Musahaqa
Kusagana (Kiarabu: المُسَاحقَة أو السِّحَاق) ni tendo la kimwili ambapo mwanamke mmoja husugua sehemu zake za siri juu ya sehemu za mwanamke mwingine kwa lengo la kupata raha ya kimwili (za kujinsia). Kitendo hichi kimekosolewa vikali katika mafundisho yaliyomo ndani ya Hadithi mbali mbali. Pia kumetolewa onyo kali la adhabu za Akhera kuhusiana na tendo hili. Hadithi hizo zinachukulia tendo la musahaqa kama ni aina ya uzinzi uliopindukia mipaka, pia Hadithi zimewalaani wale wanaofanya tendo hili.
Mafaqihi wa Kishia, wakitegemea Hadithi za Maimamu watakatifu, wameharamisha tendo la musahaqa (usagaji) na kutoa adhabu yake ya kupigwa mijeledi mia moja kwa kila atendaye tendo hili. Kwa mujibu wa fatwa nyingi, ni kwamba; ushahidi wa wanaume wanne waadilifu huwa unahitajika ili kuthibitisha tendo hilo, au pia tendo hili linaweza kuthibitishwa kwa kukiri kwa mwanamke aliyelifanya tendo hilo mara nne. Hata hivyo, kama mwanamke huyo atatubu kabla ya ushahidi kuthibitishwa, hatapata adhabu yoyote ile baada ya toba hiyo. Maoni ya mafaqihi wengi yanasema kwamba; ikiwa mwanamke atapata adhabu ya musahaqa mara tatu, basi mara ya nne adhabu yake itakuwa ni kupigwa mawe hadi kufa.
Dhana na Nafasi ya Musahaqa katika Sharia
Katika sharia ya Kiislamu, mafuqaha wa Shia wamefafanua tendo la musahaqa kama ni kitendo cha kusugua sehemu za siri za mwanamke mmoja dhidi ya tupu za mwanamke mwingine, kwa nia ya kujipatia raha ya kimwili. [1] Tendo hili ni moja ya matendo yatendwayo na baadhi ya wanawake wanaohusika na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wenzao (lesbianism), au mapenzi ya watu wa jinsia moja ikiwa ni moja ya njia za kufanikisha hisia za kimwili na kijinsia kileleni mwake. [2] Katika istilahi ya lugha ya Kiswahili, tendo hili hujulikana kwa jina la «kusagana», ambapo Waajemi wao huita tabaqezaniy. [3]
Tarehe na Nafasi yake
Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, hususan katika madhehebu ya Shia, tendo la musahaqa limeharamishwa wazi ndani ya Hadithi za Maimamu watakatifu huku likitambuliwa kuwa ni tendo la uzinzi mkuu. [4] Pia Hadithi zao zimewalani watendao tendo hilo, [5] na kuahidi adhabu kali siku ya Kiama dhidi ya wafanyao tendo hili. [6] Kulingana na Hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), wanawake wa kwanza kuhusika na musahaqa walikuwa wanawake wa kaumu ya Lut. Sababu iliyotolewa ni kwamba wanaume wa kaumu hiyo walikuwa wakijihusisha na uhusiano wa kimapenzi ya wenyewe kwa wenyewe (ubaradhuli), hivyo wakawaacha wanawake wao bila ya kuwa na waume wawezao kukidhi haja zao za kindoa. Kwa kule wao kukosa wapenzi wa kiume, wanawake hawa walijikuta wakifanya yale ambayo wanaume wao walikuwa wakifanyiana wao kwa wao, yaani kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi kati yao wenyewe kwa wenyewe. [7] Katika hadithi nyingine, imesimuliwa ya kwamba walengwa wa Ashab al-Rass, waliotajwa katika Aya ya 12 ya Surat Qaaf, walikuwa ni wale waliokuwa wakijihusisha na matendo ya musahaqa (kusagana). [8]
Kusagana kwa Mujibu wa Maoni ya Kifiqhi
Tendo la kusagana katika fiqhi ya Shia, huhisabiwa kuwa ni miongoni mwa matendo ya kukiuka mipaka, na imeelezwa wazi kuwa ni miongoni mwa matendo ya haramu kisheria. Hukumu za tendo hili na taratibu za kuthibitishwa kwake zimefafanuliwa kwa kina katika sheria za Kiislamu.
Uharamu Wake
Kulingana na maelezo ya Allama Hilli, mmoja wa mafaqihi mashuhuri wa upande wa madhehebu ya Shia wa karne ya nane Hijria, ni kwamba; mafaqihi wote wa madhehebu ya Shia wameafikiana juu ya uharamu wa amali ya kusagana. [9] Miongoni mwa sababu za kuharamishwa kwa tendo la ubaradhuli pamoja na kusagana zilizotajwa katika moja ya Hadithi iliyosimuliwa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s.), ni kule matendo haya kwenda kinyume muundo na maumbile asilia ya wanaume na wanawake katika kukidha haja za kimapenzi na kimaumbile. Na kwamba lilikusudiwa kati ya wanaume na wanawake, siyo baina ya watu wa jinsia moja kukutana kimapenzi wenyewe kwa wenyewe. [10] Zaidi ya hayo, Hadithi hii inabainisha kwamba uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja, kama vile usahagaji, unaweza kusababisha kupotea kwa kizazi cha wanadamu, kuvuruga taratibu za kijamii, na hatimaye kuleta madhara makubwa kwa jamii nzima na hata kuangamiza ustawi wa dunia. [11] Hivyo, hukumu ya kuharamisha kwa usahagaji inahusishwa moja kwa moja na kulinda mwendelezo wa kizazi na kuhakikisha utulivu wa kijamii.
