rejea
- ↑ Ḥamawī, Muʿjam al-buldān, Juz. 4, uk. 92.
- ↑ Ḥamawī, Muʿjam al-buldān, Juz. 4, uk. 92.
- ↑ Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, Juz. 4, uk. 49; Ṭabarī, Tārīkh al-Ṭabarī, Juz. 5, uk. 404.
- ↑ Balādhurī, Ansāb al-ashrāf, Juz. 3, uk. 172; Ṭabarī, Tārīkh al-Ṭabarī, Juz. 4, uk. 50.
- ↑ Jaʿfarīyān, Aṭlas-i Shīʿa, uk. 66, raman no. 35.
- ↑ Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, Juz. 4, uk. 49; Balādhurī, Ansāb al-ashrāf, Juz. 3, uk. 172; Ibn Kathīr, al-Bidāya wa l-nihāya, Juz. 8, uk. 173.
- ↑ Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, Juz. 4, uk. 50; Balādhurī, Ansāb al-ashrāf, Juz. 3, uk. 172.
- ↑ Ibn Kathīr, al-Bidāya wa l-nihāya, Juz. 8, uk. 174; Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, juz. 4, uk. 49.
- ↑ Ibn Kathīr, al-Bidāya wa l-nihāya, juz. 8, uk. 174; Balādhurī, Ansāb al-ashrāf, juz. 3, uk. 173; Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, juz. 4, uk. 50.
- ↑ Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, juz. 4, uk. 50; Ṭabarī, Tārīkh al-Ṭabarī, juz. 5, uk. 407; Ibn Miskawayh, Tajārub al-umam, juz. 2, uk. 67.
- ↑ Ibn Ṭāwūs, al-Luhūf, uk. 78.
- ↑ Ṭabarī, Tārīkh al-Ṭabarī, juz. 5, uk. 408; Ibn al-Athīr, al-Kāmil fī l-tārīkh, juz. 4, uk. 51-52; Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 83.
Vyanzo
- Abū ʿAlī Miskawayh, Aḥmad b. Muḥammad. Tajārub al-umam. Edited by Abu l-Qāsim Imāmī. Tehran: Surūsh, 1379 Sh.
- Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Jumal min ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakār & Riyāḍ al-Ziriklī. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
- Ḥamawī, Yāqūt b. ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-buldān. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1995.
- Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407AH-1986.
- Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1385 AH-1965.
- Jaʿfarīyān, Rasūl. Aṭlas-i Shīʿa. Tehran: Intishārāt-i Sāzmān-i Jughrāfīyāyī-yi Nīrūhā-yi Musallaḥ, 1387 SH.
- Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Al-Luhūf ʿalā qatlay al-ṭufūf. Tehran: Nashr-i Jahān, 1348 AH.
- Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
- Sharāb, Muḥammad Ḥasan. Maʿālim al-athīra. Tehran: Mashʿar, 1383 Sh.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.