Nenda kwa yaliyomo

Najmakhatun

Kutoka wikishia
Kaburi linalohusishwa na Najma Khatun huko Mashraba Umm Ibrahimkatika mji wa Madina kabla ya uharibifu.

Najmakhatun (Kiarabu: نجمه‌خاتون) alikuwa ni mke wa Imamu Kadhim (a.s) na mama wa Imamu Ridha (a.s) na bibi Fatima Maasuma (a.s). Bibi Najma (Najmakhatun) alikuwa ni mjakazi ambaye bibi Hamida mke wa Imamu Sadiq (as), alimnunua na kumkabidhi kwa Imamu Kadhim (a.s). Kulingana na baadhi ya Riwaya, ni kwamba bibi Hamida alionana na bwana Mtume (s.a.w.w) ndoto mwake, na kwa amri ya bwana Mtume (s.a.w.w), akamkabidhi bibi Najma kwa Imamu Kadhim (a.s). Kaburi la Bibi Najma liko katika Bustani la Mashrabah liluloko huko Madina. [Maelezo 1]

Ukoo na nasaba

Bibi Najmakhatun alikuwa ni mjakazi ambaye bibi Hamida, mke wa Imamu Sadiq (a.s), alimnunua na kumkabidhi kwa Imamu Kadhim (a.s). Yeye ndiye aliyemzalia Imamu Kadhimu (a.s) mwana anayejulikana kwa jina la Imamu Ridha (a.s). [1] Baadhi wanamzingatia yeye kuwa ni mtu wa kutokea mji wa Nubia Kaskazini mwa Afrika, na wengine wanamfahamu kuwa ni mtu wa kisiwa cha Marseille Kusini mwa Ufaransa. [2] Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea pia yeye kujulikana kama ni Khaizuran al-Marsiyya na Shaqraa Nubiyah [3].

Jina na lakabu zake

Jina lake maarufu zaidi ni Najma Khatun. Yeye pia anajulikana kwa majina mengine kama vile; Sakina Nuubiyya [4], Arwaa, Samanah, Tuktam, na Khaizuran. [5] Kulingana na Riwaya kutoka kwa Sheikh Saduqu, ni kwamba; wakati Najmakhatun alipokabidhiwa kwa Imamu Musa al-Kadhim (a.s), alimwita Tuktam [6], na pale Imamu Ridha (a.s) alizaliwa kupitia kwake, akampa jina la Tahira. [7] Jina la lakabu lilikuwa ni Shaqraa na kunia yake ni Umm al-Banina. [8]

Cheo na hadhi yake

Imepokewa kutoka kwa bibi Hamida, mke wa Imamu Sadiq (a.s), akimwambia Imamu Kadhim (a.s) ya kwamba; yeye hakumwona mjakazi mbora mwenye sifa kama Najma [9]. Kulingana na Riwaya kutoka kwa Sheikh Saduqu, ni kwamba; Hamida alimuona Mtume Muhammad (s.a.w.w) akiwa ndoto mwake, akimtaka amkabidhi Najma kwa mwanawe (Imam Kadhim) (a.s), kwa kuwa bibi huyu atamleta duniani mtu mtukufu mno. Kwa hivyo Hamida alimkabidhi bibi Najma, ambaye wakati huo alikuwa bikira, kwa Musa bin Ja'far (a.s) [10]. Pia Imamu Kadhim (a.s) amesema ya kwamba; kununuliwa kwa bibi Najma kulitimia kwa amri ya bwana Mtume (s.a.w.w). [11] Imepokewa kutoka kwa bibi Najma akisema ya kwamba; wakati wa yeye alipokuwa na ujauzito wa Imamu Ridha (a.s), katu hakuhisi uzito wa ujauzito huo, na hata usingizini alikuwa akisikia sauti za tasbihi (nyiradi) na tahlilu (Takbira) kutoka tumbo mwake, na alipoamka hakupata habari yoyote juu ya hilo [12]. Kulingana na moja ya ripoti, ni kwamba; bibi Najma aliomba kupewa mlezi wa kumlea Imamu Ridha (a.s), na sababu ya ombi hilo ilikuwa ni kwa ajili ya kuwa na wasaa wa kusali na kufanya ibada [13].

Mahali alipozikwa

Kulingana maneno ya Mohammed Baqir Husseini Jalali, ni kwamba; kaburi la bibi Najmakhatun liko karibu na kaburi la bibi Hamida, mke wa Imamu Sadiq (a.s), lililoko katika eneo la Al-‘Awaali huko Madina, Mashariki mwa makaburi ya Baqi'i. [14]

Maelezo

  1. Mashrabah ni neno linalomaanisha bustani au ardhi laini ambapo mimea inaweza kukua kwa urahisi. Pia linaweza kutumika kuelezea sehemu ya ardhi yenye kilima kikubwa katikati, au chumba au jengo juu yake. Mashrabah ilikuwa ni bustani yenye jengo ambapo Maria al-Qibtiyya alimzaa Ibrahim, mwana wa Mtume wa Mungu (amani na baraka zimshukie yeye na familia yake) ndani yake. Mashrabah hii iko kaskazini mwa Banu Quraidha katika Harrah ya mashariki, inayojulikana pia kwa jina la "Dasht." Taarifa hii ni kutoka kitabu "Wafa-u al-Wafaa bi Akhbar Daru al-Mustafa (amani iwe juu yake)," juz. 3, uk. 825.

Vyanzo

  • Ḥusaynī Jalālī, Muḥammad Bāqir. Fadak wa al-ʿwālī aw al-ḥawāyit al-sabʿa fī al-kitāb wa al-sunna wa al-tārīkh wa al-adab. Mashhad: Kungira-yi Mīrāth-i ʿIlmī wa Maʿnawī-yi Ḥaḍrat-i Fāṭima Zahrā, 1426 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Edited by Sayyid Hāshim Rasūlī Maḥallātī. Tabriz: Intishārāt-i Banī Hāshimī, 1381 AH.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Ithbāt al-waṣīyya. 3rd edition. Qom: Muʾassisat Anṣārīyān, 1426 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. 3rd edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1367 Sh.
  • Mujmal al-tawārīkh wa al-qaṣaṣ. Unknown Author. Edited by Malik al-Shuʿarā Bahār. Tehran: Kalāla Khāwar, [n.d].
  • Muzaffarī, Ḥaydar. Mādarān-i chāhārdah maʿṣūm. 1st Edition. Qom: Markaz-i Jahānī-yi ʿUlūm-i Islāmī, 1382 Sh.
  • Qāʾimī, ʿAlī. Dār maktab-i ʿālim-i āl-i Muḥammad. Tehran: Intishārāt-i Amīrī, 1378 Sh.
  • Qummī, Ḥusayn b. Muḥammad b. Ḥasan. Tārīkh-i Qom. Translated to Farsi by Ḥasan b. Alī b. Ḥasan Abd al-Malik Qummī. Edited by Sayyid Jalāl al-Dīn Tehrānī. Tehran: Intishārāt-i Ṭūs, 1361 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. Translated to Farsi by Kūh Kamaraʾī. Tehran: Kitābkhāna-yi Islāmīya, 1362 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Ḥusayn Aʿlamī. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1404 AH.