Njia za Kuthibitisha wa Kosa la Usagaji
Fiq’hi ya Shia imefafanua kwa kina misingi ya sheria za Kiislamu ya kuthibitisha kosa la usagaji. Kulingana na mafaqihi wengi wa Kishia, njia zifuatzo ndio njia kuu za kuthibitisha kosa la usagaji:
- Ushahidi wa wanaume wanne waaminifu na waadilifu: Kama ilivyo kwa makosa mengine ya zinaa, ushahidi wa wanaume wanne waadilifu na wacha Mungu wanaoshuhudia tukio hilo ndio unaoweza kuthibitisha usagaji. Kwa mujibu wa kanuni za Kiislamu, ni lazima mashahidi hao kuwa ni waadilifu na waaminifu.
- Kukiri mara nne: Mwanamke anayekubali kuwa alijihusisha na tendo la usagaji anapaswa kukiri mara nne ili ithibitike kisheria kuwa yeye mtenda kosa hilo kisheria. Hii pia ni moja ya njia kuu za kuthibitisha makosa yanayohusiana na matendo ya zinaa au usagaji. [12] Hata hivyo, kulingana na faqihi mashuhuri wa karne ya kumi Hijria, aitwaye Muqaddas Ardabili, ni kwamba; kosa la usagaji huthibiti kupitia ushahidi wa wanaume wawili waadilifu au kukiri mara mbili kwa mwanamke aliyejihusisha na tendo hio. [13] Vifungu vya 172 na 199 vya Sheria ya Adhabu za Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, vinakubaliana moja kwa moja na maoni ya mafaqihi wengi ya kwamba kosa la usagaji huthibitishwa kupitia: Ushahidi wa wanaume wanne waadilifu na Kukiri mara nne kwa mwanamke anayekiri kujihusisha na usagaji. [14]
Adhabu ya Kusagana
Kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi wote wa Kishia, tendo la gusagana ni miongoni mwa makosa ya kisheria lipaswalo kukomesha kwa kupitia adhabu maalumu za kisheria. [15] Kanuni maalum zinazohusiana na adhabu kwa wale wanaothibitika kufanya tendo hili ni kama ifuatavyo:
- Adhabu Kuu:
Kulingana na maoni ya mafaqihi wote wa Shia, mwanamke anayethibitishwa kufanya musahaqa (tendo la kusugua sehemu za siri za mwanamke mmoja dhidi ya mwingine kwa ajili ya kupata raha ya kimwili) yabidi kuhukumiwa kwa kupigwa mijeledi mia moja. Hii ni adhabu ya jumla ambayo inahusu wanawake wote, bila kujali mtendaji wa tendo hilo kuwa ni Muislamu au si Muislamu (kafiri). [16] Pia, hakuna tofauti kati ya mwanamke aliyeolewa (muhsana) na yule asiyeolewa (ghayr muhsana), hii ni kulingana na makubaliana ya mafaqihi wengi wa Kishia kama ilivyosemwa na Sahibu’l-Jawahiri ya kwamba; huo ndiyo uliokuwa mtazamo wa mafaqihi wa karne ya 13 Hijiria. [17]
- Hukumu ya Kifo kwa Muhsana:
Hata hivyo, mafaqihi wa karne ya tano Hijria, wakiwemo Sheikh Tusi, [18] Ibn al-Barraj, [19] na Ibn Hamza Tusi, [20] wamesema kwamba; iwapo aliyetenda tendo hilo la kusagana atakuwa ni mwanamke aliyeolewa (muhsana), basi adhabu yake itakuwa ni kupigwa mawe hadi kufa. Hukumu hii inatokana na kanuni za fiqhi zinazoshughulikia masuala ya zinaa kwa mtu aliyekuwa ndani ya ndoa.
- Sheria za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran:
Katika vifungu vya 239 na 240 ya Sheria ya Adhabu za Kiislamu nchini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imetajwa wazi kwamba adhabu ya usagaji ni kipigo cha bakora mia moja, bila kutofautisha kati ya mwanamke Muislamu, kafiri, muhsana (aliyeolewa), au ghayr muhsana (asiyeolewa). [21]
- Toba na Kusamehewa:
Pia mafuqihi wa Kishia wameeleza kwamba; ikiwa mwanamke atatubia kutokana na tendo hilo kabla ya kosa la kusagana kuthibitishwa kupitia ushahidi wa kisheria, basi hatatakabiliwa na adhabu yoyote ile mbele ya sheria za Kiislamu. [22] Hii inaunga mkono kanuni za Kiislamu zinazozingatia toba kama ni njia ya mtu kupata msamaha kutoka na makossa yake, kwa sharti kwamba toba hiyo iwe ya kweli.
- Hukumu ya Kuuawa kwa Kurudia:
Kulingana na fatwa za mafaqihi wengi, ni kwamba; ikiwa mwanamke atathibitishwa kufanya kosa la usagaji mara tatu, huku kila mara akawa amepigwa mijeledi kulingana na sheria za Kiislamu, basi mara ya nne itabidi ahukumiwe kuuawa. [23] Hata hivyo, faqihi Ibn Idris Hilli wa karne ya sita Hijria alisema kwamba; hukumu ya kuuawa inapaswa kutekelezwa baada ya kupatikana kwa thibitisho la mara ya tatu. Hii ni tofauti na maoni ya mafaqihi wengine wanaosema kuwa; hukumu ya kuuawa inapaswa kutolewa baada ya kuthibiti tendo hilo kwa mara ya nne. [24]