Nenda kwa yaliyomo

Mulla Asgharali Jaffer

Kutoka wikishia
Mulla Asghar Ali Jaffer

Mulla Asghar Ali Jaffer (Kiarabu: ملا اصغر علی جعفر ) mashuhuri kwa jina la Mulla Asghar (1936-2000) alikuwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Shia Khoja Ithnaasharia na mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s). Yeye ni katika shakhsia wa Khoja Shia Ithnaasharia ambaye alikuwa mwakilishi wa Sayyid Muhsin Hakim, Sayyid Abul-Qassim na Sayyid Ali Sistani miongoni mwa Marajii Taqlidi wa Kishia. Mulla Asghar ameacha athari kama vile kitabu cha Sheria za Kiislamu ambacho ni tarjuma ya Kiingereza ya Fat'wa za Ayatullah Sayyid Ali Sistani. Mulla Asghar aliaga dunia 2000 na kuzikwa katika makaburi ya Mashia Khoja Ithnaasharia mjini London.

Maisha yake

Mulla Asghar alizaliwa mwaka 1936 huko Mombasa-Kenya. Baba yake Mulla Muhammad Jaafar alikuwa mmoja wa wahubiri na mubalighina wa Kishia. Alianza elimu yake katika mji aliozaliwa kisha akaenda India kuendelea na masomo yake katika fani ya udaktari wa macho, na baada ya kifo cha baba yake, alianza kuuza miwani katika miji ya Mombasa, Arusha, Nairobi na Nakuru. [1]

Mulla Asghar alihamia Uingereza mwishoni mwa miaka ya 1960 na kuishi London. Alikuwa anajua lugha za Kiurdu, Kifarsi, Kiswahili, Kiingereza na Kigujarati. Mbali na kuwa Imamu wa Sala ya Ijumaa huko London, alitoa mihadhara kwa lugha ya Kiingereza na Kigujarati katika Husseiniya ya Hujjat katika mji huo. [2] Alikuwa na mawasiliano na Marajii Taqlidi wa Iraq na Iran na mnamo 1982, wakati wa safari yake ya Iraq, alikamatwa na kufungwa na serikali ya nchi hiyo. Mnamo mwaka wa 1370 Hijiria Shamsia, akawa mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt kufuatia hukumu ya Ayatullah Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. [3]

Mulla Asghar aliaga dunia mnamo Machi 2000 huko London, Uingereza na akazikwa katika makaburi ya Shia Khoja Ithnaasharia katika mji huo. Baada ya kifo chake, Shirikisho la Kimataifa la Shia la Khoja lilitangaza siku tatu za maombolezo ya umma na ili kuthamini huduma zake, lilianzisha mfuko uliojulikana kwa jina la Mullah Asgharali Fund kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu maskini barani Afrika. [4]

Harakati

  • Ushirikiano katika kuasisi Shirikisho la Kimataifa la Jumuiya (jamii) ya Khoja Shia Ithnaasharia.
  • Kuleta nidhamu kwa makhoja Ithnaasharia waliofukuzwa kutoka Zanzibar.
  • Kuanzisha mfuko wa kuisaidia Zanzibar kwa ushirikiano na kundi la Mashia Khoja Ithnaasharia mwaka 1963.
  • Kushiriki katika kutunga katiba ya Shirikisho la Kimataifa la Shia Khoja Ithnaasharia.
  • Kuandaa mazingira ya kukaa nchini Uingereza na mataifa mengine Makhoja waliokuwa wamefukuzwa kutoka Uganda.
  • Himaya ya kimaada kwa asasi za Kishia nchini India na Pakistan.
  • Kuasisi Madrasat al-Khui katika mji wa Birmingham.
  • Kutoa mihadhara kwa lugha ya Kigujarati na Kiingereza katika Husseiniya ya Hujjat mjini London.
  • Kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi katika mji wa Rudbar Iran. [5]

Nyadhifa

Athari

Mulla Asghar ameandika na kutarjumu vitabu mbalimbali:

  • Saumu.
  • Sala ya Jamaa.
  • Pearls of Wisdom.
  • Fiq'h na Mafuqaha.
  • Subhanallah; Maajabu ya Uumbaji Katika Qur'ani.
  • Sheria za Kiislamu (Tarjuma ya Kiingereza ya kwa mujibu wa Fat'wa za Ayatullah Sistani).
  • Tarjumat al-A'mal (nakala ya Sheikh Mufid). [7]