Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Dua ya 54 kutoka katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Hamsini na Nne ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa mnamo Sha'ban 1102 AH.

MadaDua inayofundisha namna ya kumuelekea Mwenye Ezi Mungu kwa ajili kutafuta afueni kutokana na huzuni, dhiki, pamoja na majonzi ya moyo.
Ina Mapokezi au Haina MapokeziIna Mapokezi
Imenukuliwa Kutoka kwaImamu Sajjad (a.s)
MpokeziMutawakkil ibn Harun
Vyanzo vya KishiaSahifa Sajjadiyah
Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini

Dua ya Hamsini na Nne ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الرابع والخمسون من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua adhimu iliyopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), nayo ni ile dua mahususi aliyokuwa akiisomwa kwa ajili ya kuomba faraja na kuondolewa kwa mfadhaiko na huzuni aliyonayo moyoni mwake. Ndani ya dua hii tukufu, Imamu Sajjad (a.s) anamtaja Mwenye Ezi Mungu kuwa ndiye Mtoaji faraja mkuu na pekee Mwenye uwezo wa kuondoa huzuni na mifazaiko ya nyoyo za waja Wake. Vilevile, dua hii inajumuisha ombi la kumuomba Mwenye Ezi Mungu taufiki na majaaliwa ya kupata hatima njema.

Kwa wale wanaotafuta maelezo ya kina zaidi, dua hii imefasiriwa na kufafanuliwa kwa mapana katika vitabu mbali mbali vilivyofasiri dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu hivyo ni pamoja na; Shuhudi wa Shenaht kilichoandikwa kwa lugha ya Kifarsi na Hassan Mamduhi Kermanshahi, pamoja na Riadhu al-Salikin kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na bwana Sayyid Ali Khan Madani. Vitabu hivi vimefafanua na kueleza kwa undani kabisa maana ya dua hii.

Mafunzo ya Dua ya Hasuni na Nne

Dua ya hamsini na nne inayopatikana katika Sahifa Sajjadiyya, ni miongoni mwa dua tukufu zilizonukuliwa kutoka Imamu Sajjad (a.s). Katika dua dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anafundisha namna ya kumuelekea Mwenye Ezi Mungu kwa ajili kutafuta afueni kutokana na huzuni, dhiki, pamoja na majonzi ya moyo. Bwana Hassan Mamduhi Kermanshahi katika tafsiri yake ya dua hii anatoa ufafanuzi wake akisema kwamba; mwanadamu hupitia mitihani mbali mbali ya huzuni katika maisha yake, ikiwemo mitahini hapa duniani pamoja na ile inayomkabili mbeleni huko Akhera. Pia mitihani hii hausiani na upande wa kimwili peke yake, bali kuna mitihani kadhaa inayohusiana na masuala ya kiroho. Ili mwanadamu aweze kupata afueni kutoka na tatizo hili, bwana Hassan Mamduhi anasisitiza akisema kwamba; katika mchakato wa kukabiliana na hali hizi, muumini wa kweli hutafuta (au anatakiwa) kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu, huku akiwa na unyenyekevu na matumaini ya kutatuliwa matatizo yake.[1]

Mafunzo ya dua ya hamsini na nne yamekuja kama ifuatavyo:

  • Mwenye Ezi Mungu mwenye huruma ndiye mfunguzi wa kuondoa huzuni na dhiki mbali mbali.
  • Mfumo wa kumuomba Mwenye Ezi Mungu kupitia sifa zake ili kupata faraja maishani mwetu.
  • Kuomba hatima bora kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu.
  • Kumuomba Mwenye Ezi Mungu kwa kudhihirisha ukubwa wa mahitajio yetu pamoja na upugufu na uduni wa nguvu zetu.
  • Dua ya kuomba kifo cha kwenye njia ya haki, matendo mema na maadili bora.
  • Ombi la kuomba kutokuwa na tamaa ya dunia na kuomba kuwa na raghaba ya ukaribu na Mwenye Ezi Mungu.
  • Kumuomba Mungu ulinzi dhidi ya hatima mbaya.
  • Kuomba taufiki ya kupata daraja ya imani ya haki yakinifu (haqqu al-yaqin).
  • Kuomba ombi la kupata shauku ya mapenzi ya kweli kwa ajili ya Mwenye Ezi Mungu kama yalivyo mapenzi ya wale wampendao Mola wao.
  • Kuomba kupata hofu ya kumhofu Mungu, kwa kiwango cha hofu ya wacha-Mungu wa kweli.
  • Kumtegemea na kumtumainia Mwenye Ezi Mungu peke yake, katika kila jambo maishani mwetu.
  • Ombi la kuomba hofu ya wenye kumwabudu Allah, ibada ya wanyenyekevu, na yakini ya waliotawakali kwa Mola wao.
  • Kuomba rekodi bora za matendo yetu.
  • Kuwa na hofu sambamba na kuwa na matumaini kwa Mola wetu.
  • Baraka za akhera ndiyo zawadi bora zaidi kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu.
  • Dua ya kuomba afya njema na uzima wa mwili.
  • Kuomba ulinzi dhidi ya fitina potoshi
  • Dua ya kusimama imara katika kuitekeleza dini bila kuogopa watu.
  • Baraka na amani ya Mwenye Ezi Mungu kwa Mtume wake mteule pamoja na Aali zake.[2]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Hamsini na Nne

