Nenda kwa yaliyomo

Shiati Ma In Sharibtum Maa Adhbin Fadhkuruni

Kutoka wikishia
Shairi': Enyi wafuasi wangu kila mtakapokunywa maji nikumbukeni

Shiati Ma In Sharibtum Maa Adhbin Fadhkuruni (Kiarabu: شِیعَتِی مَا إِنْ شَرِبْتُمْ ماءَ عَذْبٍ فَاذْکرُونِی) (Shia wangu kila mnapokunywa maji matamu nikumbukeni au nitajeni). Huu ni ubeti wa shairi mashuhuri linalonasibishwa na Imamu Hussein (a.s). Shairi hili linakumbusha kufa shahidi na kiu Imamu Hussein (a.s) katika tukio la Karbala. Sehemu ya kwanza ya ubeti huu wa shairi inawausia na kuwataka Mashia kila wanapokunywa maji basi wamkumbuke na kumtaja Imamu Hussein (a.s). Baadhi ya Maulamaa wakitegemea shairi hili na vilevile hadithi kadhaa kutoka kwa Maasumina wanalitambua suala la kumtaja na kumbuka Imamu Hussein (a.s) wakati wa kunywa maji kuwa ni jambo la lazima [2] na wengine wanasema ni mustahabu. [3]


أَوْ سَمِعْتُمْ بِغَرِیبٍ أَوْ شَهِیدٍ فَانْدُبُونِی[4] * شِیعَتِی مَا إِنْ شَرِبْتُمْ ماءَ عَذْبٍ فَاذْکرُونِی


Tafsiri: Enyi Shia wangu (wafuasi wangu) kila mtakapokunywa maji nikumbukeni na kila mtakaposikia kisa cha upweke wa mgeni au kuuawa shahidi mtu basi nililieni. [5]


Fadhil Darbandi anasema katika kitabu Asrar al-Shahada kwamba, shairi hili liliandikwa na Imam Hussein (a.s). [6] Baadhi ya vyanzo pia vimesimulia uandishi wa shairi hili baada ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) na kuhusisha na kuonwa mwili wake na binti yake Sakina (a.s). [7] Kaf’ami, mwanazuoni wa Kishia wa karne ya 9 Hijiria, alimnukuu Sakina (a.s) namna hii: Baada ya kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s), wakati nilipoukumbatia mwili wake, nilipata hali kama ya kukosa fahamu (kama kuzimia) ambapo nilimsikia baba yangu akisoma beti hizi za mashairi. [8] Hata hivyo, watu kama Sheikh Abbas Qomi katika Nafs al-Mahmoom na Muntaha al-A’mal [9] na Muqarram katika Muqtal al-Hussein [10], licha ya kulinukuu shairi hilo katika vitabu vyao, lakini hawajataja mapokezi au chanzo chake cha kihistoria. Sayyid Muhammad Sadr (aliyefariki: 1377 Hijiria Shamsia), akitegemea maudhui ya beti zinazoelezea kuuawa shahidi Imam Hussein (a.s) na matukio ya baada yake, alisema kwamba shairi hili kwa hakika halikutungwa na Imam Hussein (a.s); [11] yeye na baadhi ya wengine wamesema, kuna uwezekano kwamba shairi hilo ni lugha ya zama za Imam Hussein (a.s) [12]

Shairi hili, hasa ubeti wake wa kwanza, ambao unatoa taswira ya tuklio la Karbala na kufa shahidi Imamu Hussein (a.s) hali ya kuwa midomo yake imekauka kwa kiu, limeandikwa katika milango ya chemchemi za maji na vyanzo vya maji. [13] Baadhi ya wasoma mashairi na kaswida za kuwasifia Ahlul-Bayt kama Bassim Karbalai na Mahmoud Karimi wamesoma beti hizi za mashairi katika maombolezo ya Ahlul-Bayt (a.s). Beti zifuatazo ni muendelezo wa shairi hili:


وَ بِجُرْد الخَیلِ بَعْدَ القَتْلِ عَمْداً سَحِقُونی * وَ أَنا السِّبْطُ الَّذی مِنْ غَیرِ جُرْمٍ قَتَلُونی
کَیفَ أَسْتَسْقی لِطِفْلی فَاَبَوْا أَن یرْحَمُونی * لَیتَکُم فی یوْمِ عاشُورا جمیعاً تَنْظُرونی


یا لَرُزْءٍ وَ مُصابٍ هَدَّ أرْکانَ الحَجِونِ * و سَقَوهُ سَهْمَ بَغْی عِوَضَ الماءِ المَعینِ
فَالْعَنُوهُم مَا اسْتَطَعْتُم شِیعَتِی فِی کُلِّ حِینٍ * [18]وَیلَهُم قَدْ جَرَحُوا قَلْبَ رَسُولِ الثَّقَلَینِ


Tafsiri: Mimi ni mjukuu wa Mtume wa Allah waliyeniua bila kosa Na wakaukanyaga mwili wangu kwa farasi kwa makusudi baada ya kuniua Laiti nyote mngelikuweko siku ya Ashura Mngeona vipi nilitaka maji kwa ajili ya mwanangu mdogo, lakini walikataa Badala ya maji matamu wakamlenga mshale wa dhulma mwanangu mdogo Ni msiba mkubwa na wenye maumivu kiasi gani ambao ulitikisa mlima mkubwa wa Hajun (Makka) Ni msiba mkubwa kiasi gani ambao ulijeruhi moyo wa Mtume, majini na wanadamu Basi enyi Mashia wangu! Walaanini hao kadiri mnavyoweza. [19]


Rejea

Vyanzo