Nenda kwa yaliyomo

Operesheni ya Besharate Fath

Kutoka wikishia
Picha inayodaiwa kuonyesha mfumo wa mawasiliano ya satelaiti katika kituo cha Al-Udeid baada ya kuharibiwa katika Operesheni Besharat Fat-h.

Operesheni ya Besharate Fat-h (Kiarabu: عملية بشارة الفتح) (Bishara ya Ushindi) ni operesheni maalumu inayohusiana na shambulio la angani (kupitia makombora) lililofanywa na Vikosi vya Kijeshi la Iran dhidi ya kituo cha kijeshi cha Marekani cha Al Udeid kilichoko nchini Qatar. Tukio hilo la dhahania limewekwa tarehe 2 mwezi wa Tir 1404 Shamsia.[1] Shambulio hili lilifanyioka kama hatua ya kulipiza kisasi kwa shambulio la Marekani dhidi ya miundombinu ya nyuklia ya Iran. Kituo cha Al Udeid kinatambuliwa kama kituo kuu cha Kikosi cha Anga cha Marekani (USAF) katika kanda ya Asia Magharibi.[2] Baadhi ya vyanzo vinaripoti kuwa chombo-anga kisicho na rubani (drone) kilichotumika katika mauaji ya Qassim Suleimani kiliratibiwa kutoka katika kituo hicho.[3] Shambulio hili linawakilisha tukio la pili la aina yake, kufuatia shambulio la awali la mwaka 1398 Shamsia (sawa na mwaka 2020 Miladia), ambapo Kikosi cha Sepah Pasdaran (IRGC) kilikilipua kwa makombora kituo cha Ain al-Asad kilichoko nchini Iraq, kama ni jibu la moja kwa moja katika kujibu na kulipiza kisasi mauaji ya Kamanda wa Kikosi cha Quds, Qassim Suleimani.[4]

Uzinduzi wa Operesheni Besharate Fath, ulifanyika kwa kaulimbiu ya kimkakati isemayo: 'Ya Aba Abdillah al-Hussein (a.s.)' (Ukenja usemao: Ewe Abaa Abdillahi Al-Hussein). Aidha, hii operesheni ilizingatia kanuni ya jibu la kimlingano, ambapo idadi ya makombora yaliyorushwa na Iran, ilikuwa ni sawa na idadi ya mabomu yaliyotumiwa na Marekani dhidi ya miundombinu yake ya nyuklia.[5]

Kufuatia operesheni hiyo, kulizuka ripoti kadhaa zilisambaa kwenye anga za kimtandao (online) kuhusu maandamano ya wananchi nchini Qatar, kupinga uwepo wa kijeshi wa Marekani nchini humo.[6] Pia, baadhi ya uchambuzi unaamini kuwa; operesheni hii ndiyo sababu iliyoilazimisha Israeli kukubali usitishaji wa mapigano kati yake na Iran.[7] Kufuatia operesheni hii, rais wa wakati huo wa Marekani, Trump, alitoa wito rasmi wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Iran na Israeli.[8]

Rejea

Vyanzo