Mkarimu wa Ahlul-Bayt (Lakabu)

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na moja ya lakabu za Imamu Hassan al-Mujtaba (as). Ili kujua na kufahamu shakhsia na maisha ya mtukufu huyu, angalia makala ya Imamu Hassan Mujtaba (a.s).
Kitabu cha Sayyid Muhammad Taqi Madrasi, kilicho chapishwa kwa jina la (Karim Ahlul-Bayt) kuhusu historia ya maisha ya Imamu Hassan (a.s).

Mkarimu wa Ahlul-Bayt (Kiarabu: كريم أهل البيت) ni katika lakabu za Imamu Hassan al-Mujtaba (a.s) [1] ambaye alipatiwa lakabu hiyo kutokana na ukarimu na sifa yake ya upaji na takrima kwa wengine. [2] Neno karim, licha ya kuwa katika vyanzo vya awali limetumika katika kutoa wasifu kwa Hassan bin Ali (a.s), [3] lakini katika maisha ya Imamu Hassan (a.s) na kuhusiana na kuniya na lakabu, hakuna kitabu chochote cha historia na hadithi kilichotaja Karim Ahl-Bayt (mkarimu wa Ahlul-Bayt kuwa ni katika lakabu zake isipokuwa vitabu vilivyokuja baadaye. [4]

Umashuhuri wa Imamu Hassan kwa lakabu ya mkarimu wa Ahlul-Bayt unatokana na visa vilivyonukuliwa na waaandishi wa historia kuhusiana na ukarmu na upaji wa Imamu huyu. [5] Inaelezwa kuwa, Imamu Hassan (a.s) alikuwa akisaidia mafakiri na wenye kuhitaji kiasi kwamba, kitu kama hiki hakionekani katika historia ya maisha ya shakshia yeyote mkubwa. [6] Katika zama zake Imamu Hassan alikuwa mtu mkarimu zaidi na alikuwa wa kupigiwa mfano katika upaji, hisani na kukirimu. Licha ya kuwa Ahlul-Bayt wote walikuwa wakarimu, lakini yeye tu ndiye aliyepewa lakabu ya mkarimu.[7]

Ibn al-Jawzi (aliyefariki mwaka 654 AH), mmoja wa wanachuoni wa Kisunni, katika kitabu chake Tadhkrah al-Khawas, amemuita Imamu wa pili wa Mashia kuwa ni miongoni mwa shakhsia wakubwa wa upaji na ukarimu na katika kutaja fadhila zake, anaandika: Imamu Hassan Ibn Ali (a.s) alitoa mara mbili mali yake katika umri wake na alitoa vyote alivyonavyo katika njia ya Mwenyezi Mungu kama ambavyo aligawana mali yake mara tatu nusu kwa nusu na masikini; [8] kama ambavyo imenukuliwa ya kwamba alimsaidia masikini dirihamu 20,000.[9]

Kuhusiana na lakabu ya Karim Ahlul-Bayt, Baqir Sharif Qureshi (aliyefariki dunia: 1433 AH), mmoja wa wanazuoni wa Kishia, ananukuu hadithi kuhusu hilo kwamba, Imamu Hassan al-Mujtaba (a.s) aliulizwa: Kwa nini humkatishi tamaa muombaji? Imam akajibu: Mimi pia ni masikini mbele ya Mwenyezi Mungu, na ninamuomba asininyime, na ninaona haya na soni kuwakatisha tamaa masikini kwa matumaini haya na Mwenyezi Mungu anayenipa uangalizi wake juu yangu, anataka nisaidie watu [10]

Kulingana na Sayyid Hussein Bahrul Ulum (aliyefariki: 1380 Hijiria Shamsia), mtafiti wa kitabu cha Talkhis al-Shafi ni kuwa, maudhui ya ukarimu wa Imam Hassan (a.s) ni pana zaidi kuliko inavyoweza kujadiliwa na kuzungumziwa. [11]

Nchini Iran baadhi ya taasisi za kheri (utoaji huduma za misaada) zinaitwa kwa jina la Karim Ahlul-Bayt. [13]