Siddiqatu Al-Shahida (Lakabu)

Siddiqatu Al-Shahida (Kiarabu: الصديقة الشهيدة) ni jina ambatano la majina mawili ya Bibi Fatima (a.s). Jina «Siddiqatu» linatoka katika msamiati wa Kiarabu wenye maana ya mwanamke mkweli mno kupita kiasi, [1] na jina «Shahida» lina maana ya mwanamke aliyekufa katika njia ya Mwenye Ezi ya Mungu. [2] Pia majina mawili haya ya «Siddiqa» na «Shahida» yanaonekana kuumika katika moja ya riwaya kutoka kwa Imamu Kadhim (a.s), ambayo wanazuoni wamethibitisha usahihi wake, [3] ambapo kulingana na Hadithi hii, Bibi Fatima (a.s) ametambuliwa kuwa ni mwanamke mkweli aliyepoteza maisha yake katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. Hadithi imekuja ikisema: «إنَّ فاطِمَةَ (ع) صِدّیقَةٌ شَهیدَةٌ ; Hakika Fatima (a.s) ni mkweli aliyefariki shahidi». [4]
Pia tukirudi kweneye vyanzo mbali mbali vya Hadithi, tutakuta kuna ibara maalumu za Sala na Salamu kuhusiana na Bibi Fatima (a.s), zilizotumia majina mwili haya ndani yake. Miongoni mwa Hadithi zilizotumia ibara yenye majina mawili haya ndani yake, ni ile Hadithi iliyobeba ibara isemayo: «السَّلامُ عَلَیکِ أَیتُهَا الصِّدِّیقَةُ الشَّهِیدَةُ ; Amani iwe juu yako, Ewe Siddiqatu Shahida». [5] Ila kwa mujibu wa maelezo ya Muhammad Hadi Mazandarani, ni kwamba; Kidhahiri ni kwamba, Sala na Salamu zote kuhusiana na bibi Fatima (a.s) ziliandikwa na waandishi waliotunga tungo za Sala na Salamu hizi kupitia ibara zao wenyewe. [6] Kwa hiyo Sala na Salamu hii iliobeba majina mawili haya ya «Al-Siddiqatu Al--Shahida», haina msingi wowote ule wa Hadithi. Sheikh Saduq ameeleza ya kwamba; pale yeye alipofika mjini Madina akiwa katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w), alimsalimia Bibi Fatima (a.s) kwa kutumia majina mawili hayo. Ila hata yeye pia hakutoa maelezo yoyote yale yanayoashiria kwamba ibara hiyo ameipokea kutoka kwa Ma'sumina (a.s). [7]
Katika Hadithi, jina la «Siddiqatu» pia linaonekana kutumika kiupekee kwa ajili ya Bibi Fatima (a.s.), bila ya kuamabatanishwa na jina la Al-Shihida. Miongoni mwa mifano ya matumizi ya jina hili kiupekee, ni yale matumizi ya jina kupitia Imamu Ali (a.s.), ambapo alimtaja Bibi Fatima (a.s.) kwa jina hili kiupekee. [8] Imamu Sadiq (a.s) alitaja majina tisa juu ya Bibi Fatima (a.s) aliyopewa na Mwenye Ezi Mungu, moja ya majina hayo ni jina la Siddiqatu. [9] Imamu Hassan Askari (a.s), katika moja ya Hadithi zake zinazohusiana na mafunzo juu ya kumtakia rehema bwana Mtume (s.a.w.w) na warithi wake, kumhusiana na Bibi Fatima (a.s) alisema kwamba, twatakiwa kumtakia rehema kwa kusema: «...اللّٰهُمَّ صَلِّ عَلَی الصِّدّیقَةِ فاطِمَةَ الزَّکِیة ; Ewe Mwenyezi Mungu, mswalie Bibi mkweli, Fatima mtakatifu...».[10]
Mashia wanaamini kwamba; Fatima Zahra (a.s) aliuawa shahidi. [11] Miongoni mwa matukio yanayohusishwa na kifo chake ni; Matishio ya kuichoma moto nyumba ya Bibi Fatima (a.s), kumfinya Bibi Zahra (a.s) huku akiwa kati ya ukuta na mlango, kuharibika kwa mimba yake ya miezi kadhaa kupitia tukio la uvamizi wa nyumba yake, kumkanyaga Bibi Zahra (a.s), kumpiga kwa upanga na kumpiga kwa mjeledi na kuvunjika kwa mbavu katika shambulio hili. Haya ndiyo baadhi ya matukio hukusiana na taarifa zilizokuja katika baadhi ya vitabu vya Hadithi na historia juu ya kifo chake cha kuuawa kishahidi. [12]
- Pia Soma: Kufariki kishahidi kwa bibi Fatima (s.a) na Tukio la kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma (a.s)