Dua ya hamsini na nne ya Sahifa Sajjadiyya imefafanuliwa na wanazuoni wengi na kwa lugha mbalimbali ulimwenguni. Miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kifarsi vilivyochambua dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kama vile; Diare Ashiqan kilichoandikwa na mwanachuoni aitwaye Hussein Ansarian,[3] Shuhudi Shenakht cha Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi,[4] pamoja na Sherh wa Tarjume Sahife Sajjadiyye cha Sayyid Ahmad Fahri.[5]

Kadhalika, kwa upande wa lugha ya Kiarabu, kumetokea wanazuoni maalumu waliamua kuwahudumia matumiaji wa lugha ya Kiarabu katika kuelewa madhumuni ya dua hii bila ya kuacha dua nyengi zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu maarufu vilivyotoa huduma hii ni kama vile; Riadhu al-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhilali Sahifa Sajjadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyyah,[7] Riadhu Al-Arifina cha Muhammad bin Muhammad Darabi,[8] na Afaqi Al-Ruh cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Zaidi ya hayo, pia kuna jopo la wanazuoni walihisi ulazima wa kufafanua msamiati (muundo wa lugha) wa uliotumika ndani ya dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya. Uchambuzi huu wa kitaalamu unaweza kuupata kupitia kitabu kiitwacho Ta’aliqat Ala Sahifati Sajjadiyya cha Faidhu Kashani[10] pamoja na Sharhu Al-Sahifa Al-Sajjadiyya cha Izzu Al-ddin Jaza’iri.[11]

Matini ya Dua ya Hamsini na Nne Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي اسْتِكْشَافِ الْهُمُومِ

يَا فَارِجَ الْهَمِّ، وَ كَاشِفَ الْغَمِّ، يَا رَحْمَانَ الدُّنْيَا وَ الْآخِرَةِ وَ رَحِيمَهُمَا، صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ، وَ افْرُجْ هَمِّي، وَ اكْشِفْ غَمِّي.

يَا وَاحِدُ يَا أَحَدُ يَا صَمَدُ يَا مَنْ‏ «لَمْ يَلِدْ وَ لَمْ يُولَدْ وَ لَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُواً أَحَدٌ«، [12] اعْصِمْنِي وَ طَهِّرْنِي، وَ اذْهَبْ بِبَلِيَّتِي. وَ اقْرَأْ آيَةَ الْكُرْسِيِّ وَ الْمُعَوِّذَتَيْنِ وَ قُلْ هُوَاللهُ أَحَدٌ، وَ قُلْ:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ سُؤَالَ مَنِ اشْتَدَّتْ فَاقَتُهُ، وَ ضَعُفَتْ قُوَّتُهُ، وَ كَثُرَتْ ذُنُوبُهُ، سُؤَالَ مَنْ لَا يَجِدُ لِفَاقَتِهِ مُغِيثاً، وَ لَا لِضَعْفِهِ مُقَوِّياً، وَ لَا لِذَنْبِهِ غَافِراً غَيْرَكَ، يَا ذَا الْجَلَالِ وَ الْإِكْرَامِ أَسْأَلُكَ عَمَلًا تُحِبُّ بِهِ مَنْ عَمِلَ بِهِ، وَ يَقِيناً تَنْفَعُ بِهِ مَنِ اسْتَيْقَنَ بِهِ حَقَّ الْيَقِينَ فِي نَفَاذِ أَمْرِكَ.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ، وَ اقْبِضْ عَلَى الصِّدْقِ نَفْسِي، وَ اقْطَعْ مِنَ الدُّنْيَا حَاجَتِي، وَ اجْعَلْ فِيمَا عِنْدَكَ رَغْبَتِي شَوْقاً إِلَى لِقَائِكَ، وَ هَبْ لِي صِدْقَ التَّوَكُّلِ عَلَيْكَ.

أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ كِتَابٍ قَدْ خَلَا، وَ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كِتَابٍ قَدْ خَلَا، أَسْأَلُكَ خَوْفَ الْعَابِدِينَ لَكَ، وَ عِبَادَةَ الْخَاشِعِينَ لَكَ، وَ يَقِينَ الْمُتَوَكِّلِينَ عَلَيْكَ، وَ تَوَكُّلَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَيْكَ.

اللَّهُمَّ اجْعَلْ رَغْبَتِي فِي مَسْأَلَتِي مِثْلَ رَغْبَةِ أَوْلِيَائِكَ فِي مَسَائِلِهِمْ، وَ رَهْبَتِي مِثْلَ رَهْبَةِ أَوْلِيَائِكَ، وَ اسْتَعْمِلْنِي فِي مَرْضَاتِكَ عَمَلًا لَا أَتْرُكُ مَعَهُ شَيْئاً مِنْ دِينِكَ مَخَافَةَ أَحَدٍ مِنْ خَلْقِكَ.

اللَّهُمَّ هَذِهِ حَاجَتِي فَأَعْظِمْ فِيهَا رَغْبَتِي، وَ أَظْهِرْ فِيهَا عُذْرِي، وَ لَقِّنِّي فِيهَا حُجَّتِي، وَ عَافِ فِيهَا جَسَدِي.

اللَّهُمَّ مَنْ أَصْبَحَ لَهُ ثِقَةٌ أَوْ رَجَاءٌ غَيْرُكَ، فَقَدْ أَصْبَحْتُ وَ أَنْتَ ثِقَتِي وَ رَجَائِي فِي الْأُمُورِ كُلِّهَا، فَاقْضِ لِي بِخَيْرِهَا عَاقِبَةً، وَ نَجِّنِي مِنْ مَضَلَّاتِ الْفِتَنِ بِرَحْمَتِكَ يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.

وَ صَلَّى اللهُ عَلَى سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ رَسُولِ اللهِ الْمُصْطَفَى وَ عَلَى آلِهِ الطَّاهِرِينَ.

Na miongoni mwa dua zake (Imam Sajjad) (amani iwe juu yake), ni dua ile aliyokuwa akiisoma kwa ajili ya kutafuta faraja dhidi ya huzuni na dhiki za moyo.

Ewe Mfariji wa huzuni, (Mpondoaji wa dhikikwa kwa waliokumbwa na huzuni), Ewe Mpambazushi wa dhiki za moyo, Ewe Mrehemevu wa rehema kunjufu (kwa kila kiumbe) duniani na Akhera, na Mrehemevu wa rehema maalumu ndani ya nyanja mbili hizo. Mbariki (mrehemu) Mtume Muhammad pamoja na Aali zake, na unisaidie kuniondolea huzuni zangu na kunipambazulia msongo wa mawazo yangu.

Ewe Mmoja, Ewe wa Pekee (Usiyegawika kwa kigao chochote), Ewe Asiyehitaji kitu (Asiyekuwa na utegemezi wa kitu chcochote), Ewe Ewe Yule mwenye sifa ya kutohakuzaa wala kukuzaliwa, wala hana anayelingana Naye.” Ninilnde, unitakase, na uniondolee msiba wangu. (Baada kumaliza kipengele hicho) Soma Ayatul-Kursiy, Suratul-Falaq na Suratun-Nas na Suratu Al-Ikhlas, kisha unatakiwa kusema maneno yafuatayo:

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kwa ombi la mtu mwenye dhiki kumbwa mno, huku nguvu zake zikiwa zimedhoofika (huku akiwa hana nguvu tena), na dhambi zake zikiwa zimefurutu ada. (Ninakuomba) ombi la mtu asiye na msaada wa kutatua dhiki yake (asiyekuwa na mwokozi wa kumuokoa katika dhidi yake), wala hana nguvu ya kumuimarisha (kumjenga), na hana wa kufutia (kumsamehe) kosa lake (makosa yake) isipokuwa Wewe. Ewe Mwenye tukufu na ukarimu (taadhima), nakuomba unipe taufiki ya kutenda amali unazowapendea (ambazo ndio nyenzo unayowapendea kwazo) watendao amali hizo, na imani yenye yakini yenye kumnufaisha yule mwenye yakini nayo (mwenye kushikamana nayo) kwa yakini kamilifu katika utekelezaji wa amri zako.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, mbariki (mrehemu) Muhammad na Aali zake (watoharifu), na uichukue nafsi yangu hali ikiwa imesimama kwenye nguzo ya ukweli (imesimama kwenye mstari wa haki), na uniondolee haja ya kuihitajia dunia, na ielekeze raghaba yangu kwenye yale yaliyoko Kwako (yalioko katika hazina Yako), ili yawe ndiyo sababu ya kuwa na shauku ya kukutana nawe (ili yawe ndiyo chambo cha kunasa kwenye doana ya mapenzi yako). Na unipe, tawakuli ya kweli (utegemezi wa dhati) juu ya Yako.

(Ewe Mola), nakuomba mema yaliyomo katika maandiko yaliyotangulia, na najikinga Kwako na (kila) mabaya yaliyomo katika maandiko yaliyotangulia. Ninakuomba hofu ya wacha-Mungu wa kweli, ibada ya wanyenyekevu wanaonynyekea Kwako, yakini ya wanaotawakali Kwako, na utegemezi wa waumini wanaoamini Kwako.

Ewe Mwenye Ezi Mungu! Nifanye niwe na hamu katika kukuomba zangu (nifanye niwe na shaku na hisia kamili wakati wa kukuomba dua zangu), kwa kiwango cha hamu za wapenzi Wako katika maombi yao, na (ninakuomba uijaalie) hofu yangu iwe sawa na hofu ya wapenzi Wako. Nitumikishe (niajiri) kwenye (kazi ya utendaji wa) matendo yanayokupendeza, kwa namna ambayo (katu) sitapuuza kitu chochote kile katika dini Yako, kutokana na hofu ya kumuogopa mtu fulani miongoni mwa viumbe Wako.

Ewe mwenye Ezi Mungu hii ndiyo haja yangu, basi ikuze shaku yangu ndani yake, na udhihirishe udhuru wangu ndani yake (Yaani unidhirishie kuridhika kwako na maombi yangu na wala hukunikasirikia kutokana na kukuomba kile nishostahiki Kwako), na unifunze ndani yake namna ya kusimamisha hoja zangu (yaani unifunze namna ya kujenga hoja zangu ndani ya maombi yangu ya kujitetea mbele Yako, huku nikitafuta kisingizio cha kujitetea), na uupe afya mwili wangu ndani yake (yaani upe afya mwili wangu kupitia maombi haya haya).

Ewe Mwenye Ezi Mungu, ikiwa kuna mtu anayeamka (aliyeanza siku yake) akimtegemea au kumtumainia mwingine asiyekuwa Wewe (kuna wangapi wanaoanza siku yao kwa kumtegemea na kumtumainia asyekuwa Wewe), basi (kwa hakika) mimi nimeamka huku Wewe ukiwa ndiye tegemeo na tumaini langu katika masuala yangu yote. Hivyo basi, ninakuomba unihukumu kwa kunipa hatima yenye matokeo bora zaidi (katika kila jambo lililomo ndani ya siku hii), na (ninakuomba) kwa huruma Yako, uniokoe na changamoto za upotosha (zilizomo ndani yake), Ewe Mrehemevu kuliko warehemevu wote.

Na (ninakuomba) umbariki kwa amani Zako bwana wetu Muhammad, pamoja na Aali zake watoharifu, ambaye ni Mtume Mteule wa Mwenye Ezi Mungu.

🌞
🔄
➖
➕

Rejea

  1. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 380.
  2. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 380-394.
  3. ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 399-631-640.
  4. ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 377-394.
  5. ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 577-583.
  6. ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 7, uk. 413-446.
  7. ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 661-667.
  8. ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 731-738.
  9. ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 636-646.
  10. ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 103-105.
  11. ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 299-301.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.