Sala ya Ja’far al-Tayyar
Swala ya Ja’far al-Tayyar (Kiarabu: صلاة جعفر الطيار) au Swala ya Tasbih au Swalat al-Habuah ni miongoni mwa Swala za mustahabu ambayo ni Swala mbili zinazoswaliwa kwa sura ya rakaa mbili mbili. Katika Swala hii tasbihi nne hukaririwa mara 300. Tasbihi nne ni: (سُبْحَانَ اللَّهِ وَ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَ اللَّهُ أَکبَرُ).
Mtume (s.a.w.w) alimfundisha swala hii Ja’far ibn Abi Twalib baada ya kurejea kwake kutoka Uhabeshi (Ethiopia ya leo). Mtume alifanya hivyo na kumpatia zawadi Ja’afar ibn Abi Twalib kwa shabaha ya kuthamini mchango wake. Kusamehewa madhambi na kukubaliwa haja na maombi ni miongoni mwa athari zilizotajwa za Swala ya ya Ja’far al-Tayyar. Baadhi ya wanazuoni wa dini wamewausia kuiswali Swala hii kwa ajili ya mambo muhimu na kwa ajili ya kuharakishwa suala la ndoa.
Zawadi ya Mtume kwa Ja’afar al-Tayyar
Swala ya tasbihi ni Swala ambayo Bwana Mtume (s.a.w.w) alimfundisha Ja’far ibn Abi Twalib baada ya kurejea kwake kutoka Uhabeshi. Mtume alifanya hivyo na kumpatia zawadi Ja’afar ibn Abi Twalib kwa shabaha ya kuthamini mchango wake; kwa msingi huo Swala hii ikaondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Swala ya Ja’far al-Tayyar. [1] Ja’far al-Tayyar ni binamu yake Mtume na ndugu yake Imamu Ali (a.s) [2] na alikuwa miongoni mwa watu wa awali waliomuamini Mtume. [3] Ja’far alikuwa kiongozi wa kundi la waislamu waliotoka Makka na kuhajiri kwenda Uhabeshi kwa amri wa Mtume (s.a.w.w). [4] Ni kwa muktadha huo Swala hii ilikuwa zawadi ya Mtume kwa Ja’far. Swala hii inafahamika na kujulikana pia kwa jina la Swala ya Hab’wah. [5]
Namna ya Kuiswali
Swala ya Ja’far al-Tayyar ina muundo wa swala mbili ambazo huswaliwa kwa sura ya rakaa mbili mbili, ikiwa na shahada mbili na salamu ya kujitegemea. Swala hii huswaliwa kwa utaratibu huu:
- Mwanzoni mwa Swala, ni kutia nia ya Swala ya Ja’far al-Tayyar ambapo katika rakaa ya kwanza baada ya al-Hamdu, inasomwa Surat az-Zilzala. Katika rakaa ya pili baada ya al-Hamdu inasomwa Surat A’adiyaat, katika rakaa ya tatu baada ya al-Hamdu inasomwa Surat an-Nasr na katika rakaa ya nne baada ya al-Hamdu inasomwa Surat Tawhid (Qul-huwallah).
- Katika kila rakaa baada ya al-Hamdu na Sura inasomwa Tasbihi nne mara 15 (سُبْحَانَ اللَّهِ وَ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَ اللَّهُ أَکبَرُ), na katika rukuu ya kila rakaa, mara 10, wakati wa kusimama baada ya rukuu mara 10, katika sijda ya kwanza mara 10, baada ya sijida ya kwanza mara 10, katika sijda ya pili mara 10 na baada ya sijda ya pili na mara 10 kabla ya kusoma tashahudi.
- Ni mustahabu katika sijda ya pili katika rakaa ya pili baada ya kusoma dhikri ya tasbihi anayeswali swala hii aseme: (سُبْحانَ مَنْ لَبِسَ الْعِزَّ وَالْوَقارَ ، سُبْحانَ مَنْ تَعَطَّفَ بِالْمَجْدِ وَتَكَرَّمَ بِهِ ، سُبْحانَ مَنْ لَايَنْبَغِى التَّسْبِيحُ إِلّا لَهُ ، سُبْحانَ مَنْ أَحْصىٰ كُلَّ شَىْءٍ عِلْمُهُ ، سُبْحانَ ذِى الْمَنِّ وَالنِّعَمِ ، سُبْحانَ ذِى الْقُدْرَةِ وَالْكَرَمِ ، اللّٰهُمَّ إِنِّى أَسْأَلُكَ بِمَعاقِدِ الْعِزِّ مِنْ عَرْشِكَ ، وَمُنْتَهَى الرَّحْمَةِ مِنْ كِتابِكَ ، وَاسْمِكَ الْأَعْظَمِ وَكَلِماتِكَ التَّامَّةِ الَّتِى تَمَّتْ صِدْقاً وَعَدْلاً ، صَلِّ عَلىٰ مُحَمَّدٍ وَأَهْلِ بَيْتِهِ ، وَافْعَلْ بِى كَذا وَكَذا) Katika sehemu ya “Waf’al bi kadha wa kadha” aombe haja yake. [7]
- Allama Majlisi amenukuu dua katika kitabu cha Zad al-Maad kutoka kwa Mufadhal ibn Omar kutoka kwa Imam Swadiq(a.s) ambayo inasomwa baada ya Swala ya Ja’far al-Tayyar kwa ajili ya kutekelezewa haja.
Fadhila na Wakati wa Kuiswali
Imeelezwa kuhusiana na fadhila za Swala ya J’afar ya kwamba, Swala hii iswaliwe kwa ajili ya kuomba kutekelezwa haja na kusamehewa dhambi, na iendee kuswaliwa yaani mtu adumu katika kuiswali mpaka haja zake zitakapotekelezwa. [8] Baadhi ya wanazuoni wa dini wamewausia kuiswali Swala hii kwa ajili ya mambo muhimu na kwa ajili ya kuharakishwa suala la ndoa. [9] Imeusiwa pia katika hadithi kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) juu ya kuiswali Swala hii katika usiku wa nusu ya Shaaban (tarehe 15 Shaaban). [10] Siku ya Ijumaa pia ni katika nyakati zenye fadhila kwa ajili ya kuiswali Swala hii. [11]