Suwayd bin Amr al-Khath'ami

Kutoka wikishia
Faili:امگاه شهدای کربلا2.jpg
Makaburi ya halaiki ya mashahidi wa Karbala

Suwayd bin Amr bin Abi Muta' al-Khath'ami (Kiarabu: سويد بن عمرو بن أبي مطاع الخثعمي) alikuwa shahidi wa mwisho wa Karbala ambaye aliuawa shahidi muda mfupi baada ya kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s).

Suwayd bin Amr bin Abi Muta' al-Khath'ami anatokana na kabila la Khath'am. Kwa mujibu wa Samawi (aliaga dunia 1370 Hijiria) katika kitabu cha Ibsar al-Ain ni kwamba, Suwayd alikuwa mtu wa heshima, mchaji Mungu, shujaa na mwenye uzoefu na tajiriba katika vita. [1]

Kwa mujibu wa Muhammad bin Jarir al-Tabari (aliyeaga dunia 310 Hijria) katika kitabu cha Tarikh Tabari ni kwamba, Suwayd alikuwa mtu wa mwisho aliyeenda katika medani ya vita na kuuawa shahidi [2]. Alipigana kishujaa na kujeruhiwa vibaya na akawa ameangukia katika miili ya mashahidi. Watu wote wakadhani ameuawa. Baada ya muda, Suwayd akasikia watu wakisema: Hussein ameuawa shahidi. Akasimama na kushika upanga wake na kupigana kishujaa mpaka akauawa shahidi. Kwa mujibu wa Tabari [3] na Baladhuri [4] ni kwamba, Urwat bin Battan al-Tha'labi na Zayd bin Ruqad al-Janibi ndio waliomuua. Lakini katika kitabu cha Tasmiya Man Qutila Maa al-Hussein (kilitungwa karne ya 1 Hijiria), muuajii wake ametajwa kuwa ni Hani bin Thubayt Hadhrami. [5]

Vyanzo

  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1977.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1385 AH.
  • Samāwī, Muḥammad al-. Ibṣār al-ʿayn fī anṣār al-Ḥusayn. Qom: Zamzam-i Hidāyat, 1384 Sh.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1403 AH.