Nenda kwa yaliyomo

Sahmayn

Kutoka wikishia

Sahmayn (Kiarabu: السَهْمَیْن) ina maana ya hisa mbili (mafungu mawili) na hilo linaashiria hisa ya Imamu na hisa ya Masayyid (masharifu) katika Khumsi. [1] Sahm(سهم) katika lugha ya Kiarabu ina maana ya hisa au fungu, [2] kasma na mgawo. [3]

Mafakihi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kwamba, Khumsi kiujumla inagawanywa katika hisa na mafungu mawili ya Imamu na Maseyyid (watu ambao nasaba yao inaishia kwa kizazi cha Mtume): [4]

Sheikh Tusi katika kitabu cha al-Mabsut, [6] Shahidi al-Awwal katika kitabu cha Al-Lum'a al-Dimashqiyya, [7] na Shahid al-Thani katika sherh ya Lum'a [8] ni miongoni mwa mafakihi wa Kishia ambao kwa mujibu wa Aya ya Khums wameigawa Khumsi katika mafungu sita na kulitambua hilo kama kauli mashuhuri ya Shia; [9] hata hivyo hisa na mafungu haya sita pia yanarejea katika mafungu mawili makuu; mafungu matatu ya awali yaani Mwenyezi Mungu, Mtume na Dhawil Qurba (jamaa wa karibu) ni kwa ajili ya Imamu na mafungu mengine matatu yaliyobakia yaani fungu la mayatima, mafakiri na waliokwama njiani ni kwa ajili ya jamaa na watu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w) fungu ambalo linajulikana kama la maseyyid (masharifu). [10] Sababu ya kugawanywa Khumsi katika mafungu mawili imetambuliwa kuwa chimbukko lake ni hadithi. [11] Imamu Musa Kadhim (a.s) katika hadithi moja anafananua Khumsi kwamba, ni fungu kwa ajili ya mtawala (Imamu), fungu jingine ni mahususi kwa mayatima, mafakiri na waliokwama njiani miongoni mwa watu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w). [12]

Vyanzo

  • Bustani, Fu'ad Afram, Fargangg-e Abjadi, Teheran: Islami, Cet. 2, 1375 S/1997 M.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hassan, Al-Fushūl al-Muhimmah Fī Ushūl al-A'immah-Takmilah al-Wasā'il, Iran: Muassese-e Ma'aref-e Eslami-e Emam Reza Alaih as-Salam.
  • Ibn Faris, Ahmad bin Faris, Mu'jam Maqāyīs al-Lughah, Qom: Maktab al-A'lam al-Islami, 1404 H.
  • Imam Khomeini, Sayyid Ruhullah, Taudhīh al-Masā'il, Qom: Daftar-e Entesharat-e Eslami Wabaste Be Jame'e-e Mudarrisin-e Hauze Ilmiyye-e Qom, Cet. 8.
  • Mughniyah, Muhammad Jawad, Fiqh al-Imām ash-Shādiq (a.s), Qom: Muassese-e Ansharihan, 1421 H.
  • Muhammad Hilli, Ja'far bin Hassan. Al-Mukhtashar, Qom: Muassese al-Mathbu'at al-Diniyyah, Cet. 6, 1418 H.
  • Muntazeri, Hussein ali, Al-Khums Wa al-Anfāl, Qom: 1431 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawāhir al-Kalām Fī Sharh Sharāyi' al-Islām, Riset Abbas Qucani & Ali Akhundi, Beirut: Dar Ihya' al-Turath al-Arabi, Cet. 7, 1404 H.
  • Shahid Awwal, Muhammad bin Makki, Al-Lum'ah ad-Damishqiyyah Fī Fiqh al-Imāmiyyah, Riset Muhammad Taqi Murwarid, Beirut: Dar at-Turats-Ad-Dar al-Islamiyyah, 1410 H.
  • Tabataba'i Yazdi, Sayyid Muhammad Kadzhim, Al-'Urwah al-Wutsqā Fī Mā Ta'umm Bihī al-Balwā, Daftar-e Entesharat-e Eslami Wabaste Be Jame'e-e Mudarrisin-e Hauze Ilmiyye-e Qom.

{{End}