Nenda kwa yaliyomo

Shetani Mkubwa

Kutoka wikishia
Katuni yenye Kuakisi Shetani Mkuu, Mchora Katuni Carlos Latov Kutoka Brazil.

Shetani Mkubwa (Kiarabu: الشيطان الأكبر) ni jina na wasifu ambao Imam Khomeini aliipatia Marekani katika hotuba yake baada ya kutekwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran.[1] Katika hotuba yake, alitumia ushabihishaji huu kutoka katika hadithi kwamba mkubwa wa mashetani (ibilisi), baada ya Mtume (s.a.w.w) kubaathiwa aliwakusanya wenzake na kuzungumzia juu ya kutumia njia ngumu ya kupotosha watu.[2] Kwa utaratibu huu, kwa mujibu wa maneno ya Imamu Khomeini ni kuwa, katika Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran pia kuna shetani mkubwa. Marekani imekusanya mashetani wadogo wa ndani na nje na inazusha chokochoko na makelele.[3]

Inaelezwa kuwa, sifa hii imechukuliwa kutoka katika sifa za shetani ndani ya Qur'ani; kwani Qur’ani inamtambua shetani kuwa ni kafiri,[4] adui wa mwanadamu,[5] mwenye kiburi na kujiona,[6] mfarakanishaji,[7] asiyeaminika,[8] fasiki na fisadi (mharibifu au mfininishaji),[9] mwenye chama,[10] na mwenye kuyapamba matendo mabaya na kuyafanya yaonekane mazuri,[11] ambapo kwa mtazamo wa Imamu Khomeini sifa hizi zinaonekana katika siasa zinaendeshwa na Marekani.

Uchomwaji wa Bendera ya Marekani na Ishara ya Shetani, katika maandamano ya tarehe 22 Bahman huko Tehran.

Imamu Ruhullah Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliitumia mara chungu nzima ibara au neno la Shetani Mkubwa. Makusudio yake yalikuwa mambo ya kimaadili, Kiqur’ani na kiitikadi, ibilisi na nafsi ya kuamrisha maovu na katika mijadala ya kisiasa ya Marekani. Kwa maana kwamba, alikusudia kuishabihisha Marekani na shetani kutokana na mwenendo na siasa zake.[12] Kadhalika katika hotuba yake aliyotoa kuhusiana na tawala za Kiislamu kuonyesha udhaifu na kusalimu amri mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel aliutaja utawala huo kuwa ni shetani mdogo.[13]

Lakabu ya shetani mkubwa imetumiwa pia mara nyingi na Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.[14] Kwa uoni na mtazamo wake ni kuwa, pamoja na kuwa, ibilisi ndiye kiongozi wa mashetani wote, lakini anaweza kushawisha tu; kwa upande wa Marekani inahadaa na pia inaua, inafanya uporaji na kufitinisha. [15] Kadhalika wasifu na sifa hii inatumiwa katika maandamano dhidi ya Marekani ikiwa kama nara na kaulimbiu ya kutangaza chuki dhidi ya siasa za Marekani.[16]

Rejea

Vyanzo