Nenda kwa yaliyomo

Tawasin

Kutoka wikishia

Tawasin au Tawasim (الطواسين أو الطواسيم) ni jina la Sura za tatu ambazo ni Surat Al-Shu'ara na Al-Qasas zinaanza na «Taa-Siin-Miim» pamoja na Surat An-Naml inayo anza na «Taa-Siin».[1] Kunu fadhila (faida) maalumu katika kusoma Sura za Tawasin.

Imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kwamba: Yeyote atakayesoma Tawasin ndani ya usiku wa Ijumaa, huyo atakuwa ni miongoni mwa wapenzi wa Mwenye Ezi Mungu na atakuwa chini ya ulinzi na huruma yake Subhanahu Wataala. Imamu ameendelea kusema kwamba; Katu mtu huyo hatapata shida za duniani wala Akhera, ataruzukiwa Pepo hadi aridhike, bali ataruzukiwa zaidi ya ridhaa yake, na Mwenyezi Mungu atamuoza wanawake mia moja wa Peponi (Hoor al-Ayn).[2] Aidha, kwa mujibu wa Alama Hilli, ni kwamba; kusoma Tawasin, hasa usiku wa Ijumaa, ni jambo linalopendekezwa, yaani ni miongoni mwa matendo ya Sunna.[3]

Rejea

  1. Rāmyār, Tārīkh-i Qur'ān, uk. 597.
  2. Ḥurr al-ʿĀmilī, Wasāʾil al-Shīʿa, juz. 7, uk. 411, Hadith 9722; Ḥuwayzī, Nūr al-thaqalayn, juz. 4, uk. 74.
  3. Ḥillī, Tadhkirat al-fuqahāʾ, juz. 4, uk. 117.

Vyanzo

  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad bin al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1414 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan bin Yūsuf al-. Tadhkirat al-fuqahāʾ. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1414 AH.
  • Ḥuwayzī, ʿAbd ʿAlī bin al-Jumʿa al-. Nūr al-thaqalayn. Mhariri: Ḥāshim Rasūlī Maḥallātī. 4th edition. Qom: Ismāʿīlīyān, 1415 AH.
  • Rāmyār, Maḥmūd. Tārīkh-i Qur'ān. Tehran: Intishārāt-i Amīr Kabīr, 1387 SH.