Ndoa ya Misyar
Ndoa ya Misyar (Kiarabu: نِکاح مِسْیار): Ni aina ya ndoa kati ya Waislamu inayofanywa miongoni mwa wanajamii wa madhehebuya Sunni. Ndoa hii (kulingana na nao) ni ndoa yenye masharti kamili ya ndoa, ikiwemo; kusoma mkataba wa kisheria, uwepo wa mashahidi pamoja na malipo ya mahari. Lakini mwanamke katika ndoa hii -kwa hiari yake mwenyewe- huamua kuacha baadhi ya haki zake, ikiwemo haki ya matumizi (nafaqah) na haki ya kuishi pamoja na mumuwe. Katika ndoa hii, mume anaweza kumtembelea mke wakati wowote anapotaka, na mwanamke naye huwa yuko huru katika mambo yake binafsi.
Mifano ya Tofauti Kati ya Ndoa ya Misyar na Ndoa ya Muda (Mut'a)
Katika suala la kutokuwepo kwa wajibu wa haki ya makazi na matumizi ya mwanamke, ndoa ya misyar ni sawa na ndoa ya muda iliopo katika madhehebu ya Shia, ijulikanayo kwa jina la mut’a. Hata hivyo, kuna tofauti kadhaa za msingi kati ya ndoa mbili hizo, miongoni mwazo ni pamoja na; kudumu kwa ndoa ya misyar, kitowepo ruhusa ya kukiuka kiwango cha wake wanne katika ndoa hiyo (yaani mke wa misyar huingia kwenye idadi ya wake wa kawaida), jambo ambalo halipo katika ndoa ya Mut'a. Tofauti nyingine ni pamoja na taratibu za talaka na hitaji la mashahidi wakati wa kufunga ndoa (mambo ambayo yanahitajika katika ndoa yaMisyar, lakini si lazima mambo hayo kufanyika katika ndoa ya Mut'a). Ndoa ya misyar hufungika kupia mashahidi maalumu, na utenganifu wake ima huwa ni kwa njia ya talaka kutoka kwa mume, khul-'u (mke kujivua mwenyewe katika mahusiano ya ndoa) au kuvunja mkataba wa ndoa hiyo, mambo ambayo hayapo katika ndoa ya muda kwa mujibu wa madhehebu ya Kishia. Inasemekana kuwa ndoa ya Misyar ni suala jipya la kifiqhi ambalo kwa mara ya kwanza kabisa lilijitokeza katika eneo la Tamim, nchini Saudi Arabia. Fahd al-Ghanim anajulikana kuwa ndiye mtu wa kwanza aliye anza kutumia neno "ndoa ya misyar."
Wanazuoni wa Shia, wakizingatia mfanano wa mut'a na ndoa ya Misyar na hali zinazofanana katika uundwaji wake, wamewalaumu mafaqihi wa Kisunni kwa kule wao kuwa na hukumu mbili tofauti kati ya ndoa ya muda (mut’a) na ndoa ya misyar, huku wakiruhusu ndoa ya misyar na kukataza ndoa ya mut’a. Kwa mujibu wa mtazamo wa Nassir Makarim Shirazi, wanazuoni wa Shia walioitafiti ndoa ya misyar, wote wamekubali juu ya uhalali wa ndoa hiyo kwa mujibu wa masharti maalum kuhusiana na ndoa hiyo. Baadhi ya mafaqihi wa Kisunni wameruhusu ndoa ya Misyar, ingawa wengine wameikataa, na wengine wametoa hukumu ya kuhalalisha ndoa hii.
Ufafanuzi wa Dhana
Ndoa ya Misyar ni aina ya ndoa inayofuata masharti kamili ya ndoa yanayozingatia na Waislamu wa madhehebu ya Sunni. Miongoni mwayo ni pamoja na; kusoma mkataba wa sheria ya ndoa (‘aqd), uwepo wa mashahidi pamoja na kulipa mahari maalumu. Kwa upande wa mwanamke, yeye kwa hiari yake mwenyewe huamua kuachana na haki ya matumizi pamoja na haki ya kuishi pamoja wake. [1] Kwa mujibu wa maoni ya Yusuf Qaradawi, ambaye ni mufti wa Kisunni, ndoa ya misyar kwa kawaida huwa sio ndoa ya kwanza ya mwanamme, bali yeye huwa tayari ameshaoa mke wa kudumu ambaye anamhudumia kwa kumpa haki ya makazi na matumizi ya kila siku (chakula na mengineyo). [2]
Kwa mujibu wa maoni ya Abdullah Munayyi’i, mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wakuu wa Saudi Arabia, ni kwamba; Ndoa ya misyar inashikamana na sheria zote za ndoa ya kawaida, ikiwemo; urithi, mahari, pamona na uhalali wa watoto waozaliwa kupitia ndoa hiyo. Ila mwanamke anaweza kuacha na kusamehe baadhi ya haki zake, kama vile haki ya matumizi na haki ya kuishi pamoja na mumewe katika nyumba moja. [3] Wahba Zuhaili, mwanazuoni mwingine wa Kisunni, pia naye anfafanua ndoa hii kwa kusema kuwa; haki ya urithi ni miongoni mwa haki zinazohifadhiwa katika ndoa ya misyar. [4]
Katika ndoa hii, mume anaweza kumtembelea mwanamke wakati wowote ule apendapo, na mwanamke naye huwa yuko huru katika mambo yake binafsi. [5] Neno "misyar" halipatikani katika kamusi asili za rasmi lugha ya Kiarabu, ila neno hili katika lugha ya kawaida, humaanisha kitu cha muda mfupi na rahisi. [6]
Mfanano na Tofauti na Katia ya Ndoa ya Muda na Ndoa ya Misyar
Kwa mujibu wa maelezo ya Makarim Shirazi, ndoa ya misyar inafanana moja kwa moja na ndoa ya muda (mut’a); kwani katika aina hii ya ndoa, mwanamke huwa na makazi yeke mwenyewe, na pia suala la matumizi si jukumu la mume, bali ni jukumu lake yeye mwenyewe. [7] Katika ndoa zote mbili, mwanamke hana haki ya matumizi kutoka kwa mumewe, hana haki ya kuishi pamoja na mumewe katika nyumba moja, hana haki ya kudai makazi, na wala wanandoa wao huwa hawarithiani kati yao. Zaidi ya hayo, mwanamke hahitaji ruhusa kutoka kwa mume endapo atahiji kuondoka nyumbani kwake na kuelekea mahala fulani. [8]
Tofauti zilizopo kati ya ndoa ya misyar na ndoa ya muda ni kwamba; muda wa ndoa katika ndoa ya muda lazima uwe umeainishwa katika ufungwaji wa ndoa hiyo, lakini katika ndoa ya misyar, hufungwa kama ndoa ya kawaida tu (ya kudumu). Pia, kiwango cha juu katika kufunga ndoa ya misyar, ni sawa na kiwango cha ndoa ya kudumu, yaani mume hana haki ya kuoa zaidi ya wake wanne, lakini katika ndoa ya muda, hakuna kiwango maalumu cha wake kilichoainishwa katika ndoa hiyo. Tofauti nyingine zilizopo kati ya ndoa mbili hizi ni kwamba; kutengana kwa wanandoa wa ndoa ya misyar hufanywa kwa njia ya talaka, khul', au kunja mkataba wa ndoa hiyo; lakini ndoa ya muda humalizika kwa kumalizika kwa muda ulioainishwa hapo mwanzo, au kwa kusamehewa muda uliobaki wa ndoa hiyo. [9] Zaidi ya hayo, kufungwa kwa ndoa ya misyar kunahitaji uwepo wa mashahidi wawili, wakati ndoa ya muda haihitaji sharti hili. [10]
Historia na Asili ya Kuanzishwa kwa Ndoa ya Misyar
Inasemekana kuwa ndoa ya misyar ni suala geni la kifiqhi, ambalo kwa mara ya kwanza kabisa lilianza lilionekana kuibuka katika eneo la Tamim, nchini Saudi Arabia. Fahd al-Ghanim anatambuliwa kuwa ndiye mtu wa kwanza kabisa kutumia istilahi na msamiati wa "ndoa ya misyar". [11] Katika miaka ya 1990, baada ya kuenea kwa ndoa ya misyar nchini Saudi Arabia, polepole aina hii ya ndoa ilianza kuenea katika nchi mbali mbali za Kiarabu za eneo la Ghuba, kama vile Kuwait, Qatar, Bahrain, na Umoja wa Falme za Kiarabu, yawezekana pia jambo lilienea katika nchi nyingine mbali mbali. [12] Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wamejaribu kutanua msamiati wa ndoa ili kuiingiza ndoa hii ndani ya istilahi kuu zinazohusiana na masuala ya ndoa ndani ya vitabu vyoa vya fiqhi. [13]
Kuongezeka kwa gharama za ndoa ya kudumu, ikiwemo ugumu wa kupata makazi na mahari, pamoja na hamu ya wanaume ya kuficha ndoa ya pili ndani ya familia zao, ni baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa ndoa hii ya misyar miongoni mwa wafwasi wa madhehebu ya Kisunni. Kuongezeka kwa idadi ya wanawake waliotalikiwa na wasio na msaada, hitaji la wanaume kuwa na wake wengi katika hali fulani, kama vile ugonjwa wa mke wa kwanza, pamoja na suala la mwanamke kumhudumia mwanamme maskini, ni miongoni mwa sababu za kuanzishwa kwa ndoa hii ya misyar. [14]
Watafiti wa upande wa madhehebu ya Kishia wanaamini kwamba; upinzani wa fiqhi ya Kisunni dhidi ya ndoa ya muda inayotendwa na wafwasi wa madhehebu ya KIshia, na kukabiliana na hali zinazofanana kati ya ndoa mbili hizi, ndiko kulikosababisha wao kutengeneza ndoa yenye jina la ndoa ya misyar. [15]. Baadhi ya wanazuoni wa Shia, katika suala hili, wamewakosoa wanazuoni wa Kisunni na kuwashutumu kwa kuwa na hukumu mbili tofauti juu ya ndoa hizi zinazofanana. Swali la watafiti wa Kishia, ni kwamba; Nini kinachepelekea utata na kutolewa hukumu tofauti kuhisana na ndoa mbili hizi? Hali ya kwamba; hakuonekeni tofauti za msingi katia ya mut'a na ndoa ya misyar, bali kuna mfanano mkubwa katika mjengeko wa ndoa mbili hizi, ni kwa nini mafaqihi wa Kisunni wanakataa ndoa ya muda na kuiruhusu ndoa ya misyar? [16]
Hukumu ya Ndoa ya Misyar
Kwa mujibu wa nukuu za Nassir Makarim Shirazi, ni kwamba; wanazuoni wote wa Shia walioitafiti ndoa ya misyar wameruhusu hii ndoa kutendeka chini y masharti maalum ya ndoa. [17] Kwa maoni yake, ndoa hii ni sahihi katika hali mbili zifuatazo:
1. Katika mkataba wa ndoa hii haipaswi mwanamke kupewa sharti la kutodai haki zake msingi, ikiwemo haki ya matumizi, haki ya kuishi pamoja, haki ya makazi pamoja na haki yake ya urithi. Badala yake, mwanamke anatakiwa kuwa huru katika maamuzi yake juu ya haki hizo, na kwa hiari yake mwenyewe anaweza kuamua kudai au kutodai haki hizo.
2. Kuacha baadhi ya haki katika mkataba wa ndoa kunapaswa kuwa kwa njia ya sharti la kitendo (yaani kitendo hakifanyiki bila ya mwanamke kukubali sharti hiyo), na si sharti la matokeo ya kitendo; katika sharti la kitendo, mwanamke atasema kwamba; iwapo mumme huyo atamuoa, basi natija yake ni kwamba, yeye hatadai haki za matumizi na haki ya kuishi pamoja. [18]. Kwa maoni ya Makarim Shirazi, kwa kufuata mfumo wa sharti ya kitendo, mwanamke anaweza kusamehe haki zake, hata haki ya urithi pia naweza kuachana nayo. [19]
Inasemekana kuwa Sayyid Ali Sistani na Hossein Ali Montadhiri, ambao ni wanazuoni maarufu wa Shia, pia nao wameruhusu ndoa ya misyar [20].
Nafasi ya Kauli ya Wanazuoni Kuhusu Ndoa ya Misyar
Miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu ya Kisunni, kuna mitazamo mitatu kuhusu ndoa ya Misyar: Wengine wanaona kwamba ndoa hii ni halali, huku baadhi yao wakiihisabu kuwa ni ndoa haramu, na kundi la limebaki bila ya kuwa na msimamo maalumu, huku wakibaki bila ya kutoa hukumu maalumu juu ya ndoa ya misyar. [21] Waungaji mkono wa ndoa ya misyar wanaamini kwamba; ndoa hii inazingatia masharti na mihimili yote ya ndoa ya kudumu na ina manufaa muhimu katika jamii. [22] Kwa mujibu wa maelezo ya Makarim Shirazi, ni kwamba; wanazuoni wengi wa Kiislamu wa upande wa madhehebu ya Kisunni kama vile; Bin Baz, mufti wa Saudi Arabia, Qaradawi, na Nasr Farid Waasil, mamufti wa Misri, wameihisabu ndoa hii kuwa ni doa halali; Ila Jad Aal-Haq, sheikh wa zamani wa Al-Azhar, alipingana na ndoa hii. [23] Abdullah al-Mani’i, mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wakuu wa Saudi Arabia [24], na Dar al-Ifta ya Misri inayohusiana na Al-Azhar, pia wamekubaliana na uhalali wa ndoa ya misyar na wanaihisabu kuwa ni miongoni mwa ndoa sahihi. [